TANESCO wabwagwa na Dowans mahakamani

Dowans inavyotetewa...ishazaa na kupata wajukuu miaka hii michache mpaka inapendwa kiasi hicho???
 
Jamani bandugu wenye taarifa ilojaa mashiko na uhakika kutoka source yoyote inayoeleweka naomba kufahamu hatma ya hii Movie imekwishaje kwenye hii episode ya mwisho ya rufaa ya TANESCO; mahakama imeamuaje maana naona hapa JF watu wametupia vitu tofauti mwingine anasema Mahakama imetupilia mbali rufaa ya TANESCO(Dowans imeshinda), mwingine anasema TANESCO imeshinda kesi sasa yupi mkweli???

UKWELI NI KWAMBA DOWANS WAMESHINDA LAZIMA WALIPWE
Kutokana na sheria za kimataifa isingewezekana kwa mahakama
kupingana na maamuzi ya mahakama za kimataifa ambayo Tanzania
ni mwanachama...kitendo hicho kingeweza kuitia Tanzania katika
mgogoro na Jumuiya ya kimataifa jambo ambalo athari zake ni kubwa
zaidi ya kuilipa Dowans.Hapa ndipo utagundua kuwa wale walioingiza
nchi katika maktaba na Richmond/Dowans walikuwa waangalifu sana
waliyajua haya yote ndiyo maana waliweka kipengele cha usuluhishi
wa kimataifa pamoja na vipengele kadhaa vya kuikandamiza nchi
HAPA TANZANIA HAKUNA MTU AMBAYE HANA BEI...YEYOTE ANAWEZA
KUNUNULIWA KUANZIA EXECUTIVE, JUDICIARY, LEGISLATURE,VIONGOZI WA DINI, & MEDIA.
MWENYEZI MUNGU TUNUSURU ROHO ZETU!!!!!!!!!!!!!!!!!!!!!!!!!!!!!!!!!!!!!!
 
Kama dowans wameshinda kesi ina maana pingamizi Lao limekubaliwa, sasa Kama pingamizi limekubaliwa ina maana Maombi ya Tanesco yametupwa na Kama Ndio hivyo ina maana hakuna Maombi mahakamani. Lakini Kama ulisikia TBC wamesema kesi imepangwa tarehe 18 machi 2012, hii haiwezakani kabisa Kama kesi itakuja tarehe hiyo ina maana kuna kesi mahakamani (Maombi ya Tanesco).Kwa Hali hiyo haitakuwa sahihi kusema Dowans imeshinda, Kama ni hivyo then we have a long way to go in Legal reporting, waandishi wapelekwe shule.

Ngambo N

Umeelewa vizuri kabisa TBC wameamua kuweka ushabiki
 
Kama dowans wameshinda kesi ina maana pingamizi Lao limekubaliwa, sasa Kama pingamizi limekubaliwa ina maana Maombi ya Tanesco yametupwa na Kama Ndio hivyo ina maana hakuna Maombi mahakamani. Lakini Kama ulisikia TBC wamesema kesi imepangwa tarehe 18 machi 2012, hii haiwezakani kabisa Kama kesi itakuja tarehe hiyo ina maana kuna kesi mahakamani (Maombi ya Tanesco).Kwa Hali hiyo haitakuwa sahihi kusema Dowans imeshinda, Kama ni hivyo then we have a long way to go in Legal reporting, waandishi wapelekwe shule.
...sio in legal reporting tu,waende shule kwa mambo mengi,kwa kifupi imegubikwa na vilaza
 
kwa sarakasi za nchi hii, you can never tell. unaweza ukute DOWANS ilishalipwa ndo maana RA anataka kurudi kwao Malaysia. Trust no body hata kama ni baba yako (only in Tanzania)
 
Nani kashinda nani kashindwa return yake ni kidogo kwa Watanzania hapa la msingi ni kuwa Watanzania tutakuwa tumeibiwa kutokana na mzimu wa ubinafsi kwa Tanesco kulipa mabilioni hayo. AG atakuwa na kesi ya kujibu kwa Watanzania kwa kushindwa kutekeleza majukumu yake vilivyo kwa kushindwa kutoa ushauri madhubuti wa kisheria tangu hatua za mwanzo za kusaini mkataba na kuvunja mkataba na wezi hao.
 
Confused,which is which?hizi tv zetu ni tatizo kwali hasa hii inayoitwa TBC1 imekua ya magamba tu mi nilishaacha kuiangalia maana wamekua kama gazeti la uhuru
 
Hapa suala la Dowans au Tanesco kushinda silioni kilichotangazwa TBC1 na Channel Ten ni Mahakama kuu kutupilia mbali pingamizi la Tanesco kuhusu nia yake ya kukata rufaa kuhusu tozo ya ICC na imesema hukumu ya ICC ni halali kisheria. Sijui kama mfuatiliaji wa ITV alikuwa makini.

huo ndio ukweli,tanesco wameshindwa na hukumu yakuilipa dowans ni halali,chanzo chanel10 na tbc1.
 
haya mambo yanatisha sana kama mwanasheria wa tanesco kwa sasa hivi ni ametokea kampuni ya vodacom nini kitakachofata hao jamaa washatuvise
 
haya yetu macho, maana wengine leo tumenunua umeme tsh 273 , sasa dowans wakishinda utapanda ufike sh 500 kwa unit. Heri tanesco washinde tu ingawa sio guarantee
 
TANESCO wameshida pingamizi Lao la kukata rufaaa! Maana yake wanaweza pinga hukumu ya dowans. Dowans iliyokuwa ikitetewa na wakili Kennedy Fungamtama alishikwa na butwaa baada ya hukumu kusomwa. Kuna uwezekano mkubwa sana Dowans wasilipwe. Huu ni ushindi kwa watanzania

Source ITV saa 2 usiku
Kweli mwenye nacho ataongezewa, ina maana hawa akina Mwanaidi Maajar watandelea kutafuna pesa zetu kwa gia ya kujifanya wanaitetea Tanesco!!??
Tumeliwa hapa jamani mchana kweupeee!! kabla ya kushabikia hiyo kesi ni vyema kwanza muulize hiyo kampuni ya uwakili inayoiwakilisha Tanesco imeshalipwa Billioni ngapi?
 
Wanajamii, machungu zaidi Tanesco kwani Mahakama ya rufaa imetupilia mbali pingamizi la Tanesco. Hii ina maana kuwa Tanesco lazima walipe bil 104 na ushehe!

Hapa nachanganyikiwa: Taarifa ipi iko sahihi? Rev Fr Masanilo kwa moja ya post za leo anasema "TANESCO wameshida pingamizi Lao la kukata rufaaa! Maana yake wanaweza pinga hukumu ya dowans. Dowans iliyokuwa ikitetewa na wakili Kennedy Fungamtama alishikwa na butwaa baada ya hukumu kusomwa. Kuna uwezekano mkubwa sana Dowans wasilipwe. Huu ni ushindi kwa watanzania

Source ITV saa 2 usiku
"

Hapa nielewe ipi?????

Ningefarijika zaidi TANESCO wangeshinda ili hilo deni lisilipwe.
 
TANESCO wameshida pingamizi Lao la kukata rufaaa! Maana yake wanaweza pinga hukumu ya dowans. Dowans iliyokuwa ikitetewa na wakili Kennedy Fungamtama alishikwa na butwaa baada ya hukumu kusomwa. Kuna uwezekano mkubwa sana Dowans wasilipwe. Huu ni ushindi kwa watanzania

Source ITV saa 2 usiku

Wanawapiga changa la macho mtulie mafisadi wakagawane hizo gela kimya kimya
 
0 Reactions
Reply
Back
Top Bottom