Tanzania imepoteza $370M miaka ya Makanikia

Tanzania imepoteza $370M miaka ya Makanikia

Tatizo la nchi yetu hii ni siasa za blahblah si wapinzani si nani, tena kingine tuna tabia moja ambayo ni sumu sana tena sana.

Tuna desturi ya kurudishana nyuma sana ndiyo maana tunachelewa sana kuendelea, mfano tu anzisha mada hapa JF kwenye jukwaa la siasa na mada yenyewe iwe ya kupinga jambo fulani la maendeleo utaona utakavopata komenti nyingi, yote hiyo ni kwasababu ya kupenda blahblah sana, hii ni laana.

Nasema ni laana kwasababu hata ukiangalia kwa mtu mmojammoja unaweza ukawa na jamaa zako wakakushauri kua bwana hii biashara yako ili isonge unatakiwa ufanye hivi na hivi utapiga hatua na wewe ukifanya tathimini unaona ni kweli naweza kufanikiwa, fanya sasa!

Haohao jamaa zako waliokua wanakushauri wakishaona hatua unazopiga wanaanza kukutengenezea fitina na figisu nyingi.
Huyo msimuone hivo jambazi kweli anavuka boder anaenda kupora nchi za nje, wengine huyo kamgeuza mama yake mke wake yaani analala naye masharti ya mganga, ndiyo maana nchi za wenzetu wanatupiga bao kila siku.
 
Kama yameshuka inamaana hayajachimbwa na nikama hayajachimbwa bado yapo kwenye aridhi ya Tanzania na nikama bado yapo yatachimbwa badae na mapato yataongezeka kuliko mapato yawe juuu kwa kuwa na unequal exchange
Kwa mujibu wa mkataba tuonyeshe kanuni itakayotupa faida.
 
Nchi imepoteza mno kwenye sakata la Makanikia [ Fedha za kigeni $200M na TZS 430B Mapato ya Serikali]

  • mwaka 2016 Tanzania iliuza nje dhahabu iliyoingiza USD 1.8 bilioni
  • Mwaka wa Makanikia 2017 mauzo nje yalishuka mpaka USD 1.6 bilioni na;
  • Mwaka 2018, mwaka ambao athari ya Makanikia ilikuwa mwaka mzima mauzo nje yalikuwa USD 1.4 bilioni

Kati ya mwaka 2017-2018 Mauzo nje ya dhahabu yalishuka kwa jumla ya $200M saw na 11%.

Katika kipindi hicho uzalishaji wa dhahabu ulishuka kutoka tani 43 za dhahabu mwaka 2015 mpaka tani 39 mwaka 2018. Uzalishaji wa mwaka 2018 ulikuwa sawa na uzalishaji wa mwaka 2010.

Mapato ya Serikali kutoka sekta ya Madini yameshuka katika kipindi cha Makanikia. Kwa mujibu wa Kitabu cha Mapato ya Serikali kwa Wabunge ( Revenues Book Vol. 1 ).

  • mwaka 2016/17 makusanyo ya mirahaba yalikuwa TZS 341 bilioni
  • Mwaka 2017/18 makusanyo ya mirahaba yalikuwa TZS 230 bilioni
  • Mwaka 2018/19 makusanyo yalikuwa TZS 220 bilioni.
Serikali imekadiria kukusanya TZS 350 bilioni mwaka 2019/2020.

Kwa mujibu wa Dkt. Genuine Martin kwenye mada yake kwa Policy Forum Breakfast Debate Julai, 2019 Mapato yote ya sekta ya Madini yameshuka kwa 32% katika zama za Makanikia.

  • mwaka 2016 Mapato yalikuwa TZS 1.3 trilioni
  • Mwaka 2018 Mapato yalikuwa TZS 867 bilioni.
Katika Miaka 2 Mapato ya Serikali kutoka sekta ya Madini yameshuka kwa TZS 430 bilioni.

Tunapata nini kutoka Barrick Gold baada ya sakata la Makanikia?

Mapato ambayo Serikali ya Magufuli imepoteza kwenye sekta ya Madini kati ya mwaka 2017 - 2019 ni makubwa zaidi ya malipo* ambayo Serikali inasema tutalipwa na Barrick Gold Corporation ili kumaliza mgogoro baina ya Kampuni ya Acacia na Serikali.

Tumeona hapo juu kuwa tumepoteza Mapato ya Fedha za kigeni $200M na Mapato ya Serikali kushuka kwa TZS 430 bilioni. Kutoka Barrick tunatarajiwa kupata $300M ambazo chache kulinganisha na kiasi tulichopeteza.

* Malipo yenyewe hayo ya $300M kwanza yatalipwa kwa miaka 7, pili yana masharti ya wao kulipwa kwanza Fedha zao za VAT ( $240M ), na tatu watasamehewa Kodi ya Capital Gains Tax ya mauzo ya hisa za Acacia kwa Barrick Gold ($85.6M). Hatimaye Tanzania ndio itakuwa imeilipa Barrick $25M ( Net of payments and receipts to and from Barrick Gold ).

Kwa hiyo Tanzania imepoteza Mapato iliyokuwa yakusanywe kama mgogoro usingekuwepo [ $200M exports revenues and $170M tax revenues ] na imeishia kuilipa Barrick badala ya yenyewe kulipwa.

Tumepata hasara kubwa sana kutokana na maamuzi yetu wenyewe, maamuzi ambayo hayakuzingatia maslahi ya nchi yetu. Tunapaswa kuwawajibisha waliotupa hasara hiyo.


Sawa, lakini kushuka kwa uzallishaji hakumalizi madini...siku uzalishaji ukiongezeka mapato yataimarika
 
Tatizo la nchi yetu hii ni siasa za blahblah si wapinzani si nani, tena kingine tuna tabia moja ambayo ni sumu sana tena sana.

Tuna desturi ya kurudishana nyuma sana ndiyo maana tunachelewa sana kuendelea, mfano tu anzisha mada hapa JF kwenye jukwaa la siasa na mada yenyewe iwe ya kupinga jambo fulani la maendeleo utaona utakavopata komenti nyingi, yote hiyo ni kwasababu ya kupenda blahblah sana, hii ni laana.

Nasema ni laana kwasababu hata ukiangalia kwa mtu mmojammoja unaweza ukawa na jamaa zako wakakushauri kua bwana hii biashara yako ili isonge unatakiwa ufanye hivi na hivi utapiga hatua na wewe ukifanya tathimini unaona ni kweli naweza kufanikiwa, fanya sasa!

Haohao jamaa zako waliokua wanakushauri wakishaona hatua unazopiga wanaanza kukutengenezea fitina na figisu nyingi.
Huyo msimuone hivo jambazi kweli anavuka boder anaenda kupora nchi za nje, wengine huyo kamgeuza mama yake mke wake yaani analala naye masharti ya mganga, ndiyo maana nchi za wenzetu wanatupiga bao kila siku.
Aliyemuelewa huyu atufafanulie tafadhali
 
Inawezekana aliyoyaongea Musiba kuhusu haka kajamaa jana ni ya kweli.
Yaani miaka yote tangu 2008 wewe umekuwa mbele kupiga kelele juu ya wizi unaofanywa na Migodi ya Madini.

Leo ametokea mtu amejaribu kuweka mambo sawa unapiga kelele tena. Haijalishi Kama amefanikiwa au laa, lakini atleast amejaribu kupambana na kile ambacho Watanzania wengi wamekuwa wakikipigia kelele ukiwemo wewe.
Kiufupi wewe ni tapeli wa kisiasa you do things just for political stunts. Hufanyi kwa maslahi ya Taifa bali kujipatia umaarufu binafsi. The good thing JPM ameweka a benchmark ya aina ya watu wanaopaswa kuwa Marais wa Nchi hii, hadhi ya Urais ameiweka kwenye standard ya juu sana na kutufumbua macho juu ya watu wa aina yako ambao kimsingi hamna chochote ila siasa za ulaghai ziliwafanya mfike hapo mlipo.
Mnapambana kuona JPM aonekane ameshindwa ili muendelee kuonekana nanyi mnasifa za kuwa Marais, kwani akifanikiwa of which is about to hadhi ya Urais itapanda sana na you will automatically be disqualified kwani Watanzania wataanza kufikiria aina ya watu wenye vinasaba kama vyake of which nyie Pro-JK mnavikosa.

Hii umefanyainaitwa waffling. Hujajibu hata hoja moja katika alizotoa bali ume shambulia binafsi. Kinachoongelewa hapa ni kukosekana kwa maarifa yakupigana hii vita na au kufanya mambo gizani na bado kwa uficho. Inaleta mashaka kuamini maprofesa wetu ni wajinga kiasi anachosema Lissu.
 
Jipya kwa zitto hakipo tofauti na porojo na ndiyo maana watu hawastuki wanamjua vema ,hata kwenye hoja ya buzwagi aliitosa chadema nao wakamtosa siyo wa kumuamini hata kidogo.
Kwani Msiba ni msemaji wa Nssf? Jibu hoja ya Zitto acha kuwawaya
 
Sawa, lakini kushuka kwa uzallishaji hakumalizi madini...siku uzalishaji ukiongezeka mapato yataimarika
Eleza jinsi mkataba utakavyotunufaisha kinyume na ilivyokuwa kwenye mkataba wa awali.
 
Nisome vizuri Bingwa, nimesema kabisa alichokifanya JPM kwenye Mining Industry kifanikiwe au kisifanikiwe kwangu siyo issue. Ukweli ni kwamba Watanzania akiwemo Zitto tunakubaliana sekita ya Madini ina mambo ya ovyo, so mtu anayejaribu kuleta changes nitamuunga mkono bila kujali ni Nani, kama tulivyomuunga mkono Zitto wakati huo akitoa povu kuhusu Madini kabla hajawa corrupted. It is better to die trying kuliko kukaa tu wakati unaona huridhishwi na mambo yalivyo.

Mkuu ukisema afanikiwe asifanikiwe utakua umekosea kwan angefanya utafiti tu bila kuathiri mengine na kugundua upotevu na si kuna kipengele cha mahakama ukisoma vizur kwa zitto utagundua tunaenda kulipa tena gharama zaidi bi bora tungefunga kabs mgodi kuliko kubeba gharama zaidi
 
Jipya kwa zitto hakipo tofauti na porojo na ndiyo maana watu hawastuki wanamjua vema ,hata kwenye hoja ya buzwagi aliitosa chadema nao wakamtosa siyo wa kumuamini hata kidogo.
Tueleze faida tutakayoipata kwa mkataba huu! Acha porojo
 
Hii umefanyainaitwa waffling. Hujajibu hata hoja moja katika alizotoa bali ume shambulia binafsi. Kinachoongelewa hapa ni kukosekana kwa maarifa yakupigana hii vita na au kufanya mambo gizani na bado kwa uficho. Inaleta mashaka kuamini maprofesa wetu ni wajinga kiasi anachosema Lissu.
Kama ni hivo ulichofanya wewe kinatofauti gani na hicho unachoclaim nimefanya Mimi. Unajua nini kimeongelewa huko?, unajua nini kitakuwa matokeo ya mazungumzo?Kama hujui unawezaje kutoa hitimisho. Hapa busara ni kusubiri mvutano uishe ndio tujue kipi ni kipi. Lakini nimeweka wazi afanikiwe asifanikiwe, lakini Kama kiogozi amejaribu kufanya kitu ambacho wengi akiwemo Zuberi tulikuwa tunatamanj kifanyike.
 
Zitto anatakiwa atueleze kwa kubalance. Hizi data zake zimekaa kisiasa mno. Zinalenga kueneza siasa kuliko uhalisia.
Nyie mliokatabiana, mlijadili na kamati yenu ya siri mkaafikiana nao mabeberu! Tuambieni tofauti ya mkataba huu na wa awali kama ukiondoa tarehe na wajumbe wa kamati.
 
Mkuu ukisema afanikiwe asifanikiwe utakua umekosea kwan angefanya utafiti tu bila kuathiri mengine na kugundua upotevu na si kuna kipengele cha mahakama ukisoma vizur kwa zitto utagundua tunaenda kulipa tena gharama zaidi bi bora tungefunga kabs mgodi kuliko kubeba gharama zaidi
Hayo ni maomi yako wewe. Yeye Kama kiongozi aliyekabidhiwa dhamana amejaribu kufanya kile alichoona ni sawa. Halafu unatoaje hitimisho kuwa Kuna hasara wakati hata majadiliani bado hayajamalizika. Subrini mazunguzo yaishe yawekwe into effects halafu njooni mtoe Conclussion Kama Kuna faida au hasara. Acheni Ushehe Yahya.
 
Kwa hiyo zile noa zetu kwa kila mtanzania zimetaifishwa
Labda zitaingia mwakani, na hivyo hiyo hasara kugeuka kuwa si hasara tena. Labda Zitto angesubiri mapaka sakata la makinikia liishe ndipo tuchunguza kama kuna hasara au faida.
 
Mkuu ukisema afanikiwe asifanikiwe utakua umekosea kwan angefanya utafiti tu bila kuathiri mengine na kugundua upotevu na si kuna kipengele cha mahakama ukisoma vizur kwa zitto utagundua tunaenda kulipa tena gharama zaidi bi bora tungefunga kabs mgodi kuliko kubeba gharama zaidi

Amesha chagua kukaa upande flan ,so anaamua tu kujibu kama anavyo jisikia.Sasa Mtu anasema tufanikiwe au tusifanikiwe kwake yeye sio Hoja ila pongezi ni kuwa Mh Rais amejaribu walau..Utamuelewaje Mtu mwenye fikra hizo Mkuu ?
 
Kwahiyo mapato yameshuka ilihali madini yetu yanaendelea kusombwa?
Acha porojo eleza kanuni ya kimkataba inayotupa ahueni tofauti na mkataba wa awali.
Ndicho tunataka kusikia.

Usisahau kutupa taarifa za ile invoice ya TRA. Mabeberu wamekubali watalipa lini?
 
Kama ni hivo ulichofanya wewe kinatofauti gani na hicho unachoclaim nimefanya Mimi. Unajua nini kimeongelewa huko?, unajua nini kitakuwa matokeo ya mazungumzo?Kama hujui unawezaje kutoa hitimisho. Hapa busara ni kusubiri mvutano uishe ndio tujue kipi ni kipi. Lakini nimeweka wazi afanikiwe asifanikiwe, lakini Kama kiogozi amejaribu kufanya kitu ambacho wengi akiwemo Zuberi tulikuwa tunatamanj kifanyike.

Barrick ni listed company. Anachoongea Zitto ndio matokeo na public information japo huku kwetu hazija wekwa wazi. Haiwezekani kwa public listed company kuficha hiyo information. Kwa ujasili aliuonyesha hakupaswa kushindwa na tusingepata hasara tuliyopata. Zilishauriwa njia nyingi za kufanya lakini tuliamua kutosikiliza.
 
Back
Top Bottom