Kama bajeti imetengwa, nini kinachelewesha ujenzi Barabara ya Kimara – Bonyokwa?

Boran Jakutay

Senior Member
Apr 8, 2023
110
257
Kumekuwa na kilio cha muda mrefu kuhusiana na ubovu wa Barabara ya Kimara – Bonyokwa, kumekuwa na ahadi nyingi lakini utekelezaji unasuasua.

Tunafahamu juhudi za viongozi zinazofanywa, lakini tunashangaa nini hasa kinazuia ujenzi wake kutofanyika wakati tuliambia bajeti yake imetengwa katika kipindi cha mwaka wa fedha 2022/2023.

Kwa sasa tupo mwaka wa fedha 2023/2024, lakini barabara bado ina changamoto kubwa, hasa kipindi cha mvua kunakuwa na shida kubwa ya usafiri, abiria wanateseka, nauli zinapanda kiholela, lakini kama barabara ingekuwa safi kama ilivyo ile ya Kimara Korogwe – Maji Chumvi, tungeshukuru sana.

Kwa mujibu wa Mbunge wa Jimbo la Segerea, Bonnah Ladislaus Kamoli, Mei 9, 2022, aliweka taarifa katika akaunti yake ya Mtandao wa Kijamii wa Instagram akiambatanisha na picha zilizoonesha kipande cha Barabara ya Kimara – Bonyokwa.

Katika chapisho hilo, aliandika hivi: “Hii ni barabara ya Bonyokwa kuelekea Kimara ni barabara muhimu sana na inaunganisha Majimbo ya Segerea na Ubungo.

“Barabara itajengwa kwa kiwango cha lami na ipo kwenye bajeti ya Mwaka wa fedha wa 2022/2023.

“Ukamilikaji wa barabara hii utaongeza ukuaji wa uchumi wa maeneo haya kwa kiasi kikubwa, kwani biashara zitashamiri na huduma zingine za kijamii zitaboreshwa zaidi.”
Kimara.PNG
ki.PNG

Ni mwaka mmoja na miezi takribani miwili, ujenzi haujaanza, kila siku wananchi ni kilio tu, huku mbunge huyo akibainisha kwamba ujenzi wa barabara hiyo umetengewa zaidi ya shilingi bilioni 8 na uko chini ya TANROADS.

Wakati barabara hiyo ikibaki ‘yatima’ kwa upande wa Jimbo la Segerea, maboresho ya barabara za ndani yameanza ikiwemo Barabara ya Maji Chumvi - Kageni- Migombani, ujenzi wake ni kwa kiwango cha zege.

Pia kipande cha barabara ya kuanzia Bonyokwa Stendi hadi kuelekea Segerea ambacho hakikuwa na lami sasa Ujenzi wake umeanza. Hiki ni kipande cha kuanzia Bonyokwa hadi Magoza.

Sipo hapa kumlaumu Mbunge Bonnah kwa sababu sio eneo lake, lakini nimshukuru kwa kuainisha ni nani wahusika wanaopaswa kujibu maswali ya kwa nini ujenzi haufanyiki wakati bajeti ilipangwa tangu mwaka wa fedha uliopita?

Kama TANROADS mmezidiwa mzigo wa kujenga barabara, semeni ili kama kuna anayeweza kuchukua tenda aingie mzigoni kuondoa adha wanayopata wananchi.

Niliona kuna watu wanasema wameona ujenzi umenza, ila wanachotakiwa kuelewa ni kwamba, ujenzi huo ulioanza hauhusiani na barabara ya kutoka Kimara - Bonyokwa, bali ni ile Barabara ya Bonywa Stendi - Segerea kipande kilichobaki ambacho hakikuwa na lami kinachoishia Magoza.
Snapinsta.app_280209916_310277281285974_6452725434062607725_n_1080.jpg

Snapinsta.app_280204136_1276902636171938_3738841600019060498_n_1080.jpg
 
Back
Top Bottom