Tamko la vijana wa Kagera kuhusu ziara ya Nape

Nape alikuwa na majukumu mawili ya kufanya.Moja ni kutoa pole na la pili ni ziara zake za kisiasa na hilo si tatizo.Kwangu sina tatizo nalo.Mbona viongozi wengi tu wanapomaliza misiba wanaendelea na shughuri za kisiasa.Tatizo liko wapi jamani?Summary hakukataliwa kwa ajili ya taratibu za kimila ati zilikiukwa.issue watu walichoka na utawala wa kurithishana na siyo lingine.Mwacheni nape afanye kazi yake ni kweli nape ni mzalendo.Kwa hilo mimi sikatai hata kama mimi si mwanachamama wa chama chochote.

Hapo kwenye red, unaweza kumaliza msiba bila kuzika?au msiba humalizika vipi?
 
Mods, mngetenda haki kwa kuweka pia shutuma nilizotupiwa ili wasomaji waelewe kinachoendelea badala ya hivi wengi hawataelewa kilichotokea..............
Kwa lolote lilioandikwa, mkuu wangu hukutakiwa kujibu mahusiano baina ya mzee huyu na familia yako kama ulivyoandika. Kwa msomaji yeyote yule anaposoma habari hii ataelewa uzito wa msiba wa mzee yule kwa familia yako na chama halafu wewe umeenda cheza golf?. Yaani kweli wewe na chama chako mnathamini mchango wa huyu marehemu kwa Taifa hili? kama kama ndio ama sivyo ebu tueleze kwa nini chama hakikumpa heshima zote a mazishi anazostahili?..
 
Kwakweli nilijua mazishi yameshafanyika ya Dr. Kyaruzi nikiwa Dar....

Hivi kwa kauli hiyo Nape huoni unajidhalilisha na kukidhalilisha chama cha mapinduzi?unawezaje kusema bila aibu kuwa hukujua na kwa maneno mengine chama hakikujua mzee kyaruzi anazikwa lini?

Hivi kama utashindwa kuelewa na kuyapa uzito mambo madogo kama hayo hivi kweli unaweza ukaisaidia ccm kitu au you are just celebrating to be part of the collapsing rotten system?

Inakuwaje msiba wa mpigania uhuru kama mze kyaruzi msijue anazikwa lini? Inakuwaje msiba wa mtu wa kawaida kama kanumba ambaye mchango wake kwa taifa hili si muhimu kama mzee kyaruzi makenda cabinet nzima na paka mkagharamia mazishi?

Hivi ni busara gani kumtuma kiongozi mdogo kama huyo msibani eti akiwakilishe chama wakati na ww ulikuwa na ziara mkoa huo?

Kwa tamaduni za kiafrika mtoto anayeshindwa kumjali mzazi wake huwa hana maisha marefu, CCM inaelekea kaburini
 
Mbona nyie hamwatendei hak watz mnawachakachua mnajilia kivulin national cake, hamwakumbuk watz, mmekuwa jeuri baada ya kupewa madaraka, hii nchi n ya wote wajamen sio kwamba ina hat milk ya sisiemu,
 
Dharau za CCM kwa waasisi hawa wa Taifa hili haikuanza Leo!! Hata Nyerere aliwapiga Chini waasisi wote na kubakiza jina lake tu pale Mbele! Ishu hapa si Kufariki na Kuzika peke yake! Tutazame pia waasisi hawa wa taifa wanaishi vipi??
Kuhusu huyu Nape, huyu tuachane naye, kwani ni Mpango wa Mungu kutuletea mtu kama huyu kwa Maslahi ya Taifa letu hapo baadaye!!
 
Inakuwaje msiba wa mpigania uhuru kama mze kyaruzi msijue anazikwa lini? Inakuwaje msiba wa mtu wa kawaida kama kanumba ambaye mchango wake kwa taifa hili si muhimu kama mzee kyaruzi makenda cabinet nzima na paka mkagharamia mazishi?

Hivi ni busara gani kumtuma kiongozi mdogo kama huyo msibani eti akiwakilishe chama wakati na ww ulikuwa na ziara mkoa huo?

Kwa tamaduni za kiafrika mtoto anayeshindwa kumjali mzazi wake huwa hana maisha marefu, CCM inaelekea kaburini
maneno mazito na yanachoma sana, ama kweli CCM mna tatizo kubwa!
 
Hivi watoto na familia nzima ya Marehemu Mzee Kyaruzi wakisoma majibu ya Nape watajisikiaje? Kwamba hakuwa na mpango wa kwenda kwenye msiba ila ilitokea tu kwa sababu alikuwa Bukoba kikazi!
 
Nimesikitishwa sana sana NA UPOTOSHAJI MKUBWA UNAENDELEA KATIKA SAFARI YANGU YA KWENDA KAGERA! KILICHONIUMA ZAIDI NI JINSI WATU WANAVYOTAKA KUTUMIA MSIBA KAMA NGAO YAO YA KUPOTOSHA UKWELI WA SWALA ZIMA LA SAFARI YANGU KAGERA. KWA WASIOJUA AU WALIOAMUA KUPOTOSHA UKWELI KWA MAKUSUDI, DR. KYARUZI ALIKUWA RAFIKI MKUBWA WA MAREHEMU BABA YANGU MZAZI BRIG. GEN MOSES NNAUYE, HIVYO MAREHEMU KYARUZI NI SAWA NA BABA YANGU. NINA LAANI JUHUDI ZA KUTAKA KUTUMIA ZIARA YANGU KAGERA NA MSIBA WA MZEE WANGU KYARUZI KISIASA.

NAOMBA IJULIKANE KUWA KAGERA SIKWENDA RASMI KWA AJILI YA KUHANI MSIBA, ISIPOKUWA NILIKWENDA KWA SHUGHULI ZANGU ZA KICHAMA NA KWAKWELI NILIJUA MAZISHI YAMESHAFANYIKA YA DR. KYARUZI NIKIWA DAR NIKAMWOMBA KATIBU WA MKOA KUWA NIKIWA MISENYI NIENDE NYUMBANI KUWASALIMIA WAFIWA, AKANIAMBIA HAWAJAZIKA, NA ILIKUWA WAZIKE KESHO YAKE YA SIKU NILIYOENDA KAGERA, NIKAMWAMBIA BASI NITAPITA MSIBANI KUTOA POLE. NA NDIVYO NILIVYOFANYA , NILIPOFIKA TU NIKAENDA KUTOA POLE NDIO NIKAENDELEA NA SHUGHULI ZILIZONIPELEKA KAGERA.KAGERA SIKWENDA KUHANI MSIBA NILIKWENDA KWA SHUGHULI YA VIJANA, SI BUSARA HATA KIDOGO KULAUMU BILA KUULIZA HASA KWA MHUSIKA. NINASIKITISHWA NA UAMUZI WA MWANDISHI KUJIPA USEMAJI WA VIJANA KAGERA NA KUSHINDWA HATA KUWAULIZA WAHUSIKA MAANA WAPO KAGERA NAPE ALIFUATA NINI KAGERA.

LAKINI KUDHIHIRISHA NIA MBAYA YA MWANDISHI, MWANDISHI KAAMUA KUDANGANYA UMMA KUWA NILIKUWEPO KAGERA SIKU YA MAZISHI YA DR. KYARUZI, AMA KAAMUA KUKOLEZA KUSUDI LAKE BAYA AU HAJUI ALICHOKISEMA, UKWELI NI KWAMBA TAREHE 25/05/2012 NILIKWENDA KAGERA NA KURUDI DSM SIKU HIYOHIYO SASA HUYO NAPE WA TAREHE 26 NI YUPI? NI VIZURI KUPIMA TUHUMA KABLA YA KUZITOA.

NINA MSAMEHE BURE MWANDISHI NA ALIOSHIRIKIANA NAO.

Ndugu Nnape,

Kwanini CCM mnapenda kusema uongo na kuwafanya Watanzania kama vile hawana akili????
Mtu mwenye akili timammu akisoma kwenye hizo sentensi nili-zo highlight kwa RED anaona kabisa hapa husemi ukweli!

Kama kweli Marehemu Dr. Kyaruzi alikuwa rafiki wa Baba yako na wewe unasema kwako ni kama BABA ilikuwaje ukawa huna mawasialiano na familia yake mpaka ukawa unadhani wamesha zika??Na baada ya kupata taarifa kuwa hawajazika na ukapanga kuwa utafika kwenye msiba,kwanini hukushiriki mazishi kama kweli marehemu alikuwa kama Baba kwako?Je
hiyo safari yako ya KICHAMA ilikuwa na uzito gani kiasi kwamba usiisitishe kwanza mpaka baada ya msiba ndipo uende kuendelea na shughuli zako za kichama??? Hivi angelikuwa ni Baba yako mzazi Mosses Nnauye ndo ame ret in peace ungelikuwa kweli na nguvu ya kuendelea na harakati na propaganda zako za kichama za SIJUI VUA GAMBA,VUA GWANDA, VAA UZALENDO??? CCM mnajua UZALENDO gani unaowahubiria watu?? Uzalendo umekwenda na Baba wa Taifa Mwl.Nyerere pengine na huyo Marehemu babako. Kwa sasa hakuna Uzalendo wowote katika CCM yako!!!Huo ndo ukweli.

CCM ni tabia yenu kutumia MISIBA kama jukwaa la kisiasa ili kuwalaghai watu. Ndiyo maana juzi kwenye vikao vya CC na NEC wazee kina Yusuf Makamba na Peter Kisumo wamekuambia BLANK POINT kuwa unaua chama MAANA UMEKIFANYA KAMA MALI YAKO. Unafanya unavyotaka. Nataka nikwambie tu kwamba wewe na Mukama wako CCM inawafia mikononi mwenu. Propaganda zako za kutaka kushindana na CHADEMA kila kukicha badala ya kushughulikia MATATIZO SUGU YA WANANCHI hazikisadii chama chenu baali kukiangamiza!

No soon than later CCM kitakuwa chama cha Upinzani!
 
Nnauye Jr Thread hii nakushauri uichukulie kwa style ya JK tu kwamba ni upepo utapita tu, hakuna unaloweza kujitetea ukaeleweka maana siwezi kukushauri kuomba msamaha maana najuwa kwenye kamusi ya CCM hilo neno kuomba msamaha halipo.

Hivi dollar 6000 kwa CCM si ni pesa ndogo? ulishindwa nini kuiruhusu ndege irudi Dar halafu uagize ndege nyingine ikufuate siku ya pili? kinachowasikitisha watu ni Serikali nzima ya CCM kuamia kwenye msiba wa mzinzi na mbakaji Kanumba huku ikishindwa hata kutuma mwakilishi wa chama kwenye msiba wa Freedom Fighter!!
 
Last edited by a moderator:
Kwa haya NAPE INATOSHA KUJIUZULU: Lakini kwa kuwa huna uadilifu na ujasiri huo basi utaendeleza ngonjera hapa! Subiri ufukuzwe ndo dawa yako
 
Mungu alitupa masikio mawili, macho mawili na mdomo mmoja, ili tusikie mengi, tuone mengi na tuseme machache. Pole sana kwa yote, ila ukiona unazidiwa, soma nyakati, liachie hili li nyinyiemu, jiunge na vijana wenzako. Wewe hutakuwa wa kwanza kuliachia, angalia lisifie mkononi mwako.
binadamu ana midomo miwili labda kama unazungumzia kinywa,angalia namna nyingine ya kumtetea hapa. Ila huyu jamaa anatakiwa kijipanga zaidi kabla hajaleta mada hapa jamvini, mada nyingi zinakingamana, oooh mara baba yangu mara nilijua keshazikwa, ooh sikwenda kwenye mazishi, hakuna mtu atakae mwelewa
 
Nape mti wenye matunda ndio unaopigwa mawe, niliwahi kukuambia hapa narudia tena, wewe ni heavy weight kwa wapinzani koko ndio maana watapiga kelele kwa kila move yako. Uliwachoma sana huko Bukoba nadhani hizi kelele ni maumivu.

Tehe! KILAZA BANA... Tehe
 
Nape alikuwa na majukumu mawili ya kufanya.Moja ni kutoa pole na la pili ni ziara zake za kisiasa na hilo si tatizo.Kwangu sina tatizo nalo.Mbona viongozi wengi tu wanapomaliza misiba wanaendelea na shughuri za kisiasa.Tatizo liko wapi jamani?Summary hakukataliwa kwa ajili ya taratibu za kimila ati zilikiukwa.issue watu walichoka na utawala wa kurithishana na siyo lingine.Mwacheni nape afanye kazi yake ni kweli nape ni mzalendo.Kwa hilo mimi sikatai hata kama mimi si mwanachamama wa chama chochote.

Too low, extempore!
 
Hivi Nape una maana zile Salamu za Rais ulizotoa pale zilikuwa feki? Basi hasira za huyu jamaa ni za kweli. Kwamba, Muasisi wa TAA amezikwa bila kiongozi wa kitaifa. Hata mi hapo naona kuna tatizo.

Kwa kweli lengo la Eric Kimasha limetimia. Alitaka kujua hicho ulichosema. Je, ulienda kwa business zako au ulienda msibani? Kwa kuwa ulienda na hamsini zako basi, kuna tatizo pia.
 
Uwezo na uweledi huonekana mapema kinyume chake ............
 
Kimasha,
Hebu niambie wapi nilipokosea mimi , ni bora kwako ningeenda kwenye shughuli nisipate muda wa kutoa pole msibani kuliko nilivyopita msibani kutoa pole pamoja na kuwa nilikuwa naratiba nyingine??!! Usitake niamini ziara yangu Kagera imekuumiza kiasi cha kuanza ksasa kuzua mambo yasiyokuwepo! Kuna uongo mwingi wa ajabu kwenye kauli yenu, nimetoa kidogo sana lakini hata swala la KUFUNGUA MATAWI SIJUI MASHINA, SIJAFANYA POPOTE KAGERA KAZI HIYO, SASA KINACHOWAWEWESESHA NI NINI? ushauri wangu jipangeni upya kuleta tuhuma zenu, vinginevyo ni sawa na kutafuta matope kwenye simenti iliyodekiwa!

Mheshiniwa Nnauye Jr ukianza majibizano ya mtandaoni utakosa muda wa kukiimarisha chama tawala.

Zunguka matawini kurudisha imani ya chamza, mambo ya mtandaoni waachie akina ritz, malaria sugu Faiza.
 
Nape mti wenye matunda ndio unaopigwa mawe, niliwahi kukuambia hapa narudia tena, wewe ni heavy weight kwa wapinzani koko ndio maana watapiga kelele kwa kila move yako. Uliwachoma sana huko Bukoba nadhani hizi kelele ni maumivu.

Ezan Dislike this!
 
Back
Top Bottom