Wanajamii, machungu zaidi Tanesco kwani Mahakama ya rufaa imetupilia mbali pingamizi la Tanesco. Hii ina maana kuwa Tanesco lazima walipe bil 104 na ushehe!
Joshamto, nadhani unatatizo la uelewa.
1. Dowans walishashinda tuzo ya ICC na Tanesco kutakiwa kuilipa ile tozo ya Bilioni 94!.
2. Ili tozo hiyo ilipwe, hukumu ya ICC inatakiwa kusajiliwa Mahakama Kuu ili iwe binding humu nchini!.
3. Dowans wameshaisajili tozo hiyo Mahakama Kuu ili iisajili na Tanesco kutakiwa kulipa.
4. Tanesco wamekata rufaa Mahakama Kuu, isiisajili tozo hiyo ya Dowans kwa sababu inataka kukata rufaa ICC kupinga tozo hiyo.
5. Dowans wameweka pingamizi mahakama kuu kuzuia pingamizi la Tanesco lisikubaliwe kwa hoja kuwa maamuzi ya ICC hayana rufaa!.
6. Mahakama Kuu, imetupilia mbali pingamizi la Dowans na kukubali maombi ya Tanesco kuweka pingamizi dhidi ya usajili wa tuzo ya ICC.
7. Jaji Faudh ameiambia Tanesco kukata rufaa ni haki yake kisheria, wala haikupaswa kuomba kuweka pingamizi Mahakama Kuu ndipo ikate rufaa ICC, ilitakiwa ikate tuu hiyo rufaa ICC kitambo na mahakama kuu ingesitisha kuisajili tozo ya dowans kusubiria rufaa ya Tanesco ICC!.
8.Yatokanayo ni kuwa sasa Tanesco itakata rufaa ICC kupinga tozo ya Dowans ambapo rufaa hiyo itapigwa chini kwa sababu mkataba ulitamka wazi uamuzi wa ICC ni wa mwisho na hauna rufaa!.
9. Hatimaye tozo hiyo itasajiliwa na Mahakama Kuu na Tanesco itatakiwa kuilipa mara dufu kuliko hata ile ya awali!.
10. Bodi ya Tanesco, Kamati ya Zitto na CAG wamesema Tanesco haiwajibiki kulipa tozo hilo bali ni serikali ndio itawajibika!.
Hata hivyo, wanabodi msiwe na shaka, mwenye Dowans ni ndugu na yule jamaa aliyotoa zile suti, na alishakuja nchini na kusema yuko tayari kupunguza kiasi cha tozo, na kama mwenzake alitoa suti tuu mambo yake safi, huyu wa dowans akitusamehe deni lote, tunamkabidhi kabisa pande nono la ardhi ile yenye gesi asilia na mafuta kule Mtwara!.