Tanga kwetu raha

Tanga kwetu raha

Naupenda mji wa Tanga ulivopangika aisee..... halafu upo shwari kweli.. Sio makelele tu
 
Matusi ya nini tena, Njoo Tanga tukufundishe usaarabu. Watu wa Tanga hatukuzoea tabia kama izo. Muda wote ukitembea katika jiji letu hakuna vibaka wala majambazi, Tanga ndio sehemu salama ya kufanya biashara, na ndio sehemu salama yakuekeza, wauza chips wale wa balabalani wanauza hadi saa 10 usiku, muda wote ukiingia katika JIJI letu uhakika wakupata chakula upo, na hotels zote zipo wazi muda wote 24/7. Karibu sana Tanga.



Home Sweet Home.
mnafuga mno majini
 
hahahaaaaaaaaaaaaaaa! ila hao MABILIONEA uliowataja wa Tanga nimecheka karibu mbavu zangu zipasuke! mwe!
 
tanga raha sana ..watu wake niwakarimu mnoo
sema Dada zenu sifa zao kubwa SIO WACHOYO..
 
Mkuu unapaham maramba vzr,?
Mi nilikaa pale msumbiji ndani ya maramba yani pameitwa msumbuji kwasababu ya wamakonde
Kule maramba kuna wamakonde sana tena asili yao Tanga, nilishangaa sana
 
mhh wala sion uzur wa tanga hakuna hata pa kwenda kwa kweli zaid ya tanga beach na mkwabi bas mji mzima sehem mbili tu
Tanga pazuri raskazone beach amboni cave saadani kote no tanga sio sehemu 2
 
Any way ni pazuri Sana kwa wanaopenda utulivu .nikifayakazi Tangafresh Kama aka 3 hivi na nilikaa street 14, nilikuwa na demu street 11 kumuona ni usiku tuu Mida mingine yote yupo Ndani wallah ni loh. Ukiacha tu sifa tajwa ni mkoa wa kimkakati Sana ni mkoa wa uwekezaji nitarudi na kuwekeza huko one day. Nimefika mheza kicheba, nimefika Handeni chogo, nimefika korogwa Ambangulu kwenyewe kiwanda cha chai cha mkoloni, Nimefika Pangani pia ni mko mzuri kwa uwekezaji Tatizo ni kama Moro ardhi kubwa imechukuliwa na wachache.
 
Nimegeuka Juzi home Tanga asee natatafuta Walau chemba nipige kitimoto na Maji safi kidogo wapi mji mzima bar unatafuta kwa Torch i hate Tanga, Kuzama mkwabi hii supermarket mpya Ndo nakutana na Maji safi nkanunua na kushusha na nyama ingine tu pale nje, Wakuu wapi ntapata nguruwe apa Tanga mjini?
Mkuu wewe mwongo sana, Tanga ni jiji. Ulienda Sabasaba? Vp wale wamama wanaomwagilia maji keep left kwaminchi bado wanaendelea na ile adhabu?
 
Mkuu wewe mwongo sana, Tanga ni jiji. Ulienda Sabasaba? Vp wale wamama wanaomwagilia maji keep left kwaminchi bado wanaendelea na ile adhabu?
Hahaha wanaendelea mkuu japo mara moja moja nawapita wamesimama tu hawagilii na Nguo zao pendwa za Bendera yetu maridhawa
Kuna chimbo nimelifuma sahare huku ndio ninapokata maji nkishikwa na Kiu
 
Back
Top Bottom