Pongezi kwa viongozi wa TAMISEMI kwa kuleta mfumo wa ESS

Taiq

Member
Feb 14, 2023
83
71
Napenda kutoa pongezi zangu za dhati kwa viongozi wa TAMISEMI kwa kutuletea mifumo mbalimbali ya kiutumishi, ambayo ni mkombozi kwa mtumishi wa umma. Kwa nini mifumo hii ni mkombozi? Mifumo hii ni mkombozi kwa sababu zifuatazo:

1. Mifumo hii ni kipimo sahihi cha uwajibikaji.

2. Mifumo hii inakwenda kupunguza rushwa.

3. Kupitia mifumo tunaokoa muda wa kutumia nyaraka mbalimbali za kiutumishi na kupunguza urasimu kwa viongozi wasio waadilifu.

4. Pia mifumo itaipunguzia serekali ghalama za kutuma nyaraka mbalimbali za kiutumishi.

5. Mifumo ni chanzo pekee na sahihi kwa utunzaji nyaraka za kiutumishi.

Mwisho napenda kutoa ushauri juu ya baadhi ya watumishi wasio waadilifu ambao wameanza kutokutoa taarifa zisizo sahihi juu ya uwamisho kwa watumishi. Hivyo basi nawaomba viongozi watoe muongozo wa kiutumishi ambao utatoa suluhisho juu ya taratibu za uhamisho na hasa uhamisho wa kubadilishana vituo vya kazi kwa idara ya elimu na nyinginezo.

Kwa sasa kunataarifa zisizo rasimi ambazo zinadai uhamisho wa kubadilishana ni kwa ajili ya wafanyakazi wenye cheo kinachofanana. Je hizi taarifa ni sahihi na kama ni sahihi naomba mtusaidie muongozo.
 
Umeitumia tayari? Mbona ma supervisor na wakuu wa taasisi wamekalia baadhi ya data? Pia kuna ma HR wale wazembe wamekaa bila kuingiza data za watumishi wao kwa wakati.

Yote haya yanaletwa na utumishi wenyewe kazi ni kuanzisha mifumo bila kufuatilia kama mifumo hizo zinatumiwa ipasavyo...nachelea kusema kuwa utumishi ndiyo wazito.
 
Naomba kuuliza swali ,kinachowafanya mpaka watu wanahama vituo vya kazi ni nn?

Mnapelekwa mbali au hamtaki kufanya kazi kwenu?
Mtu mweusi anapenda Starehe na Matanuzi ndipo akili yake imeishia. Watumishi woooote wanataka kuhamia Mjini hasa kwenye Majiji hasa Daaaslam, hawataki kukaa Vijijini kwa Wannchi wanaowatumikia ndio maana tutaendelea kuwa maskini mpaka mwisho wa maisha yetu.
 
Naomba kuuliza swali ,kinachowafanya mpaka watu wanahama vituo vya kazi ni nn?

Mnapelekwa mbali au hamtaki kufanya kazi kwenu?
Kuhama kituo kinachangizwa na mambo mengi sana.

1. Suala la kiafya, kuwa karibu na hospitali ili kuapata huduma ya kitabibu kama ulivyoelekezwa na daktari...hapa utakuta wenda mzazi, mke, mme au mtoto ndiye anaumwa.

2. Kuwa karibu na mke au mme
 
Uko sawa kabisa na sababu nyingine ni kukaa kituo kimoja ndani ya miaka mitano ni sababu tosha inayompa ruhusa mtumishi kuhamia mazingira mengine.

Ila sababu mpya iliyoongezeka ni hii ya kubadilishana mpaka muwe na vyeo sawa ndio haikuwepo katika muongozo wa awali hasa kwa idara ya elimu.
 
Huko Utumishi kuna visheria sijui kanuni na utaratibu kibao wamezitunga ila hawawezi kuvisimamia, wanaona watumishi ambao wapo kwa ajili ya kuwasimamia wananyanyasika na hao waliowapa vyeo vya ukuu wala hawawezi kuingilia kati.
Huko utumishi ukipeleka malalamiko badala ya kuishughulikia kwa kufanya uchunguzi wanazivujisha taarifa yako kwa wakuu wako ili wakushughulikie tena....
Utumishi kumejaa rushwa sana.
 
Hiyo point no. 2 jidanganye tu.
Wanaoruhusu/Recommend maombi ni hao hao watu, hivyo kama sio waadilifu rushwa itabaki pale pale.
 
Uko sawa kabisa na sababu nyingine ni kukaa kituo kimoja ndani ya miaka mitano ni sababu tosha inayompa ruhusa mtumishi kuhamia mazingira mengine.

Ila sababu mpya iliyoongezeka ni hii ya kubadilishana mpaka muwe na vyeo sawa ndio haikuwepo katika muongozo wa awali hasa kwa idara ya elimu.

Hili suala la hovyo sana,wanakosea sana
 
Kwa taarifa yako Mkuu na wote walio juu yako bado watakufanyia unyama kama wataamua hivyo.

Usijidanganye eti rushwa imeondolewa kwa mfumo huu wa ESS.
 
Naomba kuuliza swali ,kinachowafanya mpaka watu wanahama vituo vya kazi ni nn?

Mnapelekwa mbali au hamtaki kufanya kazi kwenu?
Kuna wengine wametenganishwa na familia zao mfani mtu ana mke na watoto, mume yuko Arusha, mke na watoto wako Lindi, hii inasababisha ugumu kulea watoto na hata gharama za maisha kwa familia kuongezeka na hii ndiyo imefanya watumishi wengi hasa walimu kuwa na madeni makubwa
 
1. Suala la kiafya, kuwa karibu na hospitali ili kuapata huduma ya kitabibu kama ulivyoelekezwa na daktari...hapa utakutayuko wenda mzazi, mke, mme au mtoto ndiye anaumwa.
Na hii ndiyo wengi wanataabika nayo hadi kufikia kuwa na madeni makubwa, kwa mfano mtu yuko Wilaya ya Nyasa huko Kata ya Mwambaoni mwa Ziwa, anatakiwa kumwona Prof. Janabi Muhimbili kila mwezi, kwa ngazi yake ya mshahara D1
 
Waache tu kazi mana kazi zenyewe za utumishi ni utumwa
 
Back
Top Bottom