Majeshi ya kulinda Amani ya EAC yatimuliwa DRC. Waangalizi wa Uchaguzi wa EAC wagomewa...

Informer

JF-Expert Member
Jul 29, 2006
1,582
6,627
Kama kuna kitu kimeshangaza watu wengi ni uamuzi wa DRC kuyatimua majeshi ya kulinda amani ya EAC. Ilitarajiwa kuwa kikosi hicho cha EAC ndio kingekuwa mhimili katika shughuli za kuhakikisha amani inarejea mashariki wa DRC.

Lakini nchi hiyo imechoshwa na kikosi hicho kilichokaa nchini humo katika kipindi kisichofikia miaka miwili!

Hivi sasa DRC imeonyesha kuwa na imani zaidi ya majeshi ya SADC (Jumuiya ya Uchumi Kusini mwa Afrika) na pia Afrika Kusini.

“Hatuna imani tena na vikosi vya kulinda amani vya EAC na ndio maana tumewaambia waondoke, tunashukuru kuwa wanaondoka,” alisema Naibu Waziri Mkuu ambaye pia ni Waziri wa Ulinzi wa DRC, Jean Pierre Bemba alipozungumza na mwakilishi wa JamiiForums nchini humo hivi karibuni nyumbani kwake Maluku, nje kidogo ya Kinshasa.

Kwa mujibu wa Bemba, badala ya kulinda amani kama ilivyotakiwa askari wa EAC walijiingiza kufanya mambo mengine kiasi cha kuwachukiza wananchi katika maeneo ambayo walipelekwa.

“Tumewaondoa askari (wa EAC) kwa usalama wao maana wananchi walishaanza kuhoji wanafanya nini cha maana. Ukiona wananchi wanasema hivyo basi ujue kuwa wamechukia na si ajabu wakaanza kupambana na askari hao. Ili kuhakikisha usalama wao (askari), tukaona ni vema waondoke,” alisema Bemba.

Kisa cha waangalizi wa uchaguzi
Kwa mara ya kwanza EAC imeshindwa kuepeleka waangalizi wa uchaguzi katika moja ya nchi wanachama mwaka huu. Kwa kawaida EAC hupeleka waangalizi kila mwanachama wake anapofanya uchaguzi, lakini mwaka huu imeshindikana kwa DRC baada ya nchi hiyo kuwanyima kibali waangalizi kutoka EAC.

Mwenyekiti wa Tume Huru ya Uchaguzi (CENI), Denis Kadima alimweleza mwakilishi wa JamiiForums jijini Kishasa siku chache zilizopita kuwa wao hawajatoa kibali cha uangalizi kwa watu kutoka EAC kwa sababu hawajaelezwa na serikali iwapo watu hao walikuwa wameruhusiwa kuifanya kazi hiyo.

“Ni kweli hatujatoa kibali kwa watu wa EAC. Utaratibu ni kuwa kabla sisi hatujatoa kibali, anayetaka kuwa mwangalizi wa uchaguzi huomba kwanza kibali Wizara ya Mambo ya Nje, Wizara ikishatoa ruhusa ndio sisi tunatoa kibali. Lakini kuhusu EAC hatujui nini kimetokea. Wizara ndio inaweza kulisemea hilo,” alisema.

Baada ya majibu hayo, mwakilishi wa JamiiForums aliyepiga kambi jijini Kinshasa aliwatafuta watu wa EAC kutaka kujua kulikoni? Siku mbili baadaye ndio EAC ikatoa taarifa ikithibitisha kuwa haitakuwa na waangalizi katika uchaguzi wa DRC kwa sababu serikali ya nchi hiyo imewanyima kibali cha kufanya kazi hiyo.
 
Mwakilishi wa Jamii Forums .. title mpya hii ..
 
Safi sana EA kuna wanafiki watupu.

Ukitaka kupiga hatua kama Nchi usifunganane na watu wa EA.
 
Asante sana JF kutupa habari za Ndani kabisa
 
Akina Msevevi........wanafajya uchaguzi kama Ugaidi na bado wanasema it was free and fair🤣🤣🤣
Kama Tanzania tumasemaje?
Ujue inawezekana mimi huwa najidangamya kwamba sisi ndio kama ma godfather ukanda huu, tulipaswa kuwa na sauti
 
Sauti itoke wapi kwa Imani zipi za maana tulizo nazo leo wapi kujitofautisha na nani?

IMG_20231222_071641.jpg

IMG_20231222_042155.jpg
 
Kama kuna kitu kimeshangaza watu wengi ni uamuzi wa DRC kuyatimua majeshi ya kulinda amani ya EAC. Ilitarajiwa kuwa kikosi hicho cha EAC ndio kingekuwa mhimili katika shughuli za kuhakikisha amani inarejea mashariki wa DRC.

Lakini nchi hiyo imechoshwa na kikosi hicho kilichokaa nchini humo katika kipindi kisichofikia miaka miwili!

Hivi sasa DRC imeonyesha kuwa na imani zaidi ya majeshi ya SADC (Jumuiya ya Uchumi Kusini mwa Afrika) na pia Afrika Kusini.

“Hatuna imani tena na vikosi vya kulinda amani vya EAC na ndio maana tumewaambia waondoke, tunashukuru kuwa wanaondoka,” alisema Naibu Waziri Mkuu ambaye pia ni Waziri wa Ulinzi wa DRC, Jean Pierre Bemba alipozungumza na mwakilishi wa JamiiForums nchini humo hivi karibuni nyumbani kwake Maluku, nje kidogo ya Kinshasa.

Kwa mujibu wa Bemba, badala ya kulinda amani kama ilivyotakiwa askari wa EAC walijiingiza kufanya mambo mengine kiasi cha kuwachukiza wananchi katika maeneo ambayo walipelekwa.

“Tumewaondoa askari (wa EAC) kwa usalama wao maana wananchi walishaanza kuhoji wanafanya nini cha maana. Ukiona wananchi wanasema hivyo basi ujue kuwa wamechukia na si ajabu wakaanza kupambana na askari hao. Ili kuhakikisha usalama wao (askari), tukaona ni vema waondoke,” alisema Bemba.

Kisa cha waangalizi wa uchaguzi
Kwa mara ya kwanza EAC imeshindwa kuepeleka waangalizi wa uchaguzi katika moja ya nchi wanachama mwaka huu. Kwa kawaida EAC hupeleka waangalizi kila mwanachama wake anapofanya uchaguzi, lakini mwaka huu imeshindikana kwa DRC baada ya nchi hiyo kuwanyima kibali waangalizi kutoka EAC.

Mwenyekiti wa Tume Huru ya Uchaguzi (CENI), Denis Kadima alimweleza mwakilishi wa JamiiForums jijini Kishasa siku chache zilizopita kuwa wao hawajatoa kibali cha uangalizi kwa watu kutoka EAC kwa sababu hawajaelezwa na serikali iwapo watu hao walikuwa wameruhusiwa kuifanya kazi hiyo.

“Ni kweli hatujatoa kibali kwa watu wa EAC. Utaratibu ni kuwa kabla sisi hatujatoa kibali, anayetaka kuwa mwangalizi wa uchaguzi huomba kwanza kibali Wizara ya Mambo ya Nje, Wizara ikishatoa ruhusa ndio sisi tunatoa kibali. Lakini kuhusu EAC hatujui nini kimetokea. Wizara ndio inaweza kulisemea hilo,” alisema.

Baada ya majibu hayo, mwakilishi wa JamiiForums aliyepiga kambi jijini Kinshasa aliwatafuta watu wa EAC kutaka kujua kulikoni? Siku mbili baadaye ndio EAC ikatoa taarifa ikithibitisha kuwa haitakuwa na waangalizi katika uchaguzi wa DRC kwa sababu serikali ya nchi hiyo imewanyima kibali cha kufanya kazi hiyo.
Kwahiyo Kikwete ameenda kuuza sura tu ?
 
Back
Top Bottom