rodrick alexander
JF-Expert Member
- Feb 12, 2012
- 15,297
- 20,371
Katika ripoti ya ukaguzi wa CAG imeeleza kuwa Aprili 2022 kwa mujibu wa ripoti hiyo, Wizara ya Afya iliingia mkataba na kampuni ya Zenj Motors wa ununuzi wa magari 12 ya wagonjwa yenye thamani ya Sh1.97 bilioni kwa ajili ya hospitali za Zanzibar ambao haukutekelezwa ipasavyo.
Chini ya mkataba huo, magari hayo yalitakiwa yawe yamefikishwa wizarani ndani ya siku 90 lakini hadi Novemba 2022 (zaidi ya mwaka mmoja), magari hayo yalikuwa hayajapokewa na hakuna ushahidi wa kuongezewa muda.
Lini wizara ya afya imekuwa wizara ya muungano kwani Zanzibar pia wanayo wizara yao ya Afya au ndio zile kero tulizoambiwa na Jafo kuwa mama amezitekeleza? Pia tunaambiwa CAG anafanya ukaguzi hata kwa mambo yasio ya muungano.
Kwa upande wake Wizara ya Afya ya Zanzibar iliingia mikataba saba na wazabuni ya kuwasambazia vifaa kwa ajili ya hospitali nane, yenye thamani ya Sh10.41 bilioni, lakini hadi Novemba 22, 2022 hakuna kifaa hata kimoja kilichokuwa kimepokewa.
Pia, ripoti imebaini Wizara ya Uchumi wa Buluu na Uvuvi iliipa Comfix Engineering zabuni ya vifaa vya uvuvi vyenye thamani ya Sh139.5 milioni na vilipaswa kukabidhiwa Julai 23, 2022 lakini hadi Novemba 23 mwaka jana havikuwa vimepokewa.
CAG anasema katika ripoti hiyo Shirika la Umeme Zanzibar (Zesco) liliingia mkataba na Vuka Timbers Februari 3, 2022 wa kulipatia nguzo 10,000, lakini hadi Novemba mwaka jana walikuwa wamekabidhi nguzo 1,089 huku zilizosalia (asilimia 89) hazikuwa zimepokewa.
Wizara ya Nishati na Shirika hilo la Umeme walilazimika kukubaliana kuongeza muda wa makabidhiano kwa miezi mitatu hadi Desemba 2022, lakini nguzo hizo bado hazikukabidhiwa hata baada ya muda wa nyongeza kuisha.
Zanzibar wana mkaguzi wao kwanini watumie rasilimali za Bara kwa mambo yasio ya kimuuungano?