Tanesco; Hivi kuna mgao wa umeme kimya kimya?

Kwani mgao uliisha ? tunakatiwa masaa 12 mara 3 kwa wiki zaidi ya miaka 2 sasa,nipo Dar.
 
Kuna mgao ndugu hilo naomba uelewe! Kwa upande wa Tabora mjini tumeanza kuzoea!.... Nenda kanunue generator!....

Mkuu pigangoma nashukuru kwa taarifa. Kwa hali hii ngumu hata pesa ya matumizi sina hiyo ya generator nitaipata wapi mkuu?
 
Kwani mgao uliisha ? tunakatiwa masaa 12 mara 3 kwa wiki zaidi ya miaka 2 sasa,nipo Dar.
Poleni mkuu huku Arusha hili tatizo limeanza kama wiki sasa, walituambia wanafanya service kwenye mitambo lakini wapi, service hata usiku?
 
Jamani ndugu zangu wanajf, naomba nipate msaada kwa hili, je ni kweli mgao wa umeme umeanza au kuna matatizo ya mitambo ya uzalishaji hii nishati?

MKUU!

Yaani wewe unauliza habari za mgao wakati ndiyo sera ya TANESCO kwa hivi sasa!!!! Sisi wa MUHEZA Tanga tulisha zoea kwamba umeme ni ANASA. Juzi waziri kasema eti TANESCO wanazalisha umeme wa ziada na hajui waupeleke wapi!! Wakati huo kaacha kazi za wizara na kwenda mikoani kupokonya CHADEMA wanachama.

Hadi 2015 mbona tutaipata wakuu!
 
MKUU!

Yaani wewe unauliza habari za mgao wakati ndiyo sera ya TANESCO kwa hivi sasa!!!! Sisi wa MUHEZA Tanga tulisha zoea kwamba umeme ni ANASA. Juzi waziri kasema eti TANESCO wanazalisha umeme wa ziada na hajui waupeleke wapi!! Wakati huo kaacha kazi za wizara na kwenda mikoani kupokonya CHADEMA wanachama.
Kazi ipo mkuu kama ulivyosema
Hadi 2015 mbona tutaipata?
 
huko moro na sisi tupo kwenye giza saivi ,sijui hadi tugome ndO watangaze mgao na ratiba yake
 
Achane kujipatia misifa bana!! kumbe nyie mna umeme??? sisi hapa kijijini kwetu bwai toka dunia imeumbwa hatujawahi kuuona umeme wala hatujui unafananaje nashangaa eti kuna mgawo mbona sisi fungu letu hatujawahi kupewa?? mgao gani huu wa kupendeleana??? Twambieni sasa kama sisi siyo sehemu ya JMT, tunaweza kujianzishia kiinchi chetu au tukaomba muungano na Kenya, kama zanzibar na Danganyika.
 
Sijawahi pata kusikia raisi ana toa tamko halafu halitekelezeki
Sijawahi pataona raisi ana danganya wananchi wake
Sijawahi ona raisi ambaye hafuatilii alicho ahidi wananchi wake

Sijui tumelogwa ama ni ninikinaikumba Tz ni miaka ina karibia miwili sasa
Serikai imeshindwa kabisa ku ondoa tatizo la mgao wa umeme.

Tuliambiwa ikifika mwezi wa kuminamoja tutausahau mgao waumeme
Tukaamimba kuna makampuni mengi yanaanza kuzalisha umeme
Tukaambiwa tunapandisha bei ilikukithi mahitaji ya umeme

Raisi wetu aka simama akatoa tamko kua baada ya mwezi wa kumini mbilo hatutakua na mgao tena
Waziri nae hakua mbali kwasautikubwa tena ya majigambo eti mwezi wakumina mbili totizo linaondoka

Sas ni mwezi wa pili na mgao upo palepale huku hatuna umeme tangia asubuhi
Nikusema kua tumeshindwa kaboisa ku ondoa hili tatizo?
Je tutaendelea kudanganyana mpaka lini?
Ama historia walio sema ndo hii ya kuendelea kua na mgao?
 
Kwamba umeme utakua historia kutatulika kwa hapa tanzania we pitia upya speeches zake utamuelewa!
 
Liganga na mchuchuma tunategemea itazalisha megawatt 500 mpaka kufikia mwezi wa December mwaka huu
 
Nina hasira sn umeme makwetu umekesha unawaka na kuzma ss wamekata toka 5 asubuh hadi ss hakuna kitu!!
 
Nina hasira sn umeme makwetu umekesha unawaka na kuzma ss wamekata toka 5 asubuh hadi ss hakuna kitu!!

hata hapa maswa sa hiz hatuna umeme! Tumebaki kukumbuka tu maneno "ya kitaalam" yanayoambatana na takwimu wanayotuambia watawala wetu, msongo, kilowati,kapasiti chaji nk
 
Serikali imeshindwa kuondoa tatizo la mgao wa umeme, waliahidi mgao itakuwa historia ndani ya kipindi cha kwanza cha utawala wa Vasco da Gamba, lakini mpaka leo ahadi zimebaki kama historia.

Huku Mwanza tumeshazoea kukaa gizani muda mrefu. Huu ujanja ujanja wa kuendesha uchumi wa nchi kwa kutumia generator za kukodi hatutafika mbali kwani ni dalili ya watawala kushindwa kutawala nchi na kubaki kuwapoison wanayo ipinga.
 
Tanesco wamekuwa wanasiasa! Hapa ninapoandika, nilikuwa namalizia research report yangu, umeme umekatika, laptop imeisha charge sasa nimebaki na hasira tupu. Siwapendi Tanesco, wanatuumiza sana wananchi.
 
Tanesco wamekuwa wanasiasa! Hapa ninapoandika, nilikuwa namalizia research report yangu, umeme umekatika, laptop imeisha charge sasa nimebaki na hasira tupu. Siwapendi Tanesco, wanatuumiza sana wananchi.

Toa hayo makengeza, kila umeme ukizima uwapo nyumbani kwako basi acha kazi yako anza kuimba ..."Siiipeeeendi miiiii CCM na Tanesco yaoooooooo" ukifanya hivyo kila mara basi itasaidia hata wanao wakati wa kupiga kura siku za usoni
 
Wakuu huku Arusha inaenda siku ya pili sasa tunakaa tu.. hakuna kazi kisa hakuna umeme ukiuliza Tenesco wanasema ni mgao...ila ni Juzi tu hapa Ngeleja alisema mambo ni mazuri....

sasa najiuliza ni Arusha tu au ni kote....

Tueleweje kauli ya waziri husika kwamba hakuna shida ya umeme?
 
Back
Top Bottom