Tanga: Auawa wakigombania unga na dagaa

Chachu Ombara

JF-Expert Member
Dec 11, 2012
5,897
10,358
Jeshi la Polisi Mkoa wa Tanga linamshikilia mkazi wa kijiji cha Bwembwela wilayani Muheza kwa tuhuma za kumuua, Eliasa Omari (55) kwa kumkata mapanga akidai kumuibia unga na dagaa.

Akizungumza na waandishi wa habari leo Jumatano Aprili 20, 2022 Kamanda wa Polisi Mkoa wa Tanga, Safia Jongo amesema chanzo cha tukio hilo ni ugomvi wa kugombania unga na dagaa pamoja na simu iliyopelekea wawili hao kupigana kwa kutumia mapanga.

"Aliyeuwawa aliyekuwa anafanya kazi katika shamba la mkonge" amesema amanda Jongo.

Kamanda Jongo amesema tukio hilo limetokea usiku wa kuamkia Jumapili Aprili 17, 2022 na kwamba mtuhumiwa yupo katika Hospitali ya Teule ya Muheza akipatiwa matibabu.

Chanzo: Mwananchi
 
Watu wakisema hali ni mbaya serikali na wazee wa V8 muelewe!
Ukombozi na uhuru kichumi hautoletwa ni serikali wala mbunge nk bali wewe mwenyewe kwa jitahada zako.
 
Back
Top Bottom