Tamko la vijana wa Kagera kuhusu ziara ya Nape

ukistaajabu ya musa utayaona ya ccm.
baba yako anakufa hata kupiga simu ujue siku ya kuzika?

pamoja na roho ya huruma niliyonayo ccm mnastahili adhabu ya uma kwa hili.
 
Pole sana Nnauye Jr.

Hiyo ndiyo siasa, utasikia mengi, si lazima ujibu yote. Mungu alitupa masikio mawili, macho mawili na mdomo mmoja, ili tusikie mengi, tuone mengi na tuseme machache. Pole sana kwa yote, ila ukiona unazidiwa, soma nyakati, liachie hili li nyinyiemu, jiunge na vijana wenzako. wewe hutakuwa wa kwanza kuliachia, angalia lisifie mkononi mwako.

Mimi na marehemu Baba yako, (wakati huo akiwa mkuu wa Mkoa wa Pwani) pale Kibaha, tulikuwa waumini wazuri wa nyinyiemu, ila baadaye marehemu aliniusia kuwa nikiona linaanguka niliachie, hivyo nikatoka. na wewe karibu sana.

RIP NYINYIEMU.
 
Last edited by a moderator:
Nape alikuwa na majukumu mawili ya kufanya.Moja ni kutoa pole na la pili ni ziara zake za kisiasa na hilo si tatizo.Kwangu sina tatizo nalo.Mbona viongozi wengi tu wanapomaliza misiba wanaendelea na shughuri za kisiasa.Tatizo liko wapi jamani?Summary hakukataliwa kwa ajili ya taratibu za kimila ati zilikiukwa.issue watu walichoka na utawala wa kurithishana na siyo lingine.Mwacheni nape afanye kazi yake ni kweli nape ni mzalendo.Kwa hilo mimi sikatai hata kama mimi si mwanachamama wa chama chochote.
 
Ehe Matamko on the rise!!!! Sawa, uliyoyasema ni ya kweli kabisa, kuna haja ya kujua kama huyu kijana Nape alikwenda kwenye msiba au alikwenda kwenye shughuli zake za kisiasa na hilo la msiba liliingilia tu ratiba yake. I would think ili la msiba liliingilia tu ratiba yake kwani ufunguzi wa baraza sidhani kama uliweza kuandaliwa kwa muda mfupi kiasi hicho.

Swali la kujiuliza hili tamko limetolewa na vijana gani? Ni lini waliitisha hicho kikao na kukutana na hatimae kuamua kutoa tamko? Hawa vijana wa Bukoba mjini waishio Dar Es Salaam ni kina nani?

I am just curious?

Tiba
 
Nimesikitishwa sana sana NA UPOTOSHAJI MKUBWA UNAENDELEA KATIKA SAFARI YANGU YA KWENDA KAGERA! KILICHONIUMA ZAIDI NI JINSI WATU WANAVYOTAKA KUTUMIA MSIBA KAMA NGAO YAO YA KUPOTOSHA UKWELI WA SWALA ZIMA LA SAFARI YANGU KAGERA. KWA WASIOJUA AU WALIOAMUA KUPOTOSHA UKWELI KWA MAKUSUDI, DR. KYARUZI ALIKUWA RAFIKI MKUBWA WA MAREHEMU BABA YANGU MZAZI BRIG. GEN MOSES NNAUYE, HIVYO MAREHEMU KYARUZI NI SAWA NA BABA YANGU. NINA LAANI JUHUDI ZA KUTAKA KUTUMIA ZIARA YANGU KAGERA NA MSIBA WA MZEE WANGU KYARUZI KISIASA.

NAOMBA IJULIKANE KUWA KAGERA SIKWENDA RASMI KWA AJILI YA KUHANI MSIBA, ISIPOKUWA NILIKWENDA KWA SHUGHULI ZANGU ZA KICHAMA NA KWAKWELI NILIJUA MAZISHI YAMESHAFANYIKA YA DR. KYARUZI NIKIWA DAR NIKAMWOMBA KATIBU WA MKOA KUWA NIKIWA MISENYI NIENDE NYUMBANI KUWASALIMIA WAFIWA, AKANIAMBIA HAWAJAZIKA, NA ILIKUWA WAZIKE KESHO YAKE YA SIKU NILIYOENDA KAGERA, NIKAMWAMBIA BASI NITAPITA MSIBANI KUTOA POLE. NA NDIVYO NILIVYOFANYA , NILIPOFIKA TU NIKAENDA KUTOA POLE NDIO NIKAENDELEA NA SHUGHULI ZILIZONIPELEKA KAGERA.KAGERA SIKWENDA KUHANI MSIBA NILIKWENDA KWA SHUGHULI YA VIJANA, SI BUSARA HATA KIDOGO KULAUMU BILA KUULIZA HASA KWA MHUSIKA. NINASIKITISHWA NA UAMUZI WA MWANDISHI KUJIPA USEMAJI WA VIJANA KAGERA NA KUSHINDWA HATA KUWAULIZA WAHUSIKA MAANA WAPO KAGERA NAPE ALIFUATA NINI KAGERA.

LAKINI KUDHIHIRISHA NIA MBAYA YA MWANDISHI, MWANDISHI KAAMUA KUDANGANYA UMMA KUWA NILIKUWEPO KAGERA SIKU YA MAZISHI YA DR. KYARUZI, AMA KAAMUA KUKOLEZA KUSUDI LAKE BAYA AU HAJUI ALICHOKISEMA, UKWELI NI KWAMBA TAREHE 25/05/2012 NILIKWENDA KAGERA NA KURUDI DSM SIKU HIYOHIYO SASA HUYO NAPE WA TAREHE 26 NI YUPI? NI VIZURI KUPIMA TUHUMA KABLA YA KUZITOA.

NINA MSAMEHE BURE MWANDISHI NA ALIOSHIRIKIANA NAO.

Nape ndugu yangu kubali tuu hapo something was not right. Kama unamfananisha marehmu Dr. Kyaruzi na baba mzazi wako, then hata kama ulikuwa na ziara ya chama Bukoba either ungei-postpone au kiongozi mwingine wa chama angekuwakilisha na wewe kwenda kwenda kwenye msiba. Ndio uzalendo ambao wewe mwenyewe umekuwa ukiimba majukwaani.

Lakini kitendo cha wewe kuonekana unacheza gofu wakati wa msiba haileti picha nzuri kwa watu hasa pale unapodai kuwa marehemu alikuwa sawa na baba yako. Sometimes, ni bora kukubali something went wrong and move on badala ya kubisha kitu ambacho kipo wazi kabisa.

Bado sielewi unapose kuwa hukwenda Bukoba rasmi kwa ajili ya msiba bali kwa ajili ya shughuli zako za kichama wakati unasema kuwa marehemu ni sawa na baba yako. Pia inaonyesha personally ulikuwa hujui hata tarehe ya mazishi. It does not make any sense at all hasa unaposema kuwa marehemu ni sawa na baba yako.

Huwezi kufika na kutoa pole kwa mtu unayemthamini kama baba yako kisha kundelea na shughuli zako kama kawaida ikiwa ni pamoja na kucheza gofu. Huo si utamaduni wa Wahaya wala Watanzania kwa ujumla. Kubali tuu you got it wrong and learn from it.
 
Nape,
Mkuu wangu vipi tena mbona unajichanganya mwenyewe ktk maelezo yako. Mara huyu mzee ni kama baba yako mzazi halafu nilitegekmea umeenda Kagera kumzika baba yako kumbe hukwenda kumzika bali ulienda kisiasa na kucheza golf wakati wa msiba mkubwa kama ule...Halafu unalaani kitendo cha mwandishi kuhusisha kifo hicho na siasa. Hapa wala sintokuelewa kabisa maana wewe mwenyewe umeifanya siasa halafu unalaani kitendo chako kinapotafsirika kisiasa.

Kaaazi kweli kweli! Nadhani Nape atajuta kwa kuleta uzi huu hapa. Hii ndiyo JF bana.
 
kumbe alienda kumtangaza malinzi kuwe awe chaguo la wahaya huko misenyi poleni misenyi
 
Jaman kumbe Nape ni kijana hivi??? Mm nilijua mzee kulingana na tabia alizonazo mara nyingi zinafanywa na wazee sana!
 
am sure..kama baba yako angekuwa hai ..angekupiga risasi immediately...
 
NAOMBA IJULIKANE KUWA KAGERA SIKWENDA RASMI KWA AJILI YA KUHANI MSIBA, ISIPOKUWA NILIKWENDA KWA SHUGHULI ZANGU ZA KICHAMA NA KWAKWELI NILIJUA MAZISHI YAMESHAFANYIKA YA DR. KYARUZI NIKIWA DAR NIKAMWOMBA KATIBU WA MKOA KUWA NIKIWA MISENYI NIENDE NYUMBANI KUWASALIMIA WAFIWA, AKANIAMBIA HAWAJAZIKA, NA ILIKUWA WAZIKE KESHO YAKE YA SIKU NILIYOENDA KAGERA, NIKAMWAMBIA BASI NITAPITA MSIBANI KUTOA POLE. NA NDIVYO NILIVYOFANYA , NILIPOFIKA TU NIKAENDA KUTOA POLE NDIO NIKAENDELEA NA SHUGHULI ZILIZONIPELEKA KAGERA.KAGERA SIKWENDA KUHANI MSIBA NILIKWENDA KWA SHUGHULI YA VIJANA, SI BUSARA HATA KIDOGO KULAUMU BILA KUULIZA HASA KWA MHUSIKA. NINASIKITISHWA NA UAMUZI WA MWANDISHI KUJIPA USEMAJI WA VIJANA KAGERA NA KUSHINDWA HATA KUWAULIZA WAHUSIKA MAANA WAPO KAGERA NAPE ALIFUATA NINI KAGERA.

Mkuu Nape nimekuelewa vizuri sana kwenye hili. Na ukweli ni kwamba kwa kiasi kikubwa umewajibu vijana wa Kagera kuwa wewe hukutumwa wala hukuwa na nia ya kwenda msibani maalum kwa ajili ya kuhani (kutoa pole). Hivyo msiba wa Dr Kyaruzi haukuwa kwenye ratiba ya serikali wala chama ila imetokea as a coincidence kuwa katika pitapita zako za shughuli za chama ukakuta watu wamekaa msibani na wewe ukaona ni utanzania kuungana nao kwa muda kabla ya kuendelea na shughuli.

Kosa kubwa ulilolifanya ambalo linawapatia critics sababu za kukulaumu ni timing ya Ziara yako. kama umeeleza kuwa tokea Dar ulikuwa unajua kuwa Bukoba kuna msiba wa mtu maarufu, basi ungeahirisha safari yako angalau kwa wiki mbili ili kutoa fursa ya wanabukoba kuomboleza kabla ya kwenda kuwa-overload na pilikapilika za jukwaani. Ninaamini kuna wana-CCM waliokuwa kwenye harakati zako wangependa kuhudhuria na kuwa sehemu ya jamii waliokuwa wanamuenzi marehemu ila wasingeweza kushika mawili, na hasa ukizingatia kuwa wengi wao kazi za majukwaani ndizo zinawapatia kula ya kila siku.

Kosa lako kubwa ni 'INSENSITIVITY'- Unaweza limaliza hili kwa kuwataka radhi vijana waliokushutumu na maisha yakaendelea
 
Nape mti wenye matunda ndio unaopigwa mawe, niliwahi kukuambia hapa narudia tena, wewe ni heavy weight kwa wapinzani koko ndio maana watapiga kelele kwa kila move yako. Uliwachoma sana huko Bukoba nadhani hizi kelele ni maumivu.
 
Nimeisoma vizuri sana ile taarifa ya vijana wa bukoba, Nape ndugu yangu mtanzania mwenzangu, mwandishi wa taarifa ile amesema mengi sana lakin kikubwa nilichosikitishwa nacho kwamba kama kweli haukwenda msiban nani basi alikuwepo kutoka chamani kwa muasisi yule mzalendo kama mlivojazana pale Sinza Vatican.
 
Kimasha,
Hebu niambie wapi nilipokosea mimi , ni bora kwako ningeenda kwenye shughuli nisipate muda wa kutoa pole msibani kuliko nilivyopita msibani kutoa pole pamoja na kuwa nilikuwa naratiba nyingine??!! Usitake niamini ziara yangu Kagera imekuumiza kiasi cha kuanza ksasa kuzua mambo yasiyokuwepo! Kuna uongo mwingi wa ajabu kwenye kauli yenu, nimetoa kidogo sana lakini hata swala la KUFUNGUA MATAWI SIJUI MASHINA, SIJAFANYA POPOTE KAGERA KAZI HIYO, SASA KINACHOWAWEWESESHA NI NINI? ushauri wangu jipangeni upya kuleta tuhuma zenu, vinginevyo ni sawa na kutafuta matope kwenye simenti iliyodekiwa!
Nnauye Jr, when you decided to analyse something do it in what can be rationally and theoretically acceptable and emmotionally and pragmatically influenced. Usipende kuwa too megalomeniac kwa kitu ambacho ni dhahiri.

Kwa utamaduni wowote wa Kiafrika na hasa wa Kihaya msiba ni tukio nyeti. Unapoamua kwenda msibani shughuli zote za kisiasa, kiuchumi na nyingine huairishwa labda za ibada na shughuli muhimu kama za hospitali. Kama kufungua matawi sio bidhaa kama avacado kusema nilikuwa nakimbia zisioze hakukuwa na umuhimu wa kuunganisha vitu hivi. Ungehairisha shughuli za kichama na ukaenda kumzika mwasisi wa Taifa hili lakini wewe umeenda mbali zaidi unasema ni rafiki wa baba yako na hivyo ni kama baba yako. Kama mtu mwenye hati hiyo kitaifa na kibinafsi anenziwa hivyo unavyotaka tuamini basi it's shameful kutamka neno kuenziwa.

Wengine wamesema na mimi narudia be apologetic nad you have nothing to lose except primitive no sense and failure to do that utakuwa unatuonyesha kuwa unayo cultural supremacy na tutaendelea kukuuliza ni ya CCM au ya kwako mpaka utakapotueleza. Kuwa immotional hakusaidii na hakujawahi kuwasaidia watu. Na tatu usituletee academic arrogance tukaanza kukuchambua. Hiyo elimu isiyoheshimu intracultural and intercultural relations on dialectical basis ni ipi? Ni ya wapi? Na kama mtu anasoma na anashindwa kuwa rational in judgement na anakuwa na value judgement basi huyo inayoitwa elimu imfanye mtu kuwa critique ni argument haipaswi kuwepo. Labda tujuze kama hii inayosema umesoma ilikuwa ni Hegelian philosophy?
 
Last edited by a moderator:
Wewe nape acha ujanja wakat wa msiba n wa msiba weka usisiem pemben na wakat wa siasa n siasa, kila jambo lina wakat na majira yake, ebo!
 
Kama Nape katika msiba huo hakukukiwakilisha Chama CCM pamoja na serikalil nani aliiwakirisha serikali na CCM?

Hatujasikia bado nani aliwakilisha CCM na ni nani aliwakilisha Serikali. Nape ameishakana, hakuwakilisha Chama. Inawezekana kabisa kwamba serikali haikuwa na Mwakilishi kwenye mazishi ya mpigania uhuru, Mzalendo Mzee Kyaruzi.

Tiba
 
eh kua mwanasiasa bongo kazi kweli..mana kila siku wako kwenye magazeti habari za ukweli na uongo..eh poleni
 
hasa kama ni sawa babako mbona hukuwa na adabu kumheshimu katika ha2a zake za mwisho na kuweza kuungana na ndugu na jamaa kumhifadh kyaruz ktk makaz yake ya milele kwa kuvunja ratiba yako na kujumuika na wenzio, au kulipa muda suala la msiba , wewe ukaanza kufakamia siasa na kuzunguka kuhubir usisiemu na u2015? Na kubatiza wafuasi washo rasm? Ukaanza kutanga tanga miseny na maeneo mengine kule kwenye mkoa wa kyaruz, we kilaza2
 
Ukweli upotoshwe kwa manufaa ya nani na kwa maslahi yepi?

33978_360312760699379_1620680278_n.jpg

Hii kweli inakubalika katika maeneo yenye msiba wa Mtu unayedai kumheshimu sawa na Baba yako??????



Kwa sentensi hii wapo wanaoweza kukusamehewa kwa kisingizio kuwa ulikuwa mpita njia. Lakini sentensi yako ya awali hapo juu kuwa Dr. Kyaruzi ni sawa na Baba yako inakurudisha tena kwenye makosa. Zaidi ya hapo (niongee kama mimi binafsi) sioni kama ingekuwa hasara sana ziara ingesogezwa mbele wa siku chache. Na hii kauli yako kwamba hukwenda rasmi inathibitisha na kuweka kumbukumbu sawa sasa kwamba pamoja na mchango wa Dr. Kyaruzi kumbe hakupata heshima ya Kitaifa. Hii ni kuubeza Uzalendo wa Dr. Kyaruzi. Basi na iwekwe wazi pia kuwa Dr. Kyaruzi tunamsingizia hakuwa mzalendo na wala hakufanya lolote katika historia ya kupigania uhuru linalompa stahili ya heshima ya Kitaifa. Aibu iliyoje?

Nape, inakuwaje unategewa majibu na kukamatika kirahisi namna hii?



Kwanza Tamko hili si la vijana wa Kagera bali Vijana wa Bukoba Mjini wanaoishi Dar es Salaam. Soma tena kwa umakini! Japo, tamaduni za Buhaya katika mazishi na misiba zinafanana mkoa mzima. Ukikosea tamaduni za Bukoba, kama unajua hesabu basi utakuwa umekosea tamaduni za Kagera. Kuhusu mamlaka ya kutoa tamko, nawaachia wao waendelee au waje kutoa yaliyokatika mioyo yao.

Kukosea ndiyo kujifunza, kuomba msamaha si hasara bali uungwana!

Inafurahisha kuona ndugu Nnauye Junior katika kujaribu kujitoa kwenye matope ndio anajikuta anazama zaidi,pole Nape ulipokubali tu kufunga ndoa na CCM,ulikubali kubeba zigo la mavi na nzi watakuhusu mpaka utakapolitema hilo zigo usafishwe
 
Back
Top Bottom