Tamthilia ya Othman ya Azam TV, lengo lenu ni kuudhalilisha Ukristo. Itoeni mara moja

chipa GM

JF-Expert Member
Jan 21, 2012
1,769
2,858
Tamthilia ya Othman ni tamthilia ya Uturuki ambayo hapa nyumani inaoneshwa na Azam Media. Maudhui ya tamathilia hiyo kuwa Dini ya othman (Uislamu) ni dini bora kuliko dini ya Wakristo (waroma).

Kwenye filamu hiyo utaona kuna mapigano baina ya Waislamu (Othman) na Wakiristo (Waroma)! Mapigano ni kwa ajili ya kusimika dini ya Uislamu na kila pambano wanashinda Waislamu dhidi ya Wakristo, na wakishinda utasikia Mungu mkubwa, Mungu mkubwa, Allah mkubwa.

Na wanaopigwa wanavaa nguo zimeandikwa Roma, na wanavaa misalaba na chanzo za ugomvi ni dini. Na hii siyo mara ya kwanza na kama unawafatilia hata hivi tamthilia Wanazozitafsiri lazma wasema Assalam Aleikum au Allah. Unakuta filamu ya Kifilipino au kizungu lazima wanao tafsiri waweke maneno ya Kiislamu.

Je, huu ni mkakati wenu Azam kuutukana ukiristo. Azam acheni propaganda za kidini, mnaharibu hiki kizazi. Hata kazi za watangazaji 'Hapo Azam asilimia 80 ni Waislamu, Km Bakhresa unapenda Uislam nenda kawekeze Uarabuni. Waislamu acheni ubaguzi nyie.
 
Wakikusikia utasikia,

"Hama kwani nani kakulazimisha kununua Azam".

Mimi baada ya kumuona mwanangu anajifunza kushika mapanga na kujisifia anakula vichwa kama osman anashushia na lugha za kiarabu hata sizielewi...siku hizi silipii kifurushi.

Maana leo Osman anakula vichwa vya waroma kesho huyu mtoto atatafuta wa kujaribishia..😥😥😥
 
Tujifunze kufuatilia tunayoyapenda, sidhani kama unaweza kwazika kama jambo fulani hulifurahii na kuliweka kando.

Maisha mafupi sana wapendwa, hizo dini tumeletewa tu na hiyo tamthilia ni moja ya buradani kwa mtazamaji anaefurahishwa nayo.
 
Mkristo: Anaamini kuwa Mungu anaweza kujipigania mwenyewe. Ukristu unaaminisha hata ukifa kwa ajili ya kristo na bado una dhambi utahukumiwa tu.

Muislam: Huyu anaamini kabisa Mungu wao kawaruhusu kupigana kwa ajili ya dini yao.

Pia ikitokea mtu kafia Uislam basi yeye moja kwa moja anaenda mbinguni hata kama ana dhambi kibao
 
Another thread ...again
Ottoman series ni series iliyo based na history ya kweli ya Ottoman empire.

Wakishaitoa hiyo series ungependa kingine kipi wafanye...tuagize na Google wafute history yoote ya Ottoman empire?

Ulipaswa kuangalia hiyo history ni ya uongo...ungekuwa Una Google kila kipande ..kama ni history ya ukweli...ifutwe yote?

Hata Google nao tuwape amri wafute hizo history sababu kuna watu hawazipendi?

Next time tuwaambie wafute na history ya ukoloni ambayo ilionesha wakoloni wazungu wakinyonga babu zetu waafrika...sababu wazungu wakristo tunawachafua?
 

Similar Discussions

Back
Top Bottom