Tanzania haijawa tayari kujiunga EAC

BAK

JF-Expert Member
Joined
Feb 11, 2007
Messages
98,064
Points
2,000

BAK

JF-Expert Member
Joined Feb 11, 2007
98,064 2,000
Watanzania wakataa shirikisho Afrika Mashariki
*Asilimia 76 hawataki liwepo kabisa
*Kikwete asema maoni hayo yataheshimiwa

Na Ramadhan Semtawa

KAMATI ya kukusanya maoni kuhusu uharakishwaji (fast tracking) wa uanzishwaji wa Shirikisho la Kisiasa la Afrika Mashariki, imewasilisha ripoti yake kwa Rais Jakaya Kikwete, huku asilimia 75.9 ya Watanzania, wakipinga mpango huo.

Ripoti hiyo inaonyesha jinamizi la kero za muungano bado linaitafuna Tanzania, kwani idadi hiyo iliyopinga, imetaka kwanza kero hizo zitatuliwe kabla ya kukimbilia kwenye shirikisho.

Wakati hao wakipinga baada ya kuulizwa, wengine asilimia 3.3, bila ya kuulizwa, walituma maoni yao kukataa kabisa kuwepo kwa shirikisho hilo.

Akiwasilisha ripoti hiyo Ikulu jijini Dar es Salaam jana, Mwenyekiti wa kamati ya kukusanya maoni kuhusu mpango huo, Profesa Samwel Wangwe, alisema asilimia 20.8, waliunga mkono mpango huo kasi.

Katika ripoti hiyo, inaelezwa kuwa jumla ya Watanzania 65,000 walipata fursa ya kutoa maoni yao katika mikoa na wilaya zote, ambazo kamati ilifika.

Ripoti hiyo ambayo imegawanyika katika vitabu viwili pamoja na mkanda wa video, imegawanwa katika makundi mawili ambayo ni kisiasa na jamii.

Inaeleza kwamba Watanzania waliopinga shirikisho wamekuwa na sababu mbalimbali, ambazo moja ni ya kisiasa, kwamba hawalifahamu shirikisho hilo.

Sababu nyingine ni pamoja na demokrasi na utawala bora, ambapo Watanzania wana shaka kama vitu hivyo viwili vipo katika nchi nyingine.

Watanzania hao pia wameangalia suala la ulinzi, usalama na amani na tofauti za kiitikadi na pia walipinga kutokana na tofauti ya maendeleo ya kiuchumi kati ya nchi hizo na Tanzania hasa kulinganisha na Kenya.

Sababu nyingine ni kutaka kwanza, Tanzania itatue kero zake za muungano na Zanzibar kwani hadi sasa hazijamalizwa.

Akizungumza sababu za kuchelewa kuwasilisha ripoti hiyo, Profesa Wangwe, alisema kamati ilichukua maoni kwa njia mbalimbali ambazo ni pamoja na vyombo vya habari, kujaza dodoso na mtandao wa kompyuta kwa ajili ya kuwezesha hata Watanzania walio nje kupiga kura.

Rais Kikwete akizungumzia suala hilo, alisema maoni hayo ya Watanzania yataheshimiwa.

Alisema ingekuwa ni tatizo kama Watanzania hao wangesema hawataki shirikisho, lakini kwa kuwa hawataki liharakishwe, yeye haoni kama ni tatizo.

Rais Kikwete alisema ripoti hiyo itapelekwa katika ngazi ya Baraza la Mawaziri, ili ifanyiwe kazi na kisha kupelekwa katika wizara husika ya Afrika Mashariki kwa ajili ya kuendelea na mchakato.

Kama maoni hayo yatazingatiwa, mchakato wa kuundwa kwa shirikisho utakwenda kama ilivyoelezwa katika mkataba wa Jumuiya ya Afrika Mashariki (EAC).

Tayari hadi sasa nchi za EAC, zimeanza kutumia mfumo mmoja wa forodha (Customs Union), huku makubaliano mengine kama soko la pamoja (Common Market), sarafu ya pamoja (Monetary Union) na shirikisho la kisiasa (Political Federation) yakiwa bado hayajakamilika.

Tume hiyo ilianza kazi yake Oktoba 13 mwaka jana na imekabidhi ripoti yake Julai 13, ikiwa ni zaidi ya miezi sita imepita tangu ripoti hiyo ilipotakiwa kuwasilishwa.
 
Koba

JF-Expert Member
Joined
Jul 3, 2007
Messages
6,141
Points
1,500

Koba

JF-Expert Member
Joined Jul 3, 2007
6,141 1,500
hata wakati wa kukusanya maoni ya vyama vingi 80% ya watanzania walikuwa hawataki vyama vingi..same thing here na FEDERATION itakuja tuu na kitu kizuri sana,dunia ya leo hatutaki kubanwabanwa acha tupanue nchi na uhuru wa kwenda popote na kufanya chochote as long as unaheshimu sheria na ujinga kama watu wa BOT na Richmond nakuhakikishia hautatokea
 
Ogah

JF-Expert Member
Joined
Mar 10, 2006
Messages
6,233
Points
1,225

Ogah

JF-Expert Member
Joined Mar 10, 2006
6,233 1,225
Jamani waheshimiwa hivi mnaionaje hii EAC. Nyie mnadhani itazaa matunda yoyote au ni kuleta vita katika siku za usoni?
Karibu sana ndg muhogo

hapa JF kuna section ya EAC........mods watatusaidia kupeleka suala lako kule
 
BAK

JF-Expert Member
Joined
Feb 11, 2007
Messages
98,064
Points
2,000

BAK

JF-Expert Member
Joined Feb 11, 2007
98,064 2,000
Date::10/23/2008
Shirikisho A. Mashariki lapigwa mwereka
Na Ramadhan Semtawa
Mwananchi

UAMUZI wa wakuu wa nchi 26 za Afrika kuunganisha soko la pamoja katika nchi hizo, umeondoa ndoto ya kuanzisha shirikisho la kisiasa la Jumuiya ya Afrika Mashariki.

Hatua hiyo inatokana na mpango wa wakuu wa Jumuiya ya Afrika Mashariki (EAC), Jumuiya ya Maendeleo Kusini mwa Afrika (SADC) na Jumuiya ya Soko la Pamoja kwa Nchi za Kusini na Mashariki mwa Afrika (Comesa), kuanzisha mchakato huo ambao utameza mambo ya jumuiya hizo.

Shirikisho la Afrika Mashariki linahusisha nchi za Tanzania, Uganda, Kenya, Burundi na Rwanda na tayari nchi hizo zilishapiga hatua kubwa kuelekea kuwa kitu kimoja, huku mabilioni ya fedha yakiwa yametumika katika mchakato huo, ambao pia ulihusisha kutafuta maoni kwa wananchi.

Baadhi ya taasisi za Shirikisho la Afrika Mashariki zilishaanza kufanya kazi, ikiwemo sekretarieti inayoratibu shughuli zote za shirikisho hilo, bunge, mahakama huku mamilioni mengine yakitumika kujenga ofisi za makao makuu mjini Arusha, lakini uamuzi uliofanywa juzi unaweza kuwa mwanzo za kuzorota kwa harakati hizo.

Akijibu swali kutoka gazeti hili kuhusu uamuzi huo wakuu wa nchi 26 uliofanywa nchini Uganda, Waziri wa Mambo ya Nje na Ushirikiano wa Kimataifa, Bernad Membe alisema ni dhahiri hapo baadaye kama mchakato utakwenda kama ulivyo, shirikisho hilo halitakuwepo.

"Dah..., ndiyo, halitakuwepo, kadri tunavyokwenda katika mpango huu wa kuunganisha soko la nchi zetu hizo za jumuiya tatu, ni dhahiri kuna mambo yatabidi yajiondoe," alisema.

Membe alifafanua kuwa mpango huo wa kuunganisha jumuiya tatu unalenga kuwezesha kuwepo soko kubwa la pamoja la watu 527 milioni na mfumo wa forodha.

Hata hivyo, alisema mchakato wa kuelekea soko la pamoja kwa EAC bado unaendelea na kwamba, kama ni kusitishwa, basi hiyo itakuja kufahamika baadaye baada ya mchakato wa jumuiya hizo tatu.

"Lakini mchakato ndani ya EAC ambao tumefikia sasa kuhusu Common Market (soko la pamoja), bado unaendelea, huku taratibu za soko jipya nazo zikiendelea,"alifafanua.

Membe alisema katika mchakato huo wa jumuiya tatu, wakuu hao wameunda timu ya kuangalia taratibu za kisheria kwa ajili ya kutafuta uhalali wa jambo hilo.

"Sasa, katika kufanikisha mpango huo wa kuanzisha soko kubwa kwa kuunganisha Comesa, Sadc na EAC, wakuu wameamua kuunda timu ya wataalamu ambayo itafuta uhalali kisheria," alisisitiza.

Kwa ufafanuzi, Membe alisema timu hiyo itafanya kazi kwa kipindi cha miezi sita kuona njia bora za kuweza kufanikisha ndoto hiyo.

Alisema kuanzishwa kwa soko kubwa la pamoja katika ukanda huo kwa kuunganisha ukanda wa Kusini, Kati na Mashariki ya Afrika hadi Misri, kutakuwa na faida kubwa kwa maendeleo ya ukanda huu.

"Kwa hiyo, kuanzisha Free Trade Area, kuna manufaa makubwa ikiwa ni pamoja na kuweza kukaribiana na matatizo mbalimbali kama misuko misuko ya kuanguka kwa taasisi za kifedha katika mataifa makubwa," alisisitiza.

Membe alisema eneo hilo lina wakazi hao 527 milioni kati ya idadi jumla ya wakazi wa Afrika ambao ni 940 milioni, ambao wanachukua sehemu kubwa ya bara hilo.

Waziri Membe alitetea kuwa China imekuwa ikipata maendeleo kutokana na kuwa na idadi kubwa ya watu hivyo biashara inayofanyika nayo pia huwa kubwa.

Katika Shirikisho la Afrika Mashariki inatarajiwa kuwapo maingiliano makubwa zaidi ya kiuchumi na biashara, pia kuondolewa vikwazo vya kufanya kazi baina ya mataifa hayo pamoja na masuala muhimu ya uwekezaji katika ardhi suala ambalo limezua utata miongoni mwa mataifa hayo, huku mengine yakipinga hatua hiyo.

Katika hatua nyingine, Membe alisema wakuu hao wamejadili kwa kina mambo yanayoendelea katika nchi za Somalia, Burundi na Mauritania.

Alisema kwa upande wa Burundi msuluhishi wa mgogoro huo ambaye ni Waziri wa Usalama wa Afrika Kusini, Charles Nqakula, alitoa utekelezaji wa mpango wa amani nchini humo.

Hata hivyo, alisema hadi sasa mpango huo umekwama kutokana na kundi la FNL Palipehutu lilanalongozwa na Agathon Rwasa, kukaata kubadili jina la kundi hilo ili kuondoa dhana ya ukabila ambayo inapingana na katiba.

Kuhusu kuingizwa katika serikali, alisema kundi hilo linadai kuwa na jeshi kubwa msituni ambalo ni takriban askari 21,000 lakini linashindwa kuthibitisha huku likidai fedha nyingi kwa ajili ya kuwalipa.
 
The Quonquerer

JF-Expert Member
Joined
May 14, 2009
Messages
781
Points
0

The Quonquerer

JF-Expert Member
Joined May 14, 2009
781 0
Na Muhingo Rweyemamu (Rai)

Yapo mambo mambo matatu yaliyonisukuma kuandika uchambuzi huu. Kwanza ni kitendo cha uongozi wan chi ya Rwanda kukataa mechi ya soka katil ya Taifa Stars na Amavubi kuchezwa Jumamosi na badala yake kupangwa kuchezwa Jumapili.

Rwanda, walikuwa na taarifa kwamba Jumatatu, timu yetu ina ugeni kutoka Brazil. Na mchezo huu ni muhimu kwa nchi za Afrika Mashariki na unaweza kuitwa once in a life time.

Jambo la pili ni kauli aliyoitoa Waziri Mkuu mjii Arusha akiuliza ni nani aliyewaroga Watanzania kiasi kwamba hawawezi kujiamini ingawa wamejaliwa raslimali kubwa katika nchi nzuri.

Waziri Mkuu alikuwa akizungumza katika mkutano wa wadau wa kilimo cha mazao ya bustani na akasema anashangazwa kwamba wenzetu kwa Kenya pamoja na kuwa na ka nchi kadogo kenye raslimali kidogo, wamejaliwa sana katika suala la kilimo cha mauzo ya bustani yaliwamo maua.

Katika mkutano huo,Katibu Mkuu huyo (Wizara ya Habari), Sethi Kamhanda, aliitaka sekta ya habari nchini kujiandaa na ushindani utokanao na kufunga milango ya Jumuia ya Afrika Mashariki. Katika maelezo yake, Kamhanda alisema kila kitu kimeshakubaliwa na viongozi wa nchi hizi tatu na kwamba lililobaki ni jukumu la Watanzania kujiandaa namna ya kuingia katika sekta hii.

Alishauri kwamba Waandishi wa habari wa Tanzania, tujiandae kwenda kufanya kazi katika nchi nyingine za Afrika Mashariki na Kati kwa sababu hata waandishi wa habari wanchi hizo, wanajiandaa kuja kufanya kazi hapa nchini mwetu. Nchi hizo ni pamoja na Kenya, Uganda, Rwanda, Burundi na Tanzania yenyewe.

Wahariri wengi waliokuwapo, walipinga jambo hilo, lakini wakati wa hitimisho lake, aliyasema maneno yanayofanana na maneno aliyoyasema Waziri Mkuu Mizengo Pinda kule Arusha.

Kama alivyosema Pinda, Kamhanda naye aliwataka waandishi wa habari kuacha woga akisema kwamba siyo kweli kwamba watu wa Kenya wano uwezo kuliko Watanzania.
Naomba Watanzania kuwashangaa wote wawili. Kwa nini?

Mwaka 1989, wakimbizi wa Burundi waliokuwa katika mpaka wa Tanzani, ikiwa ni pamoja na viongozi wao ambao sasa ndiyo walioko madarakani nchini humo, waliamua kufanya jambo moja kwa ajili ya manufaa ya nchi yao.

Waliamua kuwachukua vijana wa Kirundi waliokuwa makambini na kuwatafutia vyuo vikuu hapa nchini. Chuo Kikuu kilichaguliwa,kilikuwa Chuo cha Tumaini Iringa. Vijana wengi waliokwenda kusoma Iringa, walichagua kozi tatu lakini wengi walikimbia kozi mbili. Kozi ya kwanza ilikuwa ni ya uandishai wa habari. Na ya pili ilikuwa ya uchumi. Wachache walikwenda kozi ya sheria.

Moja ya mambo ya msingi waliyoamua kujifunza, ilikuwa ni lugha ya Kiingereza na Kiswahili. Baada ya miaka mitatu ya mafunzo yao chuoni hapo, vijana hao walikuwa wameiva katika Kiswahili na Kiingereza. Walipokuwa wakitoka nyumbani kwao, walikuwa ni wataalam wa lugha za Kifaransa na Kirundi. Kwa hiyo wanarudi nyumbani wakiwa na hazina ya lugha nne. Kiingereza, Kiswahili, Kifaransa na Kirundi.

Wengi wa vijana hawa, kwa sasa wanafanya kazi Ofisi ya Rais. Lakini cha msingi zaidi, vyombo vyote vya habari muhimu nchini Burundi vimeshikwa na kuongozwa na vijana hawa waliofundishwa katika vyuo vyetu hapa nchini. Wana hazina ya lugha nne na mbili kati ya hizo wamejifunzia nchini mwetu.

Sasa tunafungua milango ya Watanzania ambao, Warundi, Waganda, Wanyarwanda na Wakenya kwenda kutafuta kazi tofauti ikiwamo ya uandishi wa habari katika mojawapo ya nchi hizo au katika nchi zote hizo.
Watanzania tuna silaha ya lugha moja tunayoijua kwa ufasaha. Kiswahili. Warundi wana silaha ya lugha nne wanazozijua kwa ufasaha. Sisi tumefungua milango ya kwenda kufanya kazi Burundi. Kirundi na Kifaransa, ndiyo lugha zinazotumika nchini Burundi. Na sisi tunaojua Kiswahili tunajidanganya kwamba tumefunguliwa milango kwenda kufanya kazi nchini Burundi.

Tunataka kufanya kazi nchini mwao, wakati hatuwezi kuzungumza nao hata sentensi moja. Pinda nikikushangaa wewe, na wewe utaendelea kunishangaa?

Viongozi wetu sawa, walikaa kwenye mikutano wakakubaliana kabisa kufungua milango ili sisi tutoke twende kufanya kazi katika nchi nyingine waje kufanya kwetu?

Nauliza mara mbili, ni mhariri yupi wa Tanzania anayeweza kwenda kufanya kazi ya uhariri katika gazeti la Nation la Kenya? Na ukweli siyo kwamba Watanzania hawajui Kiingereza, hapana je, hapo Kenya yapo mazingira ya kumruhusu Mtanzania kuhariri gazeti lao?

Kwetu sawa? Hatuna shida wanaweza kuja kuhariri, hata habari za kiulinzi,wanaweza kuja kuhariri.
Ninayo kumbukumbu nzuri ya mwaka 2005 wakati Wakenya waliokuja katika mojawapo ya magazeti ya Tanzania.Wakenya hao hawakuleta teknolojia tu, bali walikuja pia na jina la mtu wanayemtaka awe rais wa Tanzania.

Wengine tulipinga na tukafukuzwa kai. Hawa ndiyo tunataka twende kwao tuhariri habari za kisiasa za kwao na tunajidanganya kwamba wataturuhusu?

PInda unalalamika pale arusha . Hebu fikiria kama waziri mkuu mwenzio wa Kenya, Raila Odinga anaweza kuwaita raia wa nchi yake akaanza kuwalalamikia? Hawezi!

Na kwanini hawawezi kuwalalammikia ni kwa sababu tayari mfumo wa maisha wanchi hiyo umewapa nyenzo wananchi wake za kujiwezesha.

Shahada zote nchini Kenya zimeongezwa somo la entrepreneurship. Kwa hiyo wanafunzi wa Kenya hawahangaishi na vyeti vizuri tu, hawahangaishwi na alama nzuri za matokeo za mitihani ya mwisho. Kwahiyo hawezi kuhangaishwa na wizi wa vyeti au udanganyifu wa mitihani.

Wanawaza watapa wapi kipande cha ardhi ilia weze kutengeneza andiko lake la mradi.
Nani mwanafunzi wa mwaka wa mwisho wa shahada ya kwanza yeyote katika chuo chetu hapa nchini anayeweza kutengeneza andiko la mradi lenye uwezekano wa kukopesheka? na hata akiwa nalo,ni benki gani Tanzania yenye ujasiri na uthubutu wa kuwakopesha watu?

Kampuni ya Nation ya Kenya imewekeza katika tasnia ya habari nchini mwetu. Taja kampuni yoyote ya kitanzania ya habari ambayo inawza kwenda kuwekeza nchini Kenya!

Kenya Commercial Bank imefungua tawi lake hapa nchini na baada ya kugundua neno Kenya lina sumbua katika jina lake,imeamua benki hiyo iitwe KCB. Hilo ndilo jina lake la sasa. Hata account ya EAC ni Kenya Commercial Bank.

Nitajie Benki yoyote ya Tanzania inayoweza kwenda nchini Kenya ikafungua Benki nchini Kenya ikafungua benki nchini humo!taja tu!kwanza hata duka mjini Nairobi likiaminika linamilikiwa na Mtanzania hakuna atakayenunua kako eti unafungua milango ili tutoke? Tuseme tu wazi kwamba umefungua milango ili waje . tunafungua milango ili wapate mashamba
.

Tunafungua milango ili wawe na uraia wa nchi mbili kwa kificho, wanao ujasiri wa kufanya wa kufanya hivyo sisi hatuna, hatukulelewa hivyo. Kama tunataka tuanze kulea taifa kujielekeza hivyo.

Wakati Fulani ilipotangazwa kwamba nchi za Uganda na Tanzania zinapewa grace period ya miaka mitano kuuza bidhaa zao bila kutozwa ushuru na kwamba Kenya itatozwa ushuru, mmoja wa viongozi mashuhuri nchini Kenya alipinga waziwazi. Ingawa wakenya wengi pamoja na serikali yao walipinga kwa siri. Charles Njonjo akasema ni kiongozi gani mpumbavu atakwenda kuwambia wakenya kwamba wacheleweshe maendeleo ya kwamba wacheleweshe maendeleo yao kwa sababu ya Watanzania na Waganda. Alikua sahihi!kenya haina kiongozi wa aina hiyo. Hawezi kudhubutu mtu yeyote kuwambia hivyo wakenya, watampiga mawe!

Nimezungumzia suala la michezo wa soka. Wakati Tanzania alipopata ugeni wa Ivory coast, kwa kujipendekeza kwenu tukaichagua Rwanda nayo tukaipatia mechi.

Lakini Rwanda sasa iliposikia Tanzania itacheza na Brazili wanataka tuikose mechi hiyo. Wanataka Taifa Stars icheze mechi jumapili wakitaka wacheze kesho yake na Brazil. Kwanza si kitendo sahihi kiafya kuwa chezesha wachezaji mechi mbili za kiushindani chini ya saa 48. Lakini Wanyaranda ndivyo wanavyotaka.
Hawa ndiyo waliokuwa wanagombana mwaka 1992, Tanzania ilikuwa makao yao makuu ya usuhulishi, kila wakipigana nyumbani wanakimbilia kwetu.

Arusha na Dar es Salaam ilikua kama kwao. Mwaka 1994. Ikafika ukomo wa unyama wao. Wakauana. Tanzania ikaamua kubeba mizigo yao. Walio salia baada ya kusambaratishana wakaletwa kwetu.
Wakiwa hapa,wakaendeleza tabia mbaya za kwao wakaua wanyama wote kwenye misitu ya hifadhi wakaimaliza.wakageuka kuiba chakula cha wenyeji, kwao hawali ugali, UNHCR inawapa ugali.Wakaamua kuivamia migomba ya wakazi na Ngara (kwa kina Kanyabwoya) wakafyeka migomba yao na kuchukua ndizi zao.Tena wakati mwengine mwenye shamba akija juu,wanamuua.

Hawakuishia hapo, wengine wao wakaamua kuwa majambazi.wakazi wa wilaya ya Karagwe wanajua.Mtu anaweza kuingiliwa nyumbani mwake akamiminiwa risasi na wakamuibia shati au suruali. Namkumbuka mzee mmoja maarufu Simony Gabagambi ambae aliuwawa sebuleni kwake kwa kumimminiwa risasi, na kisha kuibiwa television, basi.

Hawa ndio tunawafungulia milango kwa unyenyekevu eti na sisi tukawekeze kwao. Tunaenda kuwezesha nini? Viongozi mnatuzuia kuwa wanyonge wakati hamjatupa silaha za ujasiri? Naanza kukubaliana na mwimbaji Ailen sanga, aliyeimba wimbo wake : "pangisheni hata mabafu."
 
nomasana

JF-Expert Member
Joined
Aug 14, 2009
Messages
1,021
Points
1,500

nomasana

JF-Expert Member
Joined Aug 14, 2009
1,021 1,500
this is just the usual whinning and complaining from lazy tanzanians that lack self-belief

YES it is more than possible for a tanzanian to work in the kenyan media industry. this girl TERO is proof that if you are not lazy, u can compete with just about anyone!

She is a host of velvet room show at the homeboyz radio station in kenya. she is also a host of an award winning video dj TV show(KTN TV station) in kenya . IF TANZANIANS SHAKE OFF THE YOKES OF LAZYNESS THEY CAN COMPETE WITH ANYBODY. this girl is proof that a tanzanian can work and be successfull in the kenyan media industry which effectively renders the premise of this thread as pure myth.

[FONT=arial,helvetica,sans-serif]Namtero Mde[/FONT]

"I [FONT=arial,helvetica,sans-serif]love challenges.........I may be shy but very outgoing, and I usually speak what I feel, something [/FONT][FONT=arial,helvetica,sans-serif]very[/FONT][FONT=arial,helvetica,sans-serif] valuable my father taught me. Don't be deceived, I'll only be nice to you, if your nice to me.I love meeting new people, although people tend that I look arrogant and are [FONT=arial,helvetica,sans-serif]scared to approach me, but I promise I'm harmless."[/FONT][/FONT]

BIOGRAPHY

[FONT=arial,helvetica,sans-serif]Completed her high school in 2003. Went to USIU and studied Marketing.[/FONT]​

[FONT=arial,helvetica,sans-serif]She is the middle child of a family of five. ‘The black sheep' she says.[/FONT]

CAREER:

First job was for a training company (PINNACLE) then joined Homeboyz radio in 2007 where she hosts Fun from 1 on Saturdays.

Love life: Very single and not ready to mingle!

INSPIRATION:

Her late father, because he was a positive person and loved helping people even when he didn't have to.

Musically: Keisha Cole and Mary J Blidge- they went through so much but were still

able to achieve a lot more.

INTERESTS:

She loves watching wrestling although she says that these days its

become abit too fake for her.

Music: R‘n'B and Neosoul.

Movies: Saw 1, 2&3.

Apart from bullying Rhina, eating chocolate, sleeping and singing in the shower,

traveling at night and dancing are
some of the other things she likes doing.
http://homeboyzradio.co.ke/index.php?option=com_content&view=article&id=61&Itemid=34

this is an interview from when she won an award
http://www.standardmedia.co.ke/entertainment/InsidePage.php?id=2000009476&cid=123&
there are 2 more tanzanians that work in kenyan radio stations but i forgot(shame) their names
 
MpendaTz

JF-Expert Member
Joined
May 15, 2009
Messages
1,716
Points
1,250

MpendaTz

JF-Expert Member
Joined May 15, 2009
1,716 1,250
Nomasana, this is bullshit! you know why you are trying to mislead Tanzanians. This girl must have lived and grown up in Nairobi. Provide more details about her and with courage. And you should know that this is just a one person example, how many Kenyans are in Tanzania now? Are you aware of that? Can you compare with the number of Tanzanians in Kenya? Why do you think they are not coming? or rather not interested? Your insulting words "lazy Tanzanians" is actually what our leaders should hear and understand what Tanzania is going to achieve in the EAC. There is no intelligent Politician with the slightest understanding of economics will agree to the EAC been advocated right now. A lot is left aside not yet considerred. People are starting to speak out now. I would like to warn you Nomasana together with many of you who intend to come and grab land in Tanzania, that do not underestimate Tanzanians. The leaders in power now including our honorable MPs have been asked to declare openly who has supported the EAC move and who has not for our records. At a certain point when Tanzanians will get fed up of been enslaved in their own country, you will need to go back with a few Tanzanian friends who are selfish like you.
 
again a lazy and defeated mentallity. this world is a dog eat dog world, u have to be mentally tough and prepared.
 
Geza Ulole

JF-Expert Member
Joined
Oct 31, 2009
Messages
20,713
Points
2,000

Geza Ulole

JF-Expert Member
Joined Oct 31, 2009
20,713 2,000
this is just the usual whinning and complaining from lazy tanzanians that lack self-belief

YES it is more than possible for a tanzanian to work in the kenyan media industry. this girl TERO is proof that if you are not lazy, u can compete with just about anyone!

She is a host of velvet room show at the homeboyz radio station in kenya. she is also a host of an award winning video dj TV show(KTN TV station) in kenya . IF TANZANIANS SHAKE OFF THE YOKES OF LAZYNESS THEY CAN COMPETE WITH ANYBODY. this girl is proof that a tanzanian can work and be successfull in the kenyan media industry which effectively renders the premise of this thread as pure myth.there are 2 more tanzanians that work in kenyan radio stations but i forgot(shame) their names
Pambaf when u tell a racist on a face of her or his bad habit she or he will tell you, i am not a racist by the way a black man was in my house last weekend! this is what you are trying to do for you to note this girl is a Tanzanian you prove that works in Kenya are not for Tanzanians! i won't be suprized if she gets fired tomorrow! Kwenda kulala we Ondieki! By the way you even know how many Tanzanians are working in that country of yours just like the way you know how many Luhyas, Kikuyus and Jaluos are at work! Interesting
 
Koba

JF-Expert Member
Joined
Jul 3, 2007
Messages
6,141
Points
1,500

Koba

JF-Expert Member
Joined Jul 3, 2007
6,141 1,500
..another loooooong & useless copy and paste from know nothing expert kunyaboya,hata kilichoandikwa mwenyewe haelewi, yaani so weak and dumb!
 
Koba

JF-Expert Member
Joined
Jul 3, 2007
Messages
6,141
Points
1,500

Koba

JF-Expert Member
Joined Jul 3, 2007
6,141 1,500
Nomasana, this is bullshit! you know why you are trying to mislead Tanzanians. This girl must have lived and grown up in Nairobi. Provide more details about her and with courage. And you should know that this is just a one person example, how many Kenyans are in Tanzania now? Are you aware of that? Can you compare with the number of Tanzanians in Kenya? Why do you think they are not coming? or rather not interested? Your insulting words "lazy Tanzanians" is actually what our leaders should hear and understand what Tanzania is going to achieve in the EAC. There is no intelligent Politician with the slightest understanding of economics will agree to the EAC been advocated right now. A lot is left aside not yet considerred. People are starting to speak out now. I would like to warn you Nomasana together with many of you who intend to come and grab land in Tanzania, that do not underestimate Tanzanians. The leaders in power now including our honorable MPs have been asked to declare openly who has supported the EAC move and who has not for our records. At a certain point when Tanzanians will get fed up of been enslaved in their own country, you will need to go back with a few Tanzanian friends who are selfish like you.
...she is Tanzanian,kitu gani huelewi hapo? eti enslaved? you people need to stop that fearmongering BS,it doesnt help anybody.
 
Smatta

JF-Expert Member
Joined
Nov 5, 2008
Messages
2,350
Points
1,500

Smatta

JF-Expert Member
Joined Nov 5, 2008
2,350 1,500
Like it or not we are coming, now the reality is dawning on you. No one has ever prevented Tanzanians from working in Kenya, or any where else in East Africa for that matter, I know of two doctors who are working in KEMRI Kilifi (thats Kenya Medical Research Ins. for those who dont know), I know they dont share your sentiments. Be good in what you do and you will be poached by any country to work for them, but if you stay being lethargic in your profession, you will only work for the country unlucky enough to have you as a citizen coz no one will need your services elsewhere. I didn't want to comment on this article but your fear is becoming evident daily, there is no need to be afraid, a lot of Tanzanians are working professionally in Kenya, and also a lot of Kenyans are working in Tz, we are neighbors we cant change this.
 
The Quonquerer

JF-Expert Member
Joined
May 14, 2009
Messages
781
Points
0

The Quonquerer

JF-Expert Member
Joined May 14, 2009
781 0
again a lazy and defeated mentallity. this world is a dog eat dog world, u have to be mentally tough and prepared.

Eti ni dunia ya mbwa kumla mwenzake. Kwamba wageni mnakuja kuwala watanzania, yaani unazidi kusisitiza kuwa nyie ni cannibalist. What are the chances of you doing that and get away with it! Mmeingia choo cha kike! Kwa kuwa mtawatumia Kina Koba, mamluki wenu mliowatanguliza, wakenya/wageni kama Koba (school drop out kutoka Musoma, who sneaked into our country from Kenya) and thus illegal immigrant waliojifunza Kiswahili cha Tanzania ili wawasafishie njia. Wako wangapi kama yeye? Njooni lakini tusilaumiane. What can't you keep that bravery in Kenya, and develop for your own good. Kufanya kazi nje si vibaya, lakini je umekaribishwa! Hata Marekani ina list of terrorist, of which isn't too different with Kenyan culture ya umangimeza and unyang'au!

Nyie Kina Kenyatta na Moi wamewalalia kila kitu, eti mwataka kuponea Tanzania....no nyie siyo mzigo wetu! Try somewhere else, glass imejaa maji. Kwenda hukoo...muondokeee! kabla wananchi hawajapata hasira kali na kuchukua hatua kali....zisizo za kisheria! A country of braves and strong mentality (Nomasana, 2010 pp. 4) ila yenye UNEMPLOYMENT OF STAGGERING 40%...TETEH TEH TEEEEH!!!!!!!!!!!!!!!!!!Why can't you try Comedy on your NTV, CITIZEN or KBC. You are offering JF a talent i don't think it needs!
 
The Quonquerer

JF-Expert Member
Joined
May 14, 2009
Messages
781
Points
0

The Quonquerer

JF-Expert Member
Joined May 14, 2009
781 0
..another loooooong & useless copy and paste from know nothing expert kunyaboya,hata kilichoandikwa mwenyewe haelewi, yaani so weak and dumb!

Sheria ya kuhalalisha ushoga unafaidika nayo vipi? Tunakujua wewe ni activist wa kutetea uhalalishwaji wa sheria ya ushoga, ebu twambie mwa'kwetu. Loooo! Mtanzania wa wapi unatetea uhalali wa watu kuingiliana kinyume na maumbile??? Wewe hata hao wakenya kama walikutuma Marekani, ndiyo walivyokutuma kufanya. Twambie Smatta kama ndiyo mpango wenu wa kuhalalisha ushoga kwenye nchi yetu! Wewe Koba kama ni Wakenya wanakuingilia kinyume na maumbile, usijali hata hapa kuna kina Maumba, watakuhudumia..maana huipendi Tanzania kwa sababu labda unadhani hawajui kazi! I can't be a dumb than a school drop out of your kind! Sufuria za Wamarekani zitakuchana mikono yote! Mi nakula kiyoyozi hapa kwenye nchi yangu ya ahadi, ya asali na maziwa!

Kuhusu shule, anti Koba mi ni kichwa! Uliza mlimani UDSM, Marekani (Pittsburgh, PA), Mazengo, Ihungo...miaka ile kufuru zangu nilizokuwa nafanya. Nilirudi kwetu na inanilipa kinyama! Ndiyo maana mtu sitaki mtu wa nje aje kunikanyaga kichwani nikiwa kwangu! Nimesoma thread moja hapo nyuma ya "Gay Tourims ni Israel" (siingii kwenye thread kama hizo), usije ukawa umeshawasili mjini Tel Aviv unajrusha na wenzako! Uko US au umeshakwea pipa?
 
The Quonquerer

JF-Expert Member
Joined
May 14, 2009
Messages
781
Points
0

The Quonquerer

JF-Expert Member
Joined May 14, 2009
781 0
Like it or not we are coming, now the reality is dawning on you. No one has ever prevented Tanzanians from working in Kenya, or any where else in East Africa for that matter, I know of two doctors who are working in KEMRI Kilifi (thats Kenya Medical Research Ins. for those who dont know), I know they dont share your sentiments. Be good in what you do and you will be poached by any country to work for them, but if you stay being lethargic in your profession, you will only work for the country unlucky enough to have you as a citizen coz no one will need your services elsewhere. I didn't want to comment on this article but your fear is becoming evident daily, there is no need to be afraid, a lot of Tanzanians are working professionally in Kenya, and also a lot of Kenyans are working in Tz, we are neighbors we cant change this.
Ndiyo maana kwenye Common Market Protocol tumeainisha kada ya watalaam tunaowahitaji..is that even bad, just to decide for our dear Tanzania, Smatta hutaki hata hiyo! Sisi hatukatai kila kitu, lakini nina uhakika hizo kada tunazozitaka hamna, and you won't even be willing to work at our rates! Nenda nchi za kusini, ulaya na dunia nzima utakutana ma professor na madaktari wa kitanzania wanashuka nondo kama hawana akili nzuri!
 
nomasana

JF-Expert Member
Joined
Aug 14, 2009
Messages
1,021
Points
1,500

nomasana

JF-Expert Member
Joined Aug 14, 2009
1,021 1,500
Eti ni dunia ya mbwa kumla mwenzake. Kwamba wageni mnakuja kuwala watanzania, yaani unazidi kusisitiza kuwa nyie ni cannibalist. What are the chances of you doing that and get away with it! Mmeingia choo cha kike! Kwa kuwa mtawatumia Kina Koba, mamluki wenu mliowatanguliza, wakenya/wageni kama Koba (school drop out kutoka Musoma, who sneaked into our country from Kenya) and thus illegal immigrant waliojifunza Kiswahili cha Tanzania ili wawasafishie njia. Wako wangapi kama yeye? Njooni lakini tusilaumiane. What can't you keep that bravery in Kenya, and develop for your own good. Kufanya kazi nje si vibaya, lakini je umekaribishwa! Hata Marekani ina list of terrorist, of which isn't too different with Kenyan culture ya umangimeza and unyang'au!

Nyie Kina Kenyatta na Moi wamewalalia kila kitu, eti mwataka kuponea Tanzania....no nyie siyo mzigo wetu! Try somewhere else, glass imejaa maji. Kwenda hukoo...muondokeee! kabla wananchi hawajapata hasira kali na kuchukua hatua kali....zisizo za kisheria! A country of braves and strong mentality (Nomasana, 2010 pp. 4) ila yenye UNEMPLOYMENT OF STAGGERING 40%...TETEH TEH TEEEEH!!!!!!!!!!!!!!!!!!Why can't you try Comedy on your NTV, CITIZEN or KBC. You are offering JF a talent i don't think it needs!
the only comedy is when you or any of ur family member getting laid off for a burundian to take his job. now that will be comical.

kunia-bwoya, you can call kenyans whatever u want, fact is come july KENYANS ARE COMING TO TANZANIA WETHER U LIKE IT OR NOT AND YOU CANNOT DO ANYTHING TO STOP US. THAT IS THE BRUTAL REALITY STARING U IN YOUR FACE AND YOU ARE STRUGGLING TO DEAL WITH IT.
 
Smatta

JF-Expert Member
Joined
Nov 5, 2008
Messages
2,350
Points
1,500

Smatta

JF-Expert Member
Joined Nov 5, 2008
2,350 1,500
the only comedy is when you or any of ur family member getting laid off for a burundian to take his job. now that will be comical.

kunia-bwoya, you can call kenyans whatever u want, fact is come july KENYANS ARE COMING TO TANZANIA WETHER U LIKE IT OR NOT AND YOU CANNOT DO ANYTHING TO STOP US. THAT IS THE BRUTAL REALITY STARING U IN YOUR FACE AND YOU ARE STRUGGLING TO DEAL WITH IT.
hahaha.. tell the nig*a, you cant stop an idea whose time has come.. kunia-bwoya just relax and watch the space..
 
PatPending

JF-Expert Member
Joined
Aug 17, 2007
Messages
490
Points
170

PatPending

JF-Expert Member
Joined Aug 17, 2007
490 170
Jamani huu uwoga woga na chuki pasi na sababu ya msingi zinatia aibu sasa. Ushirikiano wa raia wa hizi nchi ulikuwepo kabla hata ya mkutano wa Berlin wa mwisho wa karne ya 19 uliogawa haya maeneo kwa watawala na nchi kuzaliwa. Ushirikiano huu pamoja na misuguano (ipo mingi tu ) ni ya asili na shirikisho hili halitobadilisha mengi. Sehemu za mipakani wananchi wa nchiz zote husika wanashirikiana buila ya matatizo iwe kwenye biashara, kuoleana, doria n.k

Kwenye miaka ya sabini na themanini kulikuwa na vitu vingi sana vya magendo nchini huku kutoka Kenya mabavyo vilisaidia kupunguza makali ya kufunga mikanda enzi zile. Vile vile siku hizi wabongo mbona tunauza vingi tu kwa majirani zetu, kuanzia mbao, mahindi na vinginevyo vyingi tu.

Acheni uwoga wakuu, najua Smatta na wenzake wanawarusha roho kwa maneno yao ila kumbukeni haya ni maneno tu na "maneno matupu hayavunji mfupa" . Kuna baadhi hapa wanajigamba kwa ubora wao katika elimu na fani zingine mbalimbali sasa iweje tuogope ushindani? Nini hasa maana ya kuwa bora kama utakuwa unawakimbia washindani wako?

Ushindani huongeza ufanisi na ubora. Watu wengine mnakuwa mnawaogopa wakenya mpaka mnasahau mkono mkubwa wa Afrika Kusini hapa kwetu ambao haujanufaisha walio wengi.

Hatuwezi kuishi peke yetu peke yetu, ulimwengu huu una wadau wengi na badala ya kupinga ushindani tuuchukulie kama ni changamoto ya kuboresha pale tunapopatia na tunapokosea.

kwa mila zetu za KiAfrika, Mwanamme hamkimbii mwanamme mwenzake
 
Forum statistics

Threads 1,356,229
Members 518,868
Posts 33,127,872
Top