TANAPA yatangaza kifo cha Faru Rajabu (mtoto wa Faru John) katika Hifadhi ya Serengeti

John Haramba

JF-Expert Member
Feb 4, 2022
365
1,373
Shirikia la Hifadhi la Taifa Tanzania (TANAPA) limetangaza kifo cha Faru Rajabu aliyekuwa na umri wa miaka 43, leo Jumatatu Machi 21, 2022 akiwa katika Hifadhi ya Serengeti sababu ikitajwa kuwa ni uzee.

Faru Rajabu alikuwa mtoto wa Faru John ambaye alifariki mwaka 2015 akiwa na miaka 47.

Faru Rajabu ambaye alizaliwa mwaka 1979 eneo la Ngorongoro, mwaka 1993 alihamishiwa katika Hifadhi za Taifa ya Serengeti, ameacha watoto, wajukuu na vitukuu kadhaa.

TANAPA imeeleza kuwa wastani wa maisha ya faru Weusi ambao wapo katika kundi la Wanyama walio katika hatari ya kutoweka hukadiriwa kuwa na kati ya miaka 35 hadi 40.






affccce3-3387-4621-8e68-c03a51d6396a.jpg

 
Rest in peace Rajabu, hakika tulikupenda sana.




let’s meet at the top, cheers 🍻
 
Daah!!! natoa pole Kwa watoto,wajukuu na vitukuu wa Faru rajabu Kwa msiba huu mkubwa walioupata.......
 
Pumzika kwa amani Mzee Rajab,pole ziwaendee familia,ndugu,na jamaa waliopo hifadhi ya Serengeti na Tanzania kwa ujumla.
 
Back
Top Bottom