TANAPA yaanza Mchakato wa kuanzisha Cable Car Mlima Kilimanjaro

Roving Journalist

JF Roving Journalist
Apr 18, 2017
2,808
11,973
IMG_20201213_102959_902.jpg

Kamishina msaidizi wa Uhifadhi wa TANAPA, ACC Paul Banga amesema General Management Plan(GMP) ambayo inahusisha Wadau wote wa Utalii, walipitisha mpango wa kuanzisha cable car katika Mlima Kilimanjaro ikiwa ni Mkakati wa kuongeza idadi ya Watalii nchini. Aliyasema hayo wakati wa Kikao cha Tanapa na Wahariri na Waandishi wa habari waandamizi Jiji Dodoma.

Banga amesema Cable car hiyo itaanzia karibu na Geti la Machame la kupandia Mlima Kilimanjaro na kuishia Uwanda wa Shira. Cable car itakuwa na Urefu wa mita 3,700 kati ya mita 5,895 za Mlima Kilimanjaro. Car cable haitafika kwenye Kilele cha Mlima Kilimanjaro

Amesema Kwa sasa Serikali bado inafanya Tathimini kuona kama Mradi Wauruhusu au Wasiuruhusu.

Kutoka na hofu ya watu wengi kupoteza ajira hasa wasaidizi wa wapanda Mlima, alifafanua kwamba kazi za kupanda mlima kwa mguu zitaendelea kama kawaida kilichoongezeka ni kumuwezesha Mtalii kiwa na Chaguo la Atumie Miguu au car cable.

Banga alisema anatumbua uwepo wa Walemavu na Wazee ambao wanatamani kupanda Mlima Kilimanjaro hivyo cable car itasaidia kutimiza ndoto zao.

Cable car ni gari linalotumia waya kutoka sehemu moja kwenda sehemu nyingine bila kugusa ardhi.

 
Curiosity killed the cat, na ndio majaribio yatakayozika utalii wa nje wa kupanda mlima. Usitegemee mzungu atoke Ulaya kuja kusafiri kwenye cable car. Its completely nonsense. Hizi akili za kichina zitafuta umuhimu wa mlima Kilimanjaro

Sio hilo tu uchafuzi wa mazingira kwa kuruhusu utatili wa wapanda mlima dezo utatugharimu

Nina imani huyo kibosile aliyependekeza mpango huo anatakiwa afukuzwe mapema iwezekanazo, ni hatari sana kuliko yule aliyeshindwa kula kiapo
 
Huu mradi hauna ubunifu wa kimkakati! Hauna maono kabisa! Mlima Kilimanjaro bookings zake zinatofautiana na mgeni anataka challenges zipi! Haswa machame route aka whiskey route inapendwa kwa geographical habits zake na ugumu wake ambayo ndio challenge wageni wanapenda! ukiweka hiyo cables cars directly umeondoa the brand of whiskey route ( the tough one)

Ajira na mapato yatapungua! Itapunguza bookings za siku Saba hadi tisa mlimani na mtu atalipia 2 hours permit! Mgeni mmoja anahitaji porters ( wagumu) watatu hadi wa nne mpishi mmoja, guide mmoja hawa watu directly hawana ajira! Hapo kuna familia sio chini ya nane zitasota!

Achaneni na huu mradi gharama zake mkaboreshe vyoo, picnic sites, na mifumo ya uvunaji maji kwenye campsites areas!
let the nature challenges takes it sedition
 
Curiosity killed the cat, na ndio majaribio yatakayozika utalii wa nje wa kupanda mlima.Usitegemee mzungu atoke Ulaya kuja kusafiri kwenye cable car.Its completely nonsense. Hizi akili za kichina zitafuta umuhimu wa mlima Kilimanjaro.
Sio hilo tu uchafuzi wa mazingira kwa kuruhusu utatili wa wapanda mlima dezo utatugharimu.
Nina imani huyo kibosile aliyependekeza ujinga huo anatakiwa afukuzwe mapema iwezekanazo,ni hatari sana kuliko yule aliyeshindwa kula kiapo.
Mkuu kumbuka kuwa; MUDA na TEKNOLOJIA havijawahi kishindwa na Binadamuwa nyama.!!
 
Hamna wazo la kijinga kama hili. Watalii wanatakiwa kuwa limited kwenye huo mlima ili kulinda hali yake. Sasa ikiwa kuupanda itakuwa kama kupanda dala dala nani utabaki kweli mlima? Yaani kweli tunataka watu waende kupiga picha za harusi kwenye kilele cha Kibo? Aidha, sehemu kubwa ya kivutio cha mlima huo ni ugumu wa kuupanda. Mtu unaupanda ili kujipima afya yako na ukifanikiwa unakuwa na sense of achievement. Hiyo sense of achievement utaipataje kama umepanda kwa lifti?

Na ukweli ni kuwa mradi huu hautaishia kwenye hizo mita 3700. Kwani wazee na walemavu nia yao ni kuishia Shira na sio Kibo? Huu mradi ni kama ngamia aliyeomba aingize kidole kwenye tent kwa sababu nje kuna baridi. Baada ya muda mfupi mwenye tent anajikuta yuko nje na naamiaiset ndio yuko ndani. Promoters wa huu mradi wanajua kuwa ombi la kujenga mpaka Kibo ni non starter. Lakini wakifika Shari itakuwa rahisi ku extend mpaka Kibo.

Hili ni wazo la kijinga mno na linastahili kupingwa kwa nguvu zote.

Amandla...
 
Huyu Banga anatakiwa aondolewe kwenye nafasi yake na vyeti vyake vikaguliwe upya. Hawa ndio wanaodhani kupitisha reli Serengeti na kujenga Mahoteli makubwa mengi kwenye National Parks ni maendeleo! Tunaona sifa kumchinja bata anayetaga mayai dhahabu. Ni mwendelezo wa yale yale ya Lake Natron. Hatuwezi kuangalia mbali zaidi ya vitovu vyetu.

Amandla...
 
Curiosity killed the cat, na ndio majaribio yatakayozika utalii wa nje wa kupanda mlima.Usitegemee mzungu atoke Ulaya kuja kusafiri kwenye cable car.Its completely nonsense. Hizi akili za kichina zitafuta umuhimu wa mlima Kilimanjaro.
Sio hilo tu uchafuzi wa mazingira kwa kuruhusu utatili wa wapanda mlima dezo utatugharimu.
Nina imani huyo kibosile aliyependekeza ujinga huo anatakiwa afukuzwe mapema iwezekanazo,ni hatari sana kuliko yule aliyeshindwa kula kiapo.

Ujui chochote,cable zinakuwepo na njia za miguu zinakuwepo pia maamuzi ni ya mteja.
Mfano wagonjwa,wazee,walemavu,wasio na mda watafika vipi juu bila cable.
 
Huyu Banga anatakiwa aondolewe kwenye nafasi yake na vyeti vyake vikaguliwe upya. Hawa ndio wanaodhani kupitisha reli Serengeti na kujenga Mahoteli makubwa mengi kwenye National Parks ni maendeleo! Tunaona sifa kumchinja bata anayetaga mayai dhahabu. Ni mwendelezo wa yale yale ya Lake Natron. Hatuwezi kuangalia mbali zaidi ya vitovu vyetu.

Amandla...

Wameshafikilia kabla yako inafaa na itaongeza idadi ya watalii wasio na mda wa kupoteza siku 7 kupanda na kushuka
 
Hamna wazo la kijinga kama hili. Watalii wanatakiwa limited kwenye huo mlima ili kulinda hali yake. Sasa ikiwa kuupanda itakuwa kama kupanda dala dala nani utabaki kweli mlima? Yaani kweli tunataka watu waende kupiga picha za harusi kwenye kilele cha Kibo? Aidha, sehemu kubwa ya kivutio cha mlima huo ni ugumu wa kuupanda. Mtu unaupanda ili kujipima afya yako na ukifanikiwa unakuwa na sense of achievement. Hiyo sense of achievement utaipataje kama umepanda kwa lifti? Hili ni wazo la kijinga mno na linastahili kupingwa kwa nguvu zote.

Amandla...

Usijufungie kwenye box panua brain yako.
 
Back
Top Bottom