Na Muhingo Rweyemamu (Rai)
Yapo mambo mambo matatu yaliyonisukuma kuandika uchambuzi huu. Kwanza ni kitendo cha uongozi wan chi ya Rwanda kukataa mechi ya soka katil ya Taifa Stars na Amavubi kuchezwa Jumamosi na badala yake kupangwa kuchezwa Jumapili.
Rwanda, walikuwa na taarifa kwamba Jumatatu, timu yetu ina ugeni kutoka Brazil. Na mchezo huu ni muhimu kwa nchi za Afrika Mashariki na unaweza kuitwa once in a life time.
Jambo la pili ni kauli aliyoitoa Waziri Mkuu mjii Arusha akiuliza ni nani aliyewaroga Watanzania kiasi kwamba hawawezi kujiamini ingawa wamejaliwa raslimali kubwa katika nchi nzuri.
Waziri Mkuu alikuwa akizungumza katika mkutano wa wadau wa kilimo cha mazao ya bustani na akasema anashangazwa kwamba wenzetu kwa Kenya pamoja na kuwa na ka nchi kadogo kenye raslimali kidogo, wamejaliwa sana katika suala la kilimo cha mauzo ya bustani yaliwamo maua.
Katika mkutano huo,Katibu Mkuu huyo (Wizara ya Habari), Sethi Kamhanda, aliitaka sekta ya habari nchini kujiandaa na ushindani utokanao na kufunga milango ya Jumuia ya Afrika Mashariki. Katika maelezo yake, Kamhanda alisema kila kitu kimeshakubaliwa na viongozi wa nchi hizi tatu na kwamba lililobaki ni jukumu la Watanzania kujiandaa namna ya kuingia katika sekta hii.
Alishauri kwamba Waandishi wa habari wa Tanzania, tujiandae kwenda kufanya kazi katika nchi nyingine za Afrika Mashariki na Kati kwa sababu hata waandishi wa habari wanchi hizo, wanajiandaa kuja kufanya kazi hapa nchini mwetu. Nchi hizo ni pamoja na Kenya, Uganda, Rwanda, Burundi na Tanzania yenyewe.
Wahariri wengi waliokuwapo, walipinga jambo hilo, lakini wakati wa hitimisho lake, aliyasema maneno yanayofanana na maneno aliyoyasema Waziri Mkuu Mizengo Pinda kule Arusha.
Kama alivyosema Pinda, Kamhanda naye aliwataka waandishi wa habari kuacha woga akisema kwamba siyo kweli kwamba watu wa Kenya wano uwezo kuliko Watanzania.
Naomba Watanzania kuwashangaa wote wawili. Kwa nini?
Mwaka 1989, wakimbizi wa Burundi waliokuwa katika mpaka wa Tanzani, ikiwa ni pamoja na viongozi wao ambao sasa ndiyo walioko madarakani nchini humo, waliamua kufanya jambo moja kwa ajili ya manufaa ya nchi yao.
Waliamua kuwachukua vijana wa Kirundi waliokuwa makambini na kuwatafutia vyuo vikuu hapa nchini. Chuo Kikuu kilichaguliwa,kilikuwa Chuo cha Tumaini Iringa. Vijana wengi waliokwenda kusoma Iringa, walichagua kozi tatu lakini wengi walikimbia kozi mbili. Kozi ya kwanza ilikuwa ni ya uandishai wa habari. Na ya pili ilikuwa ya uchumi. Wachache walikwenda kozi ya sheria.
Moja ya mambo ya msingi waliyoamua kujifunza, ilikuwa ni lugha ya Kiingereza na Kiswahili. Baada ya miaka mitatu ya mafunzo yao chuoni hapo, vijana hao walikuwa wameiva katika Kiswahili na Kiingereza. Walipokuwa wakitoka nyumbani kwao, walikuwa ni wataalam wa lugha za Kifaransa na Kirundi. Kwa hiyo wanarudi nyumbani wakiwa na hazina ya lugha nne. Kiingereza, Kiswahili, Kifaransa na Kirundi.
Wengi wa vijana hawa, kwa sasa wanafanya kazi Ofisi ya Rais. Lakini cha msingi zaidi, vyombo vyote vya habari muhimu nchini Burundi vimeshikwa na kuongozwa na vijana hawa waliofundishwa katika vyuo vyetu hapa nchini. Wana hazina ya lugha nne na mbili kati ya hizo wamejifunzia nchini mwetu.
Sasa tunafungua milango ya Watanzania ambao, Warundi, Waganda, Wanyarwanda na Wakenya kwenda kutafuta kazi tofauti ikiwamo ya uandishi wa habari katika mojawapo ya nchi hizo au katika nchi zote hizo.
Watanzania tuna silaha ya lugha moja tunayoijua kwa ufasaha. Kiswahili. Warundi wana silaha ya lugha nne wanazozijua kwa ufasaha. Sisi tumefungua milango ya kwenda kufanya kazi Burundi. Kirundi na Kifaransa, ndiyo lugha zinazotumika nchini Burundi. Na sisi tunaojua Kiswahili tunajidanganya kwamba tumefunguliwa milango kwenda kufanya kazi nchini Burundi.
Tunataka kufanya kazi nchini mwao, wakati hatuwezi kuzungumza nao hata sentensi moja. Pinda nikikushangaa wewe, na wewe utaendelea kunishangaa?
Viongozi wetu sawa, walikaa kwenye mikutano wakakubaliana kabisa kufungua milango ili sisi tutoke twende kufanya kazi katika nchi nyingine waje kufanya kwetu?
Nauliza mara mbili, ni mhariri yupi wa Tanzania anayeweza kwenda kufanya kazi ya uhariri katika gazeti la Nation la Kenya? Na ukweli siyo kwamba Watanzania hawajui Kiingereza, hapana je, hapo Kenya yapo mazingira ya kumruhusu Mtanzania kuhariri gazeti lao?
Kwetu sawa? Hatuna shida wanaweza kuja kuhariri, hata habari za kiulinzi,wanaweza kuja kuhariri.
Ninayo kumbukumbu nzuri ya mwaka 2005 wakati Wakenya waliokuja katika mojawapo ya magazeti ya Tanzania.Wakenya hao hawakuleta teknolojia tu, bali walikuja pia na jina la mtu wanayemtaka awe rais wa Tanzania.
Wengine tulipinga na tukafukuzwa kai. Hawa ndiyo tunataka twende kwao tuhariri habari za kisiasa za kwao na tunajidanganya kwamba wataturuhusu?
PInda unalalamika pale arusha . Hebu fikiria kama waziri mkuu mwenzio wa Kenya, Raila Odinga anaweza kuwaita raia wa nchi yake akaanza kuwalalamikia? Hawezi!
Na kwanini hawawezi kuwalalammikia ni kwa sababu tayari mfumo wa maisha wanchi hiyo umewapa nyenzo wananchi wake za kujiwezesha.
Shahada zote nchini Kenya zimeongezwa somo la entrepreneurship. Kwa hiyo wanafunzi wa Kenya hawahangaishi na vyeti vizuri tu, hawahangaishwi na alama nzuri za matokeo za mitihani ya mwisho. Kwahiyo hawezi kuhangaishwa na wizi wa vyeti au udanganyifu wa mitihani.
Wanawaza watapa wapi kipande cha ardhi ilia weze kutengeneza andiko lake la mradi.
Nani mwanafunzi wa mwaka wa mwisho wa shahada ya kwanza yeyote katika chuo chetu hapa nchini anayeweza kutengeneza andiko la mradi lenye uwezekano wa kukopesheka? na hata akiwa nalo,ni benki gani Tanzania yenye ujasiri na uthubutu wa kuwakopesha watu?
Kampuni ya Nation ya Kenya imewekeza katika tasnia ya habari nchini mwetu. Taja kampuni yoyote ya kitanzania ya habari ambayo inawza kwenda kuwekeza nchini Kenya!
Kenya Commercial Bank imefungua tawi lake hapa nchini na baada ya kugundua neno Kenya lina sumbua katika jina lake,imeamua benki hiyo iitwe KCB. Hilo ndilo jina lake la sasa. Hata account ya EAC ni Kenya Commercial Bank.
Nitajie Benki yoyote ya Tanzania inayoweza kwenda nchini Kenya ikafungua Benki nchini Kenya ikafungua benki nchini humo!taja tu!kwanza hata duka mjini Nairobi likiaminika linamilikiwa na Mtanzania hakuna atakayenunua kako eti unafungua milango ili tutoke? Tuseme tu wazi kwamba umefungua milango ili waje . tunafungua milango ili wapate mashamba .
Tunafungua milango ili wawe na uraia wa nchi mbili kwa kificho, wanao ujasiri wa kufanya wa kufanya hivyo sisi hatuna, hatukulelewa hivyo. Kama tunataka tuanze kulea taifa kujielekeza hivyo.
Wakati Fulani ilipotangazwa kwamba nchi za Uganda na Tanzania zinapewa grace period ya miaka mitano kuuza bidhaa zao bila kutozwa ushuru na kwamba Kenya itatozwa ushuru, mmoja wa viongozi mashuhuri nchini Kenya alipinga waziwazi. Ingawa wakenya wengi pamoja na serikali yao walipinga kwa siri. Charles Njonjo akasema ni kiongozi gani mpumbavu atakwenda kuwambia wakenya kwamba wacheleweshe maendeleo ya kwamba wacheleweshe maendeleo yao kwa sababu ya Watanzania na Waganda. Alikua sahihi!kenya haina kiongozi wa aina hiyo. Hawezi kudhubutu mtu yeyote kuwambia hivyo wakenya, watampiga mawe!
Nimezungumzia suala la michezo wa soka. Wakati Tanzania alipopata ugeni wa Ivory coast, kwa kujipendekeza kwenu tukaichagua Rwanda nayo tukaipatia mechi.
Lakini Rwanda sasa iliposikia Tanzania itacheza na Brazili wanataka tuikose mechi hiyo. Wanataka Taifa Stars icheze mechi jumapili wakitaka wacheze kesho yake na Brazil. Kwanza si kitendo sahihi kiafya kuwa chezesha wachezaji mechi mbili za kiushindani chini ya saa 48. Lakini Wanyaranda ndivyo wanavyotaka.
Hawa ndiyo waliokuwa wanagombana mwaka 1992, Tanzania ilikuwa makao yao makuu ya usuhulishi, kila wakipigana nyumbani wanakimbilia kwetu.
Arusha na Dar es Salaam ilikua kama kwao. Mwaka 1994. Ikafika ukomo wa unyama wao. Wakauana. Tanzania ikaamua kubeba mizigo yao. Walio salia baada ya kusambaratishana wakaletwa kwetu.
Wakiwa hapa,wakaendeleza tabia mbaya za kwao wakaua wanyama wote kwenye misitu ya hifadhi wakaimaliza.wakageuka kuiba chakula cha wenyeji, kwao hawali ugali, UNHCR inawapa ugali.Wakaamua kuivamia migomba ya wakazi na Ngara (kwa kina Kanyabwoya) wakafyeka migomba yao na kuchukua ndizi zao.Tena wakati mwengine mwenye shamba akija juu,wanamuua.
Hawakuishia hapo, wengine wao wakaamua kuwa majambazi.wakazi wa wilaya ya Karagwe wanajua.Mtu anaweza kuingiliwa nyumbani mwake akamiminiwa risasi na wakamuibia shati au suruali. Namkumbuka mzee mmoja maarufu Simony Gabagambi ambae aliuwawa sebuleni kwake kwa kumimminiwa risasi, na kisha kuibiwa television, basi.
Hawa ndio tunawafungulia milango kwa unyenyekevu eti na sisi tukawekeze kwao. Tunaenda kuwezesha nini? Viongozi mnatuzuia kuwa wanyonge wakati hamjatupa silaha za ujasiri? Naanza kukubaliana na mwimbaji Ailen sanga, aliyeimba wimbo wake : "pangisheni hata mabafu."