DOKEZO TAMISEMI tufahamisheni, lazima Mtumishi alipie fedha ili apate uhamisho?

Hili ni dokezo maalum toka kwa mwananchi mtumiaji wa JF mwenye nia ya kuusaidia umma kuwa na taarifa 'maalum'
A

Anonymous

Guest
Naandika andiko hili nikiwa ni mmoja wa watumishi wa Serikalini, na nimelazimika kuleta andiko hapa kwa kuwa nguvu kubwa inayotumiwa na wanaofanya mambo kwa mlango wa nyuma wana nguvu kuliko Watumishi wengi ambao ndio wanaokamuliwa hela bila kupenda.

Inajulikana wazi kuwa Mtumishi anapokuwa na sababu za msingi za kutaka kuhama kituo kimoja kwenda kingine, akitaka kufanya hivyo anafuata taratibu za kuomba akiambatanisha na nyaraka zenye uthibitisho wa sababu zilizomfanya aombe uhamisho, kisha mamlaka husika ikiwemo Ofisi ya Rais, Tawala za Mikoa na Serikali za Mitaa (TAMISEMI) kutoa majibu au muongozo.

Soma pia Hongera Mchengerwa kuwa waziri TAMISEMI. Nakuomba yatazame haya, vibali vya uhamisho vina urasimu mkubwa

Lakini hiki kinachoendelea kufanywa na baadhi ya maafisa wa TAMISEMI kinatumaliza Watanzania wengi hasa wale wenye vipato vya chini. Maafisa hao ninaowazungumzia hapa wanatumia madaraka yao vibaya, pia ni kwa kuwa wana mtandao mpana wa watu wanaofanya mambo yao hayo.

Ipo hivi, Mtumishi yeyote wa Serikali unapotaka kupata uhamisho lazima utoe hela labda iwe Mamlaka yenyewe ndio inataka kukupa uhamisho, lakini kama ni maombi yao binafsi ni jambo gumu sana kupata ruhusa hiyo.

Mtumishi wa kawaida akiomba uhamisho wa kawaida, ukaguata taratibu zinazotakiwa, wanaanza kwa kukuzungusha, baadaye ukiendelea kufuatilia baada ya kuona unazungushwa unakutana na sentensi hii “Ongea na watu wa TAMISHEMI wakufanyie mpango”.

Mfano kuna dada mmoja rafiki yangu aliomba uhamisho ili awe karibu na mama yake ambaye ni mgonjwa kwa ajili ya kusaidia kumhudumia, akawasilisha nyaraka za uthibitisho, pia miezi kadhaa ya hivi karibuni alikuwa akitumia muda mwingi kwenda kumuuguza lakini hawakusikiliza badala yake anaulizwa “Una Sh ngapi?”

Ukitaka kupata “msaada” huo unaambiwa sema kisha unapewa namba ya mtu na kupewa maelekezo ya kumpigia, ukimpigia mnajadiliana bei na ukikubali unafanyiwa mpango kila kitu kinachohitajika.

Bei zao mara nyingi ili ufanikishe zoezi lako huwa inaanzia Sh Milioni 2, ukilipa kiwango hicho, unapata barua ikiwa kamili na yenye maombi ya kibali maalum, nyaraka hiyo inakuja ikiwa imeshagongwa muhuri maalum.

Watu wanaofanya michezo hiyo naweza kusema ni “Under cover” kwani hauwezi kujua yuko wapi, haujui wapo Mkoag ani na wanafanya nini hasa lakini nyaraka zao zinakubalika na zinapitishwa na mamlaka, hiyo inamaanisha mtandao wao ni mkubwa na unahusisha hadi watu wazito ndani ya TAMISEMI.

Nyaraka zao hizo zikishafika Halmashauri zinakuwa kibali maalum na hakuna anayeweza kusitisha.

Jamii Forums pazeni sauti, kuna shida kubwa TAMISEMI, Watumishi tunaishia kuwa na Msongo wa Mawazo, mishahara yenyewe midogo, unataka kuhama kwa matatizo, nao wanakuongezea matatizo ya kukuomba hela, kama inawezekana iwekwe wazi tu kuwa ukitaka kuhama unalipia kiasi fulani ili upate ruhusa.
 
Tamisemi suala la uhamisho limekua anasa,ni rushwa rushwa kwenda mbele,sa100 kawapa ruhusa.
 
Tamisemi suala la uhamisho limekua anasa,ni rushwa rushwa kwenda mbele,sa100 kawapa ruhusa.
Mkuu me mbona siwaelewi nachojua kwa sasa uhamisho ni online unafanyika kupitia Employee self service mfumo huo unaupata kupitia ess.utumishi.go.tz. Ukifanikiwa unasubiri tu barua yako. Sasa hizo hela mnaombwa kwenye hatua gn ktk mchakato.
 
Hii term ya pili hawajaachia majina ,Tena TAMISEMI haitoi sababu.

Tumeambiwa majina yapo tayari na yashakuwa proved na karibu Mkuu. Kwanini Majina hayaachiwi watu wahame?

Mmeweka ESS PORTAL nayo IPO hovyo sana na hata hiyo September 1 mliyosema mnaifungua napo IPO hovyo.
 
Hakuna kitu cha bure kwenye hii dunia, unazani huu umbeya wako utakusaidia kwa chochote, kama unataka kuhama lazima uongee herufi kubwa kama hutaki endelea kuota magaga huko vijijini.
 
Back
Top Bottom