Tangazo la ajira 1650 Wizara ya Afya

Wizara ya Afya Tanzania

Official Account
Oct 1, 2020
58
124
JAMHURI YA MUUNGANO WA TANZANIA

WIZARA YA AFYA

NEMBO YA TAIFA.png

TANGAZO LA AJIRA

Wizara ya Afya kupitia Kibali cha Ofisi ya Rais, Menejimenti ya Utumishi wa Umma na Utawala Bora chenye Kumb. Na. FA.97/128/01/”B”/40 cha tarehe 01 Aprili, 2022; Inatangaza nafasi za kazi 1,621 za Kada za Afya kama ifuatavyo:-

NA
KADA NA SIFA ZINAZOHITAJIKA
1Daktari Bingwa Daraja la II – TGHS G (NAFASI 25)

SIFA ZA MWOMBAJI

Kuajiriwa waliohitimu na kufaulu Kidato cha Nne/Sita/Stashahada, wenye Shahada ya uzamili ya Udaktari Bingwa/Udaktari Bingwa wa Meno (M.Med/M.Dent au PhD kwenye fani ya Udaktari) ya miaka mitatu au zaidi kutoka vyuo vikuu vinavyotambuliwa na Serikali. Wawe wamesajiliwa na Baraza la Madaktari Tanganyika (Medical Council of Tanganyika).

Kazi na majukumu:
  1. Kufanya kazi zote za matibabu hospitalini zinazohusiana na magonjwa mbalimbali katika fani husika.
  2. Kufundisha wanafunzi katika vyuo vya afya vilivyo eneo lake la kazi
  3. Kuchunguza, kufuatilia na kuzuia milipuko ya magonjwa
  4. Kutayarisha elimu ya kujiendeleza ya watumishi wa afya.
  5. Kufundisha na kuelekeza watumishi walio chini yake
  6. Kusimamia wafanyakazi walio chini yake
  7. Kubuni, kuendesha na kutathimini utafiti na kusambaza matokeo
  8. Kubuni na kutayarisha mikakati ya kuinua ubora wa huduma ya fani yake
  9. Kutoa huduma za outreach katika kanda
  10. Kutoa huduma za medical legal
  11. Kushiriki katika kutengeneza na kusimamia utekelezaji wa Sera na Mipango ya Serikali juu ya afya
  12. Kushauri wizara kuhusu uendeshaji wa shughuli za afya nchini.
  13. Kushiriki katika kamati ya jopo la madaktari (medical board) kwa ajili ya kustaafisha wafanyakazi kwa matatizo ya kiafya.
  14. Kutayarisha mitaala ya elimu ya kujiendeleza ya watumishi wa afya.
  15. Kuandaa mipango na makisio ya bajeti ya huduma za afya
2Daktari Daraja la II – TGHS E (NAFASI 215)

SIFA ZA MWOMBAJI

Kuajiriwa waliohitimu na kufaulu Kidato cha Nne/Sita/Stashahada, wenye Shahada ya Udaktari kutoka Vyuo Vikuu/Vyuo vinavyotambuliwa na Serikali waliomaliza mafunzo ya kazi“Internship” ya muda usiopungua miezi kumi na miwili na kupata usajili kutoka Baraza la Madaktari Tanganyika (Medical Council of Tanganyika).

Kazi na majukumu

  1. Kufanya kazi zote za matibabu hospitalini zinazohusiana na magonjwa mbalimbali yakiwemo magonjwa ya watoto, magonjwa ya akina mama na upasuaji wa kawaida na wa dharura.
  2. Kutoa na kusimamia elimu ya afya pamoja na kuboresha afya ya jamii katika Wilaya na Mikoa au eneo lake la kazi.
  3. Kuchunguza, kufuatilia na kuzuia milipuko ya magonjwa.
  4. Kutunza takwimu na kuzitumia kama inavyoelekezwa katika misingi ya MTUHA.
  5. Kupanga na kutathimini huduma za afya katika eneo lake la kazi.
  6. Kufundisha wanafunzi na watumishi waliopo kwenye eneo la kazi.
  7. Kusimamia na kuelekeza wafanyakazi walio chini yake.
  8. Kubuni na kuendesha utafiti na kusambaza matokeo.
  9. Kubuni na kutayarisha mikakati ya kuinua ubora wa huduma ya fani yake.
  10. Kuandaa mipango na makisio ya bajeti ya huduma za afya.
  11. Kushiriki, kuhakiki na kuboresha huduma za afya (medical audit and quality improvement).
  12. Kufanya kazi nyingine atakazopangiwa na mkuu wake wa kazi zinazohusiana na elimu, uzoefu na ujuzi wake.
3Mfamasia Daraja la II - TGHS D (NAFASI 15)

SIFA ZA MWOMBAJI

Kuajiriwa waliohitimu na kufaulu Kidato cha Nne/Sita/Stashahada, wenye Shahada ya Famasi kutoka Chuo kinachotambuliwa na serikali aliyehitimu mafunzo ya vitendo kazini (Internship) ya mwaka mmoja ambao wamesajiliwa na Baraza la Famasi.

Kazi na majukumu:
  1. Kuainisha mahitaji ya mwaka ya dawa na vifaa na kuandaa bajeti yake.
  2. Kuagiza, kununua, kuhifadhi na kusambaza dawa na vifaa tiba .
  3. katika kituo chake cha kazi.
  4. Kuweka kumbukumbu za dawa.
  5. Kuandaa orodha ya dawa za hospitali (Hospital Fomulary) kwa matumizi ya kituo anapofanya kazi.
  6. Kutoa dawa na vifaa tiba kwa wagonjwa.
  7. Kusimamia matumizi sahihi ya dawa.
  8. Kutengeneza dawa (compounding) kwa matumizi ya kituo anapofanya kazi
  9. Kukagua maduka ya dawa katika sekta binafsi.
  10. Kutoa taarifa juu ya madhara yatokanayo na matumizi ya dawa (adverse drug reaction).
  11. Kuelimisha watumishi walio chini yake, watumishi wengine wa sekta ya afya na jamii juu ya matumizi sahihi ya dawa.
  12. Kusimamia utekelezaji wa Sera ya Taifa ya Dawa katika kituo anapofanya kazi.
  13. Kufanya kazi nyingine atakazopangiwa na mkuu wake wa kazi zinazohusiana na elimu, uzoefu na ujuzi wake.
4Mhandisi Vifaa Tiba Daraja la II – TGHS D (Nafasi 17)

SIFA ZA MWOMBAJI

Kuajiriwa waliohitimu na kufaulu Kidato cha Nne/Sita/Stashahada, wenye Shahada ya Uhandisi (Vifaa Tiba) kutoka Chuo kinachotambuliwa na Serikali ambao wamesajiliwa na Baraza la Wahandisi Tanzania.

Kazi na Majukumu

Kufanya kazi za matengenezo ya vifaa tiba (Electronical Equipments)
Kutunza kumbukumbu za kazi za ufundi na matengenezo ya vifaa tiba.
Kufanya matengenezo ya kinga ya vifaa tiba.
Kuagiza vipuli vya vifaa tiba.
Kuandaa bejeti ya huduma za matengenezo ya vifaa tiba Kufanya kazi nyingine atakazopangiwa na mkuu wake wa kazi.
5Fundi Sanifu Vifaa Tiba Daraja la II - TGHS B (NAFASI 40)

SIFA ZA MWOMBAJI

Kuajiriwa waliohitimu na kufaulu Kidato cha Nne au Sita wenye Stashahada ya kawaida ya Ufundi Sanifu Vifaa Tiba kutoka Chuo kinachotambuliwa na Serikali.

Kazi na majukumu:

Kufanya matengenezo ya vifaa vya huduma za tiba.
Kutunza kumbukumbu za kazi za kila siku.
Kuagiza vifaa na vipuli vya kutengenezea vifaa Tiba.
Kutunza vifaa Tiba na vipuri.
Kufanya kazi nyingine atakazopangiwa na mkuu wake wa kazi.
6Afisa Muuguzi Msaidizi Daraja la II - TGHS B (NAFASI 467)

SIFA ZA MWOMBAJI

Kuajiriwa waliohitimu na kufaulu Kidato cha Nne au Sita wenye Stashahada (Diploma) ya Uuguzi, ya muda usiopungua miaka miwili kutoka Chuo kinachotambuliwa na Serikali, waliosajiliwa na Baraza la Wauguzi na Wakunga Tanzania.

Kazi na Majukumu:

Kutoa huduma za uuguzi.
Kukusanya takwimu muhimu za afya.
Kuwaelekeza kazi wauguzi walio chini yake.
Kuelimisha wagonjwa na jamii kuhusu matatizo yao ya kiafya.
Kutoa huduma za kinga na uzazi.
Kufanya kazi nyingine atakazopangiwa na mkuu wake wa kazi zinazohusiana na elimu, uzoefu na ujuzi wake.
7Mkemia Daraja la II – TGHS D (Nafasi 2)

SIFA ZA MWOMBAJI

Kuajiriwa waliohitimu na kufaulu Kidato cha Nne/Sita/Stashahada, wenye Shahada ya Sayansi (Bsc.) katika mojawapo ya fani za Kemia (Chemistry), Food Science and Technology, Health/ Medical Laboratory Sciences, Microbiology, Biochemistry, Toxocology, Environment au inayolingana na hizo kutoka chuo kinachotambuliwa na Serikali na wawe na uzoefu wa kazi kwa muda usiopungua miaka miwili.

Kazi na Majukumu

Kufanya uchunguzi wa kimaabara wa kikemia, kimicrobiologia wa vyakula, dawa, bidhaa za viwandani, dawa ya kulevya, maji na majitaka na sampuli za wagonjwa.
Kufanya uchunguzi wa kiforensiki (Forensiki) na uchambuzi wa sumu (Toxicological Analysis).
Kuchukukua sampuli zinazohitaji utaalamu maalumu na sampuli kwa ajili ya uchunguzi katika maabara nyingine.
Kufundisha wanafunzi katika Taasisi mbalimbali masomo yanayoendana na taaluma zao.
Kufanya utafiti.
Kufanya ukaguzi wa vyakula, kemikali na mazingira.
Kufanya uchunguzi wa mionzi katika sampuli mbali mbali.

8Daktari wa Meno Daraja la II – TGHS E (NAFASI 15)

SIFA ZA MWOMBAJI

Kuajiriwa waliohitimu na kufaulu Kidato cha Nne/Sita/Stashahada, wenye Shahada ya Udaktari/Udaktari wa Meno kutoka Vyuo Vikuu/Vyuo vinavyotambuliwa na Serikali waliomaliza mafunzo ya kazi“Internship” ya muda usiopungua miezi kumi na miwili na kupata usajili kutoka Baraza la Madaktari Tanganyika (Medical Council of Tanganyika).

Kazi na majukumu:
  1. Kufanya kazi zote za matibabu hospitalini zinazohusiana na magonjwa ya kinywa na meno.
  2. Kushiriki katika kutengeneza na kusimamia utekelezaji wa Sera ya Serikali juu ya afya ya kinywa na meno.
  3. Kusimamia utekelezaji wa mipango ya kitaifa inayohusu afya ya kinywa na meno.
  4. Kutayarisha elimu ya kujiendeleza ya watumishi wa afya ya kinywa na meno.
  5. Kuchunguza, kufuatilia na kuzuia milipuko ya magonjwa .
  6. Kubuni na kutayarisha mikakati ya kuinua ubora wa huduma ya fani yake.
  7. Kuandaa upatikanaji wa vifaa na mahitaji mengine ya tiba ya meno katika ngazi ya taifa.
  8. Kushauri wizara kuhusu uendeshaji wa shughuli za afya ya kinywa na meno nchini.
  9. Kubuni, kusimamia na kuendesha utafiti katika maeneo mbalimbali ya afya.
  10. Kufundisha wanafunzi katika vyuo vya afya vilivyo katika eneo lake la kazi.
9Afisa Mteknolojia Maabara/Meno/Mionzi Daraja la II – TGHS C (Nafasi 62)
Afisa Mteknolojia Daraja la II – Maabara (Nafasi 30)
Afisa Mteknolojia Daraja la II – Meno (Nafasi 15)
Afisa Mteknolojia Daraja la II – Mionzi (Nafasi 17)

SIFA ZA MWOMBAJI

Kuajiriwa waliohitimu na kufaulu Kidato cha Nne/Sita/Stashahada, wenye Shahada ya Sayansi ya Maabara za Afya/Meno kutoka Chuo kinachotambuliwa na Serikali na kusajiliwa kwa usajili wa kudumu (Full Registration Practitioners) na Baraza la Wataalamu wa Maabara za Afya.
Kazi na majukumu: Afisa Mteknolojia Maabara
  1. Kutoa sampuli ya vipimo vya maabara.
  2. Kufanya uchunguzi wa vipimo vya maabara.
  3. Kutunza kumbukumbu za majibu ya vipimo vya maabara.
  4. Kuandaa na kutumia miongozo ya kufanyia vipimo vya upimaji.
  5. Kusimamia utunzaji wa Kumbukumbu za matokeo ya vipimo vya maabara katika Rejesta.
  6. Kutunza vifaa na Vitendea kazi vya Maabara.
  7. Kusimamia na kufanya matengenezo kinga ya kila siku ya mashine za Maabara.
  8. Kuthibitisha na Kutoa tafsiri ya matokeo ya vipimo vya maabara.
  9. Kufanya kazi nyingine atakazopangiwa na mkuu wake wa kazi zinazohusiana na elimu, uzoefu na ujuzi wake.
  10. Kuhakiki na kuthibitisha njia mpya za uchunguzi wa kimaabara (new method validation and verification).

Kazi na majukumu: Afisa Mteknolojia Meno
Kutengeneza meno ya bandia ya kuvua na kuvua ya Sehemu ya kinywa (removable Partial Dentures).
Kutengeneza na kurudishia Sehemu ya Taya baada ya kufanyiwa operesheni (Obturators).
Kutengeneza vifaa vya kuvua na kuvaa vya kunyoosha na kupanga meno katika mpangilio mzuri.
Kutengeneza meno ya bandia aina zote yasiyo ya kuvua (Fixed Crown and Bridge).
Kutengeneza Vifaa vya kutanua mataya visivyo vya kuvua ( Expanders).
Kutengeza meno bandia kwa kutumia Technolojia ya kompyuta (CAD-CAM Technology).
Kuelekeza wanafunzi katika Taasisi mbalimbali utaratibu unaoendana na taaluma ya maabara ya Meno.
Kutekeleza mfumo wa uthibiti ubora wa huduma za maabara za Meno kulingana na maelekezo ya msimamizi wake (Quality management system) katika hospitali zenye maabara za meno.

Kazi na majukumu: Afisa Mteknolojia Mionzi
Kufanya vipimo vya aina mbalimbali vya radiolojia.
Kutunza mitambo na vifaa vya Radiolojia katika eneo lake la kazi
Kuhakikisha ubora wa picha za X-Ray
Kutunza picha za wagonjwa hadi majibu yanapowafikia madaktari waliowatuma wagonjwa
Kusimamia watumishi walio chini yake
Kuandaa vifaa vya tiba/uchunguzi na kusimamia utakasaji vifaa katika eneo lake la kazi (sterilization)
Kufanya kazi nyingine atakazopangiwa na mkuu wake wa kazi
zinazohusiana na elimu, uzoefu na ujuzi wake
10Mteknolojia Daraja la II – TGHS B (NAFASI 155)
  • Mteknolojia Daraja II – Maabara (Nafasi 28)
  • Mteknolojia Daraja II – Radiografa – Radiolojia (Nafasi 33)
  • Mteknolojia Daraja II – Macho (Nafasi 33)
  • Mteknolojia Daraja II –Meno (Nafasi 33)
  • Mteknolojia Daraja II – Dawa (Nafasi 28)
SIFA ZA MWOMBAJI
Kuajiriwa wahitimu wa kidato cha nne/sita wenye Stashahada katika fani ya Uteknolojia ya muda wa miaka mitatu katika moja ya fani zilizotajwa hapo juu kutoka Chuo kinachotambuliwa na Serikali na ambao wamesajiliwa na Mabaraza ya Kitaaluma.

Kazi na majukumu:

Mteknolojia Daraja II – Maabara

  1. Kupima sampuli zinazoletwa maabara.
  2. Kuhifadhi sampuli zinazotakiwa kufanyiwa uchunguzi au kupelekwa Maabara za ngazi za juu.
  3. Kufanya kazi za ukaguzi wa maabara, vitendanishi, vifaa, kemikali na hifadhi ya kemikali.
  4. Kuweka kumbukumbu za maabara ambazo zimepatikana wakati wa uchunguzi.
  5. Kufundisha watumishi walio chini yake.
  6. Kufanya kazi nyingine atakazopangiwa na mkuu wake wa kazi zinazohusiana na elimu, uzoefu na ujuzi wake.

Mteknolojia Daraja II – Radiografa – Radiolojia
  1. Kuwapima wagonjwa wanaolekezwa kwenye eneo lake la kazi
  2. Kutunza mitambo na vifaa vya Radiolojia katika eneo lake la kazi
  3. Kukagua picha za X-Ray zilizopimwa kwa ubora na kutosheleza (diagnostic quality).
  4. Kutunza picha za wagonjwa hadi majibu yanapowafikia madaktari waliowatuma wagonjwa.
  5. Kusimamia watumishi walio chini yake.
  6. Kutoa Ushauri kuhusu masuala ya na kazi za Radiolojia na Mionzi katika eneo lake la kazi.
  7. Kuandaa vifaa vya tiba/uchunguzi na kusimamia utakasaji vifaa katika eneo lake la kazi (sterilization).
  8. Kutoa mafunzo ya awali kwa watumishi wanaopangiwa kazi katika eneo lake la kazi.
  9. Kufanya kazi nyingine atakazopangiwa na mkuu wake wa kazi zinazohusiana na elimu, uzoefu na ujuzi wake

Mteknolojia Daraja II – Macho
  1. Kufanya uchunguzi wa upeo wa kuona na kutibu.
  2. Kurufaa wagonjwa kwenye ngazi za juu, zinazohitaji utaalamu zaidi.
  3. Kutoa ushauri nasaha.
  4. Kutunza na kurekebisha uharibifu wa vifaa vya macho.
  5. Kutengeneza miwani na kurekebisha miwani aina zote.

Mteknolojia Daraja II –Meno
  1. Kuchukua vipimo vya meno ya wagonjwa na kuvifanyia kazi.
  2. Kutunza mashine na vifaa vya matibabu na vifaa vya maabara ya meno.
  3. Kutunza kumbukumbu za wagonjwa wanaokuja kwa ajili ya matatizo ya meno.
  4. Kubuni na kutengeneza meno ya bandia na viungo bandia vya taya.
  5. Kufanya kazi nyingine atakazopangiwa na mkuu wake wa kazi zinazohusiana na elimu, uzoefu na ujuzi wake.

Mteknolojia Daraja II – Dawa
Kuainisha, kuandaa na kuagiza mahitaji ya dawa na vifaa tiba katika eneo lake la kazi.
Kugawa dawa na vifaa tiba kwa wagonjwa na watumishi.
Kuchanganya dawa.
Kuhifadhi dawa na vifaa tiba.
Kuelimisha jamii kuhusu matumizi sahihi ya dawa.
Kukagua dawa, vifaa tiba kemikali, vitendanishi na vipodozi katika eneo lake la kazi.
11Msaidizi wa Afya – TGHOS A (NAFASI 134)

SIFA ZA MWOMBAJI

Kuajiriwa wahitimu wa Kidato cha Nne waliofuzu mafunzo ya mwaka mmoja katika fani ya Afya, Afya Ngazi ya Jamii (NTA level 4) au mafunzo yoyote yanayofanana na hayo kutoka Vyuo vya Afya vinavyotambuliwa na Serikali.

Kazi na Majukumu

  1. Kufanya usafi wa vifaa vya kazi, maeneo ya kutolea huduma za afya pamoja na mazingira yanayozunguka kituo.
  2. Kusaidia mgonjwa asiyejiweza kwa mfano, kumlisha, kwenda haja, usafi wa mwili, nk.
  3. Kukusanya nguo chafu na kuzipeleka kufuliwa (Laundry).
  4. Kupeleka sampuli za mgonjwa kwa ajili ya vipimo vya maabara na kufuatilia majibu.
  5. Kuwasafirisha wagonjwa kati ya ldara moja na nyingine ndani ya kituo cha kutolea huduma za afya.
  6. Kutunza vifaa vya usafi.
  7. Kupokea, kupeleka chumba cha kuhifadhi, kuosha na kutunza maiti.
  8. Kufanya shughuli nyingine atakazopangiwa na kiongozi wake wa kazi.
  9. Kuelimisha jamii juu ya umuhimu wa usafi wa mazingira na mwili ili kujikinga na milipuko ya magonjwa.
  10. Kufanya shughuli nyingine atakazopangiwa na kiongozi wake wa kazi.
12Afisa Muuguzi Daraja la II – TGHS C (NAFASI 140)

SIFA ZA MWOMBAJI

Kuajiriwa waliohitimu na kufaulu Kidato cha Nne/Sita/Stashahada, wenye Shahada ya Uuguzi kutoka Chuo Kikuu kinachotambuliwa na Serikali, waliohitimu mafunzo ya vitendo kazini (Internship) ya mwaka mmoja, waliosajiliwa na Baraza la Wauguzi na Wakunga Tanzania.

Kazi na Majukumu:
  1. Kufanya kazi za kiuguzi za kuhudumia wateja katika jamii, hospitali na sehemu zote zinapotolewa huduma za afya.
  2. Kukusanya takwimu muhimu za afya.
  3. Kuwaelekeza na kusimamia wauguzi walio chini yake.
  4. Kutoa huduma kwa wagonjwa majumbani.
  5. Kutoa ushauri nasaha.
  6. Kutayarisha mpango wa kazi kwa ajili ya huduma za uuguzi.
  7. Kutoa huduma za kinga na uzazi.
  8. Kuelimisha wagonjwa na jamii.

13Mtoa Tiba kwa Vitendo Daraja la II – TGHS B ( NAFASI 15)
SIFA ZA MWOMBAJI

Kuajiriwa waliohitimu na kufaulu kidato cha nne/Sita, wenye stashahada ya Mtoa Tiba kwa Vitendo ya miaka mitatu (3) kutoka chuo kinachotambuliwa na serikali, aliyesajiliwa na Baraza la Madaktari la Tanganyika (MCT).

Kazi na majukumu
  • Kutathmini wagonjwa wa viungo na wa akili ili kutambua na mahitaji ya matibabu.
  • Kutathmini uhitaji wa vifaa saidizi kwa wenye uhitaji wa vifaa hivyo.
  1. Kufuatilia matumizi ya vifaa tiba, kuweka kumbukumbu kulingana na mazingira wagonjwa wanayoishi na aina ya vifaa tiba wanavyotumia.
  2. Kutoa usaidizi wa tiba kwa vitendo kwa maelekezo ya Afisa Mtoa Tiba kwa Vitendo.
  • Kutoa elimu ya afya kwa jamii kuhusu kutambua dalili na kuzuia ulemavu.
  • Kutimiza majukumu mengine atakayopangiwa na mkuu wake wa kazi yanayohusiana na elimu, ujuzi na uzoefu wake.
14Mfiziotherapia Daraja la II – TGHS B (NAFASI 31)

SIFA ZA MWOMBAJI

Kuajiriwa waliohitimu na kufaulu Kidato cha Nne /sita wenye Stashahada ya miaka mitatu katika fani ya Fiziotherapia kutoka Chuo kinachotambuliwa na Serikali.

Kazi na majukumu:
  1. Kutoa tiba kwa kuzoeza viungo/ kwa vitendo.
  2. Kukusanya na kutunza takwimu na taarifa za mgonjwa.
  3. Kutunza vifaa vya Idara.
  4. Kutoa elimu ya Afya kwa jamii kuhusu kutambua dalili na kuzuia ulemavu.
  5. Kufanya kazi nyingine atakazopangiwa na mkuu wake wa kazi.
15Muuguzi II – TGHS A (NAFASI 140)

SIFA ZA MWOMBAJI

Kuajiriwa waliohitimu na kufaulu Kidato cha Nne au Sita wenye cheti cha Uuguzi cha miaka miwili kutoka katika Chuo kinachotambuliwa na Serikali na kuandikishwa (Enrolled) na Baraza la Wauguzi na Wakunga Tanzania.

  2. Kusimamia na kuratibu kazi zote za wahudumu wa afya katika sehemu yake ya kazi.
  3. Kukusanya takwimu na kutayarisha taarifa za utendaji wake wa kazi.
  4. Kutoa huduma kwa wagonjwa majumbani.
  5. Kutoa ushauri nasaha.
  6. Kutoa huduma za kinga na uzazi wa mpango.
  7. Kutoa huduma za uzazi na afya ya mtoto.
  8. Kuelimisha wagonjwa na jamii kuhusu matatizo yao ya kiafya.
  9. Kufuatilia utunzaji wa vitendea kazi katika maeneo yake ya kazi.
  10. Kufanya kazi nyingine atakazopangiwa na mkuu wake wa kazi zinazohusiana na elimu, uzoefu na ujuzi wake.
16Afisa Afya Mazingira Daraja la II – TGHS C (NAFASI 40)

SIFA ZA MWOMBAJI

Kuajiriwa waliohitimu na kufaulu Kidato cha Nne/Sita/Stashahada, wenye Shahada ya Sayansi za Afya ya Mazingira na mafunzo kazini na kusajiliwa na Bodi ya Wataalamu wa Afya Mazingira.

Kazi na Majukumu

  1. Kutoa ushauri na kusimamia njia bora za usambazaji wa maji safi na salama na utupaji wa taka.
  2. Kuelimisha jamii juu ya mbinu za kujikinga na kupambana na mlipuko ya magonjwa.
  3. Kukusanya na kuchambua takwimu za Afya ya Mazingira.
  4. Kusimamia utekelezaji wa Sheria zinazohusu Afya ya Mazingira.
  5. Kuandaa taarifa za utekelezaji na kuziwasilisha katika mamlaka husika.
  6. Kuandaa na kufuatilia mikakati ya kuboresha na kusimamia usalama na afya kazini.
  7. Kuhakiki afya bandarini na mipakani.
  8. Kuratibu na kuhakiki kaguzi za vyakula, maji, kemikali, viwanda, sehemu za kazi na maeneo ya jumuiya.

17Afisa Afya Mazingira Msaidizi Daraja la II – TGHS B (NAFASI 56)

SIFA ZA MWOMBAJI

Kuajiriwa waliohitimu na kufaulu Kidato cha Nne au Sita wenye Stashahada ya Sayansi ya Afya ya Mazingira ya miaka mitatu kutoka chuo kinachotambuliwa na Serikali na awe amesajiliwa na Bodi ya Wataalamu wa Afya Mazingira.
Kazi na Majukumu:
  1. Kudhibiti na kuzuia milipuko ya magonjwa .
  2. Kupambana na kuzuia wadudu na wanyama wanaoeneza magonjwa.
  3. Kusimamia uzikaji wa maiti zisizotambuliwa na zile zinazotokana na magonjwa ya kuambukiza.
  4. Kuandaa taarifa mbali mbali za Afya ya Mazingira katika ngazi ya kata na kuziwasilisha katika mamlaka husika.
  5. Kukusanya na kuchambua takwimu za Afya ya Mazingira, katika kata na kutoa mrejesho ili kuchukua hatua zinazostahili.
  6. Kutoa elimu ya afya ya mazingira kwa jamii.
  7. Kukagua mazingira katika sehemu zinapotengenezwa vyakula ili kuhakikisha usalama na afya ya jamii.
  8. Kusimamia sheria za afya ya mazingira katika ngazi ya Kata pamoja na kusaidia jamii katika kutengeneza sheria ndogondogo.
  9. Kuhamasisha jamii katika kuboresha vyanzo vya maji na Usafi wa Mazingira.
  10. Kuhamasisha jamii kuhusu utekelezaji wa Huduma za Afya ya Msingi katika ngazi ya Kata.
  11. Kufanya kazi nyingine atakazopangiwa na mkuu wake wa kazi zinazohusiana na elimu, uzoefu na ujuzi wake

18Afisa Fiziotherapia Daraja la II -TGHS C (Nafasi 33)

SIFA ZA MWOMBAJI

Kuajiriwa waliohitimu na kufaulu Kidato cha Nne/Sita/Stashahada, wenye Shahada ya Fiziotherapia (BSc in Physiotherapy) kutoka Vyuo Vikuu vinavyotambuliwa na Serikali waliomaliza “Internship” na kupata usajili (Full Registration) kutoka Baraza la Madaktari Tanganyika (Medical Council of Tanganyika).
Kazi na Majukumu
  1. Kufanya kazi zote za Mfiziotherapia hospitalini zinazohusiana na magonjwa mbalimbali yakiwemo magonjwa ya watoto, wazee, na wote waliolazwa.
  2. Kuchunguza mgonjwa, kupanga matibabu kulingana na tatizo la mgonjwa na kufuatilia hali ya mgonjwa husika.
  3. Kutoa ushauri wa tiba na rufaa ya mgonjwa kwa kada nyingine za afya kulingana na tatizo la mgonjwa.
  4. Kutoa na kusimamia elimu ya Fiziotherapia, Utengamao na tiba na kuboresha afya ya mwili na viungo katika Wilaya na Mikoa au eneo lake la kazi.
  5. Kutoa ushauri nasaha wa utengamao kwa wagonjwa katika jamii (CBR).
  6. Kutunza takwimu za wagonjwa wa Fiziotherapia na watu wenye ulemavu na kuzitumia kama inavyoelekezwa katika misingi ya MTUHA.
  7. Kutathimini huduma za Fiziotherapia na Utengamao katika eneo lake la kazi.
  8. Kusimamia na kuelekeza watumishi walio chini yake.
  9. Kuandaa mipango na makisio ya bajeti ya huduma za Fiziotherapia katika eneo lake la kazi.
19Tabibu Meno Daraja la II – TGHS B (Nafasi 19)

SIFA ZA MWOMBAJI

Kuajiriwa waliohitimu na kufaulu Kidato cha Nne au Sita wenye Stashahada ya Tabibu Meno ya muda wa miaka mitatu kutoka Chuo kinachotambuliwa na Serikali.
Kazi na Majukumu
  1. Kutambua na kutibu magonjwa ya kawaida.
  2. Kusimamia utendaji wa watumishi walio chini yake na kufanya upasuaji mdogo.
  3. Kushiriki katika kupanga na kutekeleza Huduma za Afya Msingi.
  4. Kushauri na kuhamasisha wananchi kuchangia huduma za Afya za Mfuko wa Afya ya Jamii.
  5. Kuweka kumbukumbu za vifaa na zana za kutolea huduma.
  6. Kuweka kumbukumbu, kuandaa na kutoa taarifa za utekelezaji.
  7. Kufanya kazi nyingine atakazopangiwa na mkuu wake wa kazi.

  1. Maelekezo ya Kuzingatiwa kwa waombaji
  1. Waombaji watakaochaguliwa watapangiwa kazi kwenye maeneo yenye upungufu mkubwa wa wataalam wa Kada za Afya, na hakutakuwa na kubadilisha kituo pindi watakapopata nafasi hiyo. Maeneo hayo ni kama ifuatavyo; Hospitali za Rufaa za Mikoa; (1) Kigoma; (2) Katavi; (3) Sumbawanga; (4) Songwe; (5) Njombe; (6) Ruvuma; (7) Mtwara; (8) Lindi; (9) Simiyu; (10) Geita; (11) Shinyanga; (12) Tabora; (13) Singida; (14) Manyara; na (15) Mara; Hospitali za Kanda, Chato na Mtwara, Hospitali ya Magonjwa Ambukizi Kibong’oto pamoja na Vyuo vya Afya. Hivyo, waombaji wawe tayari kupangiwa katika maeneo yaliyoainishwa hapo juu.
  1. Waombaji ambao hawatakuwa tayari kwenda kwenye maeneo tajwa hapo juu inashauriwa kutotuma maombi.
  2. Waliopo masomoni hawaruhusiwi kuomba nafasi hizi za ajira.
  3. Kwenye barua ya maombi, mwombaji atapaswa kutaja maeneo matatu ambayo angependa kupangiwa kazi endapo atachaguliwa.
  4. Mwombaji mwenye nia ya kwenda kufundisha katika Vyuo vya Afya aainishe wakati wa kutuma maombi kwenye mfumo pamoja na barua ya maombi.
  5. Nakala za vyeti vyote vithibitishwe na Mahakama au Wakili.
  6. Waombaji wanaojitolea katika Hospitali za Rufaa za Kanda/Mikoa mbalimbali waandikiwe barua na Mganga Mfawidhi wa Hospitali husika kuthibitisha kujitolea kwao.
  1. Sifa za ujumla kwa Mwombaji:
i. Awe raia wa Tanzania.
ii. Awe na umri usiopungua miaka 18 na usiozidi miaka 45.
iii. Asiwe Mwajiriwa wa Serikali au Mwajiriwa wa Hospitali za Mashirika ya Dini ambaye mshahara wake unalipwana Serikali.
iv. Mwombaji aliyewahi kuajiriwa Serikalini na kupata cheki namba, atatakiwa kuzingatia Utaratibu wa kuomba Kibali cha kurejea katika Utumishi wa Umma na kuendelea kutumia Cheki Namba baada ya kuacha kazi kama ilivyobainishwa kwenye Waraka Na. CCB.228/271/01 wa tarehe 7 Agosti, 2012.
v. Mwombaji awe na sifa na weledi kwa Mujibu wa Waraka wa Maendeleo ya Utumishi Namba. 1 wa mwaka 2009 kuhusu kada zilizo chini ya Wizara ya Afya kama zilivyoainishwa hapo juu

  1. Maombi yote yaambatishwe na;-
  • Nakala ya cheti cha kuzaliwa.
  • Nakala ya cheti cha Kidato cha Nne au/na cha Sita au Stashahada kulingana na Kada ya Mwombaji. Kwa aliyesoma nje ya nchi au mitaala ya nje waambatishe cheti cha Ithibati kutoka Baraza la Mitihani Tanzania (NECTA).
  • Nakala ya Vyeti vya Taaluma (Cheti na Transcripts). Aidha, waliosoma vyuo vya nje ya Nchi, waambatishe cheti cha Ithibati kutoka TCU.
  • Wasifu (C.V).
  • Nakala ya cheti cha Usajili na Leseni hai ya taaluma husika (Full Registration & Valid Licence).
  • Nakala ya cheti cha Mafunzo kwa Vitendo (Internship)
  • Picha ndogo (passport size) moja ya hivi karibuni.
  • Nakala ya kitambulisho cha uraia (NIDA)/Namba ya Utambulisho ya NIDA.
  • Iwapo majina yako yanatofautiana katika vyeti vyako pamoja na cheti cha kuzaliwa na NIDA hakikisha unawasilisha kiapo cha majina (Deed Pool) kutoka kwa Msajili wa Viapo na kusajiliwa na Msajili wa Hati, Wizara ya Ardhi na Maendeleo ya Makazi.
  1. Namna ya kuwasilisha maombi:
Muda wa kutuma maombi haya ni ndani ya wiki mbili tangu tarehe ya kutoka kwa Tangazo hili (Mwisho wa kutuma maombi ni Tarehe 29/04/2022). Maombi yote yawasilishwe kupitia mfumo wa ajira wa Wizara unaopatika kupitia tovuti ajira.moh.go.tz.

Waombaji wote mnakumbushwa kuwa makini mnapowasilisha maombi kuhakikisha umejaza vizuri vipengele vyote vinavyotakiwa kwenye mfumo ikiwa ni pamoja na kuambatisha nyaraka zote zinazohitajika.

Imetolewa na:-

Prof. Abel Makubi
Katibu Mkuu
Wizara ya Afya
 
JAMHURI YA MUUNGANO WA TANZANIA

WIZARA YA AFYA

View attachment 2189442

  2. Waombaji watakaochaguliwa watapangiwa kazi kwenye maeneo yenye upungufu mkubwa wa wataalam wa Kada za Afya, na hakutakuwa na kubadilisha kituo pindi watakapopata nafasi hiyo. Maeneo hayo ni kama ifuatavyo; Hospitali za Rufaa za Mikoa; (1) Kigoma; (2) Katavi; (3) Sumbawanga; (4) Songwe; (5) Njombe; (6) Ruvuma; (7) Mtwara; (8) Lindi; (9) Simiyu; (10) Geita; (11) Shinyanga; (12) Tabora; (13) Singida; (14) Manyara; na (15) Mara; Hospitali za Kanda, Chato na Mtwara, Hospitali ya Magonjwa Ambukizi Kibong’oto pamoja na Vyuo vya Afya. Hivyo, waombaji wawe tayari kupangiwa katika maeneo yaliyoainishwa hapo juu.
  3. Waombaji ambao hawatakuwa tayari kwenda kwenye maeneo tajwa hapo juu inashauriwa kutotuma maombi.
  4. Waliopo masomoni hawaruhusiwi kuomba nafasi hizi za ajira.
  5. Kwenye barua ya maombi, mwombaji atapaswa kutaja maeneo matatu ambayo angependa kupangiwa kazi endapo atachaguliwa.
  6. Mwombaji mwenye nia ya kwenda kufundisha katika Vyuo vya Afya aainishe wakati wa kutuma maombi kwenye mfumo pamoja na barua ya maombi.
  7. Nakala za vyeti vyote vithibitishwe na Mahakama au Wakili.
  8. Waombaji wanaojitolea katika Hospitali za Rufaa za Kanda/Mikoa mbalimbali waandikiwe barua na Mganga Mfawidhi wa Hospitali husika kuthibitisha kujitolea kwao.
  9. Sifa za ujumla kwa Mwombaji:
i. Awe raia wa Tanzania.
ii. Awe na umri usiopungua miaka 18 na usiozidi miaka 45.
iii. Asiwe Mwajiriwa wa Serikali au Mwajiriwa wa Hospitali za Mashirika ya Dini ambaye mshahara wake unalipwana Serikali.
iv. Mwombaji aliyewahi kuajiriwa Serikalini na kupata cheki namba, atatakiwa kuzingatia Utaratibu wa kuomba Kibali cha kurejea katika Utumishi wa Umma na kuendelea kutumia Cheki Namba baada ya kuacha kazi kama ilivyobainishwa kwenye Waraka Na. CCB.228/271/01 wa tarehe 7 Agosti, 2012.
v. Mwombaji awe na sifa na weledi kwa Mujibu wa Waraka wa Maendeleo ya Utumishi Namba. 1 wa mwaka 2009 kuhusu kada zilizo chini ya Wizara ya Afya kama zilivyoainishwa hapo juu

  1. Maombi yote yaambatishwe na;-
  • Nakala ya cheti cha kuzaliwa.
  • Nakala ya cheti cha Kidato cha Nne au/na cha Sita au Stashahada kulingana na Kada ya Mwombaji. Kwa aliyesoma nje ya nchi au mitaala ya nje waambatishe cheti cha Ithibati kutoka Baraza la Mitihani Tanzania (NECTA).
  • Nakala ya Vyeti vya Taaluma (Cheti na Transcripts). Aidha, waliosoma vyuo vya nje ya Nchi, waambatishe cheti cha Ithibati kutoka TCU.
  • Wasifu (C.V).
  • Nakala ya cheti cha Usajili na Leseni hai ya taaluma husika (Full Registration & Valid Licence).
  • Nakala ya cheti cha Mafunzo kwa Vitendo (Internship)
  • Picha ndogo (passport size) moja ya hivi karibuni.
  • Nakala ya kitambulisho cha uraia (NIDA)/Namba ya Utambulisho ya NIDA.
  • Iwapo majina yako yanatofautiana katika vyeti vyako pamoja na cheti cha kuzaliwa na NIDA hakikisha unawasilisha kiapo cha majina (Deed Pool) kutoka kwa Msajili wa Viapo na kusajiliwa na Msajili wa Hati, Wizara ya Ardhi na Maendeleo ya Makazi.
  1. Namna ya kuwasilisha maombi:
Muda wa kutuma maombi haya ni ndani ya wiki mbili tangu tarehe ya kutoka kwa Tangazo hili (Mwisho wa kutuma maombi ni Tarehe 29/04/2022). Maombi yote yawasilishwe kupitia mfumo wa ajira wa Wizara unaopatika kupitia tovuti ajira.moh.go.tz.

Waombaji wote mnakumbushwa kuwa makini mnapowasilisha maombi kuhakikisha umejaza vizuri vipengele vyote vinavyotakiwa kwenye mfumo ikiwa ni pamoja na kuambatisha nyaraka zote zinazohitajika.

Imetolewa na:-

Prof. Abel Makubi
Katibu Mkuu
Wizara ya Afya
Wafamasia degree nafasi 15 tuuu dah.
 
Similar Discussions

11 Reactions
Reply
Back
Top Bottom