TANGAZO: Maandamano dhidi ya malipo ya DOWANS

Msanii

Platinum Member
Joined
Jul 4, 2007
Posts
26,502
Reaction score
40,185
Wakuu, Nawakilisha....
=============
UPDATE
=============
 

Attachments

Epsode ngapi hii! mkimaliza kuangalia nipeni na mimi nikaicheck pls
 
Tungesubiri matokeo ya rufaa ambayo serikali imekata.....hakuna mtu anaependa nchi ilipe fedha hizo kwa dowans...pili lile ni suala la kisheria linapaswa kupingwa kisheria mahakamani sio barabarani na mitaani kwa maandamano.wanasheria wanajua watusaidie katika hili.
 
Kwa kweli kusema tusubiri serekali imekata rufaa ni kukosea maana serekali ndio imetufikisha hapa na kwa mtiririko wa tangu Richmond inaanza mpaka hapa hakuna zaidi ya usanii tuu unafanywa na serekali na mwisho wa siku tutarudi hapahapa tulipo kwamba kisheria serekali ina makosa, sasa kuandamana ni kuiambia serekali inalazimika kuwajibika kikamilifu na hili na sio porojo za danadana hizi wanazofanya, hivi sisi watanzania tunachoogopa haswa ni nini? hizi hela zitakazolipwa tufahamu kwamba ni sisi ndio tutagharamika na sio hao viongozi wazembe ambao zaidi wataambulia lawama za mitaani pembenipembeni kama tulivyozoea kama makondoo, kweli tunahitaji kuwa serious zaidi ya maneno, tunahitaji vitendo jamani. OHOOOOOO!!!!!!!!!
 
limepitwe na wakati
serikali imekata rufaa

Jeykey na Inauma acheni ujuha au ndo mnatimiza wajibu kwa kazi mlotumwa jamvini? Kwa mujibu wa utapeli mliofanya kwenye mkataba ni kuwa mkataba hauruhusu suala hilo kupekwa nje ya Mahakama ya hao waliowapa Dowans ushindi.

Mnatufanya WaTz wote majuha. Shuhudieni hayo maandamano, labda yatawapa kujua kama sisi bado majuha au tumeerevuka.
 
Wakuu, Nawakilisha....

Naomba utuhakikishie authenticity ya hili Tangaza maana nashindwa kukuamini kwa sababu jina lako hapa JF ni msanii...kwa tafsiri ya kawaida kabisa kwa mtanzania wa kawaida, msanii ni laghai, asiyeaminika, mtu wa "SOUND" na tafsiri nyingi za aina hiyo. Je, utatuhakikishiaje kuwa hiki ulichokiweka siyo usaniii?

USHAURI WANGU: kwa vitu ambavyo ni serious kama hiki, we need to have a serious tone, ikianzia na mtoa habari mwenyewe.


That's my concern
 
limepitwe na wakati
serikali imekata rufaa
Rufaa ya serikali hiyo hiyo iliyoingia katika mkataba huo....
Najua ni sanaa tu zinatengenezwa ili kufuta kelele za wananchi...najua mwisho wa siku watalipa tu, tena with penalty!!
 
Mkuu, Mimi ni msanii kwa fani yangu wala sibabaishi ktk ninachokifanya ama kufikiria kufanya.
Hii taarifa ni wito wa kweli na hakuna blahblah ndani yake. Naamini media nyingi hili tangazo litawekwa.
Kwa uhakika zaidi wasiliana na anuani inayojionesha kwenye hilo Tangazo kwa uhakika zaidi.
Hii tabia yetu ya kupuuzia mambo kwa sababu ya uchaguzi ama ubaguzi ndo inatuletea janga kila kukicha.

Neno Msanii mmelikuza wenyewe maana hapo zamani mtu mwizi, laghai na bandidu alikuwa anaitwa PROFESA (Mfa. Prof Ndumilakuwili), Mjifunze kuheshimu fani za watu mkuu...


limepitwe na wakati
serikali imekata rufaa
...Labda kwa maslahi yako mkuuu....
 

Kwa hapa umelonga, nakumbuka waisilamu nchi nzima waliandamana dhidi ya hukumu ya mwisilam mwenzao kufungwa kwa kukashifu dini nyingine za kikiristo. hukumu hiyo ilitolewa morogoro.hawakusubiri rufaa.Hapa baada ya waislimu kuandamana, serikali na mahakama waliaingilia na ilitengua hukumu hiyo na kuachiwa huru huyo mwislam aliyekuwa amefungwa.Kwa hapa hakuna rufaa, itakayo kubalika.Swali ni kwanini serikali ilishindwa kenye mahakama ya ICC? na pia ni hatua gani zilichukuliwa tangu hawa mabwana walivyoanza kuonyesha jeuri ya kukimbilia mahakamani?Hapa watanzania hili limepangwa na mafisadi kuwa lazima walipwe , serikali kukata rufaa ni kiini macho ingekuwa madhubuti tusingeshindwa tangu kwenye kesi ya icc .maandamano ni hoja ya msingi kuonyesha watanzania si watu legelege wa kuendekeza tamithilia za mahakamani
 

Kwa hapa umelonga, nakumbuka waisilamu nchi nzima waliandamana dhidi ya hukumu ya mwisilam mwenzao kufungwa kwa kukashifu dini nyingine za kikiristo. hukumu hiyo ilitolewa morogoro.hawakusubiri rufaa.Hapa baada ya waislimu kuandamana, serikali na mahakama waliaingilia na ilitengua hukumu hiyo na kuachiwa huru huyo mwislam aliyekuwa amefungwa.Kwa hapa hakuna rufaa, itakayo kubalika.Swali ni kwanini serikali ilishindwa kenye mahakama ya ICC? na pia ni hatua gani zilichukuliwa tangu hawa mabwana walivyoanza kuonyesha jeuri ya kukimbilia mahakamani?Hapa watanzania hili limepangwa na mafisadi kuwa lazima walipwe , serikali kukata rufaa ni kiini macho ingekuwa madhubuti tusingeshindwa tangu kwenye kesi ya icc .maandamano ni hoja ya msingi kuonyesha watanzania si watu legelege wa kuendekeza tamithilia za mahakamani
 
Rufaa ya serikali hiyo hiyo iliyoingia katika mkataba huo....
Najua ni sanaa tu zinatengenezwa ili kufuta kelele za wananchi...najua mwisho wa siku watalipa tu, tena with penalty!!
maandamano ndo hoja ya msingi, nakumbuka waisilamu nchi nzima waliandamana dhidi ya hukumu ya mwisilam mwenzao kufungwa kwa kukashifu dini nyingine za kikiristo. hukumu hiyo ilitolewa morogoro.hawakusubiri rufaa.Hapa baada ya waislimu kuandamana, serikali na mahakama waliaingilia na ilitengua hukumu hiyo na kuachiwa huru huyo mwislam aliyekuwa amefungwa.Kwa hapa hakuna rufaa, itakayo kubalika.Swali ni kwanini serikali ilishindwa kenye mahakama ya ICC? na pia ni hatua gani zilichukuliwa tangu hawa mabwana walivyoanza kuonyesha jeuri ya kukimbilia mahakamani?Hapa watanzania hili limepangwa na mafisadi kuwa lazima walipwe , serikali kukata rufaa ni kiini macho ingekuwa madhubuti tusingeshindwa tangu kwenye kesi ya icc .maandamano ni hoja ya msingi kuonyesha watanzania si watu legelege wa kuendekeza tamithilia za mahakamani
 
Ole wake niskie mtu anaingiza mambo ya udini hapa, hii haina dini wala kabila msijemkadanganywa kwenye ibada zenu kuwa msiandamane ni maandamano ya dini fulani hayo, utakua ni ujinga wa hali ya juu. Kaeni kimya kabisa kama unaenda twende, kama huendi kaa kimya mie ntavaa kashati kangu ka JF
 
Hivi yale maandamano ya 14 October yaliishia wapi?? Au ndiyo kupima kina cha maji kupitia JF!!
 
Kuanzia TANESCO Ubungo mpaka Jangwani siyo kilometer kama 10!!! Haiwezekani wakakubali maandamano ya distance ndefu kiasi hicho!!
 
Ole wake niskie mtu anaingiza mambo ya udini hapa, hii haina dini wala kabila msije mkadanganywa kwenye ibada zenu kuwa msiandamane ni maandamano ya dini fulani hayo, utakua ni ujinga wa hali ya juu. Kaeni kimya kabisa kama unaenda twende, kama huendi kaa kimya mie ntavaa kashati kangu ka JF

Lazima kieleweka, nilikua nisafiri lakini siendi lazima niwepo na Mimi pia, ntakua mbele kabisa, najua kibali kimepatikana
 
Cookies are required to use this site. You must accept them to continue using the site. Learn more…