Wakuu huku Arusha inaenda siku ya pili sasa tunakaa tu.. hakuna kazi kisa hakuna umeme ukiuliza Tenesco wanasema ni mgao...ila ni Juzi tu hapa Ngeleja alisema mambo ni mazuri....
sasa najiuliza ni Arusha tu au ni kote....
Tueleweje kauli ya waziri husika kwamba hakuna shida ya umeme?
Wakuu huku Arusha inaenda siku ya pili sasa
tunakaa tu.. hakuna kazi kisa hakuna umeme ukiuliza Tenesco wanasema ni mgao...ila ni Juzi tu hapa Ngeleja alisema mambo ni mazuri....
sasa najiuliza ni Arusha tu au ni kote....
Tueleweje kauli ya waziri husika kwamba hakuna shida ya umeme?
Tumekuwa tukisikia kutoka uongozi wa TANESCO kuwa mgao wa umeme umekwisha, lakini kauli hii imekuwa ni kiini macho tu, kwani mgao unaendelea kama kawaida japo hawajatangaza, kama mikoa mingine hakuna mgao lakini waulizeni watu wa Dodoma wanaoipatapata. je, tuatafika kwa hali hii? kumbukeni hii February tu.
Nilikuwa Morogoro umeme upo lakini hauna nguvu ya kuwasha fridge au chombo kikubwa wiki yote hii labda tv na radio tu. Clouds wamezimika pale naona hawana generator
Ingawa Tanesco hawataki kukubali, lakini hiyo ndiyo hali halisi tunayokabiliana nayo hivi sasa