Kalamu,
Nimefikia uamuzi huu si kwa sababu ya kutafuta nafasi ya uongozi ndani ya Chadema. Elimu yangu ya madrasa haiwezi nipa nafasi hiyo wala sina kipaji cha uongozi zaidi ya kusimamia na kuongoza kikundi kidogo sana cha watu.
Nakwenda Chadema kwa sababu ya mada hii!... nimekuwa nikisita miaka hadi miaka kujitwika mzigo ambao sidhani kama nauweza. Lakini baada ya kutafakari sana na hasa kufikiria kuwa humu JF kuna vichwa sii mchezo ila kilichokosekana ni kuyaweka maneno yao ktk vitendo..
Kama nilivyosema Ubishi wangu utakuwa mtihani mkubwa kwa Chadema na viongozi wake, jambo ambalo binafsi nafikiri litakuwa na msaada mkubwa kwa chama kuweza kuona upande wa pili wanafikira gani. Trust me sii rahisi kabisa kutazama upande wa pili ktk sura (shilingi) ile ile. Waswahili husema:- Nyani hucheka makalio ya mwenzake!...Lakini huyo nyani hata kama atapewa Kioo kujitazama bado sii rahisi kuamini kuwa matakalio yale ni yake.
Chadema wanahitaji mtu wa pembeni lakini yumo ndani kuweza kuyaona makalio ya pande zote... kazi hiyo naiweza sana!...
Huyo Strategist ndio akina nyie ambao mnakaa pembeni kusubiri kualikwa matanga ya Kifo cha CCM. Karibu sana na naanza kabisa kutanguliza kuomba msaada wako!
Ndugu yangu nakuomba soma vizuri mada hii kisha fikiria! kweli wewe na elimu yako unasubiri nani? nani kweli atakayeweza leta mabadiliko Tanzania ikiwa sii wewe, jirani yako, mshikaji wako na wote humu ambao nyote mnaona UHURU wa Watanzania umebebwa na baadhi ya watu wachache kama vile ndio halali ya urithi wao!
Nchi imerudi ktk kutawaliwa, na sidhani kama hapo ulipo unaweza nambia tofauti ya Utawala huu hasa baada ya Marehemu Mwl. Nyerere kufa na Ule wa Mkoloni kama sio tofauti za rangi za watawala....How can you sleep at night!
Mimi nachukua kadi tu sintagombea nafasi yoyote zaidi ya kufuata maelekezo ya wenye mji! Nitaweza kufahamu zaidi jitihada zinazofanyika kuliko kubeba mzigo wa dhana na kuchuma madhambi!...hali wananchi wazee na vijana wetu wanalia kama vile Darfur!.. Darfur iko bongo mjomba kama unayo huruma kweli basi shika jembe leo.
Unajua ktk safari yangu bara Tanzania, niliona watu ktk kila hali ya maisha na kuna wakati nilikaa na kujiuliza How can these people (leaders) go to sleep after their Up country Tour?
Yaani kuna watu maisha yao yamerudi miaka 40 nyuma!.. kuna mabanda ndugu yangu yamejengwa na makaratasi ya plasitic na watu wanalala humo tena vitongoji vya mijini. Vijiji vingi vimebaki vitupu watu wamekimbilia mijini ambako wizi na Ujambazi umekuwa sugu. Watoto wa kike wamelazimishwa kuuza miili yao kwa sababu ya kutafuta ada! ati msichana wa miaka 16 leo hii ni mama mzima anatakiwa kujitegemea.
Sasa ikiwa hawa wananchi wame - turn kuwa malaya , majambazi ni watu gani watakao kuwa hatarini kimaisha?. Jibu ni wenye nacho!.. na the first victim wa Ujambazi watakuja kuwa hawa viongozi wetu wamaolimbikiza mali kwani hakuna Jambazi atakaye taka kumuibia maskini.
Tazama South Afrika leo! kuna watu wanaujutia uhuru.. kwani leo hii maskini na matajiri wote hawana usingizi!.. soon hali hiyo itaingia Tanzania na kama sio sisi kuchukua muda wetu kuhakikisha hali hiyo haifikii basi mjomba hata pepo hutaweza kuiona. Mungu kakupa kipaji na elimu ambayo umegundua mapungufu yote haya lakini umeshindwa kutumia utume wako mdogo kuwasaidia maskini wanaokufa kila siku kwa njaa na malaria tu.
Tanzania sii nchi ya kutegemea mvua hata kidogo!...Tanzania sii nchi ya kukosa maji, Umeme wala kodi ya wananchi kufikia asilimia 15 hali makampuni ya kigeni (sio ya ndani) yanapata nafuu za kodi. Kibaya zaidi ni kwamba makampuni haya mengi hayazalishi kitu ndani ya nchi ila ni mawakala wa makampuni ya nje! - Tanzania ni sokoni! na kama mjuavyo soko halizalishi kitu zaidi ya ajira ambazo mishahara yake inalipwa kutokana na mauzo ya bidhaa yaani mfuko wa maskini mkulima.
Mimi sio Mjamaa kwa mrengo wa vita baridi bali mjamaa kwa imani ya kuwa UMOJA ni nguvu na Utengano ni udhaifu. Ukipanda juu usije wasahau wa chini lakini lazima mmoja apande! Na anayepanda juu awe na uhakika kuna watu chini wameshikilia ngazi!. WE all need each other!