TAMISEMI - Hizi meseji zenu za kampeni ni ukiukwaji msingi ya faragha

Elimu ni muhimu kwa mtoto. Hakikisha mtoto wa miaka 4 anajiunga darasa la awali na mtoto wa miaka 6 anaanza darasa la kwanza. Hakuna ada kwenye shule za umma.

Elimu ya sekondari humuandaa mtoto kukabiliana na changamoto za maisha. Hakikisha mtoto anaripoti shuleni kuanza kidato cha kwanza kwa wakati masomo yameanza.
 
🤣🤣🤣🤣
 
Kwanini mchukue namba zetu za simu kutoka kwenye makampuni ya simu na kuanza tu kutuma tuma meseji bila consent?
Hapana hawaingilii faragha ya mtu.
Imavyofanyika ni wanakubaliana na makampuni ya simu sms zinaachiwa in bulk.
 
Ndio kwanza nami napokea muda huu nakomenti huu uzi. Wanahamasisha elimu ya sekondari kana kwamba ina tija kumbe ni sawa tu na elimu ya msingi. Maelfu ya wanafunzi wanahitimu hiyo elimu kisha wanaachwa wapotelee kusikojulikana bila kuandiliwa mpango mkakakati wa kuendeleza stadi na maarifa waliyoyapata sekondari
 
Hii mitandao ya cm inaona watumiaji wajinga sana, inakuwaje unaniingizia tangazo bila kuomba ridhaa yangu huu ni upimbi sana. Jana nimechukia sana na hii msg ya TAMISEMI.
 
Yaani kufungua tu huu uzi na msg ikaingia, inaboa sana hayo matangazo wangelipia kwenye radio na tv huko
Screenshot_20230131_144301_Messages.jpg
 
Back
Top Bottom