TANESCO, kukata umeme bila kuwa na ratiba maalum inatukwaza sana wateja wenu

incharge

JF-Expert Member
Jan 19, 2011
3,107
3,944
Haya mateso tunayopata kama wananchi ni makubwa mno, umeme unakatika hujui unakatwa saa ngapi wala unarudi saa ngapi, tofauti na nchi za wenzetu hata kama kuna tatizo basi ratiba ifahamike na wahusika hao wakata umeme waifuate sio wanajiamulia tu, sisi kama wateja tuna haki ya kufahamu ili tujipange kwenye shughuli zetu za uchumi na kijamii.

Leo kwa mfano hapa karibu na shule ya liberman Mbezi beach wamekata tangu saa kumi jioni hadi sasa saa tisa alfajiri hawajarudisha huku kawaida tumezoea wakikata saa kumi jioni basi saa tano usiku wanarudisha sasa hatuelewi leo bwana mkata umeme labda starehe zimemzidi katusahau au kazidiwa na usingizi, ila kwa mateso haya nayoyapata nasali hapa namuomba mungu wafanyakazi wote wa TANESCO na mawaziri wao walaaniwe wao na vizazi vyao mungu naomba ujibu maombi yangu. Amen.
 
Haya yote ni product ya uongozi mbovu wa chichiemu. Mama watch 100 Kama uko humu. Ingiza mtaani sikia vilio vya Wananchi.watu wanalia na ongezeko la nauri, maji kukata Mara kwa Mara tena bila taarifa, Mambo ni mengi saivi hata sigara hazinunuliki zimepanda kwa 50%
 
Kwani huko kwenu hamna wagroup ya TANESCO WhatsApp ya mkoa na wilaya maana huku kwetu changamoto yoyote lazima viongozi watueleze vizuri imekuaje na watashughulika nayo vipi na huko ndo ambako wanatupa taarifa zote na updates za dharura zote zinazohusiana na kukatika kwa umeme. Naona hii imesaidia kidogo huku kwetu umeme ukikata tunajua ni kwa sababu gani na utarudi baada ya mda gani.
 
Na kwa nini wapange ratiba ya kukata umeme hata baada ya zaidi ya miaka 60? Bajeti ya ununuzi wa V8s inapatikana, kulipana posho za safari, kununua magoli ya simba na yanga ila ya kuwekeza kwenye nishati inasuasua?
 
Yaani mbezi walichotufanyia, nlitamani kuamka usiku kuandika Uzi kwamba Hawa viongozi wanatuchukulia sisi kama punda hivi. Manake hata binadamu hawi treated hivi. Sijui wanatuchukuliaje wananchi nashindwa kuelewa ujue. Loh . Serikali ya hovyo hii kuwahi kutokea. Ptuuuu.
 
Mtoa hoja kwani huijui office ya tanesco kwenda kufanya push back pale ?,kulalama humu hakusaidii chochote, tanesco wanajiona wapo untouchable, kilichobaki ni kuwafanyia push back ili kuwaondoa kwenye ile comfort zone yao
 
Mbona wamekuwa wakitangaza mara kwa mara kama kuna matengenezo eneo fulani sema tu uko buzy sana na majukumu yako ndiyo maana unakosa taarifa muhumu kama hizo.
 
Kwani huko kwenu hamna wagroup ya TANESCO WhatsApp ya mkoa na wilaya??.. maana huku kwetu changamoto yoyote lazima viongozi watueleze vizuri imekuaje na watashughulika nayo vipi.. na huko ndo ambako wanatupa taarifa zote na updates za dharura zote zinazohusiana na kukatika kwa umeme.. Naona hii imesaidia kidogo huku kwetu umeme ukikata tunajua ni kwa sababu gani na utarudi baada ya mda gani
Lipo walisema utarudi after 5 hours yaani saa nne usiku..cha ajabu hadi saiv saa moja asubuhi haujarudi
 
Unavyowatetea tanesco wewe utakuwa mfanyakazi wao wewe siyo bure.
Hawa ni kumuomba mungu awalaani tu na vizazi vyao mbwa hawa wanatutesa tu na saa kumi na mbili wameshakata umeme sasa kuna umuhimu gani ya kuwa na taneaco au viongozi nchi hii ?halafu linatoka jitu linaomba eti wananchi mniombee thubutu sisi tunawalaani tu mteseke kama sisi
 
Hawa ni kumuomba mungu awalaani tu na vizazi vyao mbwa hawa wanatutesa tu na saa kumi na mbili wameshakata umeme sasa kuna umuhimu gani ya kuwa na taneaco au viongozi nchi hii ?halafu linatoka jitu linaomba eti wananchi mniombee thubutu sisi tunawalaani tu mteseke kama sisi
Mkuu Punguza Jazba tunashughulikia usimikaji wa Nguzo soon mambo yatakuwa sawa yaani utatumia umeme kwa kujimwaya mwaya hata ukitaka kuunywa utaunywa
 
Back
Top Bottom