Tanzania imelipa kampuni za China wastani wa $1B kwa mwaka kwa ujenzi pekee

Kamundu

Platinum Member
Nov 22, 2006
6,606
8,744
Kwa maelezo ya Raisi Magufuli mwenyewe Tanzania imelipa kampuzi za China $10B kwa miaka 10 iliyopita! hii ni wastani wa $1B kwa mwaka.

Hii inashutusha kwa jinsi tunavyotoa wahandisi kwenye vyuo mpaka sasa bado kazi nyingi zinafanywa na makampuni ya China.

Kazi nyingi kama za majengo, visima na barabara zingeweza kufanywa na kampuni zetu lakini hakuna utaratibu mzuri wa kuanzisha kampuni kubwa zenye uwezo mfano hizi kampuni ndogo ndogo zingeweza kuungana na kuuza hisa kwa watu na sisi tungeweza kununua hisa ili kuwapa kampuni mtaji wa kutosha na kuwa na kampuni yenye uwezo.

Sasa tuna kampuni zaidi ya 8,000 lakini nyingi zimekuwa kama za kubabaisha na haziwezi hata kupewa kazi.

Na hata kampuni za serikali za ujenzi wamekuwa vinara wa kuongeza gharama sana mfano lab ya Wizara ya kilimo badala ya kuweka Tsh milioni 500 wakaweka bilioni 1.4 kwa jengo la chini na hii ni kampuni ya serikali!

Hatuwezi kukua kwa namna hii ya ujanja ujanja wakati kampuni za nje zinapiga contract za maana!
 
Mkuu rekebisha kwanza huu uandishi wako.

Kwa kifupi 'serekale' yetu ya kishindo tumewaamini sana rafiki zetu wachina kiasi kwamba hadi matundu ya choo na daraja la mita 100 tumewapa 'shavu' lhawa akina Wang Yi
 
Wewe labda huna akili,kwa taarifa yako makampuni yote ya ujenzi ya kigeni yanatumia wataalamu na wahandisi wa Tanzania.
Wageni wanakuwa kwenye managerial level tuu kwa kuwa kampuni ni zao
Sasa Kama ni wasomi kwanini watumiwe tu
 
Hapo ndio utaelewa maana ya kuwa na viongozi wasio na akili
Mfano mdogo ni mradi wa TSCP au Tanzania strategic cities pale mbeya barabara za km 10 wakampa Mchina hivi tunavyoongea barabara zinamashimo Kila siku kurepair na Zina chini ya miaka 5 wakati kwa Mji wa Sumbawanga kwa mfano barabara za hivyo zimejengwa na mkandarasi mzalendo tena wa huku huku lakini ziko powa na maisha yanaenda
Unajiuliza hiyo michina mnaipendea nini?

Kama ni vifaa na mitaji serikali ingeweza wawezesha wazawa na pesa ingezunhuka ndani ya nchi na kuleta tija
 
Wewe labda huna akili,kwa taarifa yako makampuni yote ya ujenzi ya kigeni yanatumia wataalamu na wahandisi wa Tanzania.
Wageni wanakuwa kwenye managerial level tuu kwa kuwa kampuni ni zao
Kwa nini usiende mbali kidogo ufanye critical thinking mleta mada hii kaongekea Kwa upana kabisa pamoja sustainability ya hao wanaoajiriwa wangekuwa chini ya kampuni za Tanzania, faida, technology endelevu etc etc

anyway CCM ndiyo mlivyo, IQ ya kuku
 
Tumewapa mapesa yote hayo ila Rais kawaomba watisamehe vijisenti wanajiumauma.

Hawa wachina wafikirie mara mbili uhusiano wetu.
 
Hapo ulipo una hisa kwenye makampuni mangapi hapa Tanzania, zilizokuwa listed...
 
Wewe labda huna akili,kwa taarifa yako makampuni yote ya ujenzi ya kigeni yanatumia wataalamu na wahandisi wa Tanzania.
Wageni wanakuwa kwenye managerial level tuu kwa kuwa kampuni ni zao
Asilimia 80 unakuta ni watanzania, ila karibu 60% ya fedha zinazolipwa zinarudi huko huko asia, ulaya ambapo makampuni haya yanatoka, mfano mchina katoa mkopo wa SGR, kampuni zake zimeshinda, watafanya kazi watanzania hela zinatoka China, kisha zinakuwa transferred back to china baada ya hapo zinaletwa tena bongo kulipa level wafanyakazi sasa
 
Pamoja na kutokuwa na kampuni kubwa zenye mitaji na uwezo wa kuchukua tenda za miradi mikubwa, wabongo bado pia tuna tatizo kubwa la ubabaishaji.

Utamaduni wa ubabaishaji umetukaa sana kiasi kwamba hatuwezi kufanya kazi za maana kwa ufanisi. Utamaduni wa kufanya kazi kwa madili bila ufanisi ulijengeka ndo maana miradi mingi ktk awamu zilizopita ilikuwa ya kibabaishaji tu.

Inabidi tuondokane na na utamaduni huo kwanza ndo tunaweza kufanya mabadiliko ya maana.
 
Kuna kitu nimejifunza baada ya kufungua kampuni na kuanza kufuatilia kazi/zabuni kwa miaka miwili sasa, tofauti ya makampuni ya ndani na nje ni mtaji, unakuta project ya 10M USD kujenga barabara, kampuni za ndani na nje zote zimeomba kazi, lakini cash flow ya kampuni ya kizawa ni Mil500 hadi bil 2 za Kitanzania, wakati cash flow ya makampuni ya nje ni kuanzie bil 20 usd kuendelea, pia ukija swala la malipo, kampuni za nje zinaweza fanya kazi yote na kumaliza baadae serikali ndo ikalipa yote au ikalipa polepole, Kwahiyo serikali inaamua kuchagua kampuni za nje sio tu wanawatalaam ila mtaji.

Mfano kampuni za china, zinapokea mikopo kutoka katika mabank yao pesa nyingi na wanalipa kwa muda mrefu hata zaidi ya miaka 70 iyajo, kwa nini wasiweze kufanya kazi hizo? kama wafanyakazi wa kawaida wachina kwenye makampuni ya china wanapewa mikopo ya nyumba na walipa kwa kipindi cha miaka zaidi ya 50, je Tanzania mnaweza? kwa hiyo financial institutions za Tanzania ndio wachawi wa kwanini kampuni nyingi za wazawa hazifanya vizuri, wao wanfikiri kila mtanzania ni Backharesa.

Sasa kichekesho cha serikali zote zilizopita ni hiki hapa;
1. Wanahamasisha kampuni za ndani ziombe zabuni kweli ni wazo zuri, sasa mzabuni huyu wa kitanzania akipewa kazi huenda Bank, walau apate msaada, bank ukifika wanakuambia weka contract mezani, unawapatia, unawaambia project hii ni ya bil20, ila mimi ninakianzio cha bil 1, nataka mkopo wa bil19, nikilipwa na kwa bahati nzuri malipo yatafanyika katika Bank yenu mtachukua chenu, Bank za Tanzania wanakuambia leta dhamana isiyo hamishika unapeleka nyumba ya mil 200 ndio uliyonayo, wanadai pamoja na mkataba watatoa mkopo kulingana na dhamana uliyonayo at the end mtu huyu anapata mkopo mil100 au mil150 za Kitanzania, je hiyo kazi utaifanya vipi? kwa hiyo wanasiasa wetu Tanzania wanatakiwa wakae na mabenki waongee nao jinsi ya kuweza kuwasaidia makampuni ya kitanzania pindi wakiwa na mikataba, sio kuanza kuuliza some funny issue eti leta nyumba kama dhamana kwa kazi ya mabilions ya pesa.
2. Bank nyingi za Tanzania bado wanaoziendesha uelewa wao ni mdogo, yaani wameridhika sana kufanya biashara na kupata interests nyingi kwa wafanya kazi walio ajiliwa, yaani akili ya kusema lets look out of box na kuwasaidia wafanya biashara hilo haliko akilini mwao na hawajui, wanajiita wamesoma finance, kwa kuna shida kubwa sana Tanzania kwa hili. Nimeona mwenyewe mfanya biashara mmoja Bank ya Azania kapata zabuni ya mil 500, lakini cash flow yake ni mil 70, kasign cotract kaenda bank , bank ikaridhia kumpa mkopo wa mil 120 tu baada ya kufanya evaluation ya mali ambazo anamiliki, hatimae ikabidi auze zabuni hiyo kwa watu wengine, alikuwa anatukana sana tulipokuwa kwenye vikao vya wafanyabiashara, poor Tanzanians ,we are not lucky.
3. Tusipobadili sera na mfumo wa Kibank ni ngumu kwa makampuni ya Tanzania kusimama, mfano, makampuni mengi ya Kichina wakati yanaanza yalikuwa na technology ya kwaida, hivyo walikuwa wana hire experts kutoka nje, baadae vijana wao wanajifunza kutoka kwa watalaam hao baada ya muda wanaweza kufanya hivyo, lakini kilichowabeba na kinachowabeba wachina ni support kubwa kutoka katika mabank yao.
 
Hapo ndio utaelewa maana ya kuwa na viongozi wasio na akili
Mfano mdogo ni mradi wa TSCP au Tanzania strategic cities pale mbeya barabara za km 10 wakampa Mchina hivi tunavyoongea barabara zinamashimo Kila siku kurepair na Zina chini ya miaka 5 wakati kwa Mji wa Sumbawanga kwa mfano barabara za hivyo zimejengwa na mkandarasi mzalendo tena wa huku huku lakini ziko powa na maisha yanaenda
Unajiuliza hiyo michina mnaipendea nini? Kama ni vifaa na mitaji serikali ingeweza wawezesha wazawa na pesa ingezunhuka ndani ya nchi na kuleta tija
Shida sio Mkandarasi bali ni msimamizi na viwango vilivyokuwemo kwenye mkataba.

Amandla....
 
Pamoja na kutokuwa na kampuni kubwa zenye mitaji na uwezo wa kuchukua tenda za miradi mikubwa, wabongo bado pia tuna tatizo kubwa la ubabaishaji. Utamaduni wa ubabaishaji umetukaa sana kiasi kwamba hatuwezi kufanya kazi za maana kwa ufanisi. Utamaduni wa kufanya kazi kwa madili bila ufanisi ulijengeka ndo maana miradi mingi ktk awamu zilizopita ilikuwa ya kibabaishaji tu. Inabidi tuondokane na na utamaduni huo kwanza ndo tunaweza kufanya mabadiliko ya maana.

Mimi naona hii inatokan na kampuni kuwa ndogo za kifamilia zaidi badala ya kampuni kuendehswa kibiashara kampuni 8000 bado kazi nyingi zinaenda nje
 
Back
Top Bottom