Tanga Fresh...Mtindi

Tanga Fresh...Mtindi

Kuna kibao tu kimeandikwa "Karibu Tanga" huku maeneo ya Pongwe..lakn hakuna kibao cha "Kwa Heri Tanga"....mana ukingia hutoki

Aiseee me mwenyewe ni mlevi sna wa mtindi wa tanga, daaaa Tanga kweli rahaaaa nlikaa miezi 2 hapo 2010 sehem inaitwa Nguvumali kiukweli sikutaman kuondoka ila ilinibidi kwan nlkuwa fild tu!
 
Ndio raha zenyewe za Tanga hizo mkuu, Tanga yetu ni njema, atakaye aje! Hatuna kwaheri huku, ukija waambiwa karibu, ukiondoka twakuambia karibu!

Haaa haaa haaa ! Umenifahisha kweeeeli !
Sasa ukutane na mkenya wa narobi, ndo utachoka. Ukisema karibu atakwambia ahsante, ukimwambi karibu ahsante, karibu tena......ahsante ! Mbona mnakesha !
 
Nilikula chapati kwa mama ntilie Tanga, chapati imekwandwa na nazi, ukifunga inafunguka kama kurasa za kitabu. Ile chapati sijawahi kuiona mahali popote. Chezea Tanga wewe.

Angalia, usipewe kanga badala ya taulo, na kubebwa mgongoni kupelekwa na kutolewa bafuni.
 
kiukweli nimekunywa sana mtindi wa tanga fresh kwa miaka mingi sana and it was the best mtindi ever until I found the real and natural mtindi, si mwingine bali ni wa kilimanjaro mtindi.

Yaani haya maziwa kiukweli yako very natural, less of chemical additives na naupenda saaaana.

Kwa hapa dar bado haupo lakini siku wakiingia soko la dar, 'mitindi' yote ijiandae kutolewa sokoni.
 
Hadi sasa sijaona jibu la kisayansi...wote mwapiga porojo tu.
Hebu tuelezeni kama kuna ranchi ambayo hufugwa ng'ombe wa maziwa.
Binafsi ninahisi hawa jamaa wanatoa maziwa eneo moja laitwa Mlingano lipo Pongwe, kama sikosei kule kuna ranchi. (Hili sina uhakika bado maana nimeondoka Tanga kitambo kidogo).
 
Phew! nilikuwa nazipitia post zote huku roho ikinidunda kwa kasi ya ajabu nikidhani mie na familia yangu tumelamba misumu miaka yote hiyo! nimetetemekaje?

Yani wewe umewaza vibaya kama mimi lolz.. Yani nilisikia tumbo lanikata. Nkajua tayari uziii unaleta habari za maududu ya hayo maziwa.. Mweeee

Mungu tusaidie!

Sent from my BlackBerry 9300 using JamiiForums
 
Tangu nikute inzi kwenye hayo maziwa sina hamu nayo tena
 
Mbele yangu hapa nina packet ya Tanga Fresh(Mtindi).
Najaribu kutafuta jedwali la vilivyomo, lakini silioni na bila shaka halijabandikwa katika kifungashio hiki.
Pamoja na hilo, kuna maandishi hapa labda huenda yakawa jawabu la kitendawili hiki, nami nanukuu.

"TANGA FRESH LTD is a Dutch-Tanzanian milk processing company. Investors from Holland team-up with the farmers of Tanga Dairies Co-operative Union. TANGA FRESH LTD only works with day fresh milk straight from the cow.

TBS Reg No ni 307:1987
 
Yaani hii mambo we acha tu, lakini jamaa wamepitishwa na TBS

Yani wewe umewaza vibaya kama mimi lolz.. Yani nilisikia tumbo lanikata. Nkajua tayari uziii unaleta habari za maududu ya hayo maziwa.. Mweeee

Mungu tusaidie!

Sent from my BlackBerry 9300 using JamiiForums
 
Huu mtindi wa Tanga ni mzito mmno ukilinganisha na mitindi mingine kama wa Mara,Asaad,Kilimanjaro na tena hii uwa unasikia kabisa kaharufu kama maziwa yaliyo chacha ,ata mitindi nilikunywa vijiji hauko kama wa Tanga....labda nikahisi huu wa Tanga ni mchanganyiko wa mambo...!!!!!!!!!

mkuu mtindi wa Mara naona umeunywa juu ju,ila quality yake ipo juu sana na mtamu usipime,then unafuta wa asas..tho hata bukoba wana mtindi flan mzuri sana ila tatzo watu wa Dar hatuupati!!!
 
Mwaipopo alienda tanga kununua nazi kwa ajili ya biashara kutoka tanga mbeya, basi alipofika si akala na mtaji wote baada ya kula haya mahanjumati kutoka kwa mmama wa kitanga.....alirudi mbeya na matenga yake matupu mtaji ukiwa umebaki tanga. Chezea tanga wewe ni padogo lakini pakubwa sana tu
Nasikia kwenda bafuni, unabebwa mgongoni.Unapewa pia na visahani vidogo viwili; kimoja cha kuwekea sabuni na kingine......!
 
kiukweli nimekunywa sana mtindi wa tanga fresh kwa miaka mingi sana and it was the best mtindi ever until I found the real and natural mtindi, si mwingine bali ni wa kilimanjaro mtindi.

Yaani haya maziwa kiukweli yako very natural, less of chemical additives na naupenda saaaana.

Kwa hapa dar bado haupo lakini siku wakiingia soko la dar, 'mitindi' yote ijiandae kutolewa sokoni.

Na ule wa Mara na Bukoba ukiletwa hapa dar wengine itabidi wajipange sawasawa
 
Nimekumbuka nilipokuwa kikazi musoma mwaka 2008 nilikutana na jamaa mmoja wa musoma akaniambia ana baba yake mdogo tangu alipoenda tanga mwaka 1985 hajarudi hadi leo na ameshaoa mamaa ya tanga na kila wakiwasiliana nae anawaambia ndugu zake hatarudi tena musoma.(anajua mwenyewe)
 
Ndo maana kocha wa Yanga hakuwepo benchi leo kumbe ndo mambo ya Tanga ukienda unaweza usirudi, wanayanga fanyeni mpango mfuate kocha wenu.
 
Kuna mtindi upo pale SUA, Tanga Fresh cha mtoto.
 
Hadi sasa sijaona jibu la kisayansi...wote mwapiga porojo tu.
Hebu tuelezeni kama kuna ranchi ambayo hufugwa ng'ombe wa maziwa.
Binafsi ninahisi hawa jamaa wanatoa maziwa eneo moja laitwa Mlingano lipo Pongwe, kama sikosei kule kuna ranchi. (Hili sina uhakika bado maana nimeondoka Tanga kitambo kidogo).
Wanakusanya maziwa kutoka kwa wafugaji mbalimbali, then wanatengeneza huo mtindi.
 
Wana jamvini hivi kweli mtindi wa Tanga Fresh ni maziwa ya ng’ombe au mimi ni mpenzi sana wa mtindi lakini napata shida kidogo kuamini kama huo mtindi ni kweli maziwa ya ng’ombe….mwenye jibu jamani

.ni mtindi hasa unaotakana na maziwa ya .ng'ombe, ukifika tanga waweza fika kiwandani kange uwone wafanyacho...
 
tanga na vilivyopo tanga vyote vizuri, huo mtindi tu je ukila vibibi si utasahau kwenu.
 
Back
Top Bottom