Tanzania imepoteza $370M miaka ya Makanikia

Tanzania imepoteza $370M miaka ya Makanikia

Inaonekana uelewa wako wa masuala ni mdogo. Mbona hoja yake iko bayana kuwa wewe ni ndumilakuwili?

Matusi ya rejareja mie nimeshazoea. Ninajua ni matusi kutoka kwa watu wenye CHUKI na KIJICHO. Hayanisumbui. Unaweza sasa kujenga hoja ya kupangua hizo takwimu?
 
Kila mgodi hisa 16%×3=48 haya siyo mafanikio? unajua tupo sisi tuliokua tunafanyakazi kmcl badae barrick badae accacia Zito ni porojo hana jipya ukiona ana piga kelele hivi njaa imempiga hapewi tena bahasha kama zamani Rais magu kathubutu na anaweza.
Kwanza inabidi kuwe na Timu ya Wataalamu huru kufanya uchunguzi wa kina wa miaka 3 ya Makanikia tumepata nini na tumepoteza nini. Timu hiyo ipendekeze hatua za kuchukua kurekebisha makusa.
 
Ni sawa na kusema ukiweka sehemu fulani ya mapato yako kwenye savings account umepata hasara.

Au kusema inventory which the business holds should be classified as loss kwa mujibu wa mleta hoja.

Makanikio yako pale pale if anything mzozo ukiisha bei ya dhahabu imepanda kutoka $1200 mwaka 2017 kufikia $1400 2019 na bado bei inatarajiwa kupanda.

25170713-4CD1-47D3-92CC-9034F0A44405.jpeg



Ina maana yale makanikia yaliyozuiwa leo yanathamani zaidi sokoni na yatarudisha hela nyingi zaidi + hela za kodi + economic benefit ambazo serikari ilikuwa aizipati.

Sasa hapo serikari imepoteza mapato kivipi. Sio kila kitu kupinga tu.
 
Hayo ni maomi yako wewe. Yeye Kama kiongozi aliyekabidhiwa dhamana amejaribu kufanya kile alichoona ni sawa. Halafu unatoaje hitimisho kuwa Kuna hasara wakati hata majadiliani bado hayajamalizika. Subrini mazunguzo yaishe yawekwe into effects halafu njooni mtoe Conclussion Kama Kuna faida au hasara. Acheni Ushehe Yahya.

Mikataba yote anayo, Team ya Wataalam anayo anashindwaje kufanya Jambo kwa Uhakika mpaka aamue mwenyewe kwa atakavyoona inafaa !!?.

Nnadhani Mh Rais anayo nafasi kubwa sana ya kufanya Jambo kwa uhakika huku akifahamu Faida na Hasara zake.Haya haya Makinikia yuliambiwa tulikuwa tunaibiwa (Ref Ripoti ya Profesa Usoro) na tuliaminishwa hapa tunawadai hao Mabeberu Trillion mia nne na usheee kilicho fuatia tuliambiwa tutalipwa kishika Uchumba..

Tuombe uzima Mkuu ,tutakutafuta baadae wakati wa Matokeo ya haya yanayo fanywa na Mh Rais wetu Mtukufu na mpendwa sana.
 
Mikataba yote anayo, Team ya Wataalam anayo anashindwaje kufanya Jambo kwa Uhakika mpaka aamue mwenyewe kwa atakavyoona inafaa !!?.

Nnadhani Mh Rais anayo nafasi kubwa sana ya kufanya Jambo kwa uhakika huku akifahamu Faida na Hasara zake.Haya haya Makinikia yuliambiwa tulikuwa tunaibiwa (Ref Ripoti ya Profesa Usoro) na tuliaminishwa hapa tunawadai hao Mabeberu Trillion mia nne na usheee kilicho fuatia tuliambiwa tutalipwa kishika Uchumba..

Tuombe uzima Mkuu ,tutakutafuta baadae wakati wa Matokeo ya haya yanayo fanywa na Mh Rais wetu Mtukufu na mpendwa sana.
We ndo kichwa maji kabisa. Unajua maana ya Rais wewe.
 
Mh. Zitto unafiki wako umefanya watu wengi wasikuelewe hata kama wakati fulani unaleta hoja za maana.
Ninaomba utusaidie hiyo taarifa mliyopewa nyie waheshimiwa wabunge ili nasi tuisome kama inawezekana

Kama kuwa wazi kwa ninachoamini ni unafiki basi unafiki una tafsiri mpya. Taarifa ya Hali ya Uchumi ni public document. Kitabu cha Mapato ya Serikali ni public document. Unaweza kumwomba mbunge wako akupe pia
 
Nyie mliokatabiana, mlijadili na kamati yenu ya siri mkaafikiana nao mabeberu! Tuambieni tofauti ya mkataba huu na wa awali kama ukiondoa tarehe na wajumbe wa kamati.

Ipo tofauti kubwa sana. Ila inahitaji hekima kuliko hizi emotions zinazoendelea, ambazo hazina lolote la kuongeza. Kusema ukweli mining industry imebadilika na itabadilika sana. Kuna tofauti kubwa kati ya jana na leo.

By the way, mbona watu wengine walikuwa wanapenda kuona Acacia inashinda na serikali inashitakiwa? Walikuwa wanapata nini?
Terrible. Israel ukifanya hivyo unabadilika jina immediately. Siasa yes, lakini sio suala la compromising them
 
Kama kuwa wazi kwa ninachoamini ni unafiki basi unafiki una tafsiri mpya. Taarifa ya Hali ya Uchumi ni public document. Kitabu cha Mapato ya Serikali ni public document. Unaweza kumwomba mbunge wako akupe pia
Shida yako ni mkurupukaji sana, halafu ukipata mambo juu juu unachanganya fact na opinions, unapika midata, ili tukuone konk kumbe hakuna lolote. maskini umepoteza kabisa mvuto wa kisiasa kwa ujuaji wako. Mara Rais atangaze balaa la njaa, Mara uhaba wa Mafuta ya ndege, sasa upo na hili tena.
 
Nchi imepoteza mno kwenye sakata la Makanikia [ Fedha za kigeni $200M na TZS 430B Mapato ya Serikali]

  • mwaka 2016 Tanzania iliuza nje dhahabu iliyoingiza USD 1.8 bilioni
  • Mwaka wa Makanikia 2017 mauzo nje yalishuka mpaka USD 1.6 bilioni na;
  • Mwaka 2018, mwaka ambao athari ya Makanikia ilikuwa mwaka mzima mauzo nje yalikuwa USD 1.4 bilioni

Kati ya mwaka 2017-2018 Mauzo nje ya dhahabu yalishuka kwa jumla ya $200M saw na 11%.

Katika kipindi hicho uzalishaji wa dhahabu ulishuka kutoka tani 43 za dhahabu mwaka 2015 mpaka tani 39 mwaka 2018. Uzalishaji wa mwaka 2018 ulikuwa sawa na uzalishaji wa mwaka 2010.

Mapato ya Serikali kutoka sekta ya Madini yameshuka katika kipindi cha Makanikia. Kwa mujibu wa Kitabu cha Mapato ya Serikali kwa Wabunge ( Revenues Book Vol. 1 ).

  • mwaka 2016/17 makusanyo ya mirahaba yalikuwa TZS 341 bilioni
  • Mwaka 2017/18 makusanyo ya mirahaba yalikuwa TZS 230 bilioni
  • Mwaka 2018/19 makusanyo yalikuwa TZS 220 bilioni.
Serikali imekadiria kukusanya TZS 350 bilioni mwaka 2019/2020.

Kwa mujibu wa Dkt. Genuine Martin kwenye mada yake kwa Policy Forum Breakfast Debate Julai, 2019 Mapato yote ya sekta ya Madini yameshuka kwa 32% katika zama za Makanikia.

  • mwaka 2016 Mapato yalikuwa TZS 1.3 trilioni
  • Mwaka 2018 Mapato yalikuwa TZS 867 bilioni.
Katika Miaka 2 Mapato ya Serikali kutoka sekta ya Madini yameshuka kwa TZS 430 bilioni.

Tunapata nini kutoka Barrick Gold baada ya sakata la Makanikia?

Mapato ambayo Serikali ya Magufuli imepoteza kwenye sekta ya Madini kati ya mwaka 2017 - 2019 ni makubwa zaidi ya malipo* ambayo Serikali inasema tutalipwa na Barrick Gold Corporation ili kumaliza mgogoro baina ya Kampuni ya Acacia na Serikali.

Tumeona hapo juu kuwa tumepoteza Mapato ya Fedha za kigeni $200M na Mapato ya Serikali kushuka kwa TZS 430 bilioni. Kutoka Barrick tunatarajiwa kupata $300M ambazo chache kulinganisha na kiasi tulichopeteza.

* Malipo yenyewe hayo ya $300M kwanza yatalipwa kwa miaka 7, pili yana masharti ya wao kulipwa kwanza Fedha zao za VAT ( $240M ), na tatu watasamehewa Kodi ya Capital Gains Tax ya mauzo ya hisa za Acacia kwa Barrick Gold ($85.6M). Hatimaye Tanzania ndio itakuwa imeilipa Barrick $25M ( Net of payments and receipts to and from Barrick Gold ).

Kwa hiyo Tanzania imepoteza Mapato iliyokuwa yakusanywe kama mgogoro usingekuwepo [ $200M exports revenues and $170M tax revenues ] na imeishia kuilipa Barrick badala ya yenyewe kulipwa.

Tumepata hasara kubwa sana kutokana na maamuzi yetu wenyewe, maamuzi ambayo hayakuzingatia maslahi ya nchi yetu. Tunapaswa kuwawajibisha waliotupa hasara hiyo.
Shetani na hivi hajui hesabu yeye anaona kapata ,kapatia kweli kumbe ni mwendelezo wake wa kuitia nchi hasara juu ya hasara .
 
Zitto anatakiwa atueleze kwa kubalance. Hizi data zake zimekaa kisiasa mno. Zinalenga kueneza siasa kuliko uhalisia.

Kivipi? Hizo data za Serikali sio zangu. Hizo za malipo ya Barrick zimetolewa na Barrick. Sasa Mimi nina kosa gani? Kuwaletea humu?
 
Ongelea na wangeiba shi ngap ww
Tatizo wabongo hawanaga akili
Mtu akimuibia milion na kumpa elf30 anaona kapataa
Ila akiiacha milion iliofichika chumban kwake anaona ni hasara
 
Kivipi? Hizo data za Serikali sio zangu. Hizo za malipo ya Barrick zimetolewa na Barrick. Sasa Mimi nina kosa gani? Kuwaletea humu?
Hawa ni vibaraka na wapiga makofi hivyo wapotezee tu kiongozi.
 
Nimefika hapa nikaona hata nikishuka huko chini ni pumba tu

"Kati ya mwaka 2017-2018 Mauzo nje ya dhahabu yalishuka kwa jumla ya $200M saw na 11%."

Takwimu ulizoleta hapo ni za dhahabu iliyozalishwa sasa makinikia yalikua yakiondoka kama mineral concentrates au purified gold?

Makinikia hayakuwa yakihesabiwa kama dhahabu bali takataka

HALAFU tumepotezaje hizo pesa wakati hakuna makinikia yaliyotoka?

Akili zenu mnazijua wenyewe.
 
Zitto anatakiwa atueleze kwa kubalance. Hizi data zake zimekaa kisiasa mno. Zinalenga kueneza siasa kuliko uhalisia.
Nikweli kwanza anatakiwa atueleza kabla ya Makinikia (wakati wa shamba la bibi) zilizokuwa nizapotea ni shilingi ngapi na walidhibiti ngapi, na kwa sasa zinapotea ngapi na udhibiti ni ngapi halafu alinganishe na hoja yake. Maana kwa hoja yake anamaanisha bora tungeendelea vile vile kabla ya Makinikia.
 
Porojo mnazo nyinyi 16% kira mgodi hapo hupati kitu kivipi?acheni kufanya watanzania wajinga kiasi hiki.
Hisa daraja la ngapi?
Unajua maana ya hilo daraja?
Magufuli ameaibika pakubwa.
 
kwa sasa Zitto kaa kimya maana JPM atosha, mtabaki kuunga unga maneno ya kukatisha tamaa lakini JPM yupo njia sahihi
 
Back
Top Bottom