Awamu ya Pili ya maandalizi ya kupokea umeme kutoka kwenye mitambo yakufua Umeme JNHPP kuingia Gridi ya Taifa Januari 13-21, 2023

Roving Journalist

JF Roving Journalist
Apr 18, 2017
2,813
11,991
IMG_9589.jpeg



Shirika la Umeme Tanzania (TANESCO) linautaarifu umma kuhusu awamu ya pili ya kuunganisha kituo kipya cha kupoza umeme cha 400kV Chalinze na njia ya msongo a kilovoti 220 inayoanzia Luguruni hadi Morogoro.

Kazi hii itakapokamilika itaongeza uwezo wa kituo cha 400kV Chalinze kupokea Umeme utakaozalishwa kutoka kwenye Mitambo ya Umeme ya Bwawa la Nyerere (JNHPP) na kuingiza kwenye Gridi ya Taifa.

Zoezi hili liltaanza siku ya Jumamosi tarehe 13 Januari 2024 hadi tarehe 21 Januari 2024. Aidha, kipindi zoezi hili linapoendelea kutakuwa na athari za kutopatikana umeme kwa nyakati tofauti katika baadhi ya maeneo yaliyounganishwa na Gridi ya Taifa, kwani njia ya msongo wa kilovoti 220 Luguruni-Morogoro italazimika kuzimwa na kuiunga kwenye kituo cha 400kV Chalinze.

Kuzimwa kwa njia hii kutaathiri uwezo wa usafirishaji wa umeme kwenda mikoani na ubora wa umeme kwa mikoa ya Pwani na Dar es Salaam. Kutokana na athari hizi shirika linalazimika kupunguza matumizi ya umeme kwa wateja ili kuendana na uwezo wa njia za usafirishaji na kuwa na uhakika wa ubora wa umeme.

Kuhamishiwa kwa njia hii kwenye kituo cha kupoza meme cha chalinze, sambamba na njia nyingine za usafirishaji umeme zitakazohamishiwa kwenye kituo hicho katika siku za usoni, kutawezesha kusafirisha umeme unaozalishwa kwenye Bwawa la Julius Nyerere na kuufikisha katika maeneo mbalimbali ya nchi yetu.

Shirika linawaomba radhi wateja wake kwa usumbufu utakaojitokeza.
 
Ikikaribia mashindano makubwa kama AFCON na World Cup umeme huwa unakuwa magumashi dah.
 
nyie bakini na huo umeme wenu kama tutaendelea kulipishwa laki mbili kununua nguzo bora tukae gizani tu
 
Sawa, muhimu umeme baadae uwe wa uhakika na bei rafiki.
Kwenye bei hapo tulishapigwa na kitu kizito tangu blah blah za gesi ya mtwara. Wananchi walipewa matumaini hewa sana ila uhalisia ukawa tofauti.

Kwahiyo kaza mkanda tu
 
Back
Top Bottom