Tanzania: Adui yetu ni nani na tuna fursa gani za kumshinda? Tunamlenga au tunamkwepa?

Kitila Mkumbo

JF-Expert Member
Feb 25, 2006
3,354
1,945
Unajua nimekuwa nikatafakari sana mashambulizi yetu hapa. Halafu yule mama Anne Malecela naye amenifanya nizame kwenye fikra zaidi.

Kwa kweli tumekuwa mahodari sana wa kuonesha matatizo yetu na wakati mwingine hata kupendekeza namna ya kumaliza matatizo yetu. Juzi pia wapinzani wamefungua ukurasa mpya kabisa wa siasa zetu kwa kuweza kuwakilisha sio tu bajeti mbadala kwa mara ya kwanza lakini kwa kuwakilisha bajeti yenye akili kuliko ile ya serikali ya CCM.

Hii imethibitika zaidi baada ya hata wataalamu wa kiuchumo nchini mwetu kuishauri serikali "kuiba" baadhi ya nondo zilizomo katika bajeti ya wapinzani. Of course mimi pendekezo langu lilikuwa radical zaidi; nilimshauri dada Zakia aachene na bajeti yake uchwara na badala abebe bajeti ya kaka Hamad na Zitto nzimanzima kama ilivyo. Hata hivyo najua wataendelea na bajeti yao hiyohiyo kimkandamkanda maana wanajua tutasahau na wataibua liskendo lingine la kutusaulisha hili li bajeti.

OK, where am I going? Kuzama kwangu katika fikra hizi kumenifikisha katika hitimisho hili: sote tupo katika campaign. Lakini bahati mbaya inaonekana tunafanya campaign isiyo! Campaign yeyote lazima itambue mambo manne muhimu: muathirika ni nani? adu ni nani? fursa ya kumshinda adui ni zipi? na tukishamshinda adui tunapata nini?

Kwa maoni yangu ni wazi kwamba sisi wananchi sote tu waathirika. Adui yetu mkuu ni CCM. Fursa pekee tuliyo nayo ya kumshinda huyu adui ni uchaguzi wa 2010. Wapinzani wameonesha kwamba wanaweza wakawa mbadala mzuri. Zaidi ya yote kumbe kule CCM kuna akina Anne ambao wanafikiri kama sisi. By the way tayari tunaye Mzee ES hapa; huyu kuasi sio vigumu na anaweza akatupa mikakati ya ndani ya kumtwanga adui CCM kwenye uchaguzi.

Hivyo basi kuanzia sasa tutumie muda mwingi zaidi katika namna ya kushawishi wananchi kuelewa umuhimu wa kuifukuza CCM madarakani katika uchaguzo ujao. Hili ndiyo jambo ambalo litushughulishe zaidi kuanzia sasa hadi uchaguzi ujao. Hata wenzetu wakenya waliweza kuishinda KANU baada ya kugundua kwamba KANU ndio alikuwa adui wao mkubwa kuliko kitu kingine chochote. Ndiyo hayo tunaona leo wakenya wanaanza kutembea kifua wazi na mabega juu kwa kujivunia ukenya wao.

Huu ndio wito wangu wa leo.
 
Baada ya uchaguzi wa mwaka 2005 mimi nilimwambia mtu mmoja niliyekuwa nabishana naye kuhusu ushindi wa CCM (wa 80%) na kutofurahishwa kwangu na matokeo hayo. Nikasema hivi kweli hawa watu walistahili ushindi wa landslide kama huo...? I was dissapointed, to tell you the truth.

Sidhani kama wapiga kura waliipigia kura CCM kwa uwingi namna hiyo baada ya kuchanganua na kuchambua sera, ahadi, na rekodi ya CCM. Nikamwambia huyu mtu kwamba CCM si chama kibaya, but all we need to do is kick it to the curb for a minute and give the opposition a chance (CHADEMA in this case).

After five years we will assess it's performance and if not satisfied we can kick it to the curb also and bring back CCM. By then, hopefully, CCM will have cleaned up it's act because they will know that we, the people do not play when it comes to the future of our country (A. Moshi has also reiterated this argument). I absolutely see nothing wrong with this because we are a democracy after all.

So I enthusiastically and wholeheartedly agree with you that our chief enemy is CCM and it needs to go. Long overdue...
 
Kitila,

Swali zuri sana hili. Lina vipengele vitatu na navijibu kama ifuatavyo. Nikipata msonge unipe cheti nikatundike ukutani kwangu na nikipata karai au chini yake, basi umezee na usiwaambie wengine.

(a) Adui yetu namba moja kabisa kwetu ni UJINGA wa raia wetu; mengine yote ni derivatives za ujinga huo.

(b) Fursa yetu kumshinda adui ni kutoa elimu thabiti ya uraia kwa lugha rahisi sana kutumia njia zinazopenya sana ili raia wetu waelelewe haki na wajibu wao katika kuchagua viongozi, makosa waliyofanya siku za nyuma, na jinsi makosa yao yalivyowatia katika ufukara mkubwa wakati viongozi waliowachagua wakineemeka.

(c) Hatumkwepi adui huyu ndiyo maana anaendelea kutusumbua ila hatujamlenga kabisa katika kumshambulia; tunashambulia madhara yake huyu tukimwacha mwenyewe. Ni kama vile tunashambulia harufu ya kinyesi kwa kupulizia air freshener bila kuzoa kinyesi chenyewe.
 
Kichuguu,
c) Hatumkwepi adui huyu ndiyo maana anaendelea kutusumbua ila hatujamlenga kabisa katika kumshambulia; tunashambulia madhara yake huyu tukimwacha mwenyewe. Ni kama vile tunashambulia harufu ya kinyesi kwa kupulizia air freshener bila kuzoa kinyesi chenyewe

Mzee wangu umenipiga bonge la golii
 
Kitila,


(a) Adui yetu namba moja kabisa kwetu ni UJINGA wa raia wetu; mengine yote ni derivatives za ujinga huo.

Kichuguu

Swala la kujiuliza je huo UJINGA wa raia chanzo chake ni nini?

Unajua Mwalimu (rip) alikuwa hana upeo handaki aliposema maadui watatu wa maendeleo ni UJINGA, MARADHI, UMASKINI

Ujinga wa raia umeletwa na Serikali ambayo kwa upande mmoja au mwingine hawataki kuona raia wanaondokana na ujinga huo kwani wakiondokana nao tu, watatumbua maradhi ni yapi na nini chanzo cha umaskini wao.

Jiulize kwa nini mara baadaya mwalimu kuachia madaraka Elimu ya Watu wazima ilikufa?

If CCM wants Tanzanias to develope, i can guarantee you they can do it, but they know as soon as people develope CCM is dead as no one will be interested in Political Parties. CCM needs the party to still taxpayers money.
 
Kichuguu

Swala la kujiuliza je huo UJINGA wa raia chanzo chake ni nini?

Unajua Mwalimu (rip) alikuwa hana upeo handaki aliposema maadui watatu wa maendeleo ni UJINGA, MARADHI, UMASKINI

Ujinga wa raia umeletwa na Serikali ambayo kwa upande mmoja au mwingine hawataki kuona raia wanaondokana na ujinga huo kwani wakiondokana nao tu, watatumbua maradhi ni yapi na nini chanzo cha umaskini wao.

Jiulize kwa nini mara baadaya mwalimu kuachia madaraka Elimu ya Watu wazima ilikufa?

If CCM wants Tanzanias to develope, i can guarantee you they can do it, but they know as soon as people develope CCM is dead as no one will be interested in Political Parties. CCM needs the party to still taxpayers money.

Mzee Aljazeera,

Vipi bwana, unasikika mara moja moja sana, usjifiche hivyo. Hata kunapokuwa hakuna mada nzito uwe angalu unajitokeza mara moja moja hata kwa kukohoa tu.

Kuhusu ujinga ni kwamba binadamu wote tunazaliwa nao; kwa hiyo chanzo cha ujinga wetu ni sawa kabisa na chanzo cha uhai wetu. Binadamu tunaanza kuachana na ujinga tunapoanza kupata elimu (iwe ya darasani au ya kurithi kutoka kwa wazazi wetu au ya kujifunza kutokana na kupambana na maisha yenyewe). Sasa tatizo la ujinga wa wanchi wetu siyo ujinga wa kukosa elimu ya darasani au ya kurithiswa, ni kukosa kutambua kuwa maisha wanayoishi sivyo wanavyotakiwa waishi, na mambo yanayofanywa na viongozi wao siyo yanayotakiwa yafanywe, na vile vile kwamba viongozi siyo miungu wa kuogogpwa ila wao ndio wanatakiwa kuwaogopa raia waliowaajiri.

Wakishakuwa na elimu ya aina hiyo, itawawia rahisi sana kuwanyofoa wagombea wasiofaa wakati wa ile intavyuu hata kama pilau imeliwa.

Ni kweli kabisa elimu ya darasani inasaidia sana kuwaondoa raia kwenye ujinga huo ambao ndiyo sumu yenyewe. Kwa vile serikali haitaki kutoa elimu hiyo kwa sababau ya maslaahi ya viongozi waliopo, ndiyo maana kuna haja ya kutafuta njia nyingine ya kuuelimisha umma. Bado nina mpango wa kwenda TZ kutoa elimu ya uraia wakati wa kampeini za 2010 ingawa mipango kamili haijakamilika. Ninashirikiana na jamaa wa polical science, na tumeshatafuta pesa za kukamilisha zoezi hilo kutoka foundations kadhaa lakini bado hatujapata majibu kamili.
 
Hivi nini tofauti ya CCM na CHADEMA? Labda rangi kwenye bendera zao.

Ukombozi wa Mtanzania utatokana na Watanzania wenyewe kuamka na kuacha kuchapa usingizi huku mali zao zinaibiwa.

Watu kama akina Mtikila ni nafuu mno kuliko hawa wanasiasa wengine. Wewe angalia Mashangingi wote wamekimbilia hakuna hata mbunge wa CHADEMA aliyesema huo ni wizi wa mali ya umma. Ruzuku wote wamo, kudai nyongeza ya mishahara, wote wamo. Sasa nyie mnategemea nini toka kwa wanasiasa kama hao?

Angalia ya Kenya, Malawi, Zambia, Congo nk.

Mabadiliko Tanzania yatakuja tu kama kutakuwa na mabadiliko makubwa kwenye katiba na sheria zetu. Hata tumchague nani katika wanasiasa waliopo bado watatumia katiba hiyo hiyo kuendelea kutuibia.

Afadhali brother Mtikila angalau ana uchungu na chi yetu.
 
Mzee Kichuguu

Mimi nipo nimejaa tele si unajua majukumu mengi.

Namalizia kuandika kitabu ili kitoke mwisho mwa mwaka kama siyo September.

Mzee kichuguu uliyosema ni kweli kabisa na kama utasoma andiko mojawapo la Mwalimu (rip) "The intelectual needs of the society" utaona kuwa tatizo letu ni "elimusiha" elimu maisha.

Nitarudi muda siyo mrefu ili kuendelea na uchambuzi.
 
Mzee Kitila,

Heshima yako mkuu, maneno mazito, isipokuwa tu naomba nirekebishe kitu kimoja, nimesema kitu hiki toka tukiwa BCS, kwamba mimi ni mwanachama wa CCM, lakini mimi ni open minded individual, na ninataka mabadiliko, tena mabadiliko ya kweli, ninaifahamu CCM nje ndani, na ninavifahamu vyama vya upinzani nje ndani, ndio maana nilishakata taamaa siku nyingi, ila nipo tu na kukata ishus hapa na kutafuta ugali, lakini matumaini hakuna!

Ndugu yangu, how CCM works, sio mchezo kama tunavyoongelea hapa, na ninasikia kulia ninapoona watu hapa wakifanya utani, ninawaona watu na viongozi wa upinzani hapa wakijidanganya, sasa hivi katika siasa ya bongo angalau Mrema knows how CCM works, wengine sidhani kama wanajua, I have seen enough, ndio maana huwa ninasema mabadiliko ya kweli, not in our life time, labda generation nyingine, Seif Hamadi knows how CCM works, ndio maana unaona siku hizi maneno ya ungunguri yamemuisha, kaputi!

Maneno yako ni mazuri sana na hopefully yanaweza kufanyiwa kazi, lakini ukumbuke kuwa hii forum kumejaa watapeli wengi wanaotafuta njia ya kuingia kwenye siasa ili nao wakale, ninaweza kukutajia mmoja baada ya mwingine, ambao ni maneno mengi hapa kumbe ni mafisi wakubwa, na ndio watakao kuwa wa kwanza kukuchoma kwa authority ukianza tu something, ninasema hivyo kwa sababu mimi wananichongea kila siku, lakini ninazipata copy zao kama zilivyo, ndivyo wabongo tulivyo, sasa kama nisingekuwa mimi by now ningekuwa tayari wameshanifunga mdomo au wamenitia matatani, kwa hiyo ndugu yangu Kitila, sitaki kukudanganya, utakuwa on your own na ninakutakia mafanikio, ila mimi sinunuliki, ninasimamia ukweli na haki kwa taifa langu, na mimi sio mnazi kama wa Yanga na Simba, ubingwa tu wa EAC hawauwezi, lakini maneno mengiiiii mtaani, yaani hata kiongozi wangu ameiba wake za wananchi, mimi ninashangilia tuuuu kuwa eti kala uroda! Mwenyekiti wangu anakopa hela NSSF, kama kina Sumaye, Mkapa, na Idrisa, mimi ninashangilia tuuuu eti ni mambo ya binafsi hayo, kulikoni?

Hapana, mimi ninasimamia taifa langu I do not care nani amevuruga, ninamkoma nyani hapa hapa hadharani, Lakini amneno yako ni msumari na ninakutakia mafanikio bro!
 
Adui wetu mkubwa ni CCM na viongozi wake. Nasema hivi kwa sababu viongozi wa CCM na ambao pia ndio viongozi wa Tanzania wamekuwa ni waongo wakubwa katika kutetea maslahi ya chama chao. Kinachoniudhi zaidi ni kwamba wameipa CCM kipaumbele kuliko hata nchi yao!!! Wanajua mabaya mengi yanayotendeka ndani ya nchi yetu, lakini wabunge na viongozi mbali mbali wa juu ndani ya CCM wanayafumbia macho ili kuhakikisha wanaendelea kuwa madarakani milele.

Hivi kweli wabunge wa CCM ambao ndio wengi bungeni kama wana mapenzi ya kweli na Tanzania wakaamua kusimama kidete ili mikataba ya uchimbaji madini ipelekwe bungeni ili ikaangaliwe na kujadiliwa au bajeti haipiti mikataba hiyo kweli itaendelea kufichwa?

Pia vyama vya upinzani ni adui wetu wa pili. Nasema hivi kwa sababu ubinafsi wa viongozi wa vyama hivyo, kwa kuogopa kuunda chama kimoja chenye nguvu ambacho kitakuwa na nguvu kubwa na wafuasi wengi ambao wanaweza kuhakikisha kwamba kinapata viti vingi bungeni. Viongozi hawa pamoja na kufanya vibaya katika chaguzi za vyama vingi kila kukicha hawaelekei kuwa na mikakati yoyote ya kuangalia wapi wamekosea na nini kifanyike ili wajiimarishe kupambana na CCM.

Kwa maoni yangu cha kwanza ni kuungana ili kuunda chama chenye nguvu. Pili ni kujitangaza katika wilaya zote za Tanzania na pia kutangaza sera za chama na kuwasikiliza wananchi wana maoni gani, malalamiko yao ni yapi.

Lakini hizi njemba utazisikia ikiwa imebaki miezi 15 kabla ya uchaguzi mkuu na wakisha shindwa wanaingia mitini mpaka karibu na uchaguzi mwingine!!! Hawana mikakati yoyote. Wao wanataka tu kuingia Ikulu. Kumbe wangeweka kipaumbele katika kupata viti vingi bungeni ili wananchi waone sera na utendaji wao na kuwaamini hatimaye wananchi kuamua kuwaondoa CCM madarakani, lakini wapi ubinafsi wameweka mbele kuliko mapenzi ya kweli kwa nchi yao!!! Inasikitisha sana!
 
Mzee ES:

Ningependa kukuelimisha kuwa tunao adui wakubwa wawili nao MOJA CCM na viongozi wake, PILI ujinga wa raia.

Ni lazima uelewe kuwa CCM haitatoka madarakani kwa hiari yake!..itafanya kila namna kuhakikisha kuwa inabaki madarakani.Siyo siri katika mpambano huu kuwa wengi wataanguka na hili ndiyo kundi la watu kama akina MREMA na SEIFU. Lakini cha kutia moyo ni kwamba historia inatuelimisha vizuri kabisa kuwa mapinduzi huwa hayaanzii juu bali huanzia chini kutoka kwa wananchi ambao mara nyingi ndiyo waadhirika. Hivyo wananchi wanapoanza kuamka hakuna atakezuia hilo.

Hivyo unaposema kuwa watu kama akina KITILA waangalie sana ninakushangaa..kwa kuwa huu moto ulioanza hapa JF hautaishia kwenye mtandao tu..unakuwa na utawafikia wananchi vilivyo. Nafikiri unaweza kukumbuka jinsi vuguvugu la vyama vingi lilipoanza pale UDSM..kipindi kile cha akina Mabere Marando na akina Chachage! ilikuwa hivi hivi kwamba raia walizoeshwa chama kimoja na hakuna vyama vingine nalo sote tumeliona kuwa limekuwa hadithi ya zamani sasa.

Tatizo kuu la pili ambalo ni ujinga wa raia nalo si jipya kihistoria. Wananchi huhitaji watu wachache tu kuwafumbua macho baada ya hapo huwa ni hadithi nyingine. CCM kwa muda mwingi imewaimbia wananchi wimbo wa umasikini na kuwafanya wananchi waamini kuwa umasikini ni moja ya sehemu yao ya maisha wakati si hivyo.

CCM imewatangazia wananchi (kupitia IPPMEDIA) kuwa kuchagua chama kingine ni kuleta vita vya wenyewe kwa wenyewe..they are wrong! mfano mzuri ni kule pemba ambako hata wauza vitumbua wanajua vilivyo kuwa umasikini wao umeletwa na viongozi sio wao wenyewe.

Hivyo basi wanaJF,ili kushinda adui hawa niliowataja hapo juu ni lazima cheche hizi zinazowaka humu ndani zitoke na ziwafikie watanzania kuanzia makete hadi ukerewe na kuendelea magharibi hadi mashariki.

Bila ya kuwa na chombo cha habari kama redio hatutaweza kufika popote. Hata yule mwanamapinduzi Fidelis Castro alielewa vizuri kuwa mapinduzi yake ya watu 21 tu yasingeweza kufika popote bila ya kutumia redio kama silaha yake. Cha kushangaza wapinzani wote Tanzania wamelipuuzia hilo na sasa wanaonekana kuanguka kabisa. Wapinzani wote wanategemea IPPMEDIA na mikutano ya hadhara kufikisha ujumbe hii ni sumu..na kamwe hawataweza kuwaelimisha wananchi ipasavyo. Na ukitaka ujue kuwa redio siyo mchezo angalia CCM walivyoweka ukiritimba wa kurusha frequencies kutoka kwenye private redio.

Hivyo chondechonde wanaJF ni lazima tuelewe kuwa wananchi wengi hasa wa vijijini husikiliza redio kuliko kusoma magazeti kwa hivyo basi hiyo iwe silaha yetu namba moja ya kuwafumbua macho, kuelimisha na kufikisha ujumbe.
 
Mzee ES:

Ningependa kukuelimisha kuwa tunao adui wakubwa wawili nao MOJA CCM na viongozi wake, PILI ujinga wa raia.

Wembemkali usinikate tafadhali,

Nafiikri uflip hiyo order ya maadui hao wawili: kwanza ni ujinga halafu ndiyo CCM; wako kama kuku na yai, complete circle. Kinachowaweka CCM madarakani ni ujinga wa raia siyo kwamba kuwapo kwa CCM madarakani ndiko kunakosababisha raia kiuwa wajinga. Ukibomoa ujinga huo utakuwa ama umewaondoa CCM madarakani au utaiacha CCM madarakani huku ikiwajibika zaidi.
 
Mzee Es

Maneno uliyosema ni ukweli mtupu, kwa jinsi CCM ilivyojipanga kuiondoa madarakani ni ngumu sana kwa sasa, tusikate tamaa tuendelee kupigania taifa letu kwa manufaa ya vizazi vijavyo sisi tumeshachelewa.

kichuguu, umenena kuwa adui mkubwa ni ujinga, ukitaka kujua vita hivi kuwa ni vigumu, tokea tupate uhuru tunapambana na hayu adui lakini mafanikio yake ni adimu, tujipange upya tuje na mkakati wa kupambana na ujinga na hofu
 
Mzee ES,

Umeongea ukweli mtupu ambao baadhi ya watu hapa hawataki kuelewa. Vyama vingi sio jawabu kama watu wetu wengi ndio hao waliojaaa tamaa na ubinafsi.

Tuna viongozi wa upinzani bungeni, je wamefanya nini kilicho tofauti na wanavyofanya wabunge wa CCM? Wote wanalilia marupurupu huku wananchi wanakufa kwa umaskini wa ajabu kwenye majimbo yao.

Kwa mwendo huu CCM itaongoza milele.

Mtikila anapambana mahakamani peke yake, hao wanasiasa wa upinzani wamekaa kimya badala yake wanamrushia madongo.

Mnasema raia ni wajinga, sawa huenda kuna ukweli lakini sio kwa asilimia kubwa. Angalia mfano wa Mrema, alifanya mambo ambayo wananchi waliona yalikuwa mazuri na mpaka leo wananchi hao hao hawajamsahau. Kama wangelikuwa wajinga, pamoja na propaganda za CCM mrema leo asingeliweza kupita mitaani. Lakini hata leo Mrema akiwa na tatizo watanzania hao hao maskini watamchangia na kumsaidia. Hii ni ishara kwamba wanajua pale viongozi wanapotenda mema. Matatizo ya Mrema yalikuwa tamaa ya kuwa rais
lakini angelikuwa mjanja kidogo basi leo CCM wasingelikuwa madarakani.

Kitila, jitahidi maliza shule na kaibadili CHADEMA maana hii iliyopo sahau kwamba itachukua madaraka.
 
Mtanzania,

Huo ushauri ni mzuri sana kwa Kitila, lakini una uhakika yumo katika kundi la wateule?
 
Mzee Wembemkali,

Heshima mbele kaka, I have an idea wewe ni nani tayari, lakini siioni elimu uliyosema utanipa kwenye hiyo post yako, kwani yote uliyoyasema ninayajua tayari na nimeshawahi kuyasema na hasa kuhusu wananchi wajinga, nimeshasema mara nyingi kuwa wananchi wa Kenya wana afadhali kuliko sisi kwa kuwa na uwezo mkubwa wa kuelewa siasa ya nchi yao, as opposed na sisi wabongo tunavyoelewa siasa ya nchi yetu,

Post yako imerudia tu niliyoyasema, kuwa tatizo letu kubwa hapa forum ni kuwa kumejaa wananchi wajinga, mafisi na watapeli wa siasa, CCM sio tatizo, tatizo ni sisi wananchi wajinga na tunaanzia kwenye hii forum. Pamoja na kusoma kote kwa wabongo, bado haijatusaidia kitu, na hapa forum ndio hasa mfano wenyewe, nimemuambia Mzee Kitila kuwa maneno yake ni msumari lakini atakuwa on his own when the time come, maana we are not ready.

Maneno ya Mzee Mtanzania, yanamaliza maneno yangu yote, kuwa labda Mzee Kitila, arudi kuisadia Chadema na kuifumua nje ndani, kuhusu Pemba hata wao ueleo wao wa siasa sio solid kama unavyotaka tuamini hapa, wao ni matatizo yao ya kihistoria yanayolalia kwenye dini, na rangi, maana huwezi kuniambia kuwa ni wananchi werevu wa siasa wanaodai kuwa CCM iondoke ili arudi Sultani wa Oman,

Otherwise nimekuskia mkuu, isipokuwa ningekuomba uifuatilie kwa makini CCM ili uijue how it works, halafu usisahau kuwa CCM ipo kila kona ya bongo as opposed na upinzani ambao uko mijini tu, CCM haitegemei radio bro, wao huenda mpaka huko vijijini kupiga domo, wananchi wa Tunduru walikuwa hawamtaki kabisaaa marehemu Akukweti na CCM ilikuwa inajua wazi, kwa hiyo baada ya kufariki kwake ungetegemea kuwa wanachi wangempa jamaa wa upinzani, NO! sasa ilikuwaje CCM ikashinda wakati upinzani wote walikuwepo pale, maana kwenye uchaguzi mkuu huwa tunaelewa kuwa ni vigumu kuishinda CCM, maana upinzani wanakuwa kwenye majimbo tofauti, lakini this time wote walikuwepo kule Tunduru, CCM ilitumia uchawi gani kuwafanya wananchi waichague? Iliwatumia hao hao viongozi wa upinzani waliokuwa wamejazana kule Tunduru!

anyway nimechoka bro, Mungu Aibariki Bongo!
 
Wajemeni nimewasoma sana, na ninaendelea kutafakari. Kichuguu, Mzee Es, Aljeezera (nawe unapotea sana bwana, ah), Babu, Wembali, Mtanzania, na wengine wote maneno hayo ni mazito sana.

Napata mambo matatu yanayojitokeza katika michango iliyokwishatolewa mpaka sasa:

i) Kichuguu anasema kwamba adui mkubwa sio CCM, bali ni ujinga. Labda ni kweli. Lakini kwa mtanzao wangu naona kwamba CCM ndiye aliye adui hasa na anatumia ujinga kama silaha tu ya kuweza kututawala. Sasa swala hapa ni kuangalia kipi tuanze nacho: kumpiga adui CCM moja kwa moja au tumnyang'anye kwanza hiyo silaha aliyo nayo yaani ujinga. Kwa maoni yangu yote yanawezekana kufanyika kwa pamoja, lakini nahisi kwamba kumpiga adui CCM ni jambo la haraka zaidi na linaua ndege wawili kwa jiwe moja

ii) Kuna hoja kwamba kuitoa CCM madarakani sio rahisi; hii ni kweli kabisa. Lakini nani amesema kwamba kazi za harakati huwa ni rahisi? Hivi sisi hapa tupo kufanya mambo marahisi? Jamani mambo makubwa na mazuri hayajawahi kuwa rahisi. Sisi hatukusoma na kutembea kote huku ili tuje tufanye mambo marahisi. Kila mtu anaweza kufanya mambo rahisi. Watu wote waliopata mafanikio duniani hawakupata mafanikio kwa kufanya mambo rahisi. Naomba wale wanaotoa hii sababu waachane nayo. Tunajua kwamba kuitoa CCM madarakani ni kazi ngumu na ndio maana tunataka kuifanya. hatupo hapa kufanya kazi rahisi. Everybody can accomplish an easy task. We are here to make a difference by accomplishing a very difficult mission-removing CCM from power by the power of people

iii) Mzee ES, naheshimu na ninakubaliana nawe kuhusu matatizo yaliyopo upinzani. Nakubali kabisa kwamba baadhi ya viongozi wa upinzani wanafanya yaleyale wanaoanya viongozi wa CCM. Labda nirudie kusema hapa kuwa hakuna anayesema kuwa viongozi wa upinzani ni malaika, na kwamba hawajawahi na hawatakuja kufanya makosa. Wala hakuna anayesema viongozi wote walipo CCM ni wabovu au wameoza. No, far from it. Tunachopambana nacho hapa ni mfumo, na sio kiongozi moja moja. Hata kama Lipumba angekamata urais leo kupitia CCM nisingetarajia miujiza yeyote.

Tunachosema hapa ni kuwa CCM ni pori zito na giza tororo, yeyote aingiapo humo hupotea asijue pakwenda. Nafikri mmemsikiliza Mbunge Seleli jana ameongea kwa uchungu lakini mwisho anasema "naunga mkono bajeti hii lakini ninahumia roho sana"! Hii inakuonesha jinsi ambavyo sio rahisi tena kuleta mabadiliko kupitia hiki chama. So, all we are saying lets start afresh with the leadership system, not necessarily individuals. Cha msingi ni kuwapa wananchi hope kwamba wanaweza kubadilisha viongozi wao pale wanapoona wamekosea. Sasa hivi ilivyo ni kama vile CCM ni mornachy fulani, there to stay whether wamevurunda au la!
 
Mzee Kitila Mkumbo, heshima yako Mkuu.

Napenda kutofautiana na wewe kidogo. Binafsi nadhani kinachoiweka nchi yetu katika ukingo wa shimo la giza, sio CCM, bali ni watu wanaojiita CCM. Hivyo, yatupasa kuwa makini, ama sivyo tutaishia kwenye bottomless pit of oblivion. Ukiiondoa CCM, alafu watu wanaojiita CCM wakabaki madarakani, matatizo yetu yatabaki palepale. Hii mantiki katika hesabu inaitwa commutative law of addition and multiplication. Switching the order of any two numbers being added or multiplied together, does not change the result.

Nathubutu kusema kuwa vyama vya upinzani vya Tanzania vina mkosi. Miaka 50 iliyopita, Ghana ililikuwa nchi ya kwanza katika Afrika kupata uhuru. Hakika Kwame Nkurumah alifurahia sana siku hiyo. Alikaliliwa akisema kuwa, "kwa mara ya kwanza, sisi waafrika tumepata nafasi ya kujiamulia mambo yetu wenyewe". Hakuna shaka kwamba uhuru wa Ghana ulihamasisha wananchi wengi wa bara la Afrika. Kumbuka, wakati ule, wananchi wengi hawakuwa na elimu ya uraia, na pia walikuwa hawajasoma. Lakini wakoloni walikiona cha mtema kuni.

Bila shaka, maneno ya Nkurumah yaliingia doa, kwani toka wakati wa ukoloni, mpaka leo hii, wananchi wa Afrika hawajawahi kupata nafasi ya kujiamulia mambo yao wenyewe. Maamuzi ya mambo ya Afrika yamekuwa yakifanywa na makundi ya watu wachache. Kwa baadhi ya viongozi, na tena mara chache, baadhi ya maamuzi, wakati mwingine yamekuwa kwa manufaa ya wananchi, wakati mwingine kwa manufaa ya wachache (mfano;Tanzania). Na kwa viongozi wa mapinduzi ya Afrika waliowengi, maamuzi yote yalikuwa yakifanywa na makundi ya watu wachache kwa manufaa ya wachache (mfano;Zaire).

Vita baridi kati ya Marekani na Urusi, ilichangia kuchafua hewa katika bara la Afrika. Lakini ukweli ni kuwa viongozi wengi wa mapinduzi katika Afrika waliwaacha wananchi kwenye mataa. Wananchi walishiriki kikamilifu katika kudai uhuru wa nchi zao. Bila wananchi kujitoa muhanga, hakuna hata nchi moja ya Afrika ambayo ingepata uhuru. Baada ya walijitambua kuwa viongozi katika hizo harakati kushika kushika hatamu, wakawageuka wananchi kwa kuwanyima uwezo wa kujiamulia mambo yao wenyewe. Viongozi wengi wa mapinduzi, wamechukuwa roho za wananchi wengi waliotaka kudai hiyo haki yao ya msingi (mfano; Uganda -Obote, Malawi-Kamuzu).

Kutokana na msukumo wa ndani na nje ya nchi, Afrika ikashuhudia upepo mwingine mnamo miaka ya tisini. Huu upepo ni wa viongozi wetu wa mageuzi (mfano; Mapalala, Fundikira, Kasanga Tumbo-Tanzania, Chiluba-Zambia, Abdoulaye Wade-Senegal, Bakili Muluzi-Malawi). Wachambuzi wa mambo ya siasa walidiriki kuita haya mageuzi kuwa ni "wind of change". Nadhani walitumaini kuwa historia ingejirudia. Ghana ilivyowahamasisha wananchi wa Afrika kudai uhuru, basi hata chama kimojawapo cha upinzani kikichukuwa madaraka, wananchi wa nchi nyingine wangeiga mfano.

Ndio maana nasema kuwa, labda vyama vya upinzani vya Tanzania vina mkosi. Kwasababu vyama vya upinzani vya nchi nyingine vilivyotangulia kupata madaraka, vimevurunda. Vimefanya kosa lilelile kama walilofanya viongozi wetu wa mapinduzi (akina Nkurumah). Kama ilivyokuwa wakati wa kudai uhuru, wananchi wa hizi nchi walishiriki kikamilifu kuviangusha vyama vilivyoziletea hizo nchi uhuru. (Mfano;Ghana, Senegal, Kenya, Malawi, Zambia). Again, bila wananchi wa hizi nchi kujitoa muhanga, hawa viongozi wa vyama vya upinzani (mageuzi), wasingefika kokote. Lakini waliposhika hatamu, wamewapiga teke wananchi. Wamewanyima nafasi ya kujiamulia mambo yao wenyewe.

Viongozi wa mageuzi wa Tanzania walitamba sana Chiluba aliposhika madaraka. Waliwambia CCM kuwa mwenzio akinyolewa, wewe tia maji. Muda ulivyokwenda, majigambo ya Viongozi wa mageuzi kufifia. Mwishowe, Zambia ikaondolewa kwenye orodha ya nchi za kuigwa. Malawi je? (Akha!) Senegal je? (hao ndio wameluka mkojo na kuanguka kwenye kinyesi). Ghana je? (wanafanana na wanaCCM). Tulitaka kuunganisha vyama tuwe kama Kenya. Lakini siku zinavyozidi kuyoyoma, naona wazo hili linapigwa kaputi.

Satili za kuvurunda katika Afrika zinafanana. Mfano, nchini Kenya, hakukuwa na kitu kinaitwa KANU. Kulikuwepo na watu waliojiita KANU. Katika ule mkumbo wa kuing'oa KANU madarakani, hata wale waliojiita KANU walikuwemo. Matokeo yake, KANU ikang'olewa, lakini wale waliojiita KANu bado wako madarakani. Ndio haohao wanaowafanyia unyama wananchi wa Kenya. Mzee Kitila Mkumbo, wanaotembea kifua mbele sio wananchi wote wa Kenya, bali ni wale walioko madarakani. Ndio maana inakuwa ngumu kwa vyama vya upinzani Tanzania kutoa takwimu za Kenya, Zambia, Senegal ambazo zinaonyesha mabadiliko ya maana ya kile walichokuwa wanapigania kabla ya kuingia madarakani.

Hivyo, vyama vya upinzani Tanzania vimekuwa kama watoto wakiwa. Huu mkosi kwa vyama vyetu vya Tanzania, ni mbaya kwa vyama vyenyewe, unaineemesha CCM, lakini yawezekana ni ishara njema kwa wananchi wa Tanzania. Ni ishara njema kwa maana kuwa, vyama vya upinzani vya nchi yetu vinapata changamoto ya kuangalia hivi vyama vyote vimevurunda wapi? Bima pekee ya kuondoa huu mkosi ni kuruhusu mawazo mapya yapenye, fikra zirutubishwe na fikra nyingine, badala ya kuziacha zikavia na kuzaa watoto taahira kutokana na kujamiiana kwa muda mrefu baina ya fikra zilezile.

Hizi tabia mfu za vyama vya siasa (vyote), kujifanya kuwa wanajua matatizo ya wananchi kuzidi wananchi wenyewe wanavyoyajua zizikwe. Hakuna mbadala wa maoni ya wananchi na utashi wao. Viongozi wote wa vyama vya siasa wanawajibika kuwasikiliza wananchi wanasema nini na kuyatilia maanani hayo yasemwayo na wananchi. Haya mambo ya kungoja siku za uchaguzi na kwenda kuwahutubia wananchi yafe. Tukifanya hivyo, basi tukubali matokeo yake.

Tusiwaite wananchi wajinga eti kwa sababu wameshindwa kutuelewa tulichowaambia na kutuchagua. Tusiwaone wajinga ati kwasababu wanaona CCM wanafanya ulafi na wizi wa mchana, lakini wanashindwa kuwaondoa. Labda kila mtu ana maana tofauti ya ujinga. Kama wananchi wa kizazi hiki ni wajinga, je wale waliomng'oa mkoloni walikuwa na welevu upi? walisoma shule gani wale? Lakini wananchi wa leo wakiwa welevu wakaiondoa CCM wamuweke nani? Na kwa bima ipi?

Tujifunze kukubali matokeo ya matendo yetu. Tusiseme tumeibiwa kura. Unaweza kuwaongopea watu wote kadili unavyotaka. Lakini ukianza kumuongopea "the man in the mirror", unatafuta kiama chako. Conscience is like an open sore, only the truth can heal it. Kama unaweza kuibiwa kura milioni nane na ushee, basi hufai kuongoza nchi. Aliyekuibia hafai, lakini hata wewe hufai. Manake ukipewa nchi itaibiwa kwa ujumla wake.

Mwisho ningependa kuwagawa wananchi wetu katika mafungu ili kujua tatizo liko wapi. Kwasababu ukisema wananchi ni wajinga, ina maana kila mtu Tanzania ni mjinga? Siamini hivyo. Kundi la kwanza ni la Wakulima (90% ya watanzania wote) ni wapenzi wa nchi yao. Lakini mapenzi kwa nchi yao yamechanganyikana na unyonge. Ujinga sio unyonge. Kundi la pili ni la Wabunge (vyama vyote) pamoja na vyama vyao vya siasa. Hili kundi sio wote, lakini wengi wao wanaendekeza mambo ya kipuuzi. Kundi la tatu ni la viongozi (wote). Hawa wanaendekeza mambo ya kipumbavu. Kundi la nne ni la wasomi, na wale ambao bado wanasoma, hata "born town". Hawa ni wajuvi, na wanaendekeza mambo ya ushabiki.

Tukishajigawia vitengo na kujua nafasi zetu katika jamii. Itakuwa rahisi sana kutabiri nini kitatokea mwaka 2010. Note: makundi niliyoyaweka juu simaanishi watu wote wako hivyo. Naongelea kwa ujumla wake.

 
Tusiwaite wananchi wajinga eti kwa sababu wameshindwa kutuelewa tulichowaambia na kutuchagua. Tusiwaone wajinga ati kwasababu wanaona CCM wanafanya ulafi na wizi wa mchana, lakini wanashindwa kuwaondoa. Labda kila mtu ana maana tofauti ya ujinga. Kama wananchi wa kizazi hiki ni wajinga, je wale waliomng'oa mkoloni walikuwa na welevu upi? walisoma shule gani wale? Lakini wananchi wa leo wakiwa welevu wakaiondoa CCM wamuweke nani? Na kwa bima ipi?

Tujifunze kukubali matokeo ya matendo yetu. Tusiseme tumeibiwa kura. Unaweza kuwaongopea watu wote kadili unavyotaka. Lakini ukianza kumuongopea "the man in the mirror", unatafuta kiama chako. Conscience is like an open sore, only the truth can heal it. Kama unaweza kuibiwa kura milioni nane na ushee, basi hufai kuongoza nchi. Aliyekuibia hafai, lakini hata wewe hufai. Manake ukipewa nchi itaibiwa kwa ujumla wake.

Kyoma,

Maneno yako yana worth to be written in goldish ink nakubaliana na wewe kabisa 100%

Mimi ni miongoni mwa wale wanaosononeshwa na mambo yanavyokwenda ndani ya CCM, lakini kwa upande mwingine na struggle kuona best alternative of CCM. Najua nina jukumu mimi mwenyewe kushiriki badala ya kuwa mtazamaji tatizo ni wewe should we start? na hili ndio swali langu kwako Mr Kyoma.

Analysis yako ni nzuri sana, na summary ya uliyoyasema ni CCM kuna matatizo, upinzani bado haujaonyesha utayari wa kushika madaraka ( vina mkosi). Je what should be done now? should we leave CCM to rule 4 an indefinately period? or should we try opposition? ambao wanaweza kuibiwa easily kura mil 8.
 
Kwa maoni yangu ukiondoa CCM kama kweli hili linawezekana, basi mapenzi ya viongozi kwa nchi yao yanaweza kurudi angalau kwa kiasi fulani na badala ya kuweka kipaumbele kwa kuilinda CCM iliyowafikisha hapo walipo, labda watatoa kipaumbele kwa Tanzania.
 
Back
Top Bottom