Mzee wa Rula
JF-Expert Member
- Oct 6, 2010
- 8,171
- 3,346
Uchaguzi wa urais na wabunge uliofanyika 31 Oct, 2010 umeiacha nchi yetu katika wakati mgumu sana. Hii ni kutokana na madonda yaliyozaliwa na MATOKEO ya uchaguzi huo ambao ulilalamikiwa sana na vyama vya upinzani, waangalizi wa kimataifa, NG'Os na wananchi kwa ujumla wakilalamikia ucheleweshwaji wa utangazwaji wa matokeo hususani maeneo ambayo upinzani ulikuwa na nguvu kidogo.
Nini hatma ya Tanzania yetu mara baada ya uchaguzi huu kwa kuangalia mlolongo wa matukio haya:-
Nawakilisha.
Nini hatma ya Tanzania yetu mara baada ya uchaguzi huu kwa kuangalia mlolongo wa matukio haya:-
- Chama cha CDM kupinga kutomtambua JK na kisha baadae kumtambua kulivuta hisia kubwa kutokana na madai yao ambayo leo hii ndiyo dira ya madai ya katiba mpya. Madai yao ni tume huru ya uchaguzi, katiba ambayo imempa madaraka makubwa rais na wizi wa kura katika uchaguzi ambao CDM walisema wanaandaa ushahidi lakini walijua wazi ushahidi huo hauwasaidii chochote kwani sheria inabana kuhoji matokeo ya urais na chombo chochote kile.
- Kutokana na hoja hapo juu ni kama CDM walikuwa kimya kama wanatunga sheria, sasa uchaguzi wa mameya umekuwa kama ni weak point ya kutoa duku duku lao. Waliandaa maandamo ambayo jeshi la polisi liliyazuia pasi kuangalia kuwa kuyazuia kulikuwa na gharama kubwa kuliko kutoyazuia. Athari ya maandamano hayo ndiyo msingi wa thread hii, kutokana na maneno ya Dr. Slaa kuwa tukitaka nchi hii isitawalike basi inawezekana na Ndesamburo alipokuwa anamwambia JK kuwa haujui vurugu zangu basi ngojea nianze.
- Ninatilia mashaka endapo nao CDM wataamua kuanza siasa ya maji machafu mf tu wakiandaa documentary yao nao inayothibitisha kuwa jeshi la polisi ni waongo maandamano yale yalikuwa halali ila kutumika kwao kisiasa ndiko kulikoletea hali ile nadhani yao itakubalika kuliko ya polisi, sasa nini kitajengeka hapo?
- Kutokana na CCM kushindwa kuwajibishana kumeleteleza mambo mengi ambayo sasa wananchi wanayajua kwa msaada wa viongozi wa vyama vya upinzani, media n.k Mambo hayo ni UFISADI, AHADI ZISIZOTEKELEZEKA, KUTOWAJIBIKA KWA VIONGOZI, UKOSEFU WA VIPAUMBELE VYA TAIFA VYA KUELEWEKA hivi vyote vimetumiwa na vyama vya upinzani kuongeza joto la mabadiliko.
- Sambamba na hili, migomo kila kona ambayo sasa CCM ina amini CDM ina mkono wake vinazidi kuichanganya serikali. Ni kama mtu anayewashwa mwili mzima hajui ajikune wapi aache wapi.
Nawakilisha.