TANESCO haina tena nguzo za kusambaza umeme majumbani

Na yule Waziri wao matamko anahangaika na gesi sasa maana suala la umeme kukatika limemshinda , yaani Samia ana kazi sana hii ndio faida ya kuokota makombo ya ******** na kuyarudisha serikalini
 
Kwenye miradi ya REA, baada ya mkandarasi kuwa ameshinda Tenda, yeye ni kujenga line tu, vifaa vyote analetewa na tanesco, tanesco wao ndio huwa wanatangaza zabuni kwa makampuni, yanayoshinda yanapewa hizo kazi, za nguzo, yanaenda mfano sao hills, au kwa wazalishaji wengine wa nguzo, na kuingia nao mikataba, tanesco akiwa kama mdhamini, inategemea na makubaliano, yao lakini mala nyingi huweza kulipa advance tu, nyingine badaye.
Mkandarasi wa rea akishinda tenda ni jukumu lake kununua vifaa na kujenga line...hapelekewi kifaa hata kimoja na tanesco...tanesco kazi yake ni kukagua na kuhakiki ubora wa hivyo vifaa anavyojengea mkandarasi ili viendane na viwango vya tanesco kwa kuwa mkandarasi wa rea akishajenga anakabidhi mradi na miundombinu aliyojenga kwa tanesco kwa ajili ya uendeshaji...malipo kwa wauza vifaa yanalipwa na wakandarasi
 
Inaonekana hata hujui unachokiandika!!eti unangisha umeme wa REA?, hao wana umeme?!!totauti na TANESCO, au hujui hata maana ya REA, ndio wale unawasikia eti umeme wa REA, sio mzuri!!!kama yupo mjini huo umeme wa mradi ataupata wapi?wakati kote huku kero ni nguzo na mita?unapoona huko vijijini mnapata umeme wa mradi mnazania na watu wa mijini kuvutiwa umeme ni kazi rahisi kama huko?!!
Umeongea kwa uchungu sana😂😂
 
Katika Hali isiyo ya kawaida ,Kwa mara ya kwanza tangu awamu ya tano,imetokea Hali isiyo ya kawaida ya kukosekana Kwa nguzo za kuunganisha wateja umeme Tanzania. Hakuna wilaya hata moja nchini insyotoa huduma ya kuwapatia wateja nguzo ili wananchi waweze kupata huduma ya umeme. Kila ukiuliza unaambiwa tunaweka nguzo keenye bajeti. Ni bajeti ipi hiyo ambayo ilisomwa July na Sasa ni August.

TANESCO kwani 2020 mlikua mnapata wapi nguzo!?

Msimzingue mama
 
Mkandarasi wa rea akishinda tenda ni jukumu lake kununua vifaa na kujenga line...hapelekewi kifaa hata kimoja na tanesco...tanesco kazi yake ni kukagua na kuhakiki ubora wa hivyo vifaa anavyojengea mkandarasi ili viendane na viwango vya tanesco kwa kuwa mkandarasi wa rea akishajenga anakabidhi mradi na miundombinu aliyojenga kwa tanesco kwa ajili ya uendeshaji...malipo kwa wauza vifaa yanalipwa na wakandarasi
Mkuu nina jua ninachokiongea, vifaa vyote, hununuliwa na tanesco, na ndio maana hata mwaka jana, kuna mkandarasi alitaka simamishwa na waziri kuwa ana chelewesha kazi, yupo nyuma ya muda, pale alimwambia waziri mimi nitafanyaje kazi, kwani nguzo tumeshasimika, tatizo ni nyanya , transifoma na mita , tanesco wanasema wameagiza bado hazijafika nchini!!pale pale akaulizwa meneja wa tanesco mkoa husika, akikiri hilo!!ndio waziri akatoa maelekezo kwa mkurugenzi mkuu.Na ni kweli kuwa wakishamaliza kujenga mradi huukabidhi kwa tanesco.
 
Acha kupotosha watu.
Mkataba ni kati ya REA na Mkandarasi. Tanesco yeye ni kusimamia tu mradi ujengwe katika standards and specifications zake tu. Mkandarasi yeye ataleta materials yote as per tanesco specifications.

Unajua kitu kinachoitwa TURNKEY.
Miradi yote ya REA ni TURNKEY projects.
Mkuu mimi mwenyewe nilishawahi kufanya kazi , kwenye mradi mmoja huko Tanganyika,2017, hadi mkandarasi aliamua kusimamisha kazi, kutokana na inshu ya nyaya!!kila leo anaambiwa materials hakuna, hadi waziri kalemanyi alipokuja akakuta mradi umesimama, ndio kutoa maagizo kwa tanesco ndani ya wiki mbili nyaya ziwe zimepatikana, na kweli cjui walikwenda kuzitoa wapi, ndani ya muda nyaya zilipelekwa,
 
Watanzania tunachojua ni kuchonga maneno. Mabeberu walituambia kwa mwendo huu mtasambaza umeme walau kuwafikia 80% ya wanainchi wenu labda itakuwa 2050 mataga wakanuna. Ona sasa tunazidiwa hadi na Rwanda ambayo zaidi ya 80% wa wakazi wake wamefikiwa na huduma. Sisi ni kuchonga maneno ndo tunachoweza.
 
Mapinga wamesitisha utoaji wa Control Number kwa sababu nguzo hamna
 
4 Reactions
Reply
Back
Top Bottom