TANAPA yajipanga kukusanya Bilioni 343.8, Sasa Wanyama kupewa Majina ya Watu kwa gharama ya Milioni 5

Roving Journalist

JF Roving Journalist
Apr 18, 2017
3,067
12,497
Dodoma. Baada ya wanyama kupewa majina ya watu maarufu wa nje ya nchi, Shirika la Hifadhi za Taifa za Tanzania (Tanapa) limeanzisha utaratibu maalum wa kuwezesha watu wanaotaka baadhi ya wanyama waitwe majina yao kufanya hivyo lakini kwa kulipia Sh5 milioni.

Utaratibu huo nakuja baada ya baadhi ya wanyama akiwemo simba aliyepewa jina Bob Juniour, faru aliyepewa Faru John na Rajabu.

Hayo yamesemwa Jumatatu Julai 24, 2023 na Kamishina wa Uhifadhi wa Tanapa, William Mwakilema wakati akielezea utekelezaji wa majukumu na mwelekeo wa utekelezaji wa majukumu kwa mwaka 2023/24.
Tana1.jpeg

“Tumeanzisha utaratibu wa kuwapa majina baadhi ya wanyama lakini sio bure. Na hawa wanyama sio wote labda kama umesema kuwa unampenda sana fisi unataka huyo fisi awe na jina lako,”amesema.

Amesema bodi ya menejimenti ya Tanapa imeshapitisha utaratibu huo ambao utaanza na wanyama aina ya faru.

Pia amesema mtu yoyote ambaye anataka aendelee kumuona anaweza kumuasili na atatakiwa kuchangia gharama za kumuhifadhi za Sh1 milioni kila mwaka.

Hata hivyo, amesema wapo baadhi ya faru pia wana majina akiwemo yeye mwenyewe ambaye mmoja wa faru katika Hifadhi ya Serengeti amepewa jina lake.

Kuhusu simba aliyepewa jina la Bob Juniour, Kamishna Mwakilema amesema jina hilo alipewa na waongoza utalii baada ya kulinganisha mnyama huyo wakamlinganisha na Bob Marley ambaye alivyokuwa na rasta zake nyingi, ukubwa na kivutio kwa watalii.

“Bahati mbaya jina hilo halikutambulika hadi alipokuja kufa akaanza kuvuma kuwa Bob Junior amekufa,”amesema.

Wizara ya Maliasili na Utalii kupitia Shirika la Hifadhi za Taifa Tanzania - TANAPA limejipanga kukusanya mapato kupitia vyanzo vyake vya ndani kiasi cha Shilingi Bilioni 343.8 katika mwaka wa fedha 2023/2024 tofauti na mwaka jana ambapo ilikusanya shilingi bilioni 337.
Tana2.jpeg

Kamishna Mwakilema alisema, "shirika lina dhamana ya kusimamia na kuendeleza maeneo yaliyoteuliwa kuwa hifadhi za taifa hivyo TANAPA imeweka vipaumbele katika maeneo ya uhifadhi, ulinzi, utalii, ushirikishaji jamii na uboreshaji wa miundombinu pamoja na ukamilishaji wa miradi ya kimaendeleo ya shirika ili kufikia malengo tuliojiwekea".

Aidha, shirika limejipanga kuboresha miradi ya maendeleo kwa ukarabati wa viwanja vya ndege katika Hifadhi za Taifa za Ruaha, Mikumi na Nyerere, ikiwa ni pamoja na ununuzi wa ndege na Helikopta ili kuimarisha utalii pamoja na shughuli za ulinzi mkakati.

Hata hivyo, Kamishna Mwakilema alisema, "shirika limeendelea kujipanga katika kuboresha miradi ya maendeleo kwa kutenga bilioni 60.6 kwa mwaka wa fedha 2023/2024 ili kuwezesha utekelezaji wa maendeleo katika miradi mbalimbali inayosimamiwa na Shirika la Hifadhi za Taifa Tanzania(TANAPA)".

Sanjari na utekelezaji wa mipango hiyo itakayoweza kuimarisha uchumi kwa shirika na taifa kwa ujumla TANAPA pia, imejipanga kumaliza changamoto za uhifadhi kwa kushirikiana na taasisi nyingine za uhifadhi na serikali kwa kufanya kazi kwa weledi ili kumaliza migogoro ya wanyamapori wakali na waharibifu.

Naye, Msemaji Mkuu wa Serikali Gerson Msigwa alitoa shukrani kwa shirika kutoa ufafanuzi juu ya muelekeo wa TANAPA mbele ya wanahabari hao ambao utawaongezea uelewa kutoa taarifa sahihi zinazohusiana na ulinzi wa hifadhi za taifa na kuwa mabalozi wazuri wa kuvitangaza vivutio vya utalii kwa wananchi na namna shirika hilo linavyofanya kazi zake kwa weledi na maarifa.
Tana 3.jpeg

‘’Nikushukuru sana Kamishna wa Uhifadhi - TANAPA kwa taarifa yako yenye malengo chanya ya kukuza utalii na iliyotilia mkazo suala zima la uhifadhi wa maliasili. Hivyo ni matumaini yangu kuwa wanahabari hawa wameelewa dhana nzima ya uhifadhi wa vyanzo vya maji hivyo kupitia kalamu zenu watanzania wataelewa shughuli nzima ya uhifadhi’,’ alisema Msigwa.

Aidha, shirika linaendelea kutekeleza sera ya ujirani mwema ambapo pamoja na kutoa elimu ya uhifadhi shirika litaendelea kutekeleza miradi ya ujirani mwema iliyoanzishwa na jamii kwa kuchangia kiasi cha shilingi bilioni 2.3 kwenye miradi ya maendeleo kwa mwaka wa fedha 2023/2024, katika wilaya 20 za kipaombele.
 
Nikilipa hiyo 5m atabaki na jina langu mpaka afe au baadae watamuuza kwa mtu mwingine na kupewa jina jingine?
 
Na tracking ikoje? Kuna taasisi moja ya wenzetu walikuwa wanafanya hivi kwa sea turtles ila unaweza kuwatrack kupitia satellite
 
yaani watumishi wa serikali creativity zero kabisa.....kuwapa majina ya watu wanyama? kisha mtu alipia 1mil za kumtunza huyo mnyama ilhali myama yuko porini anakula na kunywa???
poor us watu wa ubunifu wanafanya kazi gani ifike kipindi idara kama hizo wapewe mikataba watu wenye ubunifu watuongezee tija kwenye mbuga zetu
 
Back
Top Bottom