Tanesco; Hivi kuna mgao wa umeme kimya kimya?

mwanaasha has reflected jk inteligence, amani haijawahi kuleta maendeleo au mabadiliko chanya tokea kuumbwa kwa ulimwengu ila mapambano, we either pay sweat or blood to bring changes and install serious people in the government.
 
Tanesco watoe tamko tatizo liko wapi, ni katika mfumo wa uzalishaji au katika mfumo wa usambazaji. Kutokana na ukimya wao wakati mambo hayaendi vizuri tuna kila sababu ya kusema kila tunachohisi. Watumiaji waelezwe tatizo na litaendelea mpaka lini.

Kumbe malalamiko ya kukatikakatika umeme ni makubwa sehemu nyingi wakati nilidhani ni huku kwetu tu. Je tusemeje matatizo ya muda mrefu ya mfumo wa kununua umeme kupitia vituo vya LUKU na njia zingine kama M-Pesa je nayo ni mgawo wa umeme nyuma ya pazia. Tanesco watoe tamko sababu na lini hali ya kawaida itarudi. Siku hizi ukienda vituo vya LUKU utaambiwa kuna matatizo katika mtandao na ukinunua kupitia M-Pesa / Tigo-Pesa inachukua siku moja hadi mbili kupata namba za 'token'. Usumbufu huu hadi lini ili tujiandae.
 
kaka bora huko temeke huku kwetu ndo balaa kila siku tunakosa umeme masaa manne hadi sita yaani hiyo ni kila siku afu hakuna hata tamko lolote toka tanesco mi nipo kiwira tukuyu mbeya:lol::lol:
 
Ndugu zangu hilo ni janga la kitaifa! Kwa Tabora sasa ni wiki ya sita kila siku ya jumamosi hakuna umeme kuanzia saa 2 asubuhi hadi saa1 usiku. Mwanzoni walituambia kuwa tatizo hilo litachukua muda wa wiki nne tu lakini sasa tumegonga sita! Sijui na jumamosi watakata!!!........
 
dah! Huku moshi ndo usiseme ndugu zangu tunaonewa kila baada ya muda unakatika,mbaya zaidi ni washa zima,washa zima sasa usalama wa vifaa vyetu uko wapi?au ndo kusema wanawafundisha wafanyakazi wapya jinsi ya kuwasha na kuzima kwa zamu,kama kuna mgao tangazeni kwny vyombo vya habari au mnaogopa gharama?tunaomba uungwana utumike kwa hili,
 
Wamejua watanzania tunaishi kwa imani na matumaini. Hivyo wakituambia mgawo umeisha tunaamini tu kuwa umeishi hata kama kiukweli mgawo bado upo.
 
inaonekana kuna tatizo kubwa linalopelekea kukatika kwa umeme sehemu kubwa ya nchi... TANESCO should come out clean on this matter asap, pamoja na kwamba huwa hawakosi sababu anyway...
 
Vijijini kwenu kuna umeme? Watanzania 14% ndio wenye umeme 95% kati yao ni wa mijini.

Nyie toka mhamie mijini muujuwe umeme ndio nini basi hatusemi.

Kha! Wewe kishoka unaongea kama mhandisi wa Taanesiku ati?
 
Mgao wa umeme upo naweza kulithibitisha hilo japokuwa TANESCO hawataki kusema. Kuna mgao DSM maeneo ya Kimara, Temeke, Kinondoni na Tabata. Pia kuna mgao mikoa ya Mwanza na Mara. TANESCO hawezi kikanusha hilo.
 
Jamani ndugu zangu wanajf, naomba nipate msaada kwa hili, je ni kweli mgao wa umeme umeanza au kuna matatizo ya mitambo ya uzalishaji hii nishati?
 
Back
Top Bottom