Tanga Fresh...Mtindi

Panga La Shaba

JF-Expert Member
Dec 24, 2009
209
68
Wana jamvini hivi kweli mtindi wa Tanga Fresh ni maziwa ya ng’ombe au mimi ni mpenzi sana wa mtindi lakini napata shida kidogo kuamini kama huo mtindi ni kweli maziwa ya ng’ombe….mwenye jibu jamani
 
Kwa kweli umenigusa na swali lako! hata mimi bado najiuliza? maana nimekunywa mitindi mingi lakini Tanga Fresh ni zaidi!! Kila nikinywa nazidi kuupenda sijui wameweka nini!!!
 
Ushaambiwa au kusikia wahenga wakisema ''Tanga Raha''. Ule mtindi wa ngombe kaka wala usiogope. Ndo mambo ya Tanga hayo
 
Sasa kama unautumiaga na una shaka nao... What if ulikuwa ni sumu kwako !?

Sisi tunauona kama mtindi sijui wewe unauona kama nini ?
 
Kwakweli hata mie ningependa kujua nayapenda balaa na wanangu ndo usiseme
 
99% ni maziwa ya ng'ombe,waliwapa mikopo wafugaj ili wafuge ng'ombe wa maziwa so kila siku huwa wanapokea maziwa kutoka kwa wafugaj na hupimwa kabla ya kuhifadhiwa endapo yatagundulika ya maji hata kidogo basi huyo mfugaj hupigwa faini,baada ya kutengenezwa huongeze creem test ambayo ni almost 0.92% and the rest % ni chemical ambazo huongezwa ili yasiharibike mapema,so msiwe na hofu ni maziwa halisi ya ng'ombe,I proved it nilifanya Field Tanga fresh mwaka 2011
 
Yale ni maziwa halisi ya ng'ombe na hamna chochote kinachoongezwa zaidi ya vigezo na masharti ya utengenezaji wa mtindi, Piga mtindi wa tanga fresh kwa afya yako.
 
Ushaambiwa au kusikia wahenga wakisema ''Tanga Raha''. Ule mtindi wa ngombe kaka wala usiogope. Ndo mambo ya Tanga hayo

Huu mtindi wa Tanga ni mzito mmno ukilinganisha na mitindi mingine kama wa Mara,Asaad,Kilimanjaro na tena hii uwa unasikia kabisa kaharufu kama maziwa yaliyo chacha ,ata mitindi nilikunywa vijiji hauko kama wa Tanga....labda nikahisi huu wa Tanga ni mchanganyiko wa mambo...!!!!!!!!!
 
Phew! nilikuwa nazipitia post zote huku roho ikinidunda kwa kasi ya ajabu nikidhani mie na familia yangu tumelamba misumu miaka yote hiyo! nimetetemekaje?
 
Kuna kibao tu kimeandikwa "Karibu Tanga" huku maeneo ya Pongwe..lakn hakuna kibao cha "Kwa Heri Tanga"....mana ukingia hutoki
 
Mambo ya tanga hayo, bado hujala mkate wa kumimina kutoka kwa wakina mama wanaouza usiku maeneo ya bara ya 15, 16 na 17....utabaki tanga wewe
 
Ila maziwa fresh yao sasa????

Sent from my BlackBerry 9300 using JamiiForums
 
Mambo ya tanga hayo, bado hujala mkate wa kumimina kutoka kwa wakina mama wanaouza usiku maeneo ya bara ya 15, 16 na 17....utabaki tanga wewe

Nilikula chapati kwa mama ntilie Tanga, chapati imekwandwa na nazi, ukifunga inafunguka kama kurasa za kitabu. Ile chapati sijawahi kuiona mahali popote. Chezea Tanga wewe.

 
Nilikula chapati kwa mama ntilie Tanga, chapati imekwandwa na nazi, ukifunga inafunguka kama kurasa za kitabu. Ile chapati sijawahi kuiona mahali popote. Chezea Tanga wewe.


Mwaipopo alienda tanga kununua nazi kwa ajili ya biashara kutoka tanga mbeya, basi alipofika si akala na mtaji wote baada ya kula haya mahanjumati kutoka kwa mmama wa kitanga.....alirudi mbeya na matenga yake matupu mtaji ukiwa umebaki tanga. Chezea tanga wewe ni padogo lakini pakubwa sana tu
 
Ndio raha zenyewe za Tanga hizo mkuu, Tanga yetu ni njema, atakaye aje! Hatuna kwaheri huku, ukija waambiwa karibu, ukiondoka twakuambia karibu!
 
Back
Top Bottom