Nyakijooga
Senior Member
- Dec 9, 2018
- 123
- 202
Malalamiko yangu ni kuhusu uhamisho kwa Watumishi wa Umma, kuna baadhi ya mikoa mfano Mkoa wa Kilimanjaro na Lindi viongozi wetu wanakataa kupokea barua za Watumishi wanaotaka kuhama kwa kusingizia kuwa uhamisho unafanyika kwenye mfumo wa online lakini kiuhalisia hawajui kuutumia.
Hivi karibuni Serikali kupitia TAMISEMI walitutangazia sisi watumishi wa Serikali kuwa maombi yetu ya uhamisho yatakuwa yanafanyika kwa njia ya online lakini inavyoonekana ama mfumo bado haujaanza kufanya kazi rasmi au hakuna elimu iliyotolewa jinsi ya kuutumia na wengi wetu hatujui hata huo mfumo tunautumiaje.
TAMISEMI hawasemi chochote, tukipeleka barua za kawaida viongozi wetu wanakataa kuzipokea wakidai tuombe kupitia mfumo, tukiingia huko tukiwasiliana nao wanapiga chenga kumbe hawajui kuutumia.
Changamoto hii ipo kwa Watumishi wa kawaida hadi wale wa juu mfano Maafisa Elimu, Wakuu wa Shule, Afisa Utumishi wengi wao hawajui jinsi ya kuitumia.