Nakubaliana na Salva ni habari za kudharirisha sana hizi. Lakini Salva, nadhani ungekaa kimya kabisa na kuzipuuza hizi habari,ungekuwa umefanya jambo la maana sana, lakini kwa kuzijibu , naona ndio umelikoroga zaidi.
Haya mambo ya WeakLeaks yapo Duniani kote, na yanawezwa kuwekwa mambo mengine hapa tukabaki midomo wazi. Nilihisi kuwa lazima watu wa magogoni wangelisemea hili kutokana na historia yao ya kujibu mambo mbalimbali, na kweli sikukosea.
Nadhani, tunahitaji kusikia mambo au habari nzito toka pale magogoni na wala si haya mambo ya suti. Usije jikuta kesho yakaja mengine ya vijiko na sahani na hayo tena mkaanza kuyajibu, sasa hizo zitakuwa habari au nini?