101 East
JF-Expert Member
- Feb 25, 2015
- 1,040
- 2,121
Shirika la Umeme nchini (TANESCO) Mkoa wa Mwanza limepata hasara ya zaidi ya shilingi milioni kumi baada ya watu wasiofahamika kujenga njia ya umeme, kusimika nguzo tisa pamoja na kuunganisha nishati hiyo kwenye nyumba tano kinyume cha sheria tukio hilo limetokea katika mtaa wa Kagua Iramba kata ya Nyamhongolo manispaa ya Ilemela mkoani humo.
---

Afisa Usalama wa TANESCO Mkoa wa Mwanza Jeverino Pembe amesema, watu wasiojulikana wamejenga njia ya umeme katika mtaa wa Kagua Iramba kata ya nyamhongolo manispaa ya Ilemela mkoani humo na kujiunganishia nguzo tisa kinyume na utaratibu ili waweze kujinufaisha kitendo ambacho kimeikosesha serikali mapato na kusababisha usumbufu mkubwa kwa wateja kwa kuwa taratibu sahihi hazikufuatwa.
Kaimu meneja wa wilaya ya ki-TANESCO ya Nyakato, Mhandisi Johansen Mkurusi amesema, miundombinu iliyotumika kujiunganishia umeme kwenye nyumba kinyemela ikiwemo nguzo, nyaya pamoja na mita zitang'olewa na maafisa wa shirika hilo kutokana na kujengwa kinyume na utaratibu.