Protector
JF-Expert Member
- May 20, 2019
- 414
- 877
Leo tarehe 22/11/2022 TANESCO wametoa taarifa kwa vyombo vya habari kuelezea sababu za mgao unaoendelea nchini.
Kwa habari zaidi soma Press release Hapa chini
====
Shirika la Umeme Tanzania limetangaza upungufu wa Megawati 155 za Umeme wa Maji uliosababishwa na Ukame kwenye Mabwawa ya Kihansi, Mtera, Nyumba ya Mungu, Hale na Pangani.
Pia, Mtambo mmoja wa Kidatu unaozalisha Megawati 50 umepata hitilafu na Mitambo miwili ya Ubungo III inayozalisha Megawati 40 ipo kwenye matengenezo kinga, hivyo kupunguza Takriban Megawati 300 za Umeme wa Maji na Gesi.
Hali hiyo itadumu hadi mwanzoni mwa mwezi Desemba 2022 baada ya kumalizika matengenezo na kuongezeka maji kwenye mabwawa pamoja kuingizwa Megawati 225 kwenye Gridi ya Taifa.