Wizara ya Afya Tanzania
Official Account
- Oct 1, 2020
- 58
- 124
JAMHURI YA MUUNGANO WA TANZANIA
WIZARA YA AFYA
WIZARA YA AFYA
TANGAZO LA AJIRA
Wizara ya Afya kupitia Kibali cha Ofisi ya Rais, Menejimenti ya Utumishi wa Umma na Utawala Bora chenye Kumb. Na. FA.97/128/01/”B”/40 cha tarehe 01 Aprili, 2022; Inatangaza nafasi za kazi 1,621 za Kada za Afya kama ifuatavyo:-
NA | KADA NA SIFA ZINAZOHITAJIKA |
1 | Daktari Bingwa Daraja la II – TGHS G (NAFASI 25) SIFA ZA MWOMBAJI Kuajiriwa waliohitimu na kufaulu Kidato cha Nne/Sita/Stashahada, wenye Shahada ya uzamili ya Udaktari Bingwa/Udaktari Bingwa wa Meno (M.Med/M.Dent au PhD kwenye fani ya Udaktari) ya miaka mitatu au zaidi kutoka vyuo vikuu vinavyotambuliwa na Serikali. Wawe wamesajiliwa na Baraza la Madaktari Tanganyika (Medical Council of Tanganyika). Kazi na majukumu:
|
2 | Daktari Daraja la II – TGHS E (NAFASI 215) SIFA ZA MWOMBAJI Kuajiriwa waliohitimu na kufaulu Kidato cha Nne/Sita/Stashahada, wenye Shahada ya Udaktari kutoka Vyuo Vikuu/Vyuo vinavyotambuliwa na Serikali waliomaliza mafunzo ya kazi“Internship” ya muda usiopungua miezi kumi na miwili na kupata usajili kutoka Baraza la Madaktari Tanganyika (Medical Council of Tanganyika). Kazi na majukumu
|
3 | Mfamasia Daraja la II - TGHS D (NAFASI 15) SIFA ZA MWOMBAJI Kuajiriwa waliohitimu na kufaulu Kidato cha Nne/Sita/Stashahada, wenye Shahada ya Famasi kutoka Chuo kinachotambuliwa na serikali aliyehitimu mafunzo ya vitendo kazini (Internship) ya mwaka mmoja ambao wamesajiliwa na Baraza la Famasi. Kazi na majukumu:
|
4 | Mhandisi Vifaa Tiba Daraja la II – TGHS D (Nafasi 17) SIFA ZA MWOMBAJI Kuajiriwa waliohitimu na kufaulu Kidato cha Nne/Sita/Stashahada, wenye Shahada ya Uhandisi (Vifaa Tiba) kutoka Chuo kinachotambuliwa na Serikali ambao wamesajiliwa na Baraza la Wahandisi Tanzania. Kazi na Majukumu Kufanya kazi za matengenezo ya vifaa tiba (Electronical Equipments) Kutunza kumbukumbu za kazi za ufundi na matengenezo ya vifaa tiba. Kufanya matengenezo ya kinga ya vifaa tiba. Kuagiza vipuli vya vifaa tiba. Kuandaa bejeti ya huduma za matengenezo ya vifaa tiba Kufanya kazi nyingine atakazopangiwa na mkuu wake wa kazi. |
5 | Fundi Sanifu Vifaa Tiba Daraja la II - TGHS B (NAFASI 40) SIFA ZA MWOMBAJI Kuajiriwa waliohitimu na kufaulu Kidato cha Nne au Sita wenye Stashahada ya kawaida ya Ufundi Sanifu Vifaa Tiba kutoka Chuo kinachotambuliwa na Serikali. Kazi na majukumu: Kufanya matengenezo ya vifaa vya huduma za tiba. Kutunza kumbukumbu za kazi za kila siku. Kuagiza vifaa na vipuli vya kutengenezea vifaa Tiba. Kutunza vifaa Tiba na vipuri. Kufanya kazi nyingine atakazopangiwa na mkuu wake wa kazi. |
6 | Afisa Muuguzi Msaidizi Daraja la II - TGHS B (NAFASI 467) SIFA ZA MWOMBAJI Kuajiriwa waliohitimu na kufaulu Kidato cha Nne au Sita wenye Stashahada (Diploma) ya Uuguzi, ya muda usiopungua miaka miwili kutoka Chuo kinachotambuliwa na Serikali, waliosajiliwa na Baraza la Wauguzi na Wakunga Tanzania. Kazi na Majukumu: Kutoa huduma za uuguzi. Kukusanya takwimu muhimu za afya. Kuwaelekeza kazi wauguzi walio chini yake. Kuelimisha wagonjwa na jamii kuhusu matatizo yao ya kiafya. Kutoa huduma za kinga na uzazi. Kufanya kazi nyingine atakazopangiwa na mkuu wake wa kazi zinazohusiana na elimu, uzoefu na ujuzi wake. |
7 | Mkemia Daraja la II – TGHS D (Nafasi 2) SIFA ZA MWOMBAJI Kuajiriwa waliohitimu na kufaulu Kidato cha Nne/Sita/Stashahada, wenye Shahada ya Sayansi (Bsc.) katika mojawapo ya fani za Kemia (Chemistry), Food Science and Technology, Health/ Medical Laboratory Sciences, Microbiology, Biochemistry, Toxocology, Environment au inayolingana na hizo kutoka chuo kinachotambuliwa na Serikali na wawe na uzoefu wa kazi kwa muda usiopungua miaka miwili. Kazi na Majukumu Kufanya uchunguzi wa kimaabara wa kikemia, kimicrobiologia wa vyakula, dawa, bidhaa za viwandani, dawa ya kulevya, maji na majitaka na sampuli za wagonjwa. Kufanya uchunguzi wa kiforensiki (Forensiki) na uchambuzi wa sumu (Toxicological Analysis). Kuchukukua sampuli zinazohitaji utaalamu maalumu na sampuli kwa ajili ya uchunguzi katika maabara nyingine. Kufundisha wanafunzi katika Taasisi mbalimbali masomo yanayoendana na taaluma zao. Kufanya utafiti. Kufanya ukaguzi wa vyakula, kemikali na mazingira. Kufanya uchunguzi wa mionzi katika sampuli mbali mbali. |
8 | Daktari wa Meno Daraja la II – TGHS E (NAFASI 15) SIFA ZA MWOMBAJI Kuajiriwa waliohitimu na kufaulu Kidato cha Nne/Sita/Stashahada, wenye Shahada ya Udaktari/Udaktari wa Meno kutoka Vyuo Vikuu/Vyuo vinavyotambuliwa na Serikali waliomaliza mafunzo ya kazi“Internship” ya muda usiopungua miezi kumi na miwili na kupata usajili kutoka Baraza la Madaktari Tanganyika (Medical Council of Tanganyika). Kazi na majukumu:
|
9 | Afisa Mteknolojia Maabara/Meno/Mionzi Daraja la II – TGHS C (Nafasi 62) Afisa Mteknolojia Daraja la II – Maabara (Nafasi 30) Afisa Mteknolojia Daraja la II – Meno (Nafasi 15) Afisa Mteknolojia Daraja la II – Mionzi (Nafasi 17) SIFA ZA MWOMBAJI Kuajiriwa waliohitimu na kufaulu Kidato cha Nne/Sita/Stashahada, wenye Shahada ya Sayansi ya Maabara za Afya/Meno kutoka Chuo kinachotambuliwa na Serikali na kusajiliwa kwa usajili wa kudumu (Full Registration Practitioners) na Baraza la Wataalamu wa Maabara za Afya. Kazi na majukumu: Afisa Mteknolojia Maabara
Kazi na majukumu: Afisa Mteknolojia Meno Kutengeneza meno ya bandia ya kuvua na kuvua ya Sehemu ya kinywa (removable Partial Dentures). Kutengeneza na kurudishia Sehemu ya Taya baada ya kufanyiwa operesheni (Obturators). Kutengeneza vifaa vya kuvua na kuvaa vya kunyoosha na kupanga meno katika mpangilio mzuri. Kutengeneza meno ya bandia aina zote yasiyo ya kuvua (Fixed Crown and Bridge). Kutengeneza Vifaa vya kutanua mataya visivyo vya kuvua ( Expanders). Kutengeza meno bandia kwa kutumia Technolojia ya kompyuta (CAD-CAM Technology). Kuelekeza wanafunzi katika Taasisi mbalimbali utaratibu unaoendana na taaluma ya maabara ya Meno. Kutekeleza mfumo wa uthibiti ubora wa huduma za maabara za Meno kulingana na maelekezo ya msimamizi wake (Quality management system) katika hospitali zenye maabara za meno. Kazi na majukumu: Afisa Mteknolojia Mionzi Kufanya vipimo vya aina mbalimbali vya radiolojia. Kutunza mitambo na vifaa vya Radiolojia katika eneo lake la kazi Kuhakikisha ubora wa picha za X-Ray Kutunza picha za wagonjwa hadi majibu yanapowafikia madaktari waliowatuma wagonjwa Kusimamia watumishi walio chini yake Kuandaa vifaa vya tiba/uchunguzi na kusimamia utakasaji vifaa katika eneo lake la kazi (sterilization) Kufanya kazi nyingine atakazopangiwa na mkuu wake wa kazi zinazohusiana na elimu, uzoefu na ujuzi wake |
10 | Mteknolojia Daraja la II – TGHS B (NAFASI 155)
Kuajiriwa wahitimu wa kidato cha nne/sita wenye Stashahada katika fani ya Uteknolojia ya muda wa miaka mitatu katika moja ya fani zilizotajwa hapo juu kutoka Chuo kinachotambuliwa na Serikali na ambao wamesajiliwa na Mabaraza ya Kitaaluma. Kazi na majukumu: Mteknolojia Daraja II – Maabara
Mteknolojia Daraja II – Radiografa – Radiolojia
Mteknolojia Daraja II – Macho
Mteknolojia Daraja II –Meno
Mteknolojia Daraja II – Dawa Kuainisha, kuandaa na kuagiza mahitaji ya dawa na vifaa tiba katika eneo lake la kazi. Kugawa dawa na vifaa tiba kwa wagonjwa na watumishi. Kuchanganya dawa. Kuhifadhi dawa na vifaa tiba. Kuelimisha jamii kuhusu matumizi sahihi ya dawa. Kukagua dawa, vifaa tiba kemikali, vitendanishi na vipodozi katika eneo lake la kazi. |
11 | Msaidizi wa Afya – TGHOS A (NAFASI 134) SIFA ZA MWOMBAJI Kuajiriwa wahitimu wa Kidato cha Nne waliofuzu mafunzo ya mwaka mmoja katika fani ya Afya, Afya Ngazi ya Jamii (NTA level 4) au mafunzo yoyote yanayofanana na hayo kutoka Vyuo vya Afya vinavyotambuliwa na Serikali. Kazi na Majukumu
|
12 | Afisa Muuguzi Daraja la II – TGHS C (NAFASI 140) SIFA ZA MWOMBAJI Kuajiriwa waliohitimu na kufaulu Kidato cha Nne/Sita/Stashahada, wenye Shahada ya Uuguzi kutoka Chuo Kikuu kinachotambuliwa na Serikali, waliohitimu mafunzo ya vitendo kazini (Internship) ya mwaka mmoja, waliosajiliwa na Baraza la Wauguzi na Wakunga Tanzania. Kazi na Majukumu:
|
13 | Mtoa Tiba kwa Vitendo Daraja la II – TGHS B ( NAFASI 15) SIFA ZA MWOMBAJI Kuajiriwa waliohitimu na kufaulu kidato cha nne/Sita, wenye stashahada ya Mtoa Tiba kwa Vitendo ya miaka mitatu (3) kutoka chuo kinachotambuliwa na serikali, aliyesajiliwa na Baraza la Madaktari la Tanganyika (MCT). Kazi na majukumu
|
14 | Mfiziotherapia Daraja la II – TGHS B (NAFASI 31) SIFA ZA MWOMBAJI Kuajiriwa waliohitimu na kufaulu Kidato cha Nne /sita wenye Stashahada ya miaka mitatu katika fani ya Fiziotherapia kutoka Chuo kinachotambuliwa na Serikali. Kazi na majukumu:
|
15 | Muuguzi II – TGHS A (NAFASI 140) SIFA ZA MWOMBAJI Kuajiriwa waliohitimu na kufaulu Kidato cha Nne au Sita wenye cheti cha Uuguzi cha miaka miwili kutoka katika Chuo kinachotambuliwa na Serikali na kuandikishwa (Enrolled) na Baraza la Wauguzi na Wakunga Tanzania. Kazi na Majukumu
|
16 | Afisa Afya Mazingira Daraja la II – TGHS C (NAFASI 40) SIFA ZA MWOMBAJI Kuajiriwa waliohitimu na kufaulu Kidato cha Nne/Sita/Stashahada, wenye Shahada ya Sayansi za Afya ya Mazingira na mafunzo kazini na kusajiliwa na Bodi ya Wataalamu wa Afya Mazingira. Kazi na Majukumu
|
17 | Afisa Afya Mazingira Msaidizi Daraja la II – TGHS B (NAFASI 56) SIFA ZA MWOMBAJI Kuajiriwa waliohitimu na kufaulu Kidato cha Nne au Sita wenye Stashahada ya Sayansi ya Afya ya Mazingira ya miaka mitatu kutoka chuo kinachotambuliwa na Serikali na awe amesajiliwa na Bodi ya Wataalamu wa Afya Mazingira. Kazi na Majukumu:
|
18 | Afisa Fiziotherapia Daraja la II -TGHS C (Nafasi 33) SIFA ZA MWOMBAJI Kuajiriwa waliohitimu na kufaulu Kidato cha Nne/Sita/Stashahada, wenye Shahada ya Fiziotherapia (BSc in Physiotherapy) kutoka Vyuo Vikuu vinavyotambuliwa na Serikali waliomaliza “Internship” na kupata usajili (Full Registration) kutoka Baraza la Madaktari Tanganyika (Medical Council of Tanganyika). Kazi na Majukumu
|
19 | Tabibu Meno Daraja la II – TGHS B (Nafasi 19) SIFA ZA MWOMBAJI Kuajiriwa waliohitimu na kufaulu Kidato cha Nne au Sita wenye Stashahada ya Tabibu Meno ya muda wa miaka mitatu kutoka Chuo kinachotambuliwa na Serikali. Kazi na Majukumu
|
- Maelekezo ya Kuzingatiwa kwa waombaji
- Waombaji watakaochaguliwa watapangiwa kazi kwenye maeneo yenye upungufu mkubwa wa wataalam wa Kada za Afya, na hakutakuwa na kubadilisha kituo pindi watakapopata nafasi hiyo. Maeneo hayo ni kama ifuatavyo; Hospitali za Rufaa za Mikoa; (1) Kigoma; (2) Katavi; (3) Sumbawanga; (4) Songwe; (5) Njombe; (6) Ruvuma; (7) Mtwara; (8) Lindi; (9) Simiyu; (10) Geita; (11) Shinyanga; (12) Tabora; (13) Singida; (14) Manyara; na (15) Mara; Hospitali za Kanda, Chato na Mtwara, Hospitali ya Magonjwa Ambukizi Kibong’oto pamoja na Vyuo vya Afya. Hivyo, waombaji wawe tayari kupangiwa katika maeneo yaliyoainishwa hapo juu.
- Waombaji ambao hawatakuwa tayari kwenda kwenye maeneo tajwa hapo juu inashauriwa kutotuma maombi.
- Waliopo masomoni hawaruhusiwi kuomba nafasi hizi za ajira.
- Kwenye barua ya maombi, mwombaji atapaswa kutaja maeneo matatu ambayo angependa kupangiwa kazi endapo atachaguliwa.
- Mwombaji mwenye nia ya kwenda kufundisha katika Vyuo vya Afya aainishe wakati wa kutuma maombi kwenye mfumo pamoja na barua ya maombi.
- Nakala za vyeti vyote vithibitishwe na Mahakama au Wakili.
- Waombaji wanaojitolea katika Hospitali za Rufaa za Kanda/Mikoa mbalimbali waandikiwe barua na Mganga Mfawidhi wa Hospitali husika kuthibitisha kujitolea kwao.
- Sifa za ujumla kwa Mwombaji:
ii. Awe na umri usiopungua miaka 18 na usiozidi miaka 45.
iii. Asiwe Mwajiriwa wa Serikali au Mwajiriwa wa Hospitali za Mashirika ya Dini ambaye mshahara wake unalipwana Serikali.
iv. Mwombaji aliyewahi kuajiriwa Serikalini na kupata cheki namba, atatakiwa kuzingatia Utaratibu wa kuomba Kibali cha kurejea katika Utumishi wa Umma na kuendelea kutumia Cheki Namba baada ya kuacha kazi kama ilivyobainishwa kwenye Waraka Na. CCB.228/271/01 wa tarehe 7 Agosti, 2012.
v. Mwombaji awe na sifa na weledi kwa Mujibu wa Waraka wa Maendeleo ya Utumishi Namba. 1 wa mwaka 2009 kuhusu kada zilizo chini ya Wizara ya Afya kama zilivyoainishwa hapo juu
- Maombi yote yaambatishwe na;-
- Nakala ya cheti cha kuzaliwa.
- Nakala ya cheti cha Kidato cha Nne au/na cha Sita au Stashahada kulingana na Kada ya Mwombaji. Kwa aliyesoma nje ya nchi au mitaala ya nje waambatishe cheti cha Ithibati kutoka Baraza la Mitihani Tanzania (NECTA).
- Nakala ya Vyeti vya Taaluma (Cheti na Transcripts). Aidha, waliosoma vyuo vya nje ya Nchi, waambatishe cheti cha Ithibati kutoka TCU.
- Wasifu (C.V).
- Nakala ya cheti cha Usajili na Leseni hai ya taaluma husika (Full Registration & Valid Licence).
- Nakala ya cheti cha Mafunzo kwa Vitendo (Internship)
- Picha ndogo (passport size) moja ya hivi karibuni.
- Nakala ya kitambulisho cha uraia (NIDA)/Namba ya Utambulisho ya NIDA.
- Iwapo majina yako yanatofautiana katika vyeti vyako pamoja na cheti cha kuzaliwa na NIDA hakikisha unawasilisha kiapo cha majina (Deed Pool) kutoka kwa Msajili wa Viapo na kusajiliwa na Msajili wa Hati, Wizara ya Ardhi na Maendeleo ya Makazi.
- Namna ya kuwasilisha maombi:
Waombaji wote mnakumbushwa kuwa makini mnapowasilisha maombi kuhakikisha umejaza vizuri vipengele vyote vinavyotakiwa kwenye mfumo ikiwa ni pamoja na kuambatisha nyaraka zote zinazohitajika.
Imetolewa na:-
Prof. Abel Makubi
Katibu Mkuu
Wizara ya Afya