TANESCO wamekata umeme wakati Mwenge wa Uhuru upo katika mkoa wa Mwanza

Nyanswe Nsame

Senior Member
Jul 9, 2019
158
175
Tanesco acheni dharau kwa Rais Samia

Leo katika mkoa wa Mwanza nimeona kitendo ambacho sio cha kiungwana na kinachoonesha dharau kwa mamlaka.

TANESCO wamekata umeme wakati Mwenge wa Uhuru upo katika mkoa huu.

TANESCO mnashindwa kutambua kwamba, mwenge unapopita sehemu au mkoa wowote ule ni kama Rais wa Tanzania kapita eneo hilo?
Tanesco katika mkoa wa Mwanza, ukiacha tabia hii ya siku ya Leo kukata umeme bila taarifa tena ukizingatia mwenge unakagua miradi ya maendeleo ni dharu kwa niaba ya Rais wa Tanzania Samia Suluhu Hassan ni kitendo cha kudharau mamlaka hiyo.

Tanesco wamekuwa ni kawaida yao kukata umeme mara kwa mara bila taarifa na hii wanaifanya utafikiri ni mali yao na wanatoa huduma hiyo kwa hisani tu.

Kutokana na kitendo hiki cha kukata umeme wakati mwenge upo Mwanza leo katika wilaya ya Nyamagana, viongozi wote wa tanesco mkoa wa Mwanza wanapaswa kuwajibika.

Panga linapaswa kupita kuanzia kitengo cha huduma ya wateja mpaka kwa meneja wa mkoa ambaye ndio bosi wao.

Wanasahau au hawajui kwamba juzi wakati mwenge wa uhuru unakagua miradi Ilemela kiongozi wa mbio za mwenge Josephine Mwambashi, alikataa kuzindua mradi wa mzani wa kupima magari ya samaki kutokana na ubadhirifu.

Mradi huo gharama zake au fedha zilizotolewa na Serikali ni zaidi ya milioni 300 lakini hauonyeshi uhalisia wa gharama hiyo.

Taarifa zinasema kuwa, mzani huo mpaka kukamilika kwake umetumia kiasi cha tsh.milioni 200, hivyo kiongozi wa mwenge anahoji kiasi cha zaidi ya milioni 100 zilizpo.

Taarifa zinasema, fedha hizo zimepigwa na baadhi ya viongozi wa Manispaa hiyo wakiongozwa na Mkurugenzi wake, John Wanga.

Wengine ni Meya wa Manispaa hiyo Thomas Mulungwa, mkuu wa idara ya fedha, mchumi wa Manispaa hiyo.

Kiongozi wa mbio za mwenge aliiagiza Taasisi ya kuzuia na kupambana na rushwa Takukuru kuchunguza mradi huo na kutoa taarifa ili hatua ziweze kuchukuliwa.

Kwa mifano hiyo, TANESCO wanapaswa kuheshimu mwenge wa uhuru, wasione kwamba hakuna kiongozi mkubwa wa Serikali hayupo ndo waonyeshe dharau.
 
Mwenge umepotwa na wakati, ni upotevu wa pesa za walipa kodi bila sababu za msingi.

Hoja ya Tanesco kuihujumu nchi na uchumi ni relevant kabisa. Kalemani atakuwa ameshindwa au anahusika kuihujumu serikali, mbona wakati wa JPM umeme haukuwa ukikatika ovyo namna hii?
 
Nilidhani una zungumzia Tanesco kufuta tariff 4 kimya kimya. Hawa jamaa wana tatizo kubwa sana.

Huku wana sema wana punguza gharama za umeme lakini wamefuta tariff ya wanyonge.
 
Sasa povu la nini? Umefanya utafiti kujua Kwanini walikata umeme? Mahali pa kuanzia Ni hapo. It is as if ume-confirm kuwa kilikuwa na Nia ovu katika kukata umeme.

Seems una chuki na watu wa Tanesco.
 
Jamaa ni mchochezi sana. Hapa TANESCO wakiona huu uzi lazima watetemeke.
 
Sasa povu la nini? Umefanya utafiti kujua Kwanini walikata umeme? Mahali pa kuanzia Ni hapo. It is as if ume-confirm kuwa kilikuwa na Nia ovu katika kukata umeme.

Seems una chuki na watu wa Tanesco.
SABABU ZINAZOWEZA KUSABABISHA KUKATIKA KWA UMEME

1. Utangulizi
Kwa muda mrefu kumekuwa na uelewa kutoka kwa wateja wetu kuwa kila umeme unapokatika TANESCO WAMEKATA. Nimeona ni vyema tukatoa
Maelezo kwa ufupi ili wateja wetu waelewe sababu za kiufundi na zisizo za kiufundi, zilizo ndani ya uwezo wa TANESCO na zisizo ndani ya uwezo wa TANESCO.

2. Sababu za TANESCO Kukata Umeme

TANESCO itakata tu umeme endapo kuna sababu zifuatazo BILA kuwataarifu wateja:-
a) Kuna mali inaungua (Mf. nyumba, kiwanda au mtambo)
b) Kuna mtu kanaswa na umeme.
c) Dharura emergencies (imeelezwa hapo chini namba 4)

3. TANESCO itakata umeme baada ya kuwataarifu wateja - Planned Interruptions endapo:-

a) Kuna matengenezo Kinga yaliyopangwa kufanyika ili kuimarisha miundombinu Planned Preventive Maintanance (Mf. Kubadili nguzo zilizooza, kubadili waya chakavu, kubadili transfoma ili kuongeza uwezo wa umeme nk)
b) Matengenezo ya kila mara Routine Maintanance (Mf. Kukata miti inayogusa line za umeme, kukagua vikombe na vifaa vingine kwenye line)
c) Kumuunga mteja mkubwa kwenye line ya msongo mkubwa wa umeme 11kV au 33kV

4. SABABU zinazoweza kusababisha umeme kukatika kwa dharura Emergency cases nyingi ni Unplanned Interruptions

a) Za kiasilia Natural Calamities (Mf. Radi kupiga transfoma, mvua au upepo mkali kuangusha nguzo, kukata waya, miti au minazi au matawi ya miti kuangukia line, mafuriko, wanyama kama komba, nyani, nyoka, kunguru kunasa kwenye mifumo ya umeme nk.

b) Hujuma za kibinadamu Sarbotage
(Mf. Transfoma kuibiwa mafuta, kuibwa nyaya za umeme, nguzo kuchomwa moto na kuanguka, nguzo kubwa kuibiwa vyuma na kuanguka, magari kugonga nguzo za umeme na kuanguka, malori marefu kwenda juu kukata waya za umeme, wateja kukata miti ikaangukia kwenye line nk.

Hizi ni baadhi tu ya sababu za msingi zinazoweza kusababisha umeme Kukatika. Hivyo ieleweke kuwa sio kila KUKATIKA KWA UMEME -TANESCO wamekata ni suala pana linalohitaji kujua sababu. Wakati mwingine kwa maelezo hayo hapo juu, Umeme unakatika hata TANESCO inabidi kufuatilia mifumo ili kujua sababu za kukatika.

5. Hitimisho
Tunajua jukumu la TANESCO ni kuhakikisha wateja wanapata umeme wa uhakika, pia ni ukweli kuwa mifumo mingi ya TANESCO ni ya muda mrefu hivyo inahitaji ukaratabati wa mara kwa mara na uwekezaji mkubwa ambao sote tumeona jitihada zinazofanywa na Serikali ili TANZANIA iwe na umeme wa uhakika.

Tunaomba umma uelewe sababu hizi na kuwa kama viongozi tunaamini hakuna mfanyakazi wa TANESCO anaweza kulihujumu Shirika kwa kukata umeme bila sababu au kukata umeme bila kufuata maagizo na utaratibu wa kukata line uliowekwa. Sio kila mfanyakazi au fundi anaweza kukata umeme. Upo utaratibu tena wakati mwingine wa kimaandishi unaompa fundi ruhusa, kabla ya kukata umeme. Kama yupo na anafahamika ( Kama baadhi ya wateja wetu wanavyotuhumu) tunaomba ushirikiano wenu ili tuweze kumshughulikia kwa taratibu za kisheria na tutakuwa tumelisaidia Shirika na serikali kwa ujumla.

TANESCO
Tunayaangaza Maisha Yako

Nilidhani una zungumzia Tanesco kufuta tariff 4 kimya kimya. Hawa jamaa wana tatizo kubwa sana.

Huku wana sema wana punguza gharama za umeme lakini wamefuta tariff ya wanyonge.
Hakuna mabadiliko yeyote yaliyotokea kwenye tarif bali ni utekelezaji wa miongozo iliyopo toka mwaka 2016.Wateja wote wanawekwa kwenye makundi yanayoendana na matumizi yao
 
Mda mwingine hua mnakata Umeme kama mchezo/ushindani.
Hilo nalo ni jipu.
 
Haijawahi kutokea na haitakaa itokee kwa kuwa zipo taratibu za kufata ili kukata umeme na sababu zenye kueleweka.Kumbuka tunahitaji wateja wetu wapate huduma ikiwemo sisi tunaoishi maeneo hayo kwa sababu hakuna mtaa wa watu wa TANESCO, ikitokea umekatika ni wote tunaathirika.Tutaendelea kuboresha zaidi.
 
Sawa mkuu japo wewe unaweza sema hayo maneno ukiwa Dar lakini kumbuka kuna wengine matatizo hayo tunayaona na yanatutokea nje ya huko mliko ninyi.
Haya yanatokea hasa ndani ndani mfano mzuri ni vijijini
 
Je unalalamikia eneo gani haswa?Wilaya gani na namba yako ya simu kwa hatua zaidi

Jm
 
Hakuna mabadiliko yeyote yaliyotokea kwenye tarif bali ni utekelezaji wa miongozo iliyopo toka mwaka 2016.Wateja wote wanawekwa kwenye makundi yanayoendana na matumizi yao
Mimi nina zaidi ya mwaka nimejaza fomu ya kuomba kubadilishiwa tarifu iliyopo sasa kwenda tarif 4 au 0 lakini hakuna kilichofanyika mpaka sasa, ninachoambiwa subiri watakuja sijui sasa litatekelezwa lini, japo nshatonywa na mtu toa kitu ndipo kazi yangu ifanyike, ni kweli ndio tumefikia huko? Kwanini muweke utaratibu wa kuja survey nyumba wakati mnajua hamtaweza? Sasa mtakuja au ndio mmegoma? Mita 43021733027 ofisi Tanga.
 
Nyumba ipo eneo gani haswa Tanga? Ni ni makazi au biashara?
 
Mwenge umepotwa na wakati, ni upotevu wa pesa za walipa kodi bila sababu za msingi.

Hoja ya Tanesco kuihujumu nchi na uchumi ni relevant kabisa. Kalemani atakuwa ameshindwa au anahusika kuihujumu serikali, mbona wakati wa JPM umeme haukuwa ukikatika ovyo namna hii?
Umeme unakatika hovyo mno,tofauti wa wakati wa JPM.
Tanesco wanakera.

Sent using Jamii Forums mobile app
 
Back
Top Bottom