Vijana katika vuguvugu la kupinga ukoloni 1929 - 1961

Mohamed Said

JF-Expert Member
Nov 2, 2008
20,921
30,266

DAMU CHANGA KATIKA VUGUVUGU LA KUPIGANIA UHURU WA TANGANYIKA 1929 - 1961

Huyo kijana amenihamasisha sana niingie katika kitabu cha Abdul Sykes kuangalia mambo makubwa waliyofanya wazee wetu nijue waliyafanya hayo wakiwa katika umri gani?

Waasisi wa African Association 1929:

1. Kleist Sykes (1894 – 1949) Miaka 35.
2. Mzee bin Sudi (1896 -1972) Miaka 33.

Viongozi wa TAA walioleta mabadiliko makubwa katika kukabiliana na serikali ya kikoloni 1950:

1. Dr. Vedasto Kyaruzi (1921 – 2012) Miaka 29.
2. Abdulwahid Sykes (1924 -1968) Miaka 26.

3. Hamza Mwapachu (1913 – 1962) Miaka 37.

4. Paul Bomani (1925 – 2055) TAA President Lake Region 1950, Miaka 25.

Waasisi wa TANU 1954:

1. Julius Kambarage Nyerere (1922 – 1977) Miaka 32.
2. Abdul Sykes, Miaka 30.
3. Ally Sykes Miaka 28.
4. Japhet Kirilo (1921 -?) Miaka 33.
5. Dossa Aziz (1923 – 1998) Miaka 31.
6. Saadan Abdu Kandoro (1926 -?) Miaka 28.

Wanaharakati wa TANU 1954:

1. Titi Mohamed (1926 – 2000), Miaka 28.
2. Lucy Lameck (1933 – 1993) Miaka 21.
3. Abbas Sykes (1929 - 2021) Miaka 25.

Hii ni sehemu ndogo ya vijana walioanzisha na kushiriki katika vuguvugu la kupigania uhuru wa Tanganyika kuanzia mwaka wa 1929 hadi uhuru unapatikana mwaka wa 1961.

Bahati mbaya sana wengi wao michango yao haifahamiki.

Historia imewasahau.
 
Back
Top Bottom