Nyanswe Nsame
Senior Member
- Jul 9, 2019
- 158
- 175
Tanesco acheni dharau kwa Rais Samia
Leo katika mkoa wa Mwanza nimeona kitendo ambacho sio cha kiungwana na kinachoonesha dharau kwa mamlaka.
TANESCO wamekata umeme wakati Mwenge wa Uhuru upo katika mkoa huu.
TANESCO mnashindwa kutambua kwamba, mwenge unapopita sehemu au mkoa wowote ule ni kama Rais wa Tanzania kapita eneo hilo?
Tanesco katika mkoa wa Mwanza, ukiacha tabia hii ya siku ya Leo kukata umeme bila taarifa tena ukizingatia mwenge unakagua miradi ya maendeleo ni dharu kwa niaba ya Rais wa Tanzania Samia Suluhu Hassan ni kitendo cha kudharau mamlaka hiyo.
Tanesco wamekuwa ni kawaida yao kukata umeme mara kwa mara bila taarifa na hii wanaifanya utafikiri ni mali yao na wanatoa huduma hiyo kwa hisani tu.
Kutokana na kitendo hiki cha kukata umeme wakati mwenge upo Mwanza leo katika wilaya ya Nyamagana, viongozi wote wa tanesco mkoa wa Mwanza wanapaswa kuwajibika.
Panga linapaswa kupita kuanzia kitengo cha huduma ya wateja mpaka kwa meneja wa mkoa ambaye ndio bosi wao.
Wanasahau au hawajui kwamba juzi wakati mwenge wa uhuru unakagua miradi Ilemela kiongozi wa mbio za mwenge Josephine Mwambashi, alikataa kuzindua mradi wa mzani wa kupima magari ya samaki kutokana na ubadhirifu.
Mradi huo gharama zake au fedha zilizotolewa na Serikali ni zaidi ya milioni 300 lakini hauonyeshi uhalisia wa gharama hiyo.
Taarifa zinasema kuwa, mzani huo mpaka kukamilika kwake umetumia kiasi cha tsh.milioni 200, hivyo kiongozi wa mwenge anahoji kiasi cha zaidi ya milioni 100 zilizpo.
Taarifa zinasema, fedha hizo zimepigwa na baadhi ya viongozi wa Manispaa hiyo wakiongozwa na Mkurugenzi wake, John Wanga.
Wengine ni Meya wa Manispaa hiyo Thomas Mulungwa, mkuu wa idara ya fedha, mchumi wa Manispaa hiyo.
Kiongozi wa mbio za mwenge aliiagiza Taasisi ya kuzuia na kupambana na rushwa Takukuru kuchunguza mradi huo na kutoa taarifa ili hatua ziweze kuchukuliwa.
Kwa mifano hiyo, TANESCO wanapaswa kuheshimu mwenge wa uhuru, wasione kwamba hakuna kiongozi mkubwa wa Serikali hayupo ndo waonyeshe dharau.