Tanzania: Adui yetu ni nani na tuna fursa gani za kumshinda? Tunamlenga au tunamkwepa?

Mzee Kyoma, kama kawaida maneno yako ni mazito na mshale unaochoma.

Hata hivyo nasita kukabaliana na wewe kuhusu upinzani. Wazo uliloibua ndio wazo ambalo limekuwa likiwatofautisha Shivji na Baregu. Shivji yeye haamini kabisa katika vyama vya siasa, anataka wananchi ndio washike hatamu. Na huwa ana-argue in a very intelllectually convincing way as you may know him, lakini ukimuuliza watashika hatamu vipi bila kupitia vyombo vyenye uhalali wa kisheria, hakupi jibu. Msimamo wa Baregu ni kwamba hatuna njia ingine ya kuwakomboa hawa wananchi wetu na mfumo uliopo zaidi ya kupitia katika taasisi zilizopo za kisiasa zikiongozwa na vyama vya upinzani. Mimi nakubaliana na msimamo wa Baregu.

Ninachokipata katika ujumbe wako Kyoma ni kuwa wewe unataka ideal situation, ambayo kwa kweli haipo. Ndio sote tunataka ushindi wa wananchi, lakini ushindi huu hauwezi kupatikana bila kuwa na majemedari wa mapambano. Mimi naamni katika mapambano haya ya kisiasa majemadari wetu ni vyama vya siasa vya upinzani. Labda wewe unipe mbadala, in the absence of vyama vya siasa, ni namna gani tunaweza kuwapatia hawa wananchi huo ushindi ambao tunaongelea. Tatizo linalotukumba Tanzania ni watu wengi wenye mwanga na wasomi kama wewe kukosa ujasiri wa kujiunga na vyama vya upinzani. Tumekuwa hodari wa kuhukumu tukiwa pembeni as if hivi vyama vya upinzani ni duka au shamba la mtu fulani. Inabidi tubadilike na tujue kwamba vyama vya upinzani sio mali za watu wachache, hizi ni taasisi za kijamii na vyombo mojawapo vya kuongoza mapambano katika mabadiliko tunayoyataka. Kwa mfumo wetu waa siasa na sheria tulizonazo hatuna uwanja mwingine wa mapambano nje ya vyama vya siasa. Mimi naamini kabisa kwa mujibu wa mfumo wetu wa kisiasa, kujaribu kupambana nje ya vyama vya siasa ni njia rahisi ya kukwepa mapambano!

Mwisho, naomba nitofautiane nawe sana kuhusu mafanikio ya vyama vya upinzani vilivyoshinda katika nchi zingine nchi Afrika. nafikiri umeingia katika mtego wa propaganda za CCM za kusema kwamba vyama vya upinzani vilivyoshinda katika nchi zingine havikuleta mafanikio yeyote. Hii sio kweli kwa nchi zote. Mfano wa karibu ni wa majirani zetu Kenya. Tangu KANU ifukuzwe madarakani mabadiliko mengi yamepatikana yakiwemo: kutoa elimu ya msingi bure (nasi tukawaiga), kuanzia mwakani wanaanza kutoa elimu ya sekondari bure. uchumi wao umekuwa mara mbili, wameweza kupunguza idadi ya watu maskini kwa 20%. Soma tena bajeti za Kenya na Tanzania za mwaka huu. Bajeti ya Kenya inatokana na vyanzo vya ndani kwa 95% na wanategemea misaada ya wazungu kwa 5% pekee. Sisi, tunajitegemea kwa 58% tu na tutawapigia magoti wazungu kwa 42% (note: mwaka jana ilikuwa 40%!). Kikubwa zaidi, kwa kuitoa KANU, wananchi wa Kenya walipata nguvu za ajabu; sasa wanajua kuwa wana uwezo wa kuitoa serikali madarakani kwa njia ya uchaguzi wakati wowote wakitaka. Huu kwangu ndio ushindi wa maana kuliko mwingine wowote unaoweza kuufikiria, power to people, ndiyo hayo uliyotupa mfano wa Califiornia.

Ndio NARC hawajafanikiwa kuleta mabadiliko ya katiba kama walivyoaidi. Lakini tusisahau kwamba angalau walipeleka mapendekezo ya katiba kwa wananchi na wananchi wakayakataa. Na huu ndio msingi wangu wa kusema kuwa wakenya sasa wanatembea kifua mbele. They now know they have power over their government. They know they can say no to government if they want to. Sisi je? Ni kujidanganya sana kufikiri wananchi wa Tanzania wana nguvu za kisisasa kushinda Kenya. Hakuna kitu kama hicho. Mabadiliko yaliyotokea Kenya baada ya KANU kuondoka madarakani ni makubwa mno na yanapaswa kututia moyo na wala siyo kutukatisha tamaa.

Sitaki kuingia kwa undani katika nchi zingine. Lakini fuatilia kwa makini tena ujue mabadiliko yaliyopatikana nchini Senegal baada ya Wade kushinda. Fuatilia pia Ghana baada ya Kufour,utagundua kwamba things have changed drastically for better.
 
Watanzania sio 'WAJINGA."

Wanaotoa mfano wa wananchi wa kenya kuwa wanaouelewa mzuri wa siasa kuliko waTanzania wanasahau siasa za kikabila wanazozitumia viongozi wa nchi hiyo.

Kama leo Raila Odinga (Luo), ataungana na Ruto (Kalenjin), Mudavadi (Luhya),
Musyoka (Akamba), Balala (Mijikenda) n.k. Kibaki atapata wakati mgumu sana, na sizani kama atachaguliwa pamoja na kuandaa marupurupu (rushwa) mengi ya kuwagawia jamii mbalimbali wakati wa uchaguzi ujao.

Hapa kwetu, ni CUF tu kidogo ndio walioweza kuhamasisha sehemu ndogo ya raia kwa misingi ya kidini wakati wa chaguzi za mwanzo baada ya vyama vingi kuanzishwa. Mbinu hiyo nayo imezamishwa kifundi kabisa na CCM katika uchaguziiuliopita (2005). Watu hatupendi au tunaogopa kuyazungumzia mambo haya. Hebu jaribu kufikiria kwa makini ni vipi CUF walishindwa kupata hata kiti kimoja cha ubunge bara? Au fikiria kama mteuliwa wa kugombea kiti cha urais angekuwa kwa mfano ni Mwandosya!

Sikubaliani na siasa za kimakundi ya kikabila au kidini, lakini kama zipo au ndizo zinazochangia katika mabadiliko ya kisiasa, tusijifanye hatuzijui.
 
adui yetu mkuu ni sisi wenyewe, hatujielewi, hatujui nini tunataka, na tunapojua hatujui vipi tukipate tukitakacho.
 
Kyomo

Good points bravo.

Nakumbuka baada ya vita ya Uganda Mwalimu Nyerere (RIP) alimualika rais wa Mozambique hayati Samora Machel (RIP) kuja Tanzania na kuongea na wanachi pale Uwanja wa Taifa kama sikosei. Alisema nani wanaofanya magendo na kuficha bidhaa na kuwalangua wanachi ni shangazi zetu, wajomba, baba, mama, kaka na dada zetu. Ni watu ambao tunao (Kikulacho ki nguoni mwako).

WTZ sio wajinga kama wanabodi wengi hapa jinsi walivyo fafanua. Kyomo katoa mfano mzuri sana kuhusu kupigania uhuru. Tatizo kubwa CCM (TANU na ASP) ndio chama cha kwanza kuwatatulia matatizo wabongo na kila mmoja wetu wakati fulani alikuwa CCM. Mtakumbuka hapo nyuma kila unachotaka kufanya ilikuwa lazima uonyeshe kuwa wewe ni CCM damu nakumbuka wengi walipata pasi za kusafiria baada ya kuonyesha kadi za CCM au TANU n.k. kwa hiyo hawa jamaa wamejichimbia msingi mzuri sana ambao Mwalimu Nyerere (RIP) aliuweka. Ndio sababu utaona hata wanapogombea hawaishi kumuhusisha kwa namna moja au nyingine ili wajipatie kura.

Kitu cha msingi ni kusambaza uwazi kwamba hiyo misingi ambayo iliwekwa inakiukwa na viongozi wa CCM waliopo madarakani na wananchi waondoe matongo tongo machoni ili waweze kuona vizuri. Kazi kubwa ni strategy – Lakini huwezi kufanya hiyo strategy bila kuwa na NIA THABITI za kukuwezesha kufanikiwa hayo malengo. Kwa hiyo basi inatakiwa kuwa na wale wasiotetereka kuwa na msimamo dhabiti na kuimba kile tunachoamini cha Tanzania kuwa na maisha bora.

Kama kila mwana JF akituma kwa wiki e-mail kwa marafiki na jamaa ambao na wao watatuma message kwa rafiki au jamaa message itafika hadi vijijini. Kwa kuanzia naomba tutume message hii kama ilivyoandikwa na Mogongo mogongo kwenye e-mail zetu na kila week tupendekeze cha kutuma uki-compose message copy hii na tuma: Vile vile anayeweza kuitafsiri kwa Kiswahili itakuwa poa sana. USISAHAU KUONGEZA CHINI YA MESSAGE PASS IT ON TO FRIENDS (Nafahamu imekwisha sambazwa lakini wengi hawajaiona).

Bonyeza hapa imeandikwa na Chief
 
Adui yetu mkubwa ni Umaskini na hauwezi kuisha milele na milele... leo hii nasikia bajeti imepitishwa na mafuta yamepanda, je tunakwenda wapi????? serikari yetu imalenga kupunguza umaskini au kuendeleza?????? mimi naona serikali yetu imemkubari huyu adui umaskini cos kila kitu katika nchi yetu kinategemea matufa ili kuweze kuwa......... mfano viwanda, kilimo wakulima wanategemea kusafirisha mazao kwa kutumia hayo mafuta sasa usafiri utapanda na nini kitafata??? vyakula kupanda bei, nauli kupanda, maisha sasa hivi sijui mtanzania wa hali ya chini apewe mshahara kiasi gani ili aweze kukidhi mahitaji yake ya kila siku.
 
Na tunakokwenda ni masikini kuendelea kuwa masikini mpk siku ya kufa na tajiri ataendelea kuwa tajiri...... hakuna maisha bora kwa kila mtanzania wala nini kilichobaki ni maisha bora kwa kila kigogo.
 
Yap Yap! ndio Afrika hiyo...ADUI Mkubwa wa Mwafrika ni UMASKINI wa MALI na AKILI!...

Tukizungumzia maswala ya wapinzani ebu someni hii ya Kenya!


For Kenya's President Mwai Kibaki, the last three weeks must have felt like a shadow passing over his grave.
_40332417_kibaki_ap203body.jpg
High hopes for President Kibaki have been replaced with frustration


This is the man who swept to power two years ago on an anti-corruption ticket - riding a wave of euphoria after years of rising poverty and individual greed.
His electoral victory ended former president Daniel arap Moi's rule, blamed for instituting a culture of graft and dictatorship that crippled Kenya's economic development and stunted political life for almost a quarter of a century.
But the spectre of high-level corruption has now returned with a vengeance to haunt Kibaki's own coalition government - leaving his cabinet divided and his leadership wounded.
It came in the wake of allegations that corruption has cost Kenya $1bn - nearly a fifth of its state budget - under the Kibaki administration.
The allegations went on to reinforce the increasingly widespread perception of Mr Kibaki and his inner circle as a nest of power-hungry corrupt leaders as bad as those under Mr Moi.
Aid suspended
The new corruption crisis was sparked by a speech at a dinner party by the British high commissioner in Kenya, Sir Edward Clay.
He bemoaned what he described as the "massive looting" of public funds by senior officials of the Kibaki administration.

o.gif
_40855971_githongo_body_ap.jpg

inline_dashed_line.gif


Profile: John Githongo


The UK envoy told his stunned audience that he had handed the Kenyan authorities a dossier of 20 dubious contracts and allegedly crooked procurement ventures - only six months after complaining that corrupt Kenyan ministers were "eating like gluttons" and "vomiting on the shoes of foreign donors".
A few days later, Kenya's leading anti-graft official John Githongo resigned, saying he was no longer able to continue serving the government of Kenya.
The US and German governments then acted, announcing that they were suspending all of their aid to Kenya's anti-graft agencies - several million dollars.

The European Union and Japan also warned that their aid might be jeopardised if Kenya did not put its house in order.
In response, ministers allied to President Kibaki launched a vicious personal attack on Sir Edward, accusing him of lying. The ministers cited several inquiry commissions and anti-graft agencies set up by the government as clear indication that the Kibaki government was committed to fighting graft.
Away from diplomatic circles, the coalition government edged closer to collapse when four senior members of the Kibaki cabinet launched a stinging attack on his administration, urging him to sack ministers implicated in the new corruption to redeem the image of his government.
Bitter battle
It was the latest in a series of setbacks for President Kibaki since his National Rainbow Coalition (Narc) won a landslide victory in the December 2002 elections.
From the moment of his swearing-in ceremony, cracks in the new leadership - brought about by the jumble of egos, agendas and parties making up the Rainbow Alliance - began to show as coalition partners accused President Kibaki of going back on jobs promises when he named his new team of ministers.
At the same time, Kibaki's laid-back style of government - partly blamed on injuries he sustained in a car crash on a campaign trail in 2002 - did not help matters.
His aloofness and his hands-off approach unwittingly gave the impression of a leadership in limbo for much of his two-year presidency.

o.gif
start_quote_rb.gif
His aloofness and his hands-off approach unwittingly gave the impression of a leadership in limbo for much of his two-year presidency
end_quote_rb.gif






It fuelled a growing view that he was unsuited for high office.
His critics say he failed to end the bitter internal struggle between the main two factions of the Coalition - his National Alliance of Kenya (NAK) and the Liberal Democratic Party (LDP) led by Raila Odinga, seen by many as the coalition's strongman who delivered the opposition's victory in 2002 elections.
Even more dangerously for Mr Kibaki, say local analysts, was the way he allowed two ministers allied to him - Justice and Constitutional Affairs Minister Kiraitu Murungi and Internal Security Minister Chris Murungaru - to run the government machine and antagonise other coalition partners.
Mr Murungaru's ministry, together with that of the Finance Ministry, is now at the centre of several suspect government deals.
Corruption crisis
Two of these involve the procurement of passport equipment and police forensic science labs.
Back in March last year, a sharp rift within the coalition government over a new constitution seeking to curb President Kibaki's power almost brought the government to the brink of collapse.
It prompted the government to officially withdraw from the conference convened to write a new constitution.


o.gif
_40393801_clay_ap_body.jpg

inline_dashed_line.gif


Profile: Sir Edward Clay


In an act of defiance, most of the 629 delegates - including three cabinet ministers - went ahead and voted to trim presidential powers against the government's wishes.
Facing renewed opposition from Kibaki's allies, the constitutional reform process has since then remained stalled.
Responding to the new corruption crisis, President Kibaki last week announced a cabinet reshuffle - switching his ally Chris Murungaru from internal security ministry to transport - a move donors and local critics termed too little, too late.

Death sentence?
Then, six former senior officials were put on trial on corruption charges.
President Kibaki says he has not lost the political will to fight corruption.
But demanding more blood, critics say the accused were mere small fish.
Adding further pressure on the president to act quickly to curb high level corruption in his government, the British government announced that they would enforce a travel ban on Kenyan ministers and businessmen implicated in corruption.
Media houses, religious leaders and NGOs have also been applying their own pressure, arguing that ministers tainted by corruption should be dismissed while investigations are conducted.
Some have even called for Mr Kibaki to step down.
With his government now looking weakened, his friends and foes seem to agree that the man elected as a crusader against corruption appears increasingly overwhelmed by the issue.
 
Nadhani hapa hatuelewani kutokana na mapungufu ama katika uwezo wangu wa lugha ama lugha ya kiswahili yenyewe. Ninaposema "ujinga" wa wananchi sina maana ya "stupidity", bali nina maana ya "ignorance." Nadhani kuna wachangiaji wanaona kama nimewatukana watanzania kuwaita wajinga; hapana, ni kwa vile sikupata neno zuri la kiswahili.

Ignorance ninyoongelea hapa ni ile ya kutojua kuwa wana matatizo na chanzo chanzo cha matatzio hayo; hasa kujua kuwa: (a) wao wanaishi maisha yasiyoridhisha(b) CCM ndiyo inayosababisha waishi maisha ya namna ile (c) wao wenyewe ndio wanaiweka CCM madarakani (d) viongozi wao wanaishi kama wako bustani paradiso kutokana na jasho lao wananchi wenyewe.

Kwa wanaodai kuwa generation hii siyo wajinga ukilinganisha na wazee wetu; mimi nasema hapana. Wazee wale walijua tatizo lao la kutokuwa na uhuru katika nchi yao na chanzo cha tatizo hilo na ndiyo maana walipambana nalo. Generation yetu haieleki kujua tatizo liko wapi, ndiyo maana hawapambani nalo.

Kwa wanaodai kuwa wanachi hawaoni alternative to CCM, mimi nasema hapana. Alterantive ipo ila CCM inatumia ignorance ya wanachi kudhoofisha hiyo alternative leadership; hakuna aliyezaliwa kuwa kiongozi. Utashangaa mtu akiwa upinzani hachaguliwi lakini akihamia CCM anashinda hadi kuwa waziri, kwa mfano Dr Limbu, Nsanzugwako, na wengineo wengi tu ambao sasa hivi ni wakuu wa wilaya. Vile vile akiwa CCM anakuwa ni kiongozi akihamia upinzania hachaguliwi; mifano pia ipo mingi tu. Unashangaa kuwa kuna wakati upinzani wanakuwa na mgombeaji mzuri sana kuliko CCM lakini hachaguliwi.

Kwa wanaodai kuwa wanachi wanajua CCM kuwa ndiyo iliyoleta uhuru, mimi sasema hapana. Generation hii ilizaliwa kwenye uhuru kwa hiyo haioni kabisa umuhimu wa kupigania uhuru kwa vile hawajawahi kuukosa. lakini wanaona ugumu wa maisha ya kulala na njaa. Hiyo ndiyo inayotakiwa kuwatuma kupigana na system kama vile wazee wale walivyopigana na system ya wakati huo ili wapate uhuru.

Mwisho: Huwezi kusema vyama vya upinzani sijui CUF, NCCR, TLP, CHADEMA au UDP ndivyo vitapigana dhidi ya CCM kuing'oa madarakani, hapana, ni wanachi ndio wanaoindoa CCM madarakani. Siyo lazima waiondoe kwa wachague chama kingine nchi nzima, wanaweza kuiondoa kwa kutokuchangua wagombea wake tu. Kukawa na vyama tofauti kwa kila jimbo, kwa mfano mfano Nzega wakachagua CUF, Sikonge wakachagua NCCR, Tabora mjini wakachagua UDP n.k. Na endapo CCM ikikaidi na kungang'ania madarakani bila ridhaa ya wananchi, basi wananchi hao wanaweza kuja juu kama ilivyotokea kule Ukraine (??? -Orange revolution??) au kwa Suharto.

Tatizo letu siyo CCM, tatizo letu ni Ujinga (Ignorance) wetu sisi wenyewe.
 
Ukweli ni kwamba uchumi umemkubali sana Kibaki katika miaka miwili hii inayokaribia kwenye uchaguzi. Hii ndio sababu pekee itakayomwezesha kuchaguliwa tena; na hasa endapo wapinzani wake wakubwa katika ODM-Kenya watakuwa wameshindwa kuafikiana na kumchagua mmoja wao kugombea urais.

Hatari kubwa inawasubiri Kenya, kwani kama Kibaki ataendelea na ngwe yake ya pili na ya mwisho, hapatakuwa na breki tena ya kuzuia uporaji wa mali (corruption).
 
Mwalimu Kichuguu hiyo ni summary ya yote tuliyoongea. Umeunganisha vizuri sana ujinga na kuchaguliwa kwa CCM. Pia nafikiri tofauti uliyoiweka kati ya stupidity and ignorance mimi naikubali sana. Hii nayo uliyotoa mimi nasema ni "great stuff"!
 
Ignorance ninyoongelea hapa ni ile ya kutojua kuwa wana matatizo na chanzo chanzo cha matatzio hayo; hasa kujua kuwa: (a) wao wanaishi maisha yasiyoridhisha(b) CCM ndiyo inayosababisha waishi maisha ya namna ile (c) wao wenyewe ndio wanaiweka CCM madarakani (d) viongozi wao wanaishi kama wako bustani paradiso kutokana na jasho lao wananchi wenyewe.

This is really great stuff. Nafikiri hii ndiyo inayopaswa kuwa wimbo wa kusambaza katika majukwaa

Tatizo letu siyo CCM, tatizo letu ni Ujinga (Ignorance) wetu sisi wenyewe.

Hapa ndipo tunapotofautiana. Kama CCM umesema ndiyo wanaosababisha ujinga, unafikiri tutaushindaje huu ujinga bila kwanza kumshinda CCM?
 
Hivi kwa nini wenzetu Kenya wanaendelea kufanikiwa kiuchumi..nini hasa siri ya mafanikio yao.Nini wanavyo ambavyo sisi hatuna?
 
Mwl. Kichuguu,

Tano zako..wee kichwa!

Hekima na Busara za Master SunatKumara ambaye alinichosha na kitu kama hiki:-
1. If the disease that has caught hold of a person becomes the very essence of the person, that person cannot even know that there is a disease at all.
- Mnnh! nmaradhi ya Mtazania ni yepi?
2. When ignorance is the substance of our existence, there is no way out. We require a bolt to descend on our head, in order that we may awaken to the fact of what is happening to us.
- Ni bolt gani hiyo?

Kitu kimoja tu mwalimu hii ignorance yetu inatoka na nini hasa?..maanake haiwezekani kuwa out of the blue waafrika tumekuwa wajinga ktk maisha yetu wenyewe!...
 
Nimefuatilia mjadala huu kwa kina na mawazo yenu yamenifanya na mimi nichangie mawazo yangu kwenye swali kuu ambalo ni "adui yetu ni nani". Ninakubaliana zaidi na jibu la Kichuguu ingawa tunatofautiana katika kuelezea kile ambacho ni tatizo. Yeye anakiita ni Ujinga wa Watanzania na mimi nakiita ni "Ujuha" wa wananchi wengi.

Ujinga ni hali ya ya kutojua jambo fulani kiufundi au kiusomi na hivyo kukosa uwezo siyo tu wa kulielewa bali pia wa kulielezea. Kwa mfano mimi sihafahamu mambo ya Biochemical Engineering lakini naweza kuelezea mawili matatu kuhusu Quantum Physics. Hivyo mimi ni mjinga linapokuja suala la Biochemical Engineering. Hivyo utaona basi kuwa kila mmoja ni mjinga kwenye jambo fulani na ni mjuzi wa jambo jingine. Hivyo kinyume cha Ujinga (ignorance) ni Ujuzi (acquired knowledge). Hivyo mtu mjinga wa jambo fulani anaweza kuelimishwa na ule ujinga ukamtoka akawa na yeye ni miongoni mwa wanaojua - wajuzi.

Kwa kufuatilia mjadala huu nimeona kuwa kile ambacho wengi tunaelezea kuhusu kutojua kwa watanzania kwa hakika siyo ujinga bali ni kitu kingine. Ni kichuguu ambaye ameuelezea ujinga huu kuwa wa watanzania "kutojua kuwa wana matatizo na chanzo chanzo cha matatizo hayo". Hapo ndipo tunapotofautiana; naamini watanzania wanajua wana matatizo, na wanajua kwa hakika ni nini chanzo cha matatizo yao. Ni wao waliosema wanapoichagua CCM ni kwa sababu "Zimwi likujualo halikuli likakumaliza". Wanajua tatizo ni CCM, wanajua uozo wote wa CCM, na mambo mengine lukuki. Wanajua wana matatizo ya ajira, elimu, mazingira, n.k Kwa hayo mambo Watanzania siyo wajinga.

Hata hivyo, kuna aina nyingine ya kutojua ambayo ndio HASA tatizo la watanzania wengi bila kujali itikadi, mitazamo, au mielekeo yao ya kisiasa. Waswahili wana neno jingine linaloelezea kutojua huko. Kunaitwa UJUHA. Ujuha ni hali ya kutofahamu si kielimu kama kwenda shule bali kimang'amuzi na kiuamuzi. Ni kutofahamu jambo ambalo mtu kutokana na nafasi yake anapaswa kufahamu. Mtu ambaye kiatu cha kushoto anavaa kulia na anaonekana ni mwenye akili timamu huyo si mjinga ni juha. Mtu ambaye anajua CCM ina uozo unaonuka kama taka lakini wakati huo huo anairudisha madarakani, siyo mjinga, ni juha huyo.

Ni rahisi kuundoa ujinga, lakini ujuha ni vigumu mno kuundoa kwani wakati ujinga unaweza kuondolewa kwa mtu kukubali kupewa elimu husika, ujuha hauondokani na elimu juu ya jambo fulani kwani mzizi wake ni uamuzi wa kuridhika na kila mtu anacho. Ni ujuha huu ndio unaotusumbua kwani hata tuweke kila kitu hadharani, udhaifu na mapungufu ya CCM watu bado wataichagua. Ni kwa sababu hiyo basi mtu ambaye ni Juha haijalishi ana elimu gani ya darasani! anaweza kuwa na PHD na MSc na kila aina ya shahada lakini akawa juha. Mara nyingi majuha ni watu ambao hujifanya wanajua wakati mjinga ni mtu ambaye hajui na anajua kuwa hajui. Juha ni mtu yule ambaye anajifanya anajua kumbe hajui kuwa hajui. Utaona basi kuwa wakati kinyume cha ujinga ni ujuzi, kinyume cha ujuha ni werevu.

Sasa, watanzania hawajui vitu kadhaa ambavyo vinatokana na wao kuridhika na hali iliyopo. Hawajui kuwa wao wanastahili - kwamba wanastahili viongozi wazuri, maisha mazuri, n.k, hawajui kwamba wao wanaweza - wanaweza kubadilisha viongozi,kuwakosoa, na kuwawajibisha viongozi wao, hawajui kuwa wao wanapaswa - wanapaswa kutengeneza nchi yao na kuifanya vile wao wanataka.

Ni kwa sababu hiyo basi utaona wakati tuliposema kuwa tuna maadui watatu wakubwa mmoja wao akiwa ni "Ujinga" sisi tukakazana kuwapa watu elimu ya darasani ili kuundoa ujinga huo. Tatizo na adui mkubwa siyo ujinga wa kukosa elimu, bali ujua wa kupuuzia elimu ambayo mtu anayo na badala ya kuendeleza mazoea ya vitu visivyofaa kwani kuvibadilisha kutasababisha usumbufu. Juha, hayuko tayari kusumbuka. Sasa, tunaweza vipi kuundoa ujuha wa watu wasomi na wasiosoma?
 
Mwanakijiji,
Nimezama zaidi ktk ufahamu wa hili swala lakini kidogo utata umenikuta ktk fungu la kuwaweka sisi Wadanganyika! Umesema:-

1. Mjinga ni mtu ambaye hajui na anajua kuwa hajui!.
2. Juha ni mtu yule ambaye anajifanya anajua kumbe hajui kuwa hajui.

Je, hili fungu la tatu ambalo mtu anajua lakini hajui kama anajua tuwaite kina nani?
 
Kuna mafungu matamp

a. Yupo ambaye hajui, na hajui kuwa hajui - m.pumb.avu- achana naye
b. Yupo ambaye hajui na anajua kuwa hajui - mjinga - mwelimishe
c. Yupo ambaye hajui lakini anajifanya anajua - juha - mwelekeze
d. Yupo ambaye anajua lakini hajui kuwa anajua - mshamba - mwingize mjini
e. Yupo ambaye anajua, na anajua kuwa anajua - mwerevu - mfuate!
 
Utaweza vipi tofautisha kati ya A na E ikiwa mhusika mwenyewe upo ktk mojawapo na mtuhumiwa akuweka ktk mafungu hayo hayo?...
 
Sisi wananchi wa bongo ni wajinga, waliomg'oa mkoloni walikuwa werevu wa siasa kuliko sisi tuliobaki, walikuwa werevu sana kiasi cha kujua kuwa bila ya kumpa nafasi ya kuongoza Makaputula, mtu wa bara hawataenda kokote, werevu wao uliisha pale tu (Mkakaputula)-Mwalimu, alipofariki ndio maana mpaka leo mbele giza hatuoni wala hatuelewi, tumepigwa na kinyamkera!

Yes, ninaruida kuwa sisi wananchi ni wajinga, kama Kenya siasa ya werevu ni makabila then may be that is what is needed hapa bongo, labda tuende line ya makabila, maana tuko junction na desperate tunahitaji any avenue kupata mabadiliko ya kweli kisiasa, forget about the political avenue ya vyama vingi, it has failed simple and clear, na Full Stop!

Wa-Zambia, hawana utajiri wa kutupita sisi wabongo mpaka wakawa werevu wa kujua kuwa UNIP the CCM likes ni bomu na kuwatupilia mbali, wote sisi ni masikini ila sisi ni wajinga, period! na hakuna help wala hope!

Mungu Aibariki Bongo Yetu!
 
Well, tumefahamishwa maana ya maneno 'ujinga' na 'ujuha.'

Bila ya shaka yoyote ninaweza kusema kuwa waTanzania walio wengi hawamo katika mafungu hayo mawili. Kwa hiyo hilo la ujinga wa waTanzania kuwa adui tuliondoe.

Mjadala wa aina hii sio mgeni hapa JF. Niliwahi kutoa mfano jinsi waTanzania walivyokuwa tayari kuwakubali upinzani tokea vyama vingi vya siasa vilipoanzishwa. Wananchi walikuwa tayari kabisa, hata kumkubari mtu kama Mrema katika ule uchaguzi wa mwanzo.Mrema alizoa kura nyingi tu pamoja na kwamba upinzani ulikuwa bado ni legelege kabisa.
Nilitoa pia mfano wa mzee wa CHADEMA aliyepambana vikali na Msekwa. Mkandara anaweza kutueleza vizuri zaidi kuhusu matokeo hayo. Msekwa hakuwa mtu mdogo wa kuhangaishwa na non-descript opponent. Sehemu mbalimbali nchini wabunge wengi wa upinzani waliweza kuwaangusha CCM.

Sasa leo tunakuja kuelezwa ghafla kuwa "UJINGA" au "UJUHA" wa watanzania ndio unaoendeleza hali ilivyo leo nchini? Huo ujinga au ujuha uliwaondoka hao waTz waliowahi kuwachagua wapinzani, halafu mara, BUUU, ujinga ukawarudia mara tu baada ya miaka mitano? Hili kweli linawezekana?

Leo hii Mrema anapata kura anazopata kwa sababu waTZ wamezidi kuwa majuha? I don't think so!

Okay, kufuatana na maana ya maneno 'ujuha' na 'ujinga' kama alivyoyaelezea Mkjj hapo chini, sina shaka yoyote akilini mwangu kuwa mimi ni "Mwelevu." Hata watu wa mataifa mbalimbali ninaojihusisha au niliokwishajihusisha nao pia wanakubali kuwa mimi sio juha wala mjinga. Katika hali ya kisiasa ilivyo leo hii hapa Tanzania, sina njia nyingine bali nikitakiwa kuchagua itanilazimu niwachague CCM pamoja na kuwa na maovu mengi waliyonayo. This is for lack of a better choice. Niite 'juha' au 'mjinga' sawa, lakini huo ndio ukweli ulivyo.

CCM wataendelea kuwakandamiza wapinzani, si kwa sababu ya ujinga wa wananchi au ujanja wa CCM, bali ni kwa sababu ya nyenzo nyingi inazozidi kujirundikia. Usione viongozi kukazana na wizi na mambo chungu nzima ya kutafuta kujirundikia mali. Utajiri na siasa haviko mbali. Kama huamini, jaribu kugombea cheo chochote cha kisiasa pale Marekani bila ya kuwa na pesa. Mamilioni wanayorundika akina Clinton, Obama na wengineo sio ya kuchezea.

Pengine ni mamilioni ya hela ya madafu ndiyo inayowawezesha akina Ndesambulo kule Moshi kuendelea kuwa competitive more than anythingelse, especially 'ujinga' au 'ujuha' wa waTanzania.

Juzi Uhuru Kenyatta kawaita "Delegates" wa chama chake cha Kanu kwenye 'flimsy' mkutano. Kawajazia mapesa kwenye bahasha kila mjumbe aliyehudhuria, kawalisha na kuwaweka hotelini bila ya gharama yoyote kwa kila mjumbe. CCM ni wepesi wa kujifunza. Watakapoona kuwa mbinu zao za mika yote hazifanyi kazi tena, ndipo mtakapowaona waziwazi wakinunua kuchaguliwa.
 
Kitila,

Nimechelewa kwenye sherehe za kuadhimisha mwanzo wa majira ya kiangazi (summer) kwenye eneo letu hili ambapo leo jua limezama saa nne na dakika kumi usiku huu ikiwa ndiyo siku ndefu sana kwa mwaka. Nilikuwa nataka niiwahi mada hii ya muhimu sana kabla sijaachwa mbali lakini naona tayari nimeshaachwa. Hata hivyo nitajitahidi kadri ya uwezo wangu ku-catch up.

Kabla sijazungumzia tatizo la ujinga wa raia wetu, ngoja kwanza nikubaliane na Domo Kaya na Mkandara kuwa adui yetu mwingine wa pili umaskini. Umaskini huu ndio unaofanya hata wale wasomi tulio nao kutokufanya lolote kuamsha jamii kutoka ujingani, badala yake wanaishia kushindana na matatizo ya ya umaskini wao binafsi. Niseme ukweli nadhani hata mimi niko ughaibuni nafikiri zaidi ni kwa sababu ya umaskini wangu. Mkandara ametoa somo zuri sana kutoka kwenye Hekima na Busara za Master SunatKumara. Zote hizo zinaeleza hali halisi tuliyo nayo Tanzania. Raia hwajui kama wana maradhi na inawezekana ikwa vigumu sana kuondokana na ugonjwa huo. hata hivyo nadhani kuwa bado tuna nafasi ya kujikwamua kama nitakavyoeleza huko mbeleni.

Sasa ngoja nirudie hili la ujinga kwa sababu ndiyo adui namba wani. Ujinga wa raia wetu haukuletwa na CCM kama unavyosema. Niliandika huko nyuma kuelezea kuwa kuwa kila mtu anazaliwa na ujinga, kwa hiyo tusilaumu CCM kwa ujinga wetu. Ila kadri mtu anavyokuwa ndivyo anvyooandoa ujinga wake kidogo kidogo kwa kujifunza kutoka kwa wazazi na watu wengine waliomtangulia, kwenda shule, na kujifunza kutokana na mazingira yake ya kila siku. Tatizo letu vyanzo vyote vya elimu siyo effective kumfanya raia ajue mapungufu yanayomkabili, na serikali ya CCM inachangia sana kufanya vyanzo hivyo vya elimu viswe effective.

(a) Elimu yetu ya darasani ndiyo hivyo tena; nadhani umeona mwanakijiji akiuliza kuwa wasomi wetu wamekwenda wapi. Waalimu wanaoufundisha huko shule za msingi na sekondari hawatilii maanani tena kumpa mwanafunzi uwezo wa kuelewa mazingira yao, bali wanasisitiza kukariri kitabuni na jinsi ya kupasi mitihani. Kutokuwepo kwa mijadala shule za msingi imekuwa ni kilema kikubwa sana katika elimu yetu ya msingi na nadhani hadi sekondari. Wale wanaopata kusonga mbele kielimu na kuweza kuelewa mapungufu hayo wanaishia kushughulikia umaskini wao kiasi kuwa hawasikiki kabisa. Nadhani hapa ndipo unapoweza kuilaumu kuwa serikali ya CCM kuwa imejenga mfumo wa elimu ambao haumsaidii raia kuondokana na ujinga aliozaliwa nao.

(b) Elimu ya kurithi na ile inayopatikana kutokana na uzoefu wa kupambana na mazingira nayo ni finyu sana siku hizi na ndiyo hasa inayoongezea matatizo yetu. Asilimia kubwa sana ya raia wetu hawajaona ng'ambo ya pili ya maisha; wamezaliwa katika umaskini na kukulia katika umaskini kiasi kuwa wanadhani kabisa kuwa maisha wanayoishi ndivyo wanavyotakiwa waishi. Wanarithisha watoto wao imani hizo hizo. Kupambana kwao na mazingira inakuwa ni kutafuta ugali na chakula tu. Hapa pia unaweza kuilaumu serikali ya CCM kwa kujenga mazingira ya maisha ya kimaskini ambamo raia wanadhani umaskini ni halali yao, hivyo hawajui kuwa wanastahili maisha bora zaidi ya hapo.

Kwa hiyo utakubaliana nami kuwa mchango wa CCM siyo katika kuleta ujinga bali kujenga mazingira ambamo raia wanashindwa kuondokana na ujinga. Mimi naona kuwa hapa kuna vicious circle: CCM wanatumia mapungufu ya ujinga na umaskini wa raia wetu kushikiria madaraka ambapo wanazidi kutengezeza mazingira ya raia KUendelea kuwa wajinga na masikini na hivyo kuendelea kuiweka CCM madarakani. Hata hivyo, kwa vile sisi ni jamii inayofuata kanuni za demokrasi, huwezi kuindoa CCM madarakani bila ridhaa ya wanachi, ndiyo maana ni lazima kupigana na ignorance kwanza kusudi wananchi waiondoe CCM madarakani. Kwa bahati mbaya sana, wanasiasa wa vyama vya upinzani wameshindwa kabisa kuondoa ujinga vichwani mwa raia. Nilipata bahati ya kuwepo pale dar wakati wa kampeini za mwaka 1995, Dr Lamwai kweli alifanya kazi nzuri sana ya kuwaelimisha raia pale Manzese kiasi kuwa machinga wote pale walikuwa wakivaa tai kuonyesha jinsi Lamwai (mvaa tai hata kwenye jua kali) alivyokuwa amweagusa. Ni kipindi hicho ambao ("DR") Masaburi alipotoa bastola kutishia watu kwa vile UVCCM walikuwa na nia ya kuweka masanduku ya kura haramu lakini machinga wale wakamchachamlia mpaka akaondoka na masanduku yake. Nadhani mpaka hapo ninaeleweka. Ukiwaelimisha vizuri raia wakaondokana na ujinga wao kweli wako tayari kusimama kidete kupambana na machinery yote ya CCM, na wataishinda tu.

Kwa vile CCM inasaidia kukomaza ujinga wa raia wetu kiasi kuwa wanashindwa kuona mbali katika kujitafutia maendeleao yao, ni lazima ama tuiondoe CCM madarakani au tulizamishe CCM ifanye kazi ya wananchi badala ya kujenga masilahi ya viongozi wao tu. Yote yawezekana kama tutawaelimisha raia wetu ipasavyo kwa kutumia njia tofauti na njia rasmi na za njia za asili zilizopo.

(1) Mtu mmoja mmoja, mimi na wewe, tufanye utaratibu, kwa kupitia foundations mbalimbali, kuandaa program za kuelimisha wananchi kwa kutumia video na matangazo ya redioni. Lengo liwe ni kuwaelimisha wananchi wachukie maisha ya kimaskini wanayoishi. Programa hizi zitumie mifano halisi kuwaonyesha wananchi tofauti za kimaisha zilizopo baina yao na viongozi wao, na vile vile baina yao na raia wenzao katika serikali zinazojali maendeleo ya raia wake. Kama inawezekan watumie data halisi kuonyesha jinsi viongozi wanavyovuja raslimali za nchi (k.m. mikutano na warsha za wakuu wa mikoa, safari za nje za rais na ujumbe mkubwa sana) na jinsi ambavyo raslimali hizo zingewasaidia raia kuondokana na umaskini wao.

(2) Vyama vya upinzani, wekeni mkakati imara wa kuelimisha raia kuwa maisha wanayoishi siyo wanavyotakiwa waishi na yote ni matokeo ya wao kuichagua CCM miaka yote. Haitoshi kupiga kelele kila siku kuwa CCM lazima ing'olewe madarakani bila kuwaambia wananchi mambo ambayo wenzetu wanaita "bread and butter." Mimi sioni kabisa tatizo kama vyama vya upinzani vikigwana majimbo ya concentration. CUF iimalishe elimua ya uraia katika maeneoa ambayo imejikita, CHADEMA vivyo hivyo, na TLP, UDP na vyama vinginevyo. Hivi ni vyama dhaifu sana kupambana na CCM nchi nzima kwa vile havina raslimali kama CCM. Ila vikijipanga kupambana katika maeneo madogo madogo, kwa pamoja vitainyanganya CCM eneo kubwa sana. Upuuzi ulifanyika mwaka 1995 ulikuwa ni pale viliposhindwa kuungana, kosa hilo lilirudiwa mwaka 2000 na vile vile 2005. Wameanza kuongelea muungano baada ya kuwa wamedhoofika sana, hiyo ni bahati mbaya sana kwao; hata hivyo hawajachelewa kabisa; na kama kawaida wakichukua sehemu kubwa ya majimbo ya bunge wanaanza kupanga agenda ya nchi. Wanaweza hata kumkaba koo rais akileta upuuzi kama ilivyofanyika Niger. Biashara ya kutoa pilau wakati wa kampeini hawaiwezi, kwa hiyo waache CCM itoe pilau wakati wao wanendesha neno. Nyerere alifanikiwa sana wakati wake siyo kwa sababu alikuwa anatoa takrima yoyote; neno lake ilikuwa ndiyo takrima yenyewe. Upinzani jifunzeni kutumia neno linalopenya katika kuelimisha wananchi badala ya kujiingiza katika njia za CCM ambazo hamziwezi. Na Kama ningekuwa kiranja wa upinzani ningepunguza raslimali katika presidential politics na kuziweka katika majimbo ya ubunge. Badala ya kuwa na wagombea hamsini wa urais, acheni kuwa na mgombea mmja tu kwa niaba ya upinzani wote, wengine wote kazanieani kwenye majimbo. Kwa kawaida mkifanya vizri kwenye majimbo, ni rahisi sana kuchota kura za urais pia.

Loh! Leo na mimi pia nimejitahidi kuandika article ndefu. Nitarekebisha mataipos kidogo kidogo kwa vile najua yamo mengi sana.
 
Back
Top Bottom