Mlima Kilimanjaro

Comred Mbwana Allyamtu

JF-Expert Member
Jun 28, 2016
348
847
Mlima Kilimanjaro ndio Mlima mrefu kuliko yote duniani uliosimama peke yake "unaojitegemea" (Single Free standing).

Mlima Kilimanjaro pia ni mlima mrefu kuliko yote barani Afrika ukiwa na mita 5,895 (19,341 futi) juu ya usawa wa bahari na karibu mita 4,900 (16,100 ft) juu ya msingi wake wa miinuko, pia Kilele chake ni kilele cha nne kwa umaarufu duniani.

Mlima Kilimanjaro ni mlima wa nne kwa urefu duniani na wa kwanza kwa urefu Afrika, ndio mlima pekee duniani uliopo ukanda wa Tropical wenye theruji mwaka mzima kwa vipindi vyote.

Mlima Kilimanjaro uko nchini Tanzania katika Mkoa wa Kilimanjaro, Hali halisi Kilimanjaro ni zaidi ya mlima tu, ni kama safu ndogo ya milima mitatu, Kibo, Mawenzi na Shira.

Hiyo milima mitatu inaonekana kama vilele vitatu vya mlima mmoja, hivyo si vibaya kusema Kilimanjaro ni mlima mmoja.

Kijiolojia Kilimanjaro ni mlima wa volkeno iliyolala (dormant volcano) kwa sasa, Kwenye kilele cha Kibo gesi bado inatoka, Kumbukumbu ya wenyeji inasema kuwa mlipuko wa mwisho ulitokea mnamo mwaka 1730.

Kilele cha juu cha Kibo kinaitwa Uhuru, Mtu wa kwanza kufika kileleni hapo alikuwa Johannes Kinyala Lauwo kutoka Marangu aliyewaongoza Wajerumani Hans Meyer na Ludwig Purtscheller tarehe 6 Oktoba 1889 wakati wa ukoloni wa Ujerumani.

Wakati ule waliita ncha ya juu "Kaiser-Wilhelm-Spitze" (kwa Kijerumani, Kilele cha Kaisari Wilhelm) kwa heshima ya Kaisari wa Ujerumani.

Asili ya jina "Kilimanjaro" haijulikani hasa chanzo chake, ila zipo vyanzo vya asili vinavyoeleza hasa asili ya jina Kilimanjaro.

Vyanzo vya kimaandishi vinavyo julikana kuanzia mwaka 1860 kutoka kwa wapelelezi Wazungu hudai kuwa jina hilo "Kilimanjaro" ni jina la Kiswahili lenye kutokana na neno "Kilima-Njaro".

Elezo lingine ni kwamba Wachagga walisema mlima huo hauwezi kupandwa yani "kilemanjaare" au "kilemajyaro" na wapagazi au wafasiri kutoka pwani waliichukua kuwa jina la mlima na kutafsiri vile kwa Wazungu.

Tangu hapo na mpaka miaka ya 1880 mlima umekuwa sehemu ya Afrika ya Mashariki ya Kijerumani ukaitwa "Kilima-Ndscharo".

Tarehe 6 Oktoba 1889 Hans Meyer alikuwa mtu wa kwanza anayejulikana kupanda mlima na kufika hadi kilele cha Kibo, alichagua jina la "Kaiser-Wilhelm-Spitze" ("Ncha ya Kaisari Wilhelm", jina hilo lilitumika hadi Tanzania ilipoundwa mwaka 1964, na kilele kubadilishiwa jina kuwa "Uhuru", likiwa na maana ya "Kilele cha Uhuru".

Uhuru ni sehemu ya juu kwenye ukingo wa Kibo kwenye mlima Kilimanjaro, Taasisi ya Tanzania inayoshughulikia hifadhi ya Tanzania National Parks Authority, kwa kushilikiana na Kilimanjaro national park (KINAPA) kwa ushirikiano na UNESCO zimetoa report kuwa kimo cha Uhuru Peak cha mita 5895 kilichopimwa na ukoloni wa Uingereza mwaka 1952 umekuwa ukipungua.

Report hiyo inaonyesha kuwa mlima Kilimanjaro umekuwa unapungua polepole kimo chake, Kipimo cha awali ilikuwa ni mita 5892 mwaka 1999 na sasa ni mita 5891 kwa kipimo kilichofanywa mwaka 2014.

Ndimi Comred Mbwana Allyamtu (CMCA)
Marangu Mtoni, Kilimanjaro
3/06/2022
FB_IMG_1654277992221.jpg
 
Good bandiko.

Yafaa mabandiko ya hivi yawe mengi kwa urithi wa watoto na wajukuu zetu. Siku hizi watoto wetu wanajua zaidi historia ya Marekani na ulaya kuliko hivi vitu.

Tafadhali tujitokeze zaidi na zaidi kuandika hizi makala, watoke wengine waandike kuhusu lake Victoria, Lake Tanganyika, Amboni Tanga, Makonde na mengineyo
 
Good bandiko.

Yafaa mabandiko ya hivi yawe mengi kwa urithi wa watoto na wajukuu zetu. Siku hizi watoto wetu wanajua zaidi historia ya Marekani na ulaya kuliko hivi vitu.

Tafadhali tujitokeze zaidi na zaidi kuandika hizi makala, watoke wengine waandike kuhusu lake Victoria, Lake Tanganyika, Amboni Tanga, Makonde na mengineyo
Ukoloni mambo leo, watoto wanakaririshwa mambo kibao ya wakoloni wakati hata mlima Kilimanjaro hawajui ulipo achilia mbali maliasili na mambo kibao ya nchi yao. Mwisho wa siku wanasema watoto wamefail hivi kwa silabasi hizi nani anafail?
 
Back
Top Bottom