Wadiz

JF-Expert Member
Nov 10, 2022
5,432
11,101
Uongozi ni dini na dini ni ibada na dini ni kuungama, kutubu, kuwa msafi, kukataa uwongo na unafiki.

Kwa awamu zote za utawala toka uhuru nchi hii haijapata kiongozi , ni ukweli usiopingika haijatokea.

Hoja yangu, hawa viongozi wamekuwa na watu wao wanaowaamini, they have had people whom they trust in their inner circle, but they have given no freedom to their inner circle whom they trust to openly and sincerely criticize them when the go wrong.

Kiongozi asiewapa uhuru toshelevu watu wake anao waamini kumkosoa kwa dhati sio kiongozi bali ni nyapara fulani lenye hulka ya ufalme.

Kama unabisha kiongozi gani wa Tanzania alieacha legacy ya kuwapa watu wake wa karibu, marafiki anao waamini wamkosoe kwa uwazi kwa jambo lolote, pasipo yeye kujisikia vibaya?

Anaebisha karibuni.
 
Kwa awamu zote za utawala toka uhuru nchi hii haijapata kiongozi , ni ukweli usiopingika haijatokea...
Tanzania ilikuwa na viongozi Makini tangu Uhuru hadi 2015.
 
Kama unabisha kiongozi gani wa Tanzania alieacha legacy ya kuwapa watu wake wa karibu, marafiki anao waamini wamkosoe kwa uwazi kwa jambo lolote, pasipo yeye kujisikia vibaya?
waliomkosoa mwalimu miaka hiyo walikipata cha mtema kuni, wengine walikimbia nchi.

ni katabia ketu tumejiwekea kwamba Rais wa nchi mi mtukufu hata kama suti imechanika ukimsema tu unaloo...
 
Huo upuuzi uliowekwa kwenye katiba kuwa rais hashitikiwi akiwa madarakani au ametoka, ndio kiini cha udhaifu wa viongozi wetu wote.
 
Mkubwa hakosei na akikosea umkosoe kwa adabu na kwa namna ya ushauri na unyenyekevu! Na ukimpa options.
 
Uongozi ni dini na dini ni ibada na dini ni kuungama, kutubu, kuwa msafi, kukataa uwongo na unafiki.

Kwa awamu zote za utawala toka uhuru nchi hii haijapata kiongozi , ni ukweli usiopingika haijatokea...

Kwa hiyo ili uwe kiongozi mzuri kwa mtazamo wako ni kuwa atoe uhuru usio na kifani wa wakosoaji wake. Swali la:
1. Unajuaje kama hawakuwa wakikosolewa na hiyo "inner circle".

2. Kwa tafsiri yako ya ukosoaji, vipi ikiwa uwezo wa wakososaji ni mdogo, kiongozi akikubali ukosoaji huo, ambao kimsingi mimi napenda kuuita ushauri, huoni ya kuwa kiongozi atapotea?

3. Je ubora wa kiongozi hupimwa na utayari au kuafiki wa kukosolewa?
 
Nchi imekosa KATIBA inayoendana na wakati wa sasa kisha ikapata dira ya Taifa kuanzia hapo utaona kiongozi yoyote atakaye puuzia hitajio la nchi.

Kuhusu kuwa na watu wa ndani Hilo Jambo halitoisha kamwe na siyo Tz pekee bali dunia nzima HAIWEZI TOKEA UKAMUAMINI MTU USIYE NA TAARIFA ZAKE KAMILI WALAU HATA KWA KUPITIA KWA WATU AU MTU hapo ndipo kujuana kunaingia ( Unamfahamu, umefahamishwa , Umeshikwa mkono , Matukio yamekufanya amekujua, bahati ya mtende n.k ).

Cha zaidi hao watu wa ndani wakiwa na muongozo thabiti utosikia upuuzi wowote Mambo yatasonga vyema. Watu wamepambana nyuma ya pazia kuhakikisha mtu anakaa juu (RAISI) unategemea asilipe fadhila ya utu wao( iwe kwa mabavu, udanganyifu , Fitina, uadui n.k) , Muda ni mwalimu mzuri.
 
Uongozi ni dini na dini ni ibada na dini ni kuungama, kutubu, kuwa msafi, kukataa uwongo na unafiki.

Kwa awamu zote za utawala toka uhuru nchi hii haijapata kiongozi , ni ukweli usiopingika haijatokea...
Unajiandikia tu kama unaota ukiwa usingizini.

Hii nayo ni mada unayotaka watu wapoteze muda kujadili ujinga?
 
Uongozi ni dini na dini ni ibada na dini ni kuungama, kutubu, kuwa msafi, kukataa uwongo na unafiki.

Kwa awamu zote za utawala toka uhuru nchi hii haijapata kiongozi , ni ukweli usiopingika haijatokea.

Hoja yangu, hawa viongozi wamekuwa na watu wao wanaowaamini, they have had people whom they trust in their inner circle, but they have given no freedom to their inner circle whom they trust to openly and sincerely criticize them when the go wrong.

Kiongozi asiewapa uhuru toshelevu watu wake anao waamini kumkosoa kwa dhati sio kiongozi bali ni nyapara fulani lenye hulka ya ufalme.

Kama unabisha kiongozi gani wa Tanzania alieacha legacy ya kuwapa watu wake wa karibu, marafiki anao waamini wamkosoe kwa uwazi kwa jambo lolote, pasipo yeye kujisikia vibaya?

Anaebisha karibuni.
Kwanini babakoau mamako asigombee? au na wao huwaamini. Kagombea wewe. Kapuku kweli wewe.
 
Kwa hiyo ili uwe kiongozi mzuri kwa mtazamo wako ni kuwa atoe uhuru usio na kifani wa wakosoaji wake. Swali la:
1. Unajuaje kama hawakuwa wakikosolewa na hiyo "inner circle".
2. Kwa tafsiri yako ya ukosoaji, vipi ikiwa uwezo wa wakososaji ni mdogo, kiongozi akikubali ukosoaji huo, ambao kimsingi mimi napenda kuuita ushauri, huoni ya kuwa kiongozi atapotea??
3. Je ubora wa kiongozi hupimwa na utayari au kuafiki wa kukosolewa?
Hicho nikipengele kimoja tu sijahitimisha, in fact hio ni provocative skewness kwenye fikra, kufahamu kuwa kuna other parameters za kiongozi na kuainisha mapungufu kwenye wazo langu ndio tija yenyewe ya lishe ya mawazo mtambuka , very good observations. 🙏🙏🙏
 
Uongozi ni dini na dini ni ibada na dini ni kuungama, kutubu, kuwa msafi, kukataa uwongo na unafiki.

Kwa awamu zote za utawala toka uhuru nchi hii haijapata kiongozi , ni ukweli usiopingika haijatokea.

Hoja yangu, hawa viongozi wamekuwa na watu wao wanaowaamini, they have had people whom they trust in their inner circle, but they have given no freedom to their inner circle whom they trust to openly and sincerely criticize them when the go wrong.

Kiongozi asiewapa uhuru toshelevu watu wake anao waamini kumkosoa kwa dhati sio kiongozi bali ni nyapara fulani lenye hulka ya ufalme.

Kama unabisha kiongozi gani wa Tanzania alieacha legacy ya kuwapa watu wake wa karibu, marafiki anao waamini wamkosoe kwa uwazi kwa jambo lolote, pasipo yeye kujisikia vibaya?

Anaebisha karibuni.
Mjumbe hauwawi!
 
Ulishawahi kuona mbwa waliofungiwa bandani miaka yote ya maisha Yao wanazaa kuku?, Lazima wazae mbwa wenzao kinachobadilika ni baadhi ya vinasaba vya urithi kutoka Kwa mzazi huyu au Babu huyu na bibi huyu...Maybe mbeleni kutakuwa na mbwa atakeyezaa na tai .
 
Back
Top Bottom