Babylon
JF-Expert Member
- Feb 5, 2009
- 1,332
- 82
Hell NoMazee shukurani sana.
Watu walifurahi sana siku hiyo ya December 9 1961. Lakini furaha na ndoto hii imebadilikwa kuwa jinamizi.
Miaka ya kumalizikia muongo wa 1970, nilipata bahati ya kuzungumza na Mzee Asanterabi Nsilo Swai (sasa marehemu) hapa kwenye Umoja wa Mataifa, New York, kuhusu suala la modality of decolonization and independence for Tanganyika.
Mzee Swai alikuwa ni mmojawapo wa wajumbe wazalendo wa mazungumzo ya Lanacaster House Constitutional Conference kuhusu uhuru wa Tanganyika.
Mzee Asanterabi Nsilo Swai alisema kwamba tulipewa Serikali ya Madaraka Mei 1961, ambayo ilikuwa idumu kwa mwaka mmoja. Kwahiyo, kulingana na uamuzi huo, tulikuwa tujitawale Juni 1962. Lakini tulijitawala 9 Desemba, 1961.
Moja, kwa nini Tanganyika ilijitawala mwezi Desemba 1961 na sio mwezi Juni 1962?
Mbili, ni akina nani kwa upande wa wazalendo (TANU) walioamua siku hiyo ya uhuru?
Kwenye Mkutano wa Lancaster Conference wa mwisho, uliofanyika mjini Dar es Salaam, kulikuwepo na utata wa kuamua siku hiyo ya uhuru miongoni mwa wazalendo wawakilishi wa TANU.
Macleod-Turnbull-Brown (wakoloni) walitamka kuwa mwenye kuwakilisha State ya Uingereza siku ya uhuru mwezi Juni 1962 angekuwa Malkia Elizabeth II.
Walipendekeza kuwa haingewezekana kwa Malkia Elizabeth II kuja Tanganyika mwezi wa Juni kwa sababu ya shughuli za ki-itifaki zinazofanywa mwezi huo wakati wa kusheherekea Siku ya Kuzaliwa kwa Malkia.
Malkia Elizabeth II (Elizabeth Alexandra Mary) alizaliwa tarehe 21 April, 1926; sherehe za ki-serikali zinafanywa kila mwaka mwezi Juni.
Malumbano yalieendelea kwa muda mrefu. Wakoloni walipendekeza uhuru wa Tanganyika uwe mwezi Desemba 1962. Wazalendo walikataa kata siku ya kuzaliwa kwa Malkia wa Uingereza kuchelewesha uhuru wa Tanganyika!
Hatimaye, Mwenyekiti wa mkutano huo, Bwana Ian Macleod, alishauri akutane na baadhi tu ya wajumbe wazalendo. Akashauri akutane na wajumbe watatu ili wamalize upesi malumbano yaliyokuwa yanajitokeza.
Je, Nyerere aliwachagua akina nani?
Aliwachagua Oscar Salathiel Kambona na Asanterabi Nsilo Swai.
Baadhi ya vigogo wa ujumbe wa wazalendo hawakupendezwa na uteuzi huo!
Kwenye mkutano wa kikundi hicho kidogo, ilibidi Waziri wa Makoloni Ian Macleod aukunje mkia na kuwaisha siku ya uhuru wa Tanganyika kwa miezi sita --- 9 Desemba, 1961.
Julius Nyerere alitangaza kwa wananchi mjini Dar es Salaam kuwa Tanganyika itajitawala tarehe 9 Desemba 1961. Alibebwa juu juu mabegani huku akishikilia kibango kilichoandikwa Complete Independence 1961.
Miaka ya kumalizikia muongo wa 1970, nilipata bahati ya kuzungumza na Mzee Asanterabi Nsilo Swai (sasa marehemu) hapa kwenye Umoja wa Mataifa, New York, kuhusu suala la "modality of decolonization and independence for Tanganyika."
Mzee Swai alikuwa ni mmojawapo wa wajumbe wazalendo wa mazungumzo ya "Lanacaster House Constitutional Conference" kuhusu uhuru wa Tanganyika.
Mzee Asanterabi Nsilo Swai alisema kwamba tulipewa Serikali ya Madaraka Mei 1961, ambayo ilikuwa idumu kwa mwaka mmoja. Kwahiyo, kulingana na uamuzi huo, tulikuwa tujitawale Juni 1962. Lakini tulijitawala 9 Desemba, 1961.
Moja, kwa nini Tanganyika ilijitawala mwezi Desemba 1961 na sio mwezi Juni 1962?
Mbili, ni akina nani kwa upande wa wazalendo (TANU) walioamua siku hiyo ya uhuru?
Kwenye Mkutano wa Lancaster Conference wa mwisho, uliofanyika mjini Dar es Salaam, kulikuwepo na utata wa kuamua siku hiyo ya uhuru miongoni mwa wazalendo wawakilishi wa TANU.
Macleod-Turnbull-Brown (wakoloni) walitamka kuwa mwenye kuwakilisha "State" ya Uingereza siku ya uhuru mwezi Juni 1962 angekuwa Malkia Elizabeth II.
Walipendekeza kuwa haingewezekana kwa Malkia Elizabeth II kuja Tanganyika mwezi wa Juni kwa sababu ya shughuli za ki-itifaki zinazofanywa mwezi huo wakati wa kusheherekea Siku ya Kuzaliwa kwa Malkia.
Malkia Elizabeth II (Elizabeth Alexandra Mary) alizaliwa tarehe 21 April, 1926; sherehe za ki-serikali zinafanywa kila mwaka mwezi Juni.
Malumbano yalieendelea kwa muda mrefu. Wakoloni walipendekeza uhuru wa Tanganyika uwe mwezi Desemba 1962. Wazalendo walikataa kata siku ya kuzaliwa kwa Malkia wa Uingereza kuchelewesha uhuru wa Tanganyika!
Hatimaye, Mwenyekiti wa mkutano huo, Bwana Ian Macleod, alishauri akutane na baadhi tu ya wajumbe wazalendo. Akashauri akutane na wajumbe watatu ili wamalize upesi malumbano yaliyokuwa yanajitokeza.
Je, Nyerere aliwachagua akina nani?
Aliwachagua Oscar Salathiel Kambona na Asanterabi Nsilo Swai.
Baadhi ya "vigogo" wa ujumbe wa wazalendo hawakupendezwa na uteuzi huo!
Kwenye mkutano wa kikundi hicho kidogo, ilibidi Waziri wa Makoloni Ian Macleod aukunje mkia na kuwaisha siku ya uhuru wa Tanganyika kwa miezi sita --- 9 Desemba, 1961.
Julius Nyerere alitangaza kwa wananchi mjini Dar es Salaam kuwa Tanganyika itajitawala tarehe 9 Desemba 1961. Alibebwa juu juu mabegani huku akishikilia kibango kilichoandikwa "Complete Independence 1961."