TANESCO haina tena nguzo za kusambaza umeme majumbani

Na yule Waziri wao matamko anahangaika na gesi sasa maana suala la umeme kukatika limemshinda , yaani Samia ana kazi sana hii ndio faida ya kuokota makombo ya ******** na kuyarudisha serikalini
 
Mkandarasi wa rea akishinda tenda ni jukumu lake kununua vifaa na kujenga line...hapelekewi kifaa hata kimoja na tanesco...tanesco kazi yake ni kukagua na kuhakiki ubora wa hivyo vifaa anavyojengea mkandarasi ili viendane na viwango vya tanesco kwa kuwa mkandarasi wa rea akishajenga anakabidhi mradi na miundombinu aliyojenga kwa tanesco kwa ajili ya uendeshaji...malipo kwa wauza vifaa yanalipwa na wakandarasi
 
Umeongea kwa uchungu sana😂😂
 

TANESCO kwani 2020 mlikua mnapata wapi nguzo!?

Msimzingue mama
 
Mkuu nina jua ninachokiongea, vifaa vyote, hununuliwa na tanesco, na ndio maana hata mwaka jana, kuna mkandarasi alitaka simamishwa na waziri kuwa ana chelewesha kazi, yupo nyuma ya muda, pale alimwambia waziri mimi nitafanyaje kazi, kwani nguzo tumeshasimika, tatizo ni nyanya , transifoma na mita , tanesco wanasema wameagiza bado hazijafika nchini!!pale pale akaulizwa meneja wa tanesco mkoa husika, akikiri hilo!!ndio waziri akatoa maelekezo kwa mkurugenzi mkuu.Na ni kweli kuwa wakishamaliza kujenga mradi huukabidhi kwa tanesco.
 
Mkuu mimi mwenyewe nilishawahi kufanya kazi , kwenye mradi mmoja huko Tanganyika,2017, hadi mkandarasi aliamua kusimamisha kazi, kutokana na inshu ya nyaya!!kila leo anaambiwa materials hakuna, hadi waziri kalemanyi alipokuja akakuta mradi umesimama, ndio kutoa maagizo kwa tanesco ndani ya wiki mbili nyaya ziwe zimepatikana, na kweli cjui walikwenda kuzitoa wapi, ndani ya muda nyaya zilipelekwa,
 
Watanzania tunachojua ni kuchonga maneno. Mabeberu walituambia kwa mwendo huu mtasambaza umeme walau kuwafikia 80% ya wanainchi wenu labda itakuwa 2050 mataga wakanuna. Ona sasa tunazidiwa hadi na Rwanda ambayo zaidi ya 80% wa wakazi wake wamefikiwa na huduma. Sisi ni kuchonga maneno ndo tunachoweza.
 
Mapinga wamesitisha utoaji wa Control Number kwa sababu nguzo hamna
 
Cookies are required to use this site. You must accept them to continue using the site. Learn more…