Tanesco; Hivi kuna mgao wa umeme kimya kimya?

Huwezi kuamini leo ni jumatatu sio kawaida yangu kuvaa Tshirt na Jeans lakini sikuwa na njia mbadala hizi ndio at least naweza kuvaa bila kupiga pasi-TANESCO hwana sababu ya kuona aibu sisi tushazoea matatizo yao, watutangazie tu huo mgao ili tuwezi kujipanga kama kawaida yetu!!
 
Ni wiki ya pili sasa inaelekea ya tatu hatuna umeme wa uhakika arusha,unakatwa na kurudishwa hovyo kama wanavyotaka bila hata taarifa wakati mwingini wanarudisha usiku wa manane,viongozi tanesko nao wamekuwa mabubu,bili kwa sasa hazikamatiki,umeme nao wakuimiwa,hivi mnatutakanini jamaniiii???
 
si tunajifanya chadema? ukitaka kujua CCM wanafikiria kwa masaburi type hivi kama mtu hakupendi si unatakiwa kumfanyia wema ili akupende?
 
Ni kweli hapa nilipo wamekata just before saa mbili na mpaka sasa haujarudi, hivi niulize kuna mgao wa siri siri? Tanesco tunaomba mtuambie kama ni kweli huo mgao upo.
 
Yaani mimi ndio im really dissapointed with tanesco arusha kabisa!siku ya 3 sasa hatuna umeme kisa nyaya zimekatika na tumewaeleza ,mitaa ya themi near 8-8,kwanini ni wagumu kuact hivyo
 
Yani misijui wanatuonaje kama leo wamekata kama mara tatu na sasahivi wameuchukua kabisa na kurudishwa hapo ni sa nane za usiku
 
Wana JF, hebu nisaidieni na haka kamgao ka kimya kimya. Ni karibia takribani wiki moja sasa nimekuwa nikifuatilia mwenendo wa upatikanaji wa umeme na kugundua kwamba unakatika zaidi ya masaa saba kwa siku. Sasa kama kuna mgao si wangetuambia.

Hivi huyu waziri Ngeleja mzee wa mikakati anafanya nini? Kwa nini asiondoke zake?
 
Sinza tokea jana saa mbili usiku mpaka saa hizi hatuna umeme sijui inakuwaje?? huyo Babra Masoud mbona hatuelezi chochote??
 
Wana JF, hebu nisaidieni na haka kamgao ka kimya kimya. Ni karibia takribani wiki moja sasa nimekuwa nikifuatilia mwenendo wa upatikanaji wa umeme na kugundua kwamba unakatika zaidi ya masaa saba kwa siku. Sasa kama kuna mgao si wangetuambia.

Hivi huyu waziri Ngeleja mzee wa mikakati anafanya nini? Kwa nini asiondoke zake?
Si mliwachagua wenyewe? nunueni majenereta...
 
Mgao upo ila hawataki kutangaza... Kuna siku Babra Masoud alihojiwa clouds radio akakanusha kuwa hakuna mgao ila kuna mashine mbovu zinafanyiwa matengenezo.
 
Mabwawa ya kuzalisha umeme yamepungukiwa na maji. Ila pia nadhani hilo la wahandisi nao wanamkono wao katika hili si la kulidharau maana Dar tuna mitambo kibao ya kufua umeme kuanzia ya gesi hadi ya IPTL.
 
Jamani wanajamii, hivi kwa nini tanesco wasitutangazie sisi wakazi wa Marangu, Mwika na Rombo kuwa kuna mgao wa umeme? Hii ni wiki ya tatu sasa karibia kila siku umeme unakatika kwa zaidi ya masaa 6 hadi 12. Je, hii ni hitilafu au ndo mgao wenyewe?
 
Ni tabia yao Kamanda!

Na unajua tabia haina dawa!
Kuweni wavumilivu tu mpaka UKOMBOZI utakapokuja!
 
Si huko tu ndugu yangu kwani kuna tatizo kubwa sana hata maeneo ya geita. Umeme unakatika mara kwa mara na wakati mwingine kwa muda mrefu tu! Ni tatizo ambalo limekuwepo kwa muda sasa kwanini zaidi ya mwezi mzima. TANESCO hawatatangaza kwa sababu tatizo haliko Dar es Salaam. Hivi ndivyo Tanzania yetu ilivyo kwani haki za mteja haziheshimiwi kwa namna yoyote ile na ndo maana huwasikii hao TANESCO wakisema chochote.
 
Back
Top Bottom