Tamko la vijana wa Kagera kuhusu ziara ya Nape | JamiiForums | The Home of Great Thinkers

Dismiss Notice
You are browsing this site as a guest. It takes 2 minutes to CREATE AN ACCOUNT and less than 1 minute to LOGIN

Tamko la vijana wa Kagera kuhusu ziara ya Nape

Discussion in 'Jukwaa la Siasa' started by OMEGA, May 29, 2012.

 1. O

  OMEGA JF-Expert Member

  #1
  May 29, 2012
  Joined: Jul 12, 2011
  Messages: 671
  Likes Received: 106
  Trophy Points: 60
  Wakuu nimeinasa sehemu nikaona niiweke hapa jamvini

  TAMKO LA VIJANA WA BUKOBA MJINI WAISHIO DAR ES SALAAM

  Ujio wa Nape: Kagera Tumedharauliwa na Uzalendo Umedhihakiwa

  Tumejaribu kutafakari kwa kina juu ya nini hasa kilimsukuma Nape kufika Kagera na kushiriki mazishi ya muasisi wa TAA, mzalendo na mpigania uhuru aliyetelekezwa na Taifa lake, Dr. Vedasto Kyaruzi na bado ki-ukweli hatujapata majibu.

  Tunapata shida kujua dhima ya safari ya Nape kwa kuwa shughuli mahsusi alizozifanya akiwa Kagera zina kinzana kimaadili na kitamaduni na maombolezo ya misiba ya Kiafrika na hasa misiba ya Kihaya. Mjumbe aliyetumwa mahsusi toka mbali kupeleka pole kwenye msiba hategemewi atumie muda wake mwingi majukwaani kufanya siasa, tena katika mazingira ya ugenini lakini kwenye maeneo yale yale msiba unapoendelea. Kwa mpita njia ambaye amefahamishwa tukio na akahiari kufika msibani, akiendelea na shughuli zake haitakuwa ajabu na hakuna mtu mwenye akili timamu atamshangaa hata kidogo.

  Nape aliingia Bukoba tarehe 25/05/2012. Na ni uungwana kukiri kuwa alifika Kashai-Matopeni msibani kutoa salamu za pole. Lakini baada ya hapo alielekea Missenyi ambako tunaarifiwa alikuwa na mikutano ya hadhara. Watanzania mtakumbuka vema kuwa katika mikutano hiyo ndiko Nape alitoa kauli ya kutokuwa tayari kukabidhi nchi kwa wahuni! Labda ili Watanzania muweze kupima vema uelewa na akili za Nape, tuwafahamishe kuwa Missenyi ndiko iliko Kyaka na ambako maziko ya Dr. Kyaruzi yamefanyika. Tunashindwa kuelewa, hiyo mikutano ilikuwa safisha njia ya mazishi au inahusiana vipi na mtu aliyepeleka ujumbe wa maombolezo?

  Linalochanganya zaidi ni hili la Jumamosi tarehe 26/05/2012. Hii ndiyo siku ambayo Dr. Kyaruzi alipumzishwa rasmi kaburini alale kwa amani. Lakini kwa Nape akiwa Kyaka hii ilikuwa siku maalumu ya kufungua matawi na kutangaza operation yake mpya ya kisiasa iitwayo "Vua Gamba, vua Gwanda, Vaa Uzalendo". Katika hili, ukiachilia ukinzani wa matukio kimaadili na kitamaduni, tunapata mishangao mingine; hivi Nape alikwenda Kyaka kuzika au kuzindua operation ya kisiasa? Na Je, huyu kijana anahubiri uzalendo upi? Uzalendo usiokuwa na utamaduni, Uzalendo wa kuwatelekeza na kushindwa kuwaenzi watu waliopigania uhuru wa nchi hii? Kama huo ndiyo uzalendo anaohubiri Nape, basi hauhitaji operation wala kampeni maana tayari tunao magwiji. Na hapo kwa tafsiri hii, ujio na matukio ya Nape kwenye maeneo ya msiba huu vinanapata maana halisi.

  Katika Taarifa ya Uchaguzi mdogo wa Arumeru Mashariki, Chama Tawala kimearifiwa kuwa moja ya kosa lililofanyika ni kumteua mgombea ambaye mila hazikuwa zinampa fursa na tafsiri njema kufanya shughuli kama ya siasa katika muda mfupi baada ya msiba wa Baba yake. Ikiwa kosa hili la Kitamaduni limechangia Chama kupoteza Jimbo, basi pia chama kiwe tayari kwa makosa ya Nape kupoteza zaidi ya Kijiji cha Burifani na Kata nzima ya Kyaka. Na hatutoshangaa iwapo Nape au Taasisi iliyomtuma ikishindwa kuomba radhi!

  Mbali na vioja vya Nape hapo juu, kwa wasifu wa marehemu Dr. Kyaruzi, kila mmoja atakubaliana nasi kuwa Taasisi yoyote (iwe dola au chama) kuwakilishwa na mtu wa ngazi ya Nape ni dharau ya hali ya juu na ichukuliwe ni dhihaka si kwa jamii iliyostaharabika tu, bali hata kwa watu walipendao Taifa lao na kuuenzi Uzalendo. Inakuwa vigumu kuamini kuwa pamoja na ugumu wa ratiba, Rais alikosa muwakilishi makini wa hadhi inayobeba uzito sawia na mchango wa Dr. Kyaruzi katika Taifa hili. Tukio hili linaleta hisia za ubaguzi wa Taasisi za dola na chama katika kutoa uzito kwenye majanga, matatizo na misiba ya watu wa Taifa hili.

  Ni majuzi tu Taifa lilipotelewa na Mcheza Sinema nguli ambaye hapo awali hakuwahi kupata heshima yoyote ya Kitaifa. Lakini tuliona jinsi viongozi wa Serikali na Chama walivyohamia msibani na Serikali kujipa jukumu la kuubeba msiba na shughuli za mazishi. Haikupita muda, Rais akiwa ziarani Marekani, Rais wa Malawi alifariki duniani. Pamoja na uchovu wa safari tulimwona Rais akiingia nchini na kutoka kuwahi mazishi ya Rais wa nchi jirani. Kulingana uzito na umuhimu uliowekwa na Rais katika msiba huu, hakusubiri hata atatue matatizo makubwa yaliyokuwa yanaikabili serikali yake kiasi cha kutishiwa kuanguka. Lakini pia ni kawaida kusoma taarifa za Rais anazoandika katika mitandao ya kijamii (MyKj) kila anapoelekea kwenye misiba ya watu wa kawaida walioko katika maeneo mbalimbali Jijini Dar es Salaam. Hili linatuongezea huzuni na kutuongoza kuamini kuwa misiba ya watu wa maeneo nje na Dar es Salaam haigusi hisia za Rais hata kama ni ya Watu waliotoa mchango mkubwa kwa Taifa hili.

  Haya yaliyotokea kwa Dr. Kyaruzi alimanusura yatokee pia kwenye msiba wa MKUU wa Majeshi Mstaafu Jenerali Ernest Mwita Kyaro. Marehemu Mwita alifariki siku chache baada ya mazishi ya Kanumba na msiba wake ulikosa sura ya Kitaifa. Isingekuwa kelele za wana-Mitandao ya Kijamii (MyKj) na wahandishi wa habari, hata Bunge lisingesimama kwa dakika moja kutoa salamu. Tabia hii ya kutelekeza wazalendo wa Taifa hili inaonekana kumea kwa kasi. Na uthaminisho wa serikali kwa watu wa Dar es Salaam unaonekana kuwa juu kuliko wa wale walioko nje ya Dar es Salaam.

  Kwa Tamko hili tunamtaka Nape Nnauye, Katibu Mwenezi wa CCM kama kweli alikuja kuwakilisha Taasisi yoyote katika msiba wa Dr. Kyaruzi, basi aiombe radhi jamii yetu kwa dharau kubwa aliyoonyesha katika msiba huu. Na kama alikuwa mpita njia tu, basi atujuze ili Jamii na historia ya Taifa imwandike rasmi Dr. Kyaruzi kama muasisi wa TAA na mzalendo aliyepigania uhuru wa Taifa lake ambaye hakuenziwa wakati wa uhai wake na hata mazishi yake hayakuhudhuriwa na mwakilishi wa Kitaifa.

  Na mwisho tunamtaka Rais wa Jamhuri ya Muungano Tanzania, yeye kama Taasisi awe Rais wa Watanzania wote; wa Dar es Salaam na Mikoani.


  Asiye na Utamaduni ni Mtumwa. Tanzania ni Moja

  Imetolewa na:
  Erick Mwemezi Kimasha
  Mhamasishaji Jamii Mkuu
  Vijana wa Bukoba Mjini Waishio Dar es Salaam

  Barua Pepe:
  ekimasha@ksgroup.co.tz
  Simu: 0713-177-372

  Tarehe: 27/05/2012

  MAJIBU YA NAPE
   
 2. Edson

  Edson JF-Expert Member

  #2
  May 29, 2012
  Joined: Mar 7, 2009
  Messages: 9,202
  Likes Received: 722
  Trophy Points: 280
  nimeisoma taarifa......Nape upo?
   
 3. e

  ebaeban JF-Expert Member

  #3
  May 29, 2012
  Joined: Jan 15, 2012
  Messages: 1,834
  Likes Received: 600
  Trophy Points: 280
  Ni huyu NAPE aliyetoa kauli tata hapo nyma eti Mwl. Nyerere yuko kwenye mchakato wa kupata daraja la u-wenyeheri eti kwa ajili ya uadilifu wake nadani ya CCM. nakumbuka nilimwonya vikali sana kuhusu hilo domo lake. Domo lake hulo linamponza yeye na chama chake.
   
 4. m

  mgeni wenu JF-Expert Member

  #4
  May 29, 2012
  Joined: Jan 2, 2012
  Messages: 3,669
  Likes Received: 614
  Trophy Points: 280
  Ni sawa bwana Mwemezi,ila kama una aikili timamu na unajua unachokifanya basi hutokuwaa na haja ya kugombana na Nape,labda kama huijui akili na uelewa wa Nape na Chama chake ninachokuomba ni kuitisha uchaguzi wa vijana wa kihaya halafu wakuchague kisha kila post andika cheo hicho,ila kwa sasa unaibaka Demokrasia japo una mawazo mazuri toka Nkenge,
   
 5. GIB

  GIB JF-Expert Member

  #5
  May 29, 2012
  Joined: Mar 2, 2012
  Messages: 337
  Likes Received: 0
  Trophy Points: 0
  Ndugu watakusikiliza kweli? Au nawewe watakudharua? Yetu macho ,ngoja tusubiri
   
 6. TIQO

  TIQO JF-Expert Member

  #6
  May 29, 2012
  Joined: Jan 8, 2011
  Messages: 13,832
  Likes Received: 46
  Trophy Points: 0
  Nape aliharibu alipiga two in one
  eti Vua Gamba, Vua Gwanda vaa Uzalendo
   
 7. Kakulwa P

  Kakulwa P JF-Expert Member

  #7
  May 29, 2012
  Joined: Feb 8, 2012
  Messages: 200
  Likes Received: 1
  Trophy Points: 0
  Maneno uliyotamka ni mazuri sana, haiyumkiniki huyu kijana amekuja moto sana hata bila kuuliza wale wenyeji wake.

  Amekuwa bingwa wa matamko kama marehemu DITOPILE R.I.P halafu baya zaidi amepata watu wakiwepo wazee wa Kyaka kwenye mambo yake yasiyoenda na tamaduni zetu sisi hasa wakati wa Msiba.

  Nilishasikia kwa baadhi ya wanachama CCM wakimsema huyu kijana kuwa atakuwa chanzo cha kuleta mipasuko maana haulizi aseme lipi na wakati gani.

  Msimamo wenu nawaunga mkono ingawa sijui kama kuna wenzenuCCM wenye uwezo wa kuyasoma na kuwa na neno la kuomba RADHI, naamini yatabaki hapa JF lakinimmetimiza wajibu wenu kusema EMPISI EKANYAMPILA EIBALE...................Mmeonyesha njia.
   
 8. sir.JAPHET

  sir.JAPHET JF-Expert Member

  #8
  May 29, 2012
  Joined: May 18, 2012
  Messages: 700
  Likes Received: 0
  Trophy Points: 33
  duuu, kweli nchi IMEPOTEZA DIRA
   
 9. SHIEKA

  SHIEKA JF-Expert Member

  #9
  May 29, 2012
  Joined: Dec 20, 2011
  Messages: 8,138
  Likes Received: 947
  Trophy Points: 280
  Kwa tamaduni nyingi za kiafrika, kama unakwenda kuomboleza msibani hutakiwi kufanya shughuli nyingine kama alivyofanya Nape.

  Bwana Nape, hebu jitokeze uombe radhi mapema kabla muda haujaenda sana.
   
 10. S

  Sheshejr JF-Expert Member

  #10
  May 29, 2012
  Joined: Jan 14, 2012
  Messages: 435
  Likes Received: 7
  Trophy Points: 0
  Nape ni janga la taifa.
   
 11. Trustme

  Trustme JF-Expert Member

  #11
  May 29, 2012
  Joined: Jan 7, 2011
  Messages: 1,172
  Likes Received: 9
  Trophy Points: 0
  mmmmh kumbe na nyie mmeona eeeh! Bora mmwambie nyie wana ccm wenzake!
   
 12. A

  Analytical Senior Member

  #12
  May 29, 2012
  Joined: Mar 7, 2011
  Messages: 149
  Likes Received: 1
  Trophy Points: 0
  Mmh, Hivi kumbe Nape alienda kuhani msiba? Mbona picha zilizokuwa reported ni za kucheza gofu tu?
   
 13. N

  Ndinani JF-Expert Member

  #13
  May 29, 2012
  Joined: Aug 29, 2010
  Messages: 5,413
  Likes Received: 734
  Trophy Points: 280
  Wenzie katika hicho chama cha magamba wamesema huyu Nape vuvuzela amekifanya hicho chama mali yake kwani anafanya na kusema vile atakavyo yeye na hakuna wa kumzuia; kwani katibu wake mkuu wilson Mukama amekuwa mzigo kwa chama chao!!

  Wako mbioni kubadilisha sekretariet yao na kumrudisha Jaka Mwambi kama katibu mkuu, mtu waliemuengua hapo awali kwa ubadhilifu wa fedha za chama na kumficha ubalozini Urusi!! Kama ni kweli basi CCM ndio mwisho kwani huyu mwanamtandao ndio atazidisha mipasuko kwenye hilo chama la magamba!!
   
 14. NG'OMBE

  NG'OMBE JF-Expert Member

  #14
  May 29, 2012
  Joined: Mar 26, 2011
  Messages: 362
  Likes Received: 0
  Trophy Points: 33
  Nape ni kansa inayoitafuna ccm, huku wakijifariji kuwa wana afya njema, watakuja shituka siku ya mazishi ya ccm hapo ndipo watakapo amini kumbe tulikuwa tunaumwa.
   
 15. H

  Honey K JF-Expert Member

  #15
  May 29, 2012
  Joined: Sep 14, 2008
  Messages: 629
  Likes Received: 2
  Trophy Points: 0
  Nimesikitishwa sana sana NA UPOTOSHAJI MKUBWA UNAENDELEA KATIKA SAFARI YANGU YA KWENDA KAGERA! KILICHONIUMA ZAIDI NI JINSI WATU WANAVYOTAKA KUTUMIA MSIBA KAMA NGAO YAO YA KUPOTOSHA UKWELI WA SWALA ZIMA LA SAFARI YANGU KAGERA. KWA WASIOJUA AU WALIOAMUA KUPOTOSHA UKWELI KWA MAKUSUDI, DR. KYARUZI ALIKUWA RAFIKI MKUBWA WA MAREHEMU BABA YANGU MZAZI BRIG. GEN MOSES NNAUYE, HIVYO MAREHEMU KYARUZI NI SAWA NA BABA YANGU. NINA LAANI JUHUDI ZA KUTAKA KUTUMIA ZIARA YANGU KAGERA NA MSIBA WA MZEE WANGU KYARUZI KISIASA.

  NAOMBA IJULIKANE KUWA KAGERA SIKWENDA RASMI KWA AJILI YA KUHANI MSIBA, ISIPOKUWA NILIKWENDA KWA SHUGHULI ZANGU ZA KICHAMA NA KWAKWELI NILIJUA MAZISHI YAMESHAFANYIKA YA DR. KYARUZI NIKIWA DAR NIKAMWOMBA KATIBU WA MKOA KUWA NIKIWA MISENYI NIENDE NYUMBANI KUWASALIMIA WAFIWA, AKANIAMBIA HAWAJAZIKA, NA ILIKUWA WAZIKE KESHO YAKE YA SIKU NILIYOENDA KAGERA, NIKAMWAMBIA BASI NITAPITA MSIBANI KUTOA POLE. NA NDIVYO NILIVYOFANYA , NILIPOFIKA TU NIKAENDA KUTOA POLE NDIO NIKAENDELEA NA SHUGHULI ZILIZONIPELEKA KAGERA.KAGERA SIKWENDA KUHANI MSIBA NILIKWENDA KWA SHUGHULI YA VIJANA, SI BUSARA HATA KIDOGO KULAUMU BILA KUULIZA HASA KWA MHUSIKA. NINASIKITISHWA NA UAMUZI WA MWANDISHI KUJIPA USEMAJI WA VIJANA KAGERA NA KUSHINDWA HATA KUWAULIZA WAHUSIKA MAANA WAPO KAGERA NAPE ALIFUATA NINI KAGERA.

  LAKINI KUDHIHIRISHA NIA MBAYA YA MWANDISHI, MWANDISHI KAAMUA KUDANGANYA UMMA KUWA NILIKUWEPO KAGERA SIKU YA MAZISHI YA DR. KYARUZI, AMA KAAMUA KUKOLEZA KUSUDI LAKE BAYA AU HAJUI ALICHOKISEMA, UKWELI NI KWAMBA TAREHE 25/05/2012 NILIKWENDA KAGERA NA KURUDI DSM SIKU HIYOHIYO SASA HUYO NAPE WA TAREHE 26 NI YUPI? NI VIZURI KUPIMA TUHUMA KABLA YA KUZITOA.

  NINA MSAMEHE BURE MWANDISHI NA ALIOSHIRIKIANA NAO.
   
 16. Ruhazwe JR

  Ruhazwe JR JF-Expert Member

  #16
  May 29, 2012
  Joined: Jan 31, 2011
  Messages: 3,414
  Likes Received: 21
  Trophy Points: 135
  najua Nape atakuja tu hapa,mtaona pumba atakazo mwaga hapa,mi nipo hapa mtaniambia
   
 17. Arvin sloane

  Arvin sloane JF-Expert Member

  #17
  May 29, 2012
  Joined: Jul 18, 2011
  Messages: 963
  Likes Received: 36
  Trophy Points: 45
  Siasa bana haya yetu macho.
   
 18. Ringo Edmund

  Ringo Edmund JF-Expert Member

  #18
  May 29, 2012
  Joined: May 10, 2010
  Messages: 4,895
  Likes Received: 28
  Trophy Points: 0
  Natamani wazee wastaafu wa afrika mashariki waisome hii.
  Itasaidia na wapigania uhuru waliobaki watafute namna ya kumalizia maisha yao hapa nchini bila kutegemea serikali katika kuwaenzi.

  Ujio wa nape ccm kwa wakati huu ni maalum katika mpango wa mungu wa kuisafisha nchi.
   
 19. K

  Kitungamirwa JF-Expert Member

  #19
  May 29, 2012
  Joined: Mar 28, 2012
  Messages: 320
  Likes Received: 0
  Trophy Points: 33
  Kyoma uliyosema yanasikitisha kuona mtu aliyepigania taifa hili kutoka mikononi mwa wakoloni na leo watu wanaenjoy matunda ya kazi yake halafu wanamdump.

  Kama si mchango wake wangekuwa wanajisifia na amani hewa ya nchi hii? Tuungane pamoja Watanzania kuikataa ccm na mambo yake yote maana kama hawawezi kuwaenzi waasisi wa taifa hili vipi kwetu ambao uasisi wake tunausoma kwenye historia watatujali vipi?

  Apigwe marufuku asikanyage BK tena make yeye ndo muhuni
   
 20. Ericus Kimasha

  Ericus Kimasha Verified User

  #20
  May 29, 2012
  Joined: Oct 27, 2006
  Messages: 488
  Likes Received: 126
  Trophy Points: 60
  Ukweli upotoshwe kwa manufaa ya nani na kwa maslahi yepi?

  [​IMG][​IMG]
  Hii kweli inakubalika katika maeneo yenye msiba wa Mtu unayedai kumheshimu sawa na Baba yako??????

  Kwa sentensi hii wapo wanaoweza kukusamehewa kwa kisingizio kuwa ulikuwa mpita njia. Lakini sentensi yako ya awali hapo juu kuwa Dr. Kyaruzi ni sawa na Baba yako inakurudisha tena kwenye makosa. Zaidi ya hapo (niongee kama mimi binafsi) sioni kama ingekuwa hasara sana ziara ingesogezwa mbele wa siku chache. Na hii kauli yako kwamba hukwenda rasmi inathibitisha na kuweka kumbukumbu sawa sasa kwamba pamoja na mchango wa Dr. Kyaruzi kumbe hakupata heshima ya Kitaifa. Hii ni kuubeza Uzalendo wa Dr. Kyaruzi. Basi na iwekwe wazi pia kuwa Dr. Kyaruzi tunamsingizia hakuwa mzalendo na wala hakufanya lolote katika historia ya kupigania uhuru linalompa stahili ya heshima ya Kitaifa. Aibu iliyoje?

  Nape, inakuwaje unategewa majibu na kukamatika kirahisi namna hii?

  Kwanza Tamko hili si la vijana wa Kagera bali Vijana wa Bukoba Mjini wanaoishi Dar es Salaam. Soma tena kwa umakini! Japo, tamaduni za Buhaya katika mazishi na misiba zinafanana mkoa mzima. Ukikosea tamaduni za Bukoba, kama unajua hesabu basi utakuwa umekosea tamaduni za Kagera. Kuhusu mamlaka ya kutoa tamko, nawaachia wao waendelee au waje kutoa yaliyokatika mioyo yao.

  Kukosea ndiyo kujifunza, kuomba msamaha si hasara bali uungwana!
   
Loading...