Ezekiel Kamwaga: Hata kama tuna uchungu na bandari ndiyo tumfokee Rais?

comte

JF-Expert Member
Dec 11, 2011
8,226
5,948

Akina Nshala na ushindi wa Pyrrhic​

Ezekiel Kamwaga

Ezekiel Kamwaga​

Nshala-1024x576.jpeg

Wakili Rugemeleza Nshala. Picha kwa hisani ya Katiba TV

Na Ezekiel Kamwaga

MARA nyingi huwa nafanya rejea kupitia maandishi ya hayati Profesa Samuel Huntington wa Marekani. Katika kitabu chake cha mwaka 1993, The Third Wave: Democratization in the Late Twentieth Century, msomi huyu alieleza kwa undani kuhusu ni wakati gani unaweza kubashiri mwisho wa utawala uliodumu madarakani kwa muda mrefu.

Mojawapo ya dalili za mwisho wa utawala unaoelekea ukingoni – kwa mujibu wa Huntington, ni mgawanyiko wa dhahiri miongoni mwa tabaka la watawala. Ukianza kuona wale walioshika hatamu wakiwa wanagawana mbao, ujue mchezo umekwisha.

Hivyo, Yoweri Museveni amedumu madarakani kwa muda mrefu kwa sababu amejua namna ya kushika watu wa tabaka la juu. Anaweza kuwapoteza akina Kizza Besigye na Jenerali Mugisha Muntu kwa nyakati tofauti lakini kwa ujumla sehemu kubwa ya Bunge, Jeshi, Mahakama na sekta binafsi bado inafanya naye kazi.

Wiki mbili zilizopita, jaribio la Yevgeny Prigozhin kutaka kumpindua Vladmir Putin liligonga mwamba – kwa sababu, hakukuwa na watu wengine wakubwa katika tabaka la watawala la Russia aliyekubali walau kumuunga mkono hadharani. Kama Prigozhin alijaribu kucheza kamari, itakuwa imebuma.

Nakumbuka jioni moja ya Oktoba mwaka 2019 wakati nilipofanya mazungumzo na mmoja wa wanasiasa mashuhuri wa Tanzania aliyekuwa kwenye upande tofauti na hayati Rais John Magufuli. Akiwa hana wadhifa wowote na amesukumwa mbali ya chama na serikali, kigogo yule aliniambia jambo moja.

“Pamoja na yote anayonifanyia Magufuli, naona bado ni afadhali kwa sababu CCM iko madarakani. Nina imani kama Lowassa (Edward, aliyekuwa mgombea wa Chadema kwenye uchaguzi wa mwaka 2015) angeshinda, labda hali yangu ingekuwa mbaya zaidi,” aliniambia kwa uwazi kigogo huyo.

Na kama utafanya uchunguzi wa ndani kuhusu utawala wa Magufuli, utabaini kwamba pamoja na mambo yote anayolaumiwa wakati wa utawala wake, jambo moja huwezi kumlaumu – kwamba kulikuwa na wakati alikuwa anaiweka CCM matatani.

Ingawa baadhi ya watu wa tabaka la juu walikuwa wakilalamika, wengi wa wanaofaidika kifursa kupitia CCM, waliweza kumvumilia wakijua kwamba ili mradi chama chao kiko madarakani, kuna siku Magufuli atatoka na zamu yao itafika tena.

Hii ndiyo namna ambayo CCM na vyama vingine vingi vilivyodumu madarakani kwa muda mrefu vimekuwa vikitumia ndoano hiyo ya kuwaweka watu wa tabaka la watawala katika mazingira ambayo hawaoni maisha mengine nje ya chama hicho. Kama ningekuwa mwanasiasa au mwanaharakati, jambo la kwanza ambalo ningefanya kuhakikisha mabadiliko makubwa yanatokea Tanzania, ni kufanya mambo ambayo yangesababisha mpasuko ndani ya CCM au tabaka la watawala.

Jambo ambalo ningeogopa kulifanya ni kufanya aina ya siasa au harakati ambazo zinalifanya tabaka hili kuatamiana pamoja au kusema kwamba hatutaweza kuruhusu mabadiliko. Mambo yanaweza kubadilika leo au kesho lakini kama tabaka la watawala limefungamana, kazi inakuwa ngumu zaidi.

Ndiyo sababu nimeshangazwa sana na maneno aliyoyazungumza mmoja wa wanasheria wanaoheshimika sana nchini Tanzania, Dk. Rugemeleza Nshala, dhidi ya Rais Samia Suluhu Hassan, katika mahojiano aliyofanya na chombo kimoja cha habari cha mitandaoni kuhusu suala la uwekezaji kwenye bandari ya Dar es Salaam unaotarajiwa kufanywa na kampuni ya DP World kutoka Dubai.

Mahojiano yale yalikuwa ni dhidi ya Rais Samia na tabaka zima la watawala hapa Tanzania. Mengi alizungumza lakini nakumbuka kauli yake ya kuwaita wabunge wa Bunge la Tanzania kuwa ni wahaini kwa sababu ya kupitisha Azimio la Kuridhia Makubaliano baina ya Tanzania na Dubai. Wiki moja iliyopita, nilimsikia Nshala akieleza kwamba anamfahamu Spika wa Bunge, Dk. Tulia Ackson, kwa sababu alipokuwa mwanafunzi wa Chuo Kikuu cha Dar es Salaam (UDSM) alikuwa anakwenda ofisini kwake kufanya tafiti za kisomi. Ingawa kufanya tafiti ni jambo la kawaida, kwa namna Ruge alivyozungumza ilikuwa sawa na kusema ‘huyo spika naye ni mtoto tu kwangu’.

Katika miaka yangu takribani 20 ya uandishi wa habari, nimefanya kazi na Bunge na wabunge. Kama kuna mambo nayafahamu kuhusu taasisi hiyo ni namna wabunge walivyo na wivu mkubwa katika kuilinda taasisi hiyo dhidi ya wale wanaoonekana kuibagaza. Nilikuwa mwandishi mchanga enzi za Bunge la Spika Pius Msekwa ambako mmoja wa waliolipa umaarufu mkubwa alikuwa aliyekuwa Mwenyekiti wa Kamati ya Hadhi ya Bunge, Eliachim Simpasa. Nyakati hizo, matamko yoyote yanayoshusha hadhi ya Bunge yalikuwa yakijibiwa kwa wivu mkubwa na kamati hiyo.

Hili si Bunge la Msekwa wala Simpasa, lakini tabia ya wabunge ni ileile. Sioni ni kwa vipi Nshala atafanya kazi zake za utetezi na uchechemuzi kwa kushirikiana na Bunge baada ya kauli zake za wiki hii. Sioni ni kwa vipi serikali itamsikiliza tena na kuzungumza naye kwa namna ilivyokuwa awali baada ya mahojiano yake niliyoyasikia mtandaoni. Nimefuatilia suala la Bandari kwa karibu. Jambo moja ambalo naliona kwa karibu ni kwamba hadi sasa halijaleta mpasuko miongoni mwa tabaka la watawala kwa kiwango cha kudhani kuna mabadiliko yanaweza kutokea sasa.

Ninafahamu kwamba sekta binafsi ya Tanzania iko katika makundi mawili; mosi la watu walioharibikiwa biashara zao wakati wa utawala wa Magufuli na sasa wanataka kurejea katika hali ya kawaida na wengine wanaona huu ndiyo wakati wao wa kufanya tena biashara. Hii ni sekta ambayo haiwezi kuingia kwenye mgogoro na Rais kwa sasa.

Nimesikia watu tofauti wakizungumzia kuhusu suala hili kwa mrengo wa kuitaka serikali ifanye mabadiliko. Hata hivyo, wengi wa wazungumzaji ni watu ambao hawana kiota (political base), miongoni mwa makundi yaliyomo ndani ya CCM hivi sasa. Hivyo CCM iko vilevile.

Kwa namna ilivyosukwa tangu enzi za Baba wa Taifa, Idara ya Usalama wa Taifa Tanzania (TISS) ina majukumu mengi lakini miongoni mwa majukumu ya kipaumbele ni kumlinda Rais. Kwenye sakata hili linaloendelea – na kwa sababu bado hakuna mpasuko wa tabaka la watawala, idara itahakikisha Rais anafanikiwa kwenye dhamira anayoitaka.

Kwa mahojiano yale, kwa wakati mmoja, naamini Nshala amevunja madaraja na watu ambao baadaye wangekuwa msaada kwenye kazi zake za kitetezi. Naamini, huu ni wakati mzuri zaidi wa kujenga madaraja kuliko kubomoa.

Jambo la mwisho linahusu ukali wa lugha na matumizi ya maneno kwenye mazungumzo. Kwa asili, Watanzania na Waafrika ni watu wanaoamini katika heshima kwa wakubwa au viongozi. Kwenye lugha yangu ya Kijaluo, tunatumia neno Mwalo na jirani zake Nshala kule kwa Waganda huiita kwa jina la Obufuura. Kutoa lugha isiyofaa kwa mkubwa huwa si sifa bali linapunguza sifa.

Unapokuwa na Rais ambaye ni wa jinsia ya kike na kutumia maneno ya kumkosoa, kwa mfano, “badala ya kuchutama, yeye anachanua”, linatuma ujumbe ambao haukubaliki hata kwa mila na desturi zetu za Kiafrika. Kwa lugha za namna hii, huwezi kuwakusanya watu na kuwaambia wafanye unachotaka wakati wanakuchukulia kama mtu usiye na adabu kwa wakubwa au viongozi ambayo ni sehemu ya utamaduni wetu.

Kimkakati, naamini kwamba staili ya kufoka na kutoa matamshi makali ilikuwa na mashiko enzi za utawala wa Rais Magufuli. Yapo maandishi ya kisomi yanayoonyesha kwamba dawa ya moto ni moto. Nshala angekuwa anafoka namna hii enzi za utawala wa Magufuli, pengine ingekuwa sawa. Lakini kufoka na kutoa lugha zisizo za kiungwana kwa Rais ambaye anazungumza kwa uungwana pasi na chembe ya ukatili ni goli la kujifunga. Kama Nshala anataka kuwa moto, Samia ameonyesha kuwa ni maji. Moto unapokutana na maji ya kutosha, ushindi unajulikana utaelekea wapi.

Namna pekee ya kuongeza ushawishi wa kumshinda Samia na CCM kwa ujumla, ni kuzidi kutoa hoja kinzani na majibu namna tofauti ya kupambana na kero za Watanzania. Namna bora ni kujenga kuaminika na taasisi zinazotengeneza tabaka la watawala wa nchi hii. Wapinzani na wanaharakati wanapaswa kujenga kuaminiwa na kuwa na mahusiano mazuri na sekta binafsi, Bunge, asasi za kiraia na vyombo vya ulinzi na usalama ili kuwa tayari kutumia fursa yoyote itakayotokana na kubomoka au mpasuko kwa tabaka hilo.

Kwa maneno yale makali, Nshala anaweza kusifiwa sana na akapata ushindi kama mtu jasiri na asiyeogopa kusema chochote kwa watawala. Lakini, kwa maoni yangu, kama huo ni ushindi – basi ni ule ambao unanikumbusha jina moja; Pyrrhic (280-279 BC).

Mwandishi ni Msomi wa Masuala ya Maridhiano ya Kisiasa mwenye Shahada ya Uzamili katika African Politics kutoka Chuo Kikuu cha London School of Oriental and African Studies (SOAS) nchini Uingereza.
 
Sijapata muda wa kusoma andiko kwahio najibu heading pekee....

Unadhani hii Monarchy..., Nadhani watu hawadharau Taasisi (Urais) bali yule aliyepo pale au matendo yake ndio yanafanywa watu wapate Jazba..., nadhani mwenye makosa atakuwa huyo aliyekalia kiti kutokuwasikiliza maboss wake wanachomwambia (by the way akiona kelele zimezidi hakatazwi kuondoka wala hakulazimishwa kuingia)
 
Unataka kazi ya uchawa?
 
Nshara siyo mwanasiasa. Anaongea kama raia na mwanasheria. Period. Hakuna alichokiongea ambacho ni kinyume na sheria au amemtukana mtu.

Kwa hali inayoendelea kwa sasa ni Waandishi wa habari ndiyo wamekuwa spin masters wa serikali. Hatuwaamini.
 
Thanks umemaliza kila kitu.
 
..tusipindishe pindishe.

..madudu yaliyoko kwenye mkataba wa Tanzania na Dubai ndio yaliyosababishwa watu wazungumze kwa lugha kali, au maneno magumu.

..Rais amepoteza heshima yake kwa kuonekana hajali na hana uchungu na rasilimali za nchi yetu.
 
Anataka uteuzi, amuulize Pascal Mayalla
 
Hakuna lolote alichoandika ni upumbavu mtupu..ukitaka kuheshimiwa fanya mambo kwa kuheshimu wengine! ni mjinga ndiye anafanya tone kuwa substance na kufanya mjadala badala ya content ya kinachozungumzwa. Kashindwa kusoma shule za hapa anatuonyesha vyuo hata havieleweki..kimwaga ni kanjanja mchumia tumbo toka zamani..wala Nshala hajaanza leo harakati za utetezi wa haki na tone yake ni hiyo hiyo!
 
Rais ni mtumishi sio Mungu, akikosea ni haki kukosolewa, na akiambiwa ukweli kwa lugha kali kulingana na kosa la makusudi alilotufanyia watanganyika, kosa linalompa mgeni haki ya kujitawala ndani ya mipaka ya nchi yetu, kosa lililopelekea kuvunja sheria zetu za ndani, hapo hakuna tusi.
 
Back
Top Bottom